Ndoto huchukua muda gani mpaka inaisha?

Ndoto huchukua muda gani mpaka inaisha?

Wadau mm Nina ndoto mbaya sana yaan naota huko naongea kwa sauti kubwa...wakati mwingine Hadi naamka kitandani, hapo ndipo nashtuka! hii husababishwa na nini? Na nn solution kwa hili tatizo.
 
Dah kuna kitu kinanishangaza kwenye ndoto, yaana unaota ndoto juu ya ndoto, kwa hiyo una kazi ya kutafakari ndoto 2 kwa wakati mmoja
 
Haya mambo ni yaajabu sana ndugu, Mimi huwa nikiota ndoto mbaya huwa najiuliza hivi hapa niko kwenye ndoto au ni kawaida, maana nikijiuliza tu hivo huwa nakurupuka na kujihakikishia kuwa ulikuwa ni uongo.

Sasa siku moja nikiwa nimeajiriwa kwenye duka fulani nikaota bosi wangu amenipa pikipiki nipeleke ela kwa mfanyabiashara mwenzake kiasi cha sh milioni 13, nikawasha boxer nikaondoka, nilipofika njiani nikamgonga mtoto akafa palepale, pikipiki ikasambaratika na nikijicheck mfukoni ile ela haipo.
Ile tabia yangu ya kujitingisha na kujiuliza kama naota niliijaribu tena lakini haikusaidia nikaona huu ni uhahisia na sio ndoto.

Nikajikatia tamaa kabisa nikaona habari yangu kwisha, nikajaribu tena kujiuliza naota au lah ndio nikakurupuka nikakuta ilikuwa ni ndoto tu.
Nikashukuru sana nikaendelea na maisha kama mwaka mmoja na nusu ambapo ndani ya hapo nilifanya mambo mengi ya maendeleo na mikasa midogomidogo, pia hata kukua niliona nimekuwa kidogo kimwili na kiakili. Lakini Kumbe ilikuwa ndoto ndani ya ndoto,

(Nikakurupuka tena nikayaendeleza maisha pale nilipoachia/pale kabla ile ndoto ya kupewa ela na pikipiki nipeleke kwa mfanyabiashara mwenzake na bosi wangu haijanitokea) nikaendelea na maisha hadi nilipoacha kazi na hadi leo naendelea na maisha.

Kwasasa sijui kama nipo ndotoni au lah. Hata wewe hapo unaesoma hii comment hujui upo ndotoni au ni uhahisia, kama unabisha hebu dhibitisha uko upande gani.
Unawakati mgumu, mimi huota ndoto kama zako, namaanisha kujitambua kuwa sasa naota, baada ya hapo huwa naamua kufanya lolote iwe kupiga polisi au uchokozi wowote niutakao na nikizidiwa ktk mapambano hujiamulia tu kustuka na kuwaacha wabaya wangu huko huko tulipokuwa tunapambana.
 
Ndoto halisi haizidi dakika 1, tofauti na hapo ni maruerue. Kuota kunatumia nishati nyingi kutoka kwa ubongo. Ikizidi dk 1 mtu anaweza kufa.
Sidhani kama ni kweli, kuna kipindi nilikuwa na uwezo wa kuota ndoto mfano nipo na mtu au watu sehemu au kijiweni tunajadili jambo, kabla halijaisha nikabanwa na haja ndogo, basi mimi huwaaga watu hao kuwa naenda kukojoa, hapo hugutuka ndotoni na kujipata ninamkojo kweli, natoka kwenda kukojoa nje na kurejea kitandani na ndani ya muda kidogo tu hupitiwa na usingizi na kwenda kuendelea na kijiwe changu na mtu au watu walewale na stori ileile. Sasa ukiniambia ndoto ni chini ya dakika moja ilhali mkojo haumbani mtu ndani ya dakika 1 napata walakini.
 
mimi nahis ndoto ni mfululizo wa mawazo ya binadam baaada ya kua amelala na ndoto huendelea mpaka atakapo amka ila ndani ya ndoto binadam anaweza akaota vitu vingi ambavyo huungana kuijua ndoto imeisha ya mwanzo ni ngumu
 
Haya mambo ni yaajabu sana ndugu, Mimi huwa nikiota ndoto mbaya huwa najiuliza hivi hapa niko kwenye ndoto au ni kawaida, maana nikijiuliza tu hivo huwa nakurupuka na kujihakikishia kuwa ulikuwa ni uongo.

Sasa siku moja nikiwa nimeajiriwa kwenye duka fulani nikaota bosi wangu amenipa pikipiki nipeleke ela kwa mfanyabiashara mwenzake kiasi cha sh milioni 13, nikawasha boxer nikaondoka, nilipofika njiani nikamgonga mtoto akafa palepale, pikipiki ikasambaratika na nikijicheck mfukoni ile ela haipo.
Ile tabia yangu ya kujitingisha na kujiuliza kama naota niliijaribu tena lakini haikusaidia nikaona huu ni uhahisia na sio ndoto.

Nikajikatia tamaa kabisa nikaona habari yangu kwisha, nikajaribu tena kujiuliza naota au lah ndio nikakurupuka nikakuta ilikuwa ni ndoto tu.
Nikashukuru sana nikaendelea na maisha kama mwaka mmoja na nusu ambapo ndani ya hapo nilifanya mambo mengi ya maendeleo na mikasa midogomidogo, pia hata kukua niliona nimekuwa kidogo kimwili na kiakili. Lakini Kumbe ilikuwa ndoto ndani ya ndoto,

(Nikakurupuka tena nikayaendeleza maisha pale nilipoachia/pale kabla ile ndoto ya kupewa ela na pikipiki nipeleke kwa mfanyabiashara mwenzake na bosi wangu haijanitokea) nikaendelea na maisha hadi nilipoacha kazi na hadi leo naendelea na maisha.

Kwasasa sijui kama nipo ndotoni au lah. Hata wewe hapo unaesoma hii comment hujui upo ndotoni au ni uhahisia, kama unabisha hebu dhibitisha uko upande gani.
Hahahahahaa. Kaka umetisha. Hata mimi hapa sijijui kama nimefurah kiuhalisia au ni ndoto.
 
Inategemea ndoto yenyewe ina session ngapi!
Zingine huwa na sessions 5 mpaka 10 na zote zina part 1 mpaka 2
Hizo huchukua muda mrefu!
 
Dah kuna kitu kinanishangaza kwenye ndoto, yaana unaota ndoto juu ya ndoto, kwa hiyo una kazi ya kutafakari ndoto 2 kwa wakati mmoja

Tena mimi ndio huwa nina mtindo wa kuota ndoto juu ya ndoto. Yaan naota ndoto kisha namsimulia mtu kuwa nimeota hivi wakati niko ndani ya ndoto nyingine..
 
Sio kweli kwamba ndoto huchukuwa dakika moja tu , Ukweli nikwamba ndoto haina muda maalumu, nakumbuka kipindi nasoma ndoto za asubuhi zilikuwa ziki ni chelewesha shule..hai wezekani ndoto ya dakika moja ika nichelewesha kuamka, kwa vyovyote vile ndoto zikuwa ni ndefu.
 
Ndoto zingine ni balaaa.

Nakumbuka niliwahi kumtongoza mwanamke mmoja, kwenye ndoto bila ya mimi kujua ni ndoto kesho yake nika jipanga fresh kwaajili ya,kwenda kupiga Mbunye...Nili jifanyia maandalizi yote kwaajili ya kwenda ku sexsika ila wakati nataka kwenda, nyumbani kwa huyo demu nika kumbuka demu mwenyewe alikuwa amesafiri kwa muda kama wiki iliyo pita hapo ndipo akili zika nijia kwamba jana niliota.

Nilicheka paka basi.
 
Nakumbuka piya niliwahi kuota mama yangu, akinipa maagizo , kwamba,kesho usi ende shule kwani kesho nataka twende sokoni tuka uze ndizi.

Kweli kesho yake nika amka sikuji andalia chochote kwaajili yakwenda shule, mama tangu aka niuliza "kwanini huji andai kwenda shule ???.

Mimi nikaanza kushangaa na kumuuliza kwani jana tuli kubaliana nini ??.

Mama yangu akaniuliza jana saa ngapi na wapi ??.

Mimi nika mwambia jana hukuniambia nisiende shule leo ili nipeleke ndizi sokoni??.

Mama yangu akaniuliza "ivi wewe nilini uli changanyikiwa ?. Mimi naweza kukuambia usiende shule ??.

Hapo ndipo nikajua zilikuwa ni ndoto tu!
Nili mwambia huwenda niliota aka nicheka sana.
 
Haya mambo ni yaajabu sana ndugu, Mimi huwa nikiota ndoto mbaya huwa najiuliza hivi hapa niko kwenye ndoto au ni kawaida, maana nikijiuliza tu hivo huwa nakurupuka na kujihakikishia kuwa ulikuwa ni uongo.

Sasa siku moja nikiwa nimeajiriwa kwenye duka fulani nikaota bosi wangu amenipa pikipiki nipeleke ela kwa mfanyabiashara mwenzake kiasi cha sh milioni 13, nikawasha boxer nikaondoka, nilipofika njiani nikamgonga mtoto akafa palepale, pikipiki ikasambaratika na nikijicheck mfukoni ile ela haipo.
Ile tabia yangu ya kujitingisha na kujiuliza kama naota niliijaribu tena lakini haikusaidia nikaona huu ni uhahisia na sio ndoto.

Nikajikatia tamaa kabisa nikaona habari yangu kwisha, nikajaribu tena kujiuliza naota au lah ndio nikakurupuka nikakuta ilikuwa ni ndoto tu.
Nikashukuru sana nikaendelea na maisha kama mwaka mmoja na nusu ambapo ndani ya hapo nilifanya mambo mengi ya maendeleo na mikasa midogomidogo, pia hata kukua niliona nimekuwa kidogo kimwili na kiakili. Lakini Kumbe ilikuwa ndoto ndani ya ndoto,

(Nikakurupuka tena nikayaendeleza maisha pale nilipoachia/pale kabla ile ndoto ya kupewa ela na pikipiki nipeleke kwa mfanyabiashara mwenzake na bosi wangu haijanitokea) nikaendelea na maisha hadi nilipoacha kazi na hadi leo naendelea na maisha.

Kwasasa sijui kama nipo ndotoni au lah. Hata wewe hapo unaesoma hii comment hujui upo ndotoni au ni uhahisia, kama unabisha hebu dhibitisha uko upande gani.
Nimeisoma zaidi ya mara mbili hii comment...

Yaani nimefurahi, nimecheka nimeenjoy....

Ntasikitika sana kma ntakuwa naota

Haahahahahahahaha, umetisha sana mkuu
 
Ndoto zangu huwa zinaenda kama siries hivi sasa niko season ya 4 episode ya 21 wait ikufika mwisho nitatoa jibu ndoto ina chukua muda gani
 
Back
Top Bottom