Ndoto huchukua muda gani mpaka inaisha?

Ndoto huchukua muda gani mpaka inaisha?

leop

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
550
Reaction score
523
Mara nyingi huwa nikiota najiulizaga hivi imenichukua muda wa dakika ngapi kuota hii ndoto?! Nisaidieni wataalam kwa hilo tafadhali.
 
Na mimi nina hamu ya kusikia majibu hayo.
 
Mara nyingi huwa nikiota najiulizaga hivi imenichukua muda wa dakika ngapi kuota hii ndoto, nisaidieni wataalam kwa hilo tafadhali.

ndoto huchukua mda usiozidi dakika 1, ngoja nikumbuke halaf ntarud kutililika kuanzia mwanzo wa kulala hadi kuamka,
 
Mara nyingi huwa nikiota najiulizaga hivi imenichukua muda wa dakika ngapi kuota hii ndoto, nisaidieni wataalam kwa hilo tafadhali.

kwa kifupi ndoto huchukua mda usiozidi dakika 1, ngoja nikumbuke halaf ntarud kutililika kuanzia mwanzo wa kulala hadi kuamka,
 
Ungefikiria vizuri usingeuliza hili swali maana unaweza ukaota ndoto yenye maelezo mengi ambapo ukiichukulia kikawaida itachukua hata mwezi mzima Lakini chaajabu utaiota ndani ya dakika hata moja au tano.

Namaanisha kuwa unaweza kujiegesha hata kwenye kiti tu ukasinzia kidogo lakini utaota umeenda kijijini ukapanda mahindi yakamea, yakakomaa, ukavuna na stoo ukayaweka kabisa.
Sasa jiulize ulime, upande mahindi yamee mpaka yakomae alafu uvune uyaweke na stoo 🙂 hapo ilitakiwa hiyo ndoto ikuchukue miezi kama minne lakini hayo yote umeyafanya ndani ya dakika 2-5.
 
Umenifungua ndugu, kweli ndoto zina maajabu yake! dk moja ya kidunia inaweza kuwa siku nzima ndotoni! means ulimwengu wa kifizikia tunaoishi una muda mwingi wa kufanya mambo mengi kama tunaweza elewa thamani ya muda
 
Haya mambo ni yaajabu sana ndugu, Mimi huwa nikiota ndoto mbaya huwa najiuliza hivi hapa niko kwenye ndoto au ni kawaida, maana nikijiuliza tu hivo huwa nakurupuka na kujihakikishia kuwa ulikuwa ni uongo.

Sasa siku moja nikiwa nimeajiriwa kwenye duka fulani nikaota bosi wangu amenipa pikipiki nipeleke ela kwa mfanyabiashara mwenzake kiasi cha sh milioni 13, nikawasha boxer nikaondoka, nilipofika njiani nikamgonga mtoto akafa palepale, pikipiki ikasambaratika na nikijicheck mfukoni ile ela haipo.
Ile tabia yangu ya kujitingisha na kujiuliza kama naota niliijaribu tena lakini haikusaidia nikaona huu ni uhahisia na sio ndoto.

Nikajikatia tamaa kabisa nikaona habari yangu kwisha, nikajaribu tena kujiuliza naota au lah ndio nikakurupuka nikakuta ilikuwa ni ndoto tu.
Nikashukuru sana nikaendelea na maisha kama mwaka mmoja na nusu ambapo ndani ya hapo nilifanya mambo mengi ya maendeleo na mikasa midogomidogo, pia hata kukua niliona nimekuwa kidogo kimwili na kiakili. Lakini Kumbe ilikuwa ndoto ndani ya ndoto,

(Nikakurupuka tena nikayaendeleza maisha pale nilipoachia/pale kabla ile ndoto ya kupewa ela na pikipiki nipeleke kwa mfanyabiashara mwenzake na bosi wangu haijanitokea) nikaendelea na maisha hadi nilipoacha kazi na hadi leo naendelea na maisha.

Kwasasa sijui kama nipo ndotoni au lah. Hata wewe hapo unaesoma hii comment hujui upo ndotoni au ni uhahisia, kama unabisha hebu dhibitisha uko upande gani.
 
Umenifungua ndugu, kweli ndoto zina maajabu yake! dk moja ya kidunia inaweza kuwa siku nzima ndotoni! means ulimwengu wa kifizikia tunaoishi una muda mwingi wa kufanya mambo mengi kama tunaweza elewa thamani ya muda

Kwa tunaoamini uwepo wa Mungu na biblia hii ni proof kuwa Mwenye enzi Mungu baba alipo sema "MIAKA ELFU MOJA KWA MWANADAMU NI SIKU MOJA KWANGU NA SIKU MOJA KWA MWANADAMU NI MIAKA ELFU MOJA KWA MUNGU KWA ATAKAE TUBU"Mwisho wa kunukuu ila sikumbuki ni mstari au kitabu gani ila ipo ivyo.

Na ndo huo upekee wenyewe amabao Mungu baba ametuumba na kutupa uungu ambao ni pumzi na ufanano wake amabao hata wanaobisha hatuna uungu huwa wana prove kwa kuota dakika mbili uhalisia wa miezi kadhaaa.
 
Angalia movie moja inaitwa "INCEPTION" ya Leonardo Di Caprio afu Ntakuja kupokea asante yangu
 
Ndoto fupi huwa si zaidi ya dakika 1 Au ndoto ndefu huchukua hadi dakika 35 hizi ni zile ndoto za asubuhi kabla haujaamka ukiwa kwenye usingizi mzito.
 
Dah.... Sasa hii yangu kali, mie huwa naota ndoto kisha naanza kumsimulia mtu ndoto niliyoota ndotoni. Hii hunitokea mara kwa mara mpaka nakoswa amani, kwanini niote ndoto kisha nimsimulie mtu hiyo ndoto bado nikiwa ndotoni??

Hii ina maana gani???
 
Ndoto halisi haizidi dakika 1, tofauti na hapo ni maruerue. Kuota kunatumia nishati nyingi kutoka kwa ubongo. Ikizidi dk 1 mtu anaweza kufa.
 
Back
Top Bottom