Ndoto niliyooya

Ndoto niliyooya

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Leo jumapili tarehe 10/10/2021, nikiri kwamba sijaenda kanisani. Hii sio kawaida yangu. Niliamua tu kushika laptop yangu na kuanza kuangalia mambo ya kazini kwangu. ghafla, usingizi ulinipitia, nikaota kama kuonyeshwa hivi ndoto ambayo imeshakuja kwangu mara ya tatu sasa na inakuwa na mvuto na uhamasisho wa nguvu sana ambao haupotei moyoni kwa muda mrefuuu hadi hapa ninavyoandika, it becmes so touching as if sauti kabisa inaongea ndani yangu ikijirudiarudia.

kilichonifanya niandike hapa, ni mara yangu ya tatu sasa ndani ya miezi hii miwili naota ndoto kwamba siku ya mwisho wa dunia imekaribia mno, wanadamu tuwe tayari. na inaambatana na uthibitisho na msukumo wa uhakika mno wenye uwepo wa Mungu ukinithibitishia hilo. Thibitisho hilo kwa mara zote 3 za ndoto nilizoota (siku tatu tofautitofauti na sio mfululizo ila ndani ya miezi hii miwili) linaongea na mimi moja kwa moja kwamba dunia imeisha na Yesu Kristo yu karibu kulichukua kanisa lake, hivyo nitengeneze maisha yangu. kama leo ndio kama nimeonyeshwa naman dunia ilivyopatwa na giza nene watu wanatapatapa na kuhangaika, hadi mimi nilikuwa nimesahau sehemu niliyopaki gari baada ya giza hilo kutukuta tukiwa kazini, nikachanganyikiwa na kuanza kuomba lift kwa wenzangu wanikimbize barabarani nikachukue bus, hawakunipa lift kwani kila mtu alikuwa anahangaika kukimbia atakavyoweza, nikatembea kitambo fulani nimeshika ufunguo mara nikakumbuka kumbe gari nilikuw analo na nililipaki nje ya jengo, nikarudi kulitafuta niondoke kwa haraka nikaangalie familia yangu, ila nje kuna upepo sio upepo, sunami sio sunami tena iliyambatana na giza la kutisha mfano kama vile ya kupatwa kwa jua inavyokuaga...nashindwa hata nielezeje.

Nikiri wazi, pamojana kuota hayo yote, nimekuwa nikijichanganya mara kwa mara ndani ya miezi hii miwili kwenye maisha ya kimungu na maisha ya kidunia. nilikuwa mchafu na mdhambi. ndio napata amani sasahivi ninavyoandika baada ya kupiga magoti na kumlilia Mungu anisamehe, nimetubu na nimepata amani ya moyo namshukuru Mungu kwa hilo, najua sasa kwa sasa mimi nimesharudi kundini mwa watoto wa Mungu kama alivyokuwa ananitaka. nilijichanganya sana kwa uchafu wa dunia hii, uzinzi, pornal ambazo huanzia kwenye picha chafu zinazotumwa na watu whatsapp, fg na twitter (hizo connections etc ambazo mwisho wa siku zinakupeleka kiu ya kuingia kwenye mitandao yenyewe ya pornal), na kila baada ya kuangalia picha hizo kilifuatia kufanya mapenzi sanaaa, kama nipo home ninafanya na mke wangu, kama niko mbali na home nitapiga punyeto na kinachofuatia hata baada ya punyeto ni kutafuta mwanamke yeyote hata malaya au wale ninaojuana nao kawaida kama wafanyakazi wenzangu etc nawatongoza na kulala nao. maisha haya niliyaishi sana miaka ya nyuma hadi huwa siamini kwanini sikupata ngoma, ni neema ya Mungu tu. ilifika kipindi nikaacha na kusogea kwa Mungu lakini kwa miezi hii miwili nilimuudhi tena Mungu. nimekuja kujikuta moyo wangu unanuka harufu ya uchafu wa dhambi, hakuna amani ya Mungu wala uongozi wake, lakini baada ya kutubu hakika najisikia amani na furaha ya tofauti kabisa na ninamwomba Mungu anisaidie nisimtende dhambi tena. why nimejianika hivi mbele zenu tena bila aibu?

1. madhara ya picha chafu kwenye mitandao ya kijamii ambayo lazima itakupelekea kwenye mitandao halisi ya porn. hii nidhambi kwa anayesambaza, na anayeangalia na ni mtego wa shetani kutuchafua ili tutoke kwenye uwepo wa Mungu na yeye atupoteze.

2. upendo wa Mungu. Mungu amenipenda sana, sikustahili kwa mengi niliyomfanyia kwamba angenisamehe, nilistahili adhabu tu. lakini kwa kifo cha Yesu Kristo Msalabani Mungu anasamehe kabisa na kusahau. ikumbukwe kwamba katika agano hili, huwezi kusogea mbele za Mungu na kuongea chochote na kukubalika bila kupitia kwa Yesu Kristo. Yesu Kristo ndiye njia kweli na uzima na Mungu anatusamehe kwasababu ya kafara ya Yesu Kristo. zamani wenzetu walikuwa wanachinja makafara ya damu za wanyama, lakini Yesu Kristo alimwaga damu yake iwe kafara na agano la msamaha wa dhambi na wokovu kwetu once and for all, anatuombea kwa Baba na hata pale tunapofanya dhambi anatusamehe kama tukitubu kwa kumaanisha kuacha. tukisema hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu, ila tukiziungama, Mungu ni wa haki atatusamehe. but lasima uungame kwa kupitia Jina la Yesu. Hakuna jina lingine tulilopewa sisi wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo ila Jina la Yesu.

3. Wito wa watu kuacha dhambi na kuokoka. Natumia nafasi hii, kuwaasa wote tunaosambaza uchafu mitandaoni, kufanya dhambi za aina mbalimbali n.k, hii ndoto nimeota ilikua very real kwamba dunia hii tunayohangaika nayo ipo ukingoni, kuna watu wataachwa ukifanya mchezo.upande wangu nimechukua hatua, nikaona bora nisambaze na wengine wanaotaka wachukue hatua. dunia imekwisha hii. shuguli za dunia tunazifanya hata mimi nafanya kutafuta hela kujenga majumba na kutumikia familia lakini kuna siku yote haya yatapita, sote tutawekwa mbele za Mungu kuwa accountable kwa maisha tuliyoishi hapa duniani.

4. sijatumwa na Mungu kwa sauti yake kabisa niyaseme haya kwenu, ila nahisi nisiposema damu yenu itakuja kudaiwa kwa kutokuwaonya jambo ambalo nimehakikishiwa kabisa. Tubuni mkaache dhambi, Mungu atawapokea nanyi mtapata uzima wa milele. Mungu awabariki.
 
Nonsense
 
Hapo utakuwa uliacha kwenda ibada ukujifungia ku view porn ndipo ukakutana na Roho wa Mungu.

Hongera mkuu kwa kufunuliwa hilo maana imendikwa "Wale Baba alionipa, hawatapotea kamwe"
 
Back
Top Bottom