Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,201
- 2,599
Hamjambo wapendwa.
Mnamo mwaka 2014 mwezi na tarehe sikumbuki kwasababu sikuandika popote ndoto hii. Mimi naishi kwa kumwamini Mungu kama muumbaji na mlinzi wa kila kitu kwangu.
Siku moja nikiwa nimelala usiku wa manane ilitokea nikaanza kuota ndoto hii; Niliona mbali juu ya anga kichwa chenye kofia ya kifalme chenye mfano wa binadamu kikiwa kimezingirwa na mawingu mepesi mfano wa yale yatokeayo baada ya Rocket kupita angani, kichwa kile kilinena maneno kama kichwa chenye mamlaka lakini maneno yale sikuyaelewa yote isipokuwa nilielewa haya~ 'BAADA YA SIKU 38' baada ya kunena maneno hayo kichwa kile kilipotea ghafla na mimi nikaamka muda ule nikiwa najisikia hali isiyo ya kawaida kabisa, nikaanza kwa kusali kisha nikatoka nje kushuhudia juu angani kama kichwa kile bado kipo au hakipo.
Wapendwa sikukiona kile kichwa tena bali niliona mawingu yale yale niliyoyaona kwenye ndoto. Baada ya hapo Nikawahi sana kanisani kwa ajili ya maombi ya asubuhi ambapo nilisali vyema na kwenda kwa shughuli zingine. Hata hivyo baada ya hapo niliazimu moyoni kuwa ningefatilia tukio gani lingeweza kutokea baada ya siku 38, ajabu ya kilichotokea ni kuwa baada ya siku ya 38 alifariki msanii maarufu wa hiphop wa hapa Tanzania, sitamtaja jina maana sijui ndugu au washabiki wake watanichukuliaje, bhasi nikafikiria sana maswali haya; kwanini ndoto ile inijie mimi?
Je kile kichwa chenye kofia ya kifalme kilimaanisha nini? Je yale mawingu yalimaanisha nini?
Je kwanini nilipotoka nje niliona mawingu tu yakiwa vilevile nilivyoota bila kuwepo kile kichwa?
Sasa wapendwa ulimwengu wa roho unanishangaza sana maana hadi leo sijapata majibu ya maswali hayo hapo juu, karibuni kwa mchango/majibu yenye mwanga zaidi.