Ndoto na Mafanikio

KAZMAR

New Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
4
Reaction score
1
UTANGULIZI

NDOTO NI NINI?

Ndoto ni taaswira, mawazo, tamaa au hisia ambazo zinapita katika akili yako. Mara nyingi Sana ndoto ni kitu unachoweza kukitengeneza katika taaswira yako kulingana na malengo yako ya baadae. Ndoto ni kitu unachokitamania kukitimiza siku moja katika maisha yako. Lakini pia kuna ndoto za usiku tunazoziota tukiwa tumelala. Hizi ni picha na mawazo yanayopita katika akili yako ukiwa umelala.

JE, NDOTO GANI INAWEZA KUTIMIA?

Ndoto zote ambazo ni taaswira na shauku ulizonazo ukiwa macho unawaza pamoja na picha na mawazo ya usiku au mchana ukiwa umelala zinaweza kutimia. (Ni kuamua tu). Ndoto ni uhalisia wa kesho. Ndoto hutimia kwa wale wanaoamka baada ya kuota. Kama unaweza kutoa, basi unaweza kufanya, kama unaweza kufanya basi unaweza kuwa, ukomo wako ni wewe mwenyewe tu utakavoamua. Ndoto hutimia kama tutakua na matarajio makubwa zaidi. Unaweza kupata kila kitu katika maisha kama utajitolea kuachana na vitu vingine vyote kwa ajili ya kitu ukitakacho.

NDOTO NDANI YA NDOTO
Unaweza ukaota ndoto ukiwa ndani ya ndoto, ni kama vile unavoangalia runinga na ukaona watu ndani ya runinga yako nao wanaangalia runinga, lakini watachokua wanakiangalia wao kitakua ndani ya runinga yako. Kwahio unakua na mawazo mawili kwa wakati mmoja. wazo la kwanza utakua unawaangalia jinsi walivyo keti na kuangalia runinga na wazo la pili ni kuangalia wanachokiangalia wao. Hivyo doto hufika katika uhalisia kwa vitendo. Kutokana na vitendo hivyo hutokea ndoto nyengine, na hatua hizi hutoa mfumo mkubwa wa kuishi katika ndoto na uhalisia. WAOOH! 😊Kumbe unaweza kulitumia wazo la mtu mwengine kuota ndoto yako kulingana na shauku yako na ukapata mafanikio.

VIPI TUNAWEZA KUFANIKIWA?

Ili kukamilisha vitu vikubwa, Hatutakiwi tu kuingiza, bali tunatakiwa kuwa na ndoto, na wala sio tu kuwa na mipango, bali kuwa na imani pia. Usiufanye uwoga wako kuwa ndio mpaka wa kutimiza ndoto zako
Tofauti ya ndoto na mafanikio ni bidii ya kufanya kazi. Usishauriane na uwoga wako, bali shauriana na matumaini na ndoto zako. Wala usifikirie kuhusu kuhangaika kwako bali fikiria ambayo bado hujayakamilisha na unapaswa kuyatimiza. Katika maisha watu waliofanikiwa niwale ambao walisubutu kuzifuata ndoto zao wakati wa shida na raha bila kuwa na visingizio. Mafanikio hayaji tu kwa kukaa na kusubiri fursa zikukute ulipo. Unapaswa kuamka na kufanya kazi ili kujitengenezea fursa wewe mwenyewe na ndoto zako zitatimia.

UWEZO WAKO UTAKUA KULINGANA NA NDOTO ZAKO

Kila binaadam ana nguvu ya kufanya mawazo yake kuwa kitu halisia, kila mtu anaweza kuwa na ndoto na kila mmoja anaweza kutimiza ndoto zake. Ni kuamua tu? Tunatakiwa kutambua kwamba hata ukiwa umelala na unaota ukiwa ucngizini ndoto ndo itakayokuamsha nawala siokuamka kutoka ndotoni. Sasa maamuzi ni yakwako kufukuzia hiyo ndoto ili iwe uhalisia au kuendelea kulala na ndoto yako. Kwakuongezea, naamini kabisa hata hizi ndoto zote tuotazo usiku au mchana tukiwa tumelala tunaweza kuzitimiz. (Ukiota unakimbizwa na mbwa ukitaka ukimbizwe kweli utakimbizwa, ukiota unanyongwa na ukitaka ndoto yako itimie utanyongwa tu, na hata ukiota unaendesha gari lako ambalo huna kwa sasa ukitaka ndoto hiyo itimie utalimiliki ni wewe tu kuamua)

KIPIMO CHA MAFANIKIO
Kipimo Cha mafanikio ni kufikia malengo yako, kutimiza ndoto zako na kupata ulichokitarajia. Lakini mafanikio hayo hufikiwa kwa kufanya kazi kwa bidii, kuwa na muendelezo na kuamua! Kama unataka kuwa na mafanikio katika maisha, hiyo ni juu yako wewe mwenyewe ni wajibu wako. Mafanikio sio kuwa na pesa tu, mafanikio ni kuwa na rasilimali na uwezo wa kuishi maisha ya ndoto zako.

Huwez ukaota ndoto kubwa Saaana, lakini unaweza ukafikiria kidogo sana. Kama unaweza kuwa na ndoto lakini ukaifikiria vibaya, kinachofata ukweli hautajificha. Wakati mwengine washindi ni wanandoto ambao hawakukata tamaa. Mafanikio huja pale unapokuwa na ndoto kubwa kuliko uwoga wako.

Chukua wazo moja na ulitendee kazi, Lifanye kuwa ndio wazo la maisha Yako, lifikirie hilo, lala ukiliota hilo na ishi nalo hilo, Ruhusu ubongo, misuli, damu na kila kiungo Cha mwili wako kuwa ndani ya wazo hilo moja na achana na mawazo mengine. Hii ndio njia ya mafanikio. Fanya vitu vya ajabu sio tu kukaa na ndoto, Ushindi katika mafanikio nusu yake ni pale mtu anapokua na tabia ya kupanga malengo na kuyafanikisha.

Miaka ishirini ijayo utakua umekata tamaa Zaidi kwa vitu ambavyo hukuvifanya na kwa vitu ulivyovifanya. Kwahio jitoe kwenye njia iliopinda ambayo huoni mbele yako kunanini na uanze safari mpya kutoka kwenye bandari salama. Fuata upepo wa biashara unakoelekea. Chunguza, otea na gundua.Kupitia ndoto zetu na matarajio tunaweza kuona fursa.

HITIMISHO
Kila kitu katika hii dunia ni ndoto. Vyote tunavyoviona na kuvitumia ni ndoto za watu ambazo zimetimia. Hata wewe unaesoma hii kurasa jua unasoma ndondo ya mtu kwenye ndoto za watu. Kifaa unachokitumia kusoma ni ndoto ya mtu iliotimia, kitu ulicho kalia ni ndoto ya mtu, nguo ulizovaa ni ndoto za watu, usafiri unaotumia ni ndoto za ya mtu, Kiujumla unatakiwa ujistukie unaishi kwenye ndoto za watu tu je lini nawewe utaishi kwenye ndoto yako? Ifanye ndoto yako ionekane katika maisha halisia ili watu wengine waishi kwayo!

Kila kinachotokea kilianza na ndoto. Unaona tu vitu vipya kila siku unashangaa na kujiuliza (kwanini imekuwa hivi?) Fikiria ndoto yako na ujiulize (kwanini isiwe hivi?) Kisha fanya jambo ili iwe kweli na ushangaze wengine
 
Kuna masai alikuwa ana ndoto ya kuowa mtoto wa Obama sijui yupo wapi yule pimbi [emoji28]hata passport hana
 
Kuna masai alikuwa ana ndoto ya kuowa mtoto wa Obama sijui yupo wapi yule pimbi [emoji28]hata passport hana
Kama angeondoa hofu na kuwa na Imani na kufanya kazi katika wazo hilo angemuowa na Dunia ingeshangaa maana ndoto kubwa ndizo zinazoleta maajabu zikitimia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…