SirLuke
Member
- Dec 1, 2014
- 75
- 8
Story of change.
Hadithi yangu inaanzia asubuhi ya Mei 9, 2017 baada ya kupokea simu. Haikuwa ni namba ngeni kwenye simu yangu, alikuwa ni mtu mwenye nilikuwa nikimfahamu na ni mtu wa karibu sana. Baada ya kupokea simu, ndipo upande wa pili akaanza kuongea maneno mazito na yenye uchungu ndani yake.
“Habari Engneer Kabuki! Bila shaka uko sawa. Aisee nimekuwa nikikushirikisha juu ya kijana wangu jinsi gani anashindwa kunisikiliza. Hii inamaanisha kuwa ameshindwa na hataki kujifunza kila ninachomfunza. Yeye kila siku habari zake ni mpira mpira tu hakuna lingine.
Hakika inachosha, maana kama ni mpira sioni akisonga, hebu niambie Luke una mawazo gani kuhusu hili Engneer wangu maana sielewi?”
Lakini kaka usijali kuhusu hilo, tafadhali nipatie hiyo kijana wako kesho ofisini kwetu mimi nina hakika nitamfunza na ataelewa na ikiwezekan atapata ajira hapa ofisini kwetu ninapofanyia kazi. Hakika wewe ni mwalimu bora, kama ulinifunza mimi nikaelewa hakika mimi pia nitamfunza kijana wako ataelewa.”
Sawa Engneer Kabuki, nakuaminia kijana wangu. Ndio maana nimekuwa nikikushirikisha katika. Haijalishi umri wako ni mdogo kiasi gani, ila naamini katika ubongo wako.”
Basi maongezi yetu yalikuwa hivyo, na kweli kesho yake kijana wake (Mpwa wake) akamleta ofisini kwetu.
Kazi ya kuanza kumfundisha ndio ikaanza, hii ni hadithi ya kweli ambayo hakika niliipitia.
Sasa hapa shida ya huyu kijana haikuwa katika uelewa, kwa haelewi kile anacho fundishwa, lah! Tatizo lake ilikuwa ni yeye ana ndoto ya kucheza mpira tu. Alikuwa akiona kuwa mpira pekee ndio utakuja kumtoa katika maisha yake. Na wakati huo mjomba wake amekwisha angalia akaona kuwa ndoto yake inaweza isitimie hivyo akaona ni vyema amfunze kile kuchapa fulana n.k kwa maana ndio kazi ambayo alikuwa akiifanya na mimi pia amenifunza hiyohiyo.
Lakini huyu kijana hakuwa akielewana kabisa na mjomba wake na hataki kabisa kujifunza hiyo kitu.
Hivyo kazi niliyokuwa nayo kwa wakati huo ilikuwa ni kuhakikisha nambadirisha mawazo yake na kumshawishi aipende ile kazi ambayo nafaa nimfunze.
“Sikiliza George, maisha wakati mwingine hayaendi vile unavyopanga, bali yanaenda vile Mungu amekupangia. Mimi hivi unavyoniona, elimu yangu ni ndogo sana ni darasa la saba. Lakini elimu hii hii haikunifanya nikate tamaa ya maisha, kitu ambacho kimenifikisha hapa nilipo ni kwamba huwa naamini katika kila fursa ambayo inakuwa mbele yangu kwa wakati huo. Kwa maana hiyo fursa ndio inaweza kunifikisha katika malengo yangu. Sasa basi, wewe ndoto yako ni mpira, lakini kwa wakati huu hujapata nafasi hata ya kuchezea Simba ya watoto bado unacheza tu mtaani. Unachotakiwa ni kuitumia hii fursa iliyopo mbele yako, kubali nikufunze hii kazi na nitahakikisha nabonga na boss wangu unapata ajira hapa ofisini pale utapokuwa umehitimu. Na wakati huu ukifanya hii kazi jioni bado unakuwa una nafasi ya kufanya mazoezi yako ya mpira, huwezi jua hii ndio ikawa nafasi yako ya kutokea. Huenda mtu atakayekufikisha katika ndoto yako akatokea hapa maana hapa tunakutana watu maarufu wengi,. Tafadhali usichezee hii fursa mdogo wangu, mimi na mjomba wako tumeishi vizuri sana na ananiamini ndio maana unaona aliamua kuniita Engneer ali ya kuwa sina elimu hiyo 😂😂.”
Namshukru Mungu huyu kijana leo ninavyo simulia hadithi hii George anafanya kazi katika kampuni moja kubwa sana, anaendesha maisha yake vyema. Anaipenda hii kazi ya kuprint na mpira haupi tena kipaumbele.
Kitu ambacho naweza kukuambia hata wewe ndugu msomaji,tuna ndoto zetu ila wakati mwingine zinweza zisitimie. Lakini la msingi ni kuwa hakikisha hauchezei fursa inayokuwa mbele yako. Hiyo huenda ikakufikisha katika ndoto yako.

Upvote
0