NDOTO: Rais Magufuli kutawala awamu moja tu...

NDOTO: Rais Magufuli kutawala awamu moja tu...

Mkuu @TangataUnyakeWasu, hiyo ndoto yako ni ndoto ya ajabu sana, ambayo inakupa hadi the reasons behind!.

Kwa kawaida ndoto huwa unaoteshwa kitu lakini bila majibu, halafu majibu yatakuja kupatikana kwenye tafsiri ya ndoto hiyo.

Nilitegemea ungesema hii ni mara ya tatu unaoteshwa kuwa rais Magufuli ni one term president.

Ndoto za aina hii nyingine huwa ni sauti ya Mungu au maono. Mungu akikuotesha jambo, hakupi majibu bali utaona tuu matokeo, sasa wewe na hii ndoto yako imekuambia Magufuli atapigwa chini na mchakato wa ndani wa CCM? . Kwani CCM huwa inamchakato wa ndani kabla ya miaka 10?. Kwa kukusaidia tuu wewe na hiyo ndoto yako ya uongo, CCM haina mchakato wa ndani wa urais kwa mwaka 2020 bali aliyepo huendelea, hakuna hata utoaji wa fomu! .

Kama ungesema Mungu amekuotesha bila kukupa sababu, hiyo ndio ingeweza kuwa ni ndoto ya kweli ya maono kama ile ndoto ya Lema.

Paskali
Pascal Mayalla
 
Magufuli ataendelea kuwa rais kwa miaka 10. Tena binafsi natamani hata awe rais kwa miaka 20 au zaidi maana Tanzania tulihitaji rais kwa ma huyu tokea miaka mingi ilopita. Kwa nyie wazembe msiotaka kula kwa jasho ndo mnamchukia. Ila sisi ambao tulitamani atawle hata kabla hajachukua form ya kugombea ndo tunampenda na tunamwombea asubuhi na usiku.
🤣tatizo lila jambo mnatanguliza ushabiki na uchawa
 
Wana Jf wenzangu......!!

Leo ni mara ya 3 nikitokewa na ndoto kuwa Rais wa JPM atakuwa kiongozi pekee atakayeliongoza Taifa kwa kipindi cha Miaka 5 tu na sababu pekee ni kwamba atapigwa chini katika mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama chake.

Hii ni kutokana na makundi mengi ambayo yameanza kujipanga kwa kutumia mbinu mbalimbali ndani ya chama kwani wengi wao awapendezwi na aina ya utawala anaoendelea nao kwa sasa ndani ya chama na Taifa.

Ni hayo tu nimeona niwashirikishe....!!
Nakuamuru utuambie alipo Magu...
 
Back
Top Bottom