Ndoto ya kurudi tena masomoni, huwa inamaanisha nini?

Spiritual world controls the physical world
 
Hata mimi iliwahi nitokea ndoto kama hiyo, eti niko napambana kumaliza pepa na dakika zinakaribia kuisha, halafu maswali ndio kwanza nimejibu mawili kati ya 50, hafu wenzangu washamaliza wanakusanya, yaani huwa inatesa ndoto ya namna hiyo, acheni tu.
 
Nimekua na teswa mara kwa mara na ndoto kama yako mkuu.. Na mara nyingine nipo kabisa kwenye chumba cha mtian ila sijasoma chochote.. Mwenye ujuzi wa maswala ya ndoto atusaidie
Hyo ndoto ata mim niliota hvyo ila nilikuja kuambiwa na nabii flni kuwaa kuna maswala yangu hayako poa kuna watu wanakurudisha nyuma awataki wew uende mbelee kemee sanaaa
 
Kama umeota uko shule ya msingi Jaribu kukumbuka ni somo gani Au mtihani gani Au ni suala Au mazingira gani Au watu gani ulikua nao kwenye ndoto . LAZIMA ktk hiyo ndoto kimoja wapo kitakuwepo. Hayo mazingira ndio yanajawabu kwa kile unachokipitia sasa ktk maisha Iwe ndoa, biashara Au kazi etc. MAANA YAKE KUNA MATATIZO YA FIKRA AU MTIZAMO AU UMEKOSA MSINGI MZURI WA KUFANYA HILO JAMBO.
 
Hii ndoto wengi inatusumbua, wakati mwingine napata hofu kwamba nasubiri mtihani, kumbe nishamaliza
 
Mimi niliishia form four sikuwah kusoma A level ila naota Mara Kwa mara nipo darasani ila form five au nipo kwenye chumba cha mtihani wa kumaliza kidato cha sita na katika shule ile ile niliyokuwa nasoma.
 
Mimi niliishia form four sikuwah kusoma A level ila naota Mara Kwa mara nipo darasani ila form five au nipo kwenye chumba cha mtihani wa kumaliza kidato cha sita na katika shule ile ile niliyokuwa nasoma.
Nyota yako imeibwa inatumika mahala angalia maisha yako hayaeleweki
 
Ubarikiwe kwa andiko zuri
 

Kuota unafanya Mtihani.

Hii ni moja ya ndoto ambayo inaotwa na watu wengi sana, na hii huwa inachukua maumbile tofauti tofauti, wengine utakuta wanaota wanafanya mitihani na hawajajiandaa, wanachoshtukia tu ni wakati wa mtihani umefika, hakuna chochote walichofanya wanajiuliza siku zote alikuwa wapi…wengine wanaota wanafanya mtihani mgumu sana lakini wenzake wanaonekana wanafahamu cha kujaza yeye hajui, wengine wanaota kama walikatisha masomo wakaondoka, baadaye aliporudi muda umeshapita mitihani ya mwisho imekaribia, wengine wanaota wamerudi madarasa ya nyuma ambayo tayari wameshayavuka siku nyingi na ni lazima wayavuke ili waendelee na madarasa ya mbele, wengine wanaota wapo wanafundishwa, wengine wanapewa adhabu n.k.…


Na ndoto hizi huwa zinatesa sana, zinaweza kujirudia hata kila baada ya wiki au mwezi, au miezi kadhaa, inategemea na mtu na mtu, lakini ni ndoto ambazo haziachi kuja.


Biblia inasema..Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”

Mungu sikuzote huwa anapenda kutumia vitu vinavyotuzunguka kutufukishia sisi ujumbe fulani au kutufundisha, na ndio maana utaona Bwana Yesu alipokuwa anafundisha mifano yake yote alikuwa anatumia mambo ya kawaida tu yanatozunguka sikuzote ili kutufikishia sisi ujumbe na tuulewe utaona wakati mwingine alitumia mifano ya ndege, wanafanyabiashara, wafalme, harusi n.k…Hivyo na Mungu ili kukufikisha ujumbe wako wa wokovu huwa anapenda kutumia mfano wa kitu ambacho kimetukuka sana mbele yako, kitu chenye maana sana kwako ambacho ukikisoma anajua kabisa umekosa maisha na hicho si kingine zaidi ya ELIMU.


Kufunua kuwa Ipo elimu iliyokuu ambayo inafungua ufunguo sio tu wa maisha ya hapa bali pia wa maisha ya ulimwengu unaokuja, na hiyo si nyingine zaidi ya Elimu ya Ufalme wa Mbinguni..Mungu anakuonyesha hali yako ya kiroho ilivyo kupitia maisha yako ya shuleni, kama unavyojiona upo shuleni hujajiandaa, au mtihani ni mgumu basi katika roho ndivyo hivyo ulivyo.. kuwa upo nyuma, na unapaswa ushinde, yapo madarasa haujayavuka bado, upo pale pale kiroho umekwama, unatamani uendelee mbele unashindwa au unaona ni ngumu kwasababu bado hujayamaliza madarasa ya nyuma Mungu aliyokupa.


Hivyo unapaswa uongeze bidii yako kwa Mungu, ili ufike pale Mungu anapotaka kufika, ongeza kiwango chako cha maombi, jifunze Neno la Mungu sana, ishi maisha yanayompendeza Mungu, punguza muda wa kuihangaikia dunia, na ongeza muda wako wa kumtafuta Mungu, kwasababu yeye ndio ufunguo wa kweli wa maisha yako ndugu. Ukimpata Mungu umepata vyote.


Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

Hivyo ukiwa na bidii na Mungu akaridhika na wewe basi atakuvusha na kukupeleka katika kiwango kingine cha kiroho na kiufahamu. Kumbuka Mungu anakupenda na ndio maana anakuonyesha ndoto kama hizo, Hivyo usipuuzie ungeza bidii yako kwake.


Ubarikiwe.

 
Inamaanisha ulipo sio pazuri kimaisha. Yaani ni kama bado upo kipindi unasoma
Bado hujafikia ulivyotakuwa kuwa kwenye level inayotakiwa kuwa. Pambana bado haujachelewa kuwa katika level unayotakiwa kuwepo.
 
Inamaanisha ulipo sio pazuri kimaisha. Yaani ni kama bado upo kipindi unasoma
Bado hujafikia ulivyotakuwa kuwa kwenye level inayotakiwa kuwa. Pambana bado haujachelewa kuwa katika level unayotakiwa kuwepo.
hivi huwa mnajuaje hizi tafsiri
 
Unafanya kazi kwa juhudi zaidi kuliko maarifa....jitahidi kusoma kuongeza weredi katika kazi zako ili upate mafanikio.
 
Mm nshawai sikia huwa ina maana kua Kuna mahali uliachwa na wenzio wa Rika lako hasa maendeleo yaan Kuna sehem ulkwama inatakiw ufanyie kaz
 
Wenzio tuna miaka 40 na usheee na bado tunaota tunaenda darasani bila viatu, tunaenda choo kimejaa vinyesi, tunaota hakuna wa kutuonglesha. Hii inanitokea kila mara mpaka nimezoea. Si shwari inauma ila nimempata mwenzangu anayeteseka kama mimi. nilimaliza 0 level 1976 lakini mpaka leo naandamwa. Kuna somo nilidhani nilipta sana nikalifail lakini kwenye ndoto naonyeshwa mwalimu wangu alivyolibadili kumpa mtu. Nina maisha mazuri sana ila siwezi sahau na ndoto huwa inanirudia kunionesha kilichotokea.
 
acha ushirikina mkuu ,ndoto ni mindset tu wengi humu kipindi kirefu cha maisha yetu tangu utotoni tumetumia shuleni hivyo hizo moments mara nyingi hujirudia hasa kile kipindi cha mateso cha mitihani .walokole na waganga wanadanganya sana watu ili wapige pesa
 
Umetekwa kwa namna fulani fanya haraka sana kutoka hapo, watu wanafaidika na wewe, msukule sio lazima atoweke wengi wanaishi na ni watu wa kawaida sana ila hawajui kinachoendelea nyuma ya pazia, wahi ndugu!
sijui imani za kujinga kama hizi zitaishi lini kwenye jamii zetu
 
ndoto ni memory tu kwenye ubongo hakuna lolote,wengi wanaoota hivyo ni wale ambao muda wao mwingi waliutumia shuleni na moments za mitihani na masomo zilikua zinaumiza sana akili ,hiyo memory sio rahisi kutoka akili ni sawa na kumuota mtu aliyefariki kitambo na ulikua unampenda kumuona amerudi upo nae.walokole na waganga hutumia hii fursa kudanganya watu ila kiukweli hakuna lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…