Ndoto ukisafari/ kuendesha chombo cha usafiri na tafsiri yake

Ndoto ukisafari/ kuendesha chombo cha usafiri na tafsiri yake

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Ndoto ni dirisha ambalo unaweza kuchungulia na kuona nini kinachokuja mbele yako, au ni jambo gani ambalo limekuzunguka lakini hujatambua au hulioni katika fikra na macho yako.

Sasa ni Mungu huleta picha/ video kukuonesha ukiwa wewe ni mmoja wa wahusika wa matukio.

Unahitaji kujua nini unapewa tahadhari kuhusu au unaoneshwa nini ili uweze kujua unahitaji malekebisho ya jambo gani la kimaisha.

Maisha ya binadamu yanafanananishwa na Safari, ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Inaweza kuwa safari ya miguu, baskeli, pikipiki, basi, meli, ndege, na n.k Lengo inatakiwa Kufika salama na kujua wapi unakwenda.

Kwahiyo sitofahamu yoyote Katika safari unayoiona ndoto ni sitofahamu ambayo utakutananayo mwilini kwenye maisha yako.

Ndoto yako ya Kusafiri inaonesha nini?

mfano: Unaota ndoto ukiendesha Gari au Bus na kwenye bus kapanda rafiki au mzazi wako au mwenza wako,
Ikitokea yupo aliyekupinga kuwa hujui njia au huwezi kuendesha gari
Basi Tafsiri yake inakuwa mtu huyo ambae ni mmoja kati ya mtu wa karibu kwako, atakuja kuwa kikwazo katika safari yenu ya Maisha, na wewe ndio umepewa jukumu la kuwa kiongozi kwani ndiwe ulikuwa dereva wa gari.

Ukiota ndoto umepotea njia.
- Tafsiri yake ni kwamba utapoteza muelekeo wa maisha.

Ndoto umeachwa na gari, kwa sababu fulani.
- Unasemeshwa kuna mambo unayafanya yasio ya msingi, yanakuchelewesha katika hatima yako kubwa

Adui barabarani
- Tafsiri yake hapo jiongeze...

Unaota ndoto ukiendesha gari au pikipk kwa kasi sana na hukua makini barabarani au kupoteza njia na kupata ajari
- Tafsiri yake ni kwamba utapitia nyakazi za kujisahau na kuacha kuwa makini na mambo unayoyafanya, umekua na tabia ya kutake risk zisizo za msingi, ukipata na ajari na kuumia viabaya basi kuna anguko la kimaisha linakuja.

Unatembea ukakutqna na mto au maji mengi na ukakosa njia.
- Tafsiri yake ni kwamba kuna upinzani wa nguvu za giza kukuzuhia safari yako

Ndoto yako ya Safari imebeba Muonekano gani?
 
Mkuu kuwa tu makini ikifika wakati wa kuchimba dawa ndotoni usije jinyea kitandani🤒🤒🤒
 
Niliwahi kuota ndoto nimepanda gari inayoendeshwa na rafiki yangu, haikua na abiria wengine.. Baadae akaja kupanda na kaka yangu kwenye gari hiyo.

Ni ya muda mrefu kidogo, almost 6 months now. Sasa sijajua ndoto inajaribu kutuelezea jambo kwa wakati huo au even after years.
 
Tafsiri ya ndoto kuota umefanya tabia mbaya na mwenza wa jirani yako / mfanyakazi mwenzio ipoje?
Sex - or to become intimacy au kuwa connected /muunganiko.

Sex tafsiri yake ni nzuri kama unafanya muunganiko au urafik na mtu mzuri ila kama ni jini au roho fulani linafanya na wewe kwa lazima, basi imekula kwako. 😂

Angalia nani alionyesha kumtamani zaidi mwenzie, kama ni huyo mfanyakazi mwenzio basi jua kweli anatamani ukaribu zaidi na wewe
 
Naota ndoto za maji sana,

Naota naogelea

Naota mafuliko maji yamejaa kila sehemu mimi nakuwa na kimtumbwi tu

Naota nipo ufukweni naangalia maji yametuliaaa au nipo ufukweni naangalia mawimbi makubwa ya bahari
 
Naota ndoto za maji sana,

Naota naogelea

Naota mafuliko maji yamejaa kila sehemu mimi nakuwa na kimtumbwi tu

Naota nipo ufukweni naangalia maji yametuliaaa au nipo ufukweni naangalia mawimbi makubwa ya bahari
Unajitahidi kushinda vikwazo na upinzani mwingi wa nguvu za giza
 
Naota ndoto za maji sana,

Naota naogelea

Naota mafuliko maji yamejaa kila sehemu mimi nakuwa na kimtumbwi tu

Naota nipo ufukweni naangalia maji yametuliaaa au nipo ufukweni naangalia mawimbi makubwa ya bahari
Mara nyingi ndoto za maji tunaambiwa zinahusu masuala ya emotions, ila kwa kiasi kikubwa hizi symbols kwenye ndoto zetu tafsiri zake inakuwa inategemea na mtu mwenyewe binafsi ndio mana watu wanaweza kuota ndoto zenye kufanana ila tafsiri zinatofautiana kabisa.
 
Niliwahi kuota ndoto nimepanda gari inayoendeshwa na rafiki yangu, haikua na abiria wengine.. Baadae akaja kupanda na kaka yangu kwenye gari hiyo.

Ni ya muda mrefu kidogo, almost 6 months now. Sasa sijajua ndoto inajaribu kutuelezea jambo kwa wakati huo au even after years.
Cheki safari ilikuaje, huyo rafik alikua dereva mzuri ? kama sio basi unaelewa kuwa unapewa tahadhari juu ya yale unayoyasikiliza na kufanyia kwazi kutoka kwa huyo rafiki yako. Na kaka yako nae atapendezwa na kanuni zenu za kimaisha kwa kujiunga gari moja na nyie
 
Back
Top Bottom