Ndoto ya 500/50 ilivyobadilisha muelekeo wangu

zee_latown

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2026
Posts
677
Reaction score
1,234
wanajamvi wote habarini,heri ya sikukuu ya eid.
mimi si muandishi mzuri sana, nimekuwepo jamii forums muda kidogo, ila kulikuwa na kitu moyoni mwangu nikitaka ku share pamoja

ndoto zipo za aina mbalimbali. unaweza kuota unafukuzwa na wanyama wakali, unakula, unahesabu pesa, nk
nataka niseme jambo oja hapa, dreams are mosty real.

siku moja nikiwa high school somewhere in Ilboru Arusha, niliota ndoto. Niliota naokota noti ya sh 500 iliyoandikwa "500/50>50000". niliona ni normal coz sikuwa sana mtu wa kutilia maanani masuala ya ndoto..

nilipomaliza high school, siku moja nikiwa chuoni nje ya nchi, miaka mitano baada ya kuota ndoto ile, niliiota tena. vile vile ila this time noti ilikuwa ni ya dolla 100, huenda ni kwa sababu nilikuwa nipo kwenye nchi inayotumia dola.
at that time nilikuwa mwaka wa pili, na of course nilikuwa sijui after there nitafanya kazi gani, ukizingatia hela ya kufika hapo chuoni ni ndugu zangu walijichanga changa tu.

so, nikaiona ile dola mia, then na maandishi yameandikwa "500/50>50000"
yaani miatano uigawe kwa kumi kisha jawabu liwe ni zaidi ya elfu hamsini? haikuingia akilini.

nilianza kushangaa kidogo, kwa nini inajirudia mara mbili ile ndoto...
kwa taratibu za havard ilikuwa lazima u complete 128 credits kwa semester nane.
so, nilikuwa na wakati mgumu ku-manage stress na masomo, kwa sababu kumbuka nasoma kwa pesa za michango ya ndugu, na nawaza nikifeli nitauficha wapi uso wangu.

nilimaliza salama, na kumbuka, around 2011, kwa kutumia ujanja ujanja tu nilikuwa nimenunua bitcoins 10. ilikuwa ni muda mrefu mpaka nikasahau, miaka kadhaa mbele bitcoin ilifika juu ya 50k usd. bado nilikuwa na bitcoin zangu kumi.

Mpaka muda huu, sijauza hata btc moja, ninazo zote kumi. jana usiku wakati natafakari, nikaelewa maana ya zile ndoto mbili nilizoota katika mazingira mawili tofauti. kumbe 500/50 ni btc 10 nilizonazo, na ile >50000 ni bei ya btc wakati huo.

sijisifu na sina majisifu, ila naweza kusema siamini kama nina 10btc yaani $500k.
siyo pesa nyingi sana ila imenifunza jambo.

ndoto tusizidharau, Mungu ana njia nyingi za kumpa mtu, kutoka kusoma kwa pesa za kusaidiwa na ndugu mpaka kupata mtaji wa $500K. ni jambo la kumshukuru muumba.

niliona niandike ili ni share nanyi huenda kuna watu wakawa wanaota ndoto wasizozielewa halafu wakawa wanazizadharau. tujifunze kutochukulia mambo kwa wepesi.

kwa sasa bado nadunduliza ili kufikia malengo yangu zaidi.
ni hayo.
ahsanteni
 
Mkuu ulisoma shule gani bongo ukapata Admission Harvard? na ulikuwa campus gani ya Harvard?
 
Back
Top Bottom