habari ya asubuhi wadau!
usiku wa leo ni mara kama ya saba hivi (sio mfululizo lakini) inanitokea ndoto hii ya kuota kuwa kuna radi kali zinapiga!
ninakuwa kama niko nusu macho na nusu nimelala, radi kali inapiga pale nilipo ikifuatiwa na ngurumo kubwa sana. leo niliota niko na mwenzangu. nakumbuka nilimuuliza, "hivi huu umeme si umepiga hapa hapa tulipo?", akajibu "ndiyo!". tukawa kama tunataka kujadiliana kitu na ghafla radi ikapiga tena......nikarudi katika fahamu zangu zote. niliiinuka kabisa na kuchungulia dirishani kuona kama kuna mvua huko nje sababu kiukweli haya mambo yanatokea wakati sehemu flani ya fahamu zangu ziko sawa kabisa kabisa. nilishangaa kuona kuwa hakuna dalili yoyote ya mvua wala radi!!
nilikuwa nachukulia kawaida tu hapo mwanzo, sasa kuendelea kwa hili nimeona ngoja niilete hii hoja humu pengine naweza kushauriwa kitu kutoka kwa wadau wenye ujuzi mbalimbali humu. kwa mbaali kuna kahofu na kamshangao kameanza kuniganda. sina kawaida ya kuzifuatilia ndoto kwa sana laini hii nimelazimika kuja kwenu.
naomba kuwasilisha!