Umenifungua ndugu, kweli ndoto zina maajabu yake! dk moja ya kidunia inaweza kuwa siku nzima ndotoni! means ulimwengu wa kifizikia tunaoishi una muda mwingi wa kufanya mambo mengi kama tunaweza elewa thamani ya muda
Haya mambo ni yaajabu sana ndugu, Mimi huwa nikiota ndoto mbaya huwa najiuliza hivi hapa niko kwenye ndoto au ni kawaida, maana nikijiuliza tu hivo huwa nakurupuka na kujihakikishia kuwa ulikuwa ni uongo.
Sasa siku moja nikiwa nimeajiriwa kwenye duka fulani nikaota bosi wangu amenipa pikipiki nipeleke ela kwa mfanyabiashara mwenzake kiasi cha sh milioni 13, nikawasha boxer nikaondoka, nilipofika njiani nikamgonga mtoto akafa palepale, pikipiki ikasambaratika na nikijicheck mfukoni ile ela haipo.
Ile tabia yangu ya kujitingisha na kujiuliza kama naota niliijaribu tena lakini haikusaidia nikaona huu ni uhahisia na sio ndoto.
Nikajikatia tamaa kabisa nikaona habari yangu kwisha, nikajaribu tena kujiuliza naota au lah ndio nikakurupuka nikakuta ilikuwa ni ndoto tu.
Nikashukuru sana nikaendelea na maisha kama mwaka mmoja na nusu ambapo ndani ya hapo nilifanya mambo mengi ya maendeleo na mikasa midogomidogo, pia hata kukua niliona nimekuwa kidogo kimwili na kiakili. Lakini Kumbe ilikuwa ndoto ndani ya ndoto,
(Nikakurupuka tena nikayaendeleza maisha pale nilipoachia/pale kabla ile ndoto ya kupewa ela na pikipiki nipeleke kwa mfanyabiashara mwenzake na bosi wangu haijanitokea) nikaendelea na maisha hadi nilipoacha kazi na hadi leo naendelea na maisha.
Kwasasa sijui kama nipo ndotoni au lah. Hata wewe hapo unaesoma hii comment hujui upo ndotoni au ni uhahisia, kama unabisha hebu dhibitisha uko upande gani.