Ndoto: JF get together

Ndoto: JF get together

Augustine Genius

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
1,216
Reaction score
1,486
Hello family,hope mko bye!

Moja kwa moja kwenye uzi,kwa kifupi sana ndoto yenyewe ni kwamba JF ina utaratibu wa get together party kwa kila mwisho wa mwaka (December) kwa members wote wa JF na ndoto hii ni kuhusu party ya mwaka huu Dec 2022.

Utaratibu wa hii party ni kwamba wahudhuriaji (JF Members) wanaendelea kuwa anonymously hata siku hiyo ya tukio yaani hakuna utaratibu wala ulazima wa kujitambulisha kuanzia kwa viongozi wa JF walioandaa hiyo party mpaka kwa JF Members ila ikitokea mkaonana watu mnaofahamiana au kama mtahitaji kufahamiana ni juu yenu.

Kama zilivyo shughuli zingine, vyakula na vinywaji vilikuwepo vya kutosha (waandaaji wa shughuli hawakukusanya michango kwa Members ila havikutolewa buree), pia burudani ilikua ya kubamba mixer singeli, reggae, hip hop, rnb n.k (hakukua na msanii/wasanii walioarikwa).

Kwa kifupi ndio ilikua hivyo sema wewe mdada uliyevaa suruali nyeusi ya jeans, tshirt nyeupe na visendo vya kimasai tafadhali uhusiano wetu usiishie kwenye ndoto😄 wewe mwamba wa kuitwa popoma (jina la kwenye ndoto) uliupiga mwingi sana ulivyokua unaushambulia ukoko wa pilau ukiwa na yule mdada mwenye manyonyo makubwa aliyevalia skirt fupi ya dark blue. 😅😅😅

NB: Kwa wale wataalamu wa kutafsiri ndoto naomba mnipe tafsiri yake lakini itapendeza kama hii party iandaliwe kwenye ulimwengu halisi.😊😊
 
Back
Top Bottom