Ndoto yangu ni kuepukana na umasikini sijui nini kitatokea

Ndoto yangu ni kuepukana na umasikini sijui nini kitatokea

Episode ya 5/6 umepuyanga kidogo ila sio mbaya. Humu tu
 
SEHEMU YA TISA



Bibi alikuja anakimbia pamoja na Esau, ile wanafika mlangoni wanakutana na Jolvin akiondoka, kashidwa kuvumilia maumivu anayoyapata Gorii! Ilibidi akae nje kwanza mpaka watakapomaliza kumhudumia.

Huku kwa Gorii” aliendelea kuugumia maumivu huku akilalamika

“” Ni Moto hii dawa naungua, naunguuua!”

Kelele za maumivu zikamfanya hata Rich akimbie chumbani, Kama walikuwa wote huenda hata yeye anakidonda, asije pakwa bure maumivu anayoyapata Gorii akayasikia Kwake.

Baada ya matibabu kukamilika, Jolvin ndio anaingia! Alimkuta Gorii” kalala kwenye sofa ubavu mmoja, ilibidi asogeze kiti kilichokuwa Karibu Kisha alitizama vizuri kile kidonda, muda huo Gorii” alikuwa akisikilizia maumivu kwa mbali huku akijaribu kutafuta usingizi.

“” Polee Goryanah!”

Gorii” alisikia vizuri ile sauti kaitwa jina lake kwa kirefu, alimtizama Jolvin Kisha aliongea.

“” Leo umeniita Kama mama kabisa! Mamangu hupenda kuniita kwa kirefu “” Goryanah”

“” Basii… Wewe pumnzika kukiwa na shida toa taarifa! Halafu kwasasa unatakiwa uwe na Simu make waweza zidiwa!”

“” Mimi Simu ya Nini? Wakati Sina hata Ndugu wa kumpigia! Halafu kule kijijini ninae Mamangu anaitwa Ma Muddy nisaidie basi nipate kuwasiliana nao! Sijui hata Muddy anaendeleaje huko!?”

“” Siku ukipona nitakupeleka ukaione familia yako!”

“” Ooh! Wao Kaka White… Nitashukuru Sana Kaka White!”

“” Tulia sasa! Utaumia ukijilazimisha kuamka! Nitakuja baadae kukuona!!”

Huku Chumbani kwa Esau, walikuwa wamekaa wote na wadogo zake Joely na Rich wakimzungumzia Jolvin.

“” Mimi naona Jolvin! Ameanza kumjali Sana Gorii” huenda kaanza kumpenda vile!”

“” Aaah! Ka Joely! Yule ni mdogo kwake, afadhari hata Mimi naendana nae kwa Kila kitu.

Rich alidakia….

Esau yeye huwa siyo muongeaji Sana alibaki kucheka tu!

“” Mi naona aendelee kuwa vile hata hivyo tabia zake za hasira hasira Gorii kamnyosha, Unajua huwa anatabia ya kuzira zira vitu, naona sahii haifanyi.”

“” Na Da Anelisa Itakuwaje!? ” Make huwa anampenda kweli Jolvin japo Yeye anachukuliwa Kama rafiki tu!”

Joely alimhoji Esau huenda anajua zaidi kuhusu moyo wa Jolvin.

“” Anelisa ni rafiki tu! Hata yeye analijua Hilo kwa Jolvin anachukuliwa Kama rafiki!”

“” Ila Bibi sijui kwanini tu hampendagi Anelisa! Hutaamini humu ndani Gorii” ndie anapedwa kuliko wote! Siku yenyewe ameletwa na Ma Doreen hutaamini Gorii” alikataa kukaa hapa! Bibi akadeshi kuumwa mguu, Gorii akamsaidia hapo hapo Bibi alilazimisha Gorii” abakie!”

Maneno ya Rich yaliwasitua kwanza ilibidi wabaki wakitazamana, Muda huo huo Jolvin aliingia Kisha alijilaza kitandani kwa Essau, aliongea.

“” Vipi Kama tutashilikiana kumtafuta Mamake Gorii” akipatikana haraka inabidi aondoke hapa! Make naona Kama kichwa changu kinaniuma kuhusu yeye!”

“” Mhuuu aondoke tenaa!! Mimi naona upo Karibu nae iweje utake aondoke!?”

Joely alijibu.

“” Akakae kwao make anatufanya tubaki tunamtizama yeye! Mpaka tunashidwa kujisomea kwa wakati.”

Maneno ya Jolvin yaliwachanganya huenda wao walihisi tofauti kuwa anampenda, kumbe kafanya vile ni huruma ya Gorii kuwa mgonjwa.

Baade walisikia mlango ukibishwa hodi, ni mama yao alirudi Baada ya kutokuwepo wiki moja alipelekwa dolia ya wiki kulinda mipaka, wakati wa kurudi alirudi pamoja na familia ya Ma Doreen.

Mama aliingia huku akiita Gorii”, Doreen nae pia alikuwa kamumisi kweli Dadake japo wanatofautiana Kama miezi miwili tu, ile wanafungua mlango ndio wanamkuta Gorii” kalala huko jasho jingi likimtoka.

Rich yeye Baada ya kusikia mama karudi alitoka moja kwa moja kumuona.

“” Rich nambie! Gorii” kawaje tena!?”

Rich ilibidi amweleze ilivokuwa ndio Mama akashusha pumnzi huku akimshika kichwani.

“” Hii familia iliyofanya hivi lazima itatutwe, Kuna siku watamuumiza zaidi.”

“” Maama! Ka Jolvin tayari kaanza kuifatilia hii familia!”

Gorii” yeye alikuwa busy na Doreen wakiongea sitori zao, kweli walikumbukana Sana.

“” Sasa Gorii… Inuka tutembee tembee hata hapo nje upugwe upepo!”

Waliongozana kwa pamoja Hadi nje huku wakiwaacha kina mama wakiongea kuhusu maendeleo ya Gorii, hata hivyo Gori alikuwa amependeza Sana sio Kama kipindi kile anaingia kwenye nyumba hio. Mama Rich alimwelezea jinsi Bibi anavyomkubali Gorii pamoja na familia yake kwa ujumla.

Huku nje Doreen pamoja na Gorii” waliendelea kupiga sitori nyingi lakini alimwomba siku moja afike Nyumbani kwao tena! Hata hivyoo wamemumisi.

“” Sawa Doreen nitafika’ Vipi kuhusu Baba make alinichukia siku ya kwanza tu aliponiona! Maskini Baba sijui nilimkosea nini tu, mpaka nikawa na wasiwasi huenda tuliwahi kukatana ghafra nikamfanyia kitu kibaya, hata siku ile kaniona akataka kulipiza kisasi.”

“” Achana nae, huwa inatokea tu mtu unaonana nae siku moja lakini damu zinashidwa kuendana, yaani unamchukia Ghafra!”



Muda huo Jolvin alikuwa akipigiwa Simu na Anelisa, alitoka akizungumza.

“” Kwamba Yule Mama anaefanya kazi za ndani katoroka na pesa! Kwanini Sasa kafanya hivyoo!? Okay nakuja.”

Gorii” alimsikia vizuri Jolvin akiongea, Alishangaa ghafra anapata mshituko ilibidi amfuate Jolvin. Jolvin muda huo alikuwa akiingia kwenye gari alimkata jicho Kali lilionesha hataki mazoea.

Doreen alimfuata Kisha alimshika mkono, wakirudi sehemu walipokuwa wamekaa.

“” Sijui hata nafanya Nini tu, nimejikuta namhurumia huyo mama alieiba pesa! Huenda hata alikuwa na uhitaji wa hiyo pesa!””

“” Gorii” usiwe unaingilia vitu visivyo kuhusu! Achana nae, hapa ni mchini Kuna watu huwa wanaomba kazi za ndani kumbe wanayao kichwani!”

Jolvin alifika Hadi Nyumbani kwao Anelisa, aliikuta nyumba ipo kwenye simanzi kila mtu anawazua kivyake.

“” Anelisa nikuone kwanza…!”

Walitoka nje huku wakizunguka uwani, Anelisa akimwelezea.

“” Ni mama mpole hivi, ana nywele ndefu huwa anapenda kubana, Mimi nahisi kachukua zile pesa ni kwaaajili ya matibabu, Mwanzoni alivyokuja hapa alikuwa ana afya mbaya! Mwili wake ulikuwa umejaa mapele, Baba alivyomuona vile aliongea na Mama aongee nae vizuri kuhusu huo ugonjwa, Mama Baada ya kuongea nae alikuwa muwazi kweli yeye ni Muathirika wa Ukimwi wa muda mrefu pia huwa anasumbuliwa na kifua! Mama alirudisha majibu kwa Baba, ilibidi Kama familia ikae muda huo na Kaka alikuwepo wakaona kazi kumfukuza ikabidi wamruhusu aendelee kukaa huku akiendelea kutumia dose, afya yake ilianza kukaa vizuri wote tukawa tumemwamini, hata hivyo alikuwa ni mcheshi Sana muda wote uwepo wake humu ndani ilikuwa ni furaha! Sielewi hata amewaza Nini kachukua pesa chumbani kwa baba akawa ametoroka, tumeamka asubuhi tunakuta kachukua nguo baadhi tu huku nguo zingine kaziacha.

“” Usijali Anelisa! Atapatikana tu! Huyu atakuwa hayupo mbali, labda unapicha zake nimuonee!”

Anelisa alichukua Simu yake, Kuna picha nyingi alikuwa akimpiga, muda mwingine wapo wote au na familia kwa ujumla.

“” Una uhakika ndie huyu? Mbona hafananii? Halafu sura Kama naijua.

“” Sura…!!?”

“” Yaaah!! Sijui nimemuona wapi kweli…!?”

Jolvin alifungua Simu yake, Kuna picha ile siku kaziona chumbani kwa Gorii” alizipiga picha, mpaka kile kipepelushi alichokuwa akisambaza kumtafuta.

“” Nitakuwa nimemfananisha au macho yangu tu!?”

Anelisa alidaka ile Simu Kisha alianza kuzipitia zile picha.

“” Mbona ni yeye kabisa, unaona hapa alivyobana nywele! Hii sitaili anaipenda kweli! Wewe unamfahamu!?’

“” Ni Mamake na Yule Binti anaeishi Nyumbani!?”

“” Kile mnakiita ki Gorii” siku yenyewe ulikisaidia kikiwa na Rich kimejaa tope!?”

“” Jolvin alimukubalia kwa kichwa.

Bila kuongea na wazazi wa Anelisa walichukua Gari kuelekea Nyumbani wakapate majibu kutoka kwa Gorii”

Ile kufika tu Jolvin alikuwa na hasira nyumba nzima alisikika akimuita Gorii” aje sebuleni.. Familia yote nayo ilifika pale wasikilize kipi tena kimejili, muda huo hata Ma Doreen alikuwepo bado.

Gorii” ndio anatoka chumbani akiwa na Doreen huku akishangaa..

“” Kaka White… Ndio Wewe unaniita kwa sauti hivyoo! Huoni naumwa!?”

“” Unaumwa Wewe tapeli mkubwa, yaani mmee……..!”

Jolvin aliwahi kumustopisha Anelisa, Alichofanya ni kumuonesha picha katika Simu yake.

Gorii” alichukua Simu huku akipekua picha.

“” Huyu si Mama? Kaka White mamangu yupo wapi!? Mbona hukuniambia Kama umempata!?”

Aliendelea kupekua zaidi picha, Baada ya kumaliza kukagua alianza kumuonesha Bibi yake.

“” Bibi huyu ndio Mama’ngu Mimi ninae mtafuta siku zote! Kumbe yupo hai mama siku zote anaishi!?”

Kabla hajamaliza kuongea, anashangaa wazazi wa Anelisa wanaingia huku wakiwa na police.

Wote walitoa macho hawakuamini, Sikuzote unaambiwa familia yenye uwezo huwa wanafanya kile wanachokitaka na sio kinachotakwa.

“” Police tenaaa…..!!?”

Kila mtu aliduwaa asiamini hata Jolvin hakujua itakuwa vile, ilibidi amgeukie Anelisa.

“” Wewe ndio umefanya hivyoo!?”

Anelisa alitabasamu Kwanza Kisha alimsogelea Gorii” amjibu kipi kinaendelea..

“” Mamako wewe ni mwizi! Kaiba million tano Nyumbani! Haijulikani kakimbilia wapi!? Nahisi tukikukamata Wewe mamako atajisalimisha kwahiyo sahii upo chini ya ulinzi.”

“” A aah! Mamangu hawezi kuiba pesa nyingi vile! Kwanza hanaga hiyo tabia! Ndio umemtengenezea kesi Mama’ngu! Ni kwakuwa hunipendi Mimi ee? Kwakuwa ni Mama nitaenda kutumikia kifungo… kikubwa aishi tu! Madaam yupo hai halafu leo hii nakamatwa na Police… Nafurahi kusikia anaishi ila naumia kwasababu amesingiziwa.

Babake Anelisa aliona Kama Gorii” anafanya maigizo aliamuru Police wamkamate
 
SEHEMU YA KUMI



“” Hapana hicho sio kigezo Mjukuu wangu akawekwa ndani! Na hawezi kupelekwa kituoni kwa kudhalilishwa njia nzima, nyie tangulieni atapanda kwenye gari yangu! “Jolvin naomba unipakie.”

” Aaa.. lakini Bibi.. Mtuhumiwa ni Mtuhumiwa tu! Acha aende!”

Wakati huo wakiendelea kuvutana, Ma Doreen, na Ma Rich wote waliingilia wakisema wataenda wote. Rich yeye alivunja ukimya kabisa alikimbilia kwenye gari la Police akidai watakuwa wote na Gorii”

Jolvin alibaki kushangaa, Esau na Joely walimfuata.

“” Hivi ni kweli kinachoendelea ni sahihi!?”

“” Mimi sikutegemea Kama Police wangefika hapa! Ilikuwa ni kumuuliza Gorii Kama zile picha ndie Mamake, halafu ndio tuone namna!!”

Anelisa alifika pale alimshika mkono Jolvin akimhitaji waondoke.

“” Usijali kwasasa hutawaza tena kuhusu Gorii, hapa tutamuweka ndani akitoka hapo ataenda kuanza maisha na Mamake kijijini kwao!”

Muda huo Bibi alikuwa tayari kakaa kwenye gari akimsubili Jolvin amwendeshe, lakini kwa Nyuma alikuwa amekaa Gorii katulia huku kajinamia, Jolvin alifanya kumuangalia kwa hasira Kisha alishika usukani kuelekea kituoni.

Baada ya kufika Wazazi wa Anelisa walitangulia ndani, huku akifatiwa Bibi pamoja na mwanae Mama Rich, siku hiyo kituo kiliwakishwa mwenye pesa, na mwenye pesa mwenzake kitakachomuonesha mwenzake mshindi ni uharaka wa kudadavua tatizo kwa uelewa zaidi.

Gorii Baada ya kushuka aliaambiwa asaini jarada la kesi ili waendelee kuifanyia Uchunguzi. Baada ya kumaliza kusaini alienda kujitenga mwenyewe huku akizunguka akikumbuka taswira ya Mamake alivyomuona kwenye picha.

“” Kumbe Mamangu anaishi vizuri tu, anae mavazi mazuri, nywele yake kaiosha vizuri pia katana, na shingoni anacho kidani kizuri!”

“” Gorii….!!!”

Bibi alimuita Baada ya kuona anaongea pekee.

Gorii ndio anageuka.

“” Bibi!! Mama kanifuata!? Kwasasa sitakaa mbali nae!”

Bibi alitikisa kichwa akiashilia hamna. Muda huo huo Anelisa alifika, alimuijia Gorii ikawa wameongozana lakini Bibi alimkuta hilo jicho huku akiongea kimya kimya.

“” Kama Mjukuu wangu atakuoa.. labda Mimi Bibi yake niwe kipofu nisione!”

“” Gorii kwasasa unaweza kurudi Nyumbani! Ila muda wote tutakuita tukuhoji kuhusu familia yako! Huenda hiki ndio chanzo Cha mamako kuiba pesa nyingi!”

Anelisa aliongea huku akimuacha Gorii kaduwaa asimjibu chochote! Rich alifika pale alimpatia mkono Gorii akimuomba waondoke!

“” Rich…!! Kwani imekuwaje tena mpaka wameniruhusu niende Nyumbani? Mimi nataka nibaki hapa ili Mama akisikia nimekamatwa lazima atakuja kuniona!”

“” Gorii!! Bibi anakungoja pamoja na Mama!

Joely aliamua kuwafuata! Lakini kwa Gorii” hakuwa anataka kwenda Nyumbani aliangalia namna ya kubaki pale, aliinama akachukua jiwe lilokuwa chini Kisha alimlenga Askari mmoja kati ya wale walokuwa wakimhoji.

Alipiga kelele kwa maumivu, huku akigeuka kumtizama aliyemponda, alikutana na Gorii kasimama wala hajali alimsogelea Yule Askari huku akimtolea maneno makali.

“” Lazima nitakuua tu!”

Watu wote walishituka, Kwanini Gorii” aseme hivyo au wanafahamiana?

Muda huo huo Police walimrudisha Gorii selo make kamtishia kumuua mtu.

Habari zikaenea kwa muda mfupi hadi zikamfikia Anelisa, ambae muda huo alikuwa bado yupo kituoni na familia yake wakitoa baadhi ya Picha za Mama Gorii” ili atafutwe.

“” Unaona Mwanangu! Itakuwa kweli huyu Mtoto alivyomkorofi Ni harali Mamake aibe pesa! tabia ya Binti yake ndio imeonekana hapa!

Baba Anelisa aliongea mbele ya Askari lengo lilikuwa ni kuongea na Binti yake lakini ujumbe ulifika mikononi mwa Askari, Maneno yale yaliwafanya kila mtu atikise kichwa, “Kweli, kwelii”

Panapo Selo, Goriii alikuwa akihangaika na ile harufu ya pale! Mbaya zaidi ni pale alipoletewa chakula Kuna Askari alikuwa amechomekewa pesa ya kumsulubisha Gorii, alifanya kutumia kazi yake vizuri kutokana na hongo ya pesa.

Huku Nyumbani familia ilikuwa haina raha kabisa, hasa Bibi ndio alikataa hata kula! Jolvin ilibidi akae na Bibi kumbembeleza lakini Bibi nae alimchunia alijua yeye ndio mwanzilishi wa yote.

“” Lakini Bibi,” “Mbona unanichukia hivyo!? Utazani mimi ndie nilimshikisha jiwe Gorii amponde Askari!!?”

“” Adhabu anayopata Gorii” huko yote ni kwaajili yako! Nishakwambia achana na Anelisa bado unajenga nae mazoea! Wazani ungekuwa umenisikiliza huko kupekenyua maneno kuwa Mamake Gorii kapatikana,, hii yote ni mazoea ulojijengea kwa Anelisa. Gorii binti mdogo anapitia mitihani mikubwa katika maisha bado Yule kijana majuzi kamtoa ngeu begani! Sina hata amani huko aliko Kama wanamchukulia ni binti mdogo! Hawanaga huruma wale, nahisi kile kidonda kimekuwa mara tatu yake sahiii!”



Bibi alizidi kuongea, Kuna namna anamjua Mjukuu wake huwa anaogopa Sana kidonda! Ni Kama alimtekenya sehemu.

“” Kwahiyoo Bibi! Watakuwa wakimjeruhi Tena kwenye kile kidonda nilichokihangaikia kipone!?”

“” Tena sanaa! Masikini Gorii sijui hata Kama anatembea huko aliko! Akigeuka kila sehemu ni Rungu hadi kukapambazuke! Sizani Kama atakuwa Gorii tenaa! halafu nahisi wanaweza kumfanyia mchezo mbaya…..

“” Basi Bibi usiseme… Ngoja nimuwahi kabla hawajamjeruhi kidonda chake!”

“” Kwasasa ni usiku! Hapa Hadi kesho Asubuhi!”

Ilibidi waagane pale lakini maneno ya Bibi yalikuwa yamemkaa Jolvin. Asubuhi yake yeye ndie alikuwa wa kwanza kufika kituoni, aliomba aonane na Gorii. Mawazo ya Bibi hayakuwa mbali na fikra zake, alimkuta Gorii” kaegama ukutani huku nguo aliokuwa kavaa imetapakaa damu, alikumbuka maneno ya Bibi tena huenda hata wamemfanyia michezo mibaya!

Alisogea karibu yake Kisha alimbeba akitoka nae nje.

“” Vipi Mishoki… Mtuhumiwa wetu Kazidiwa Adhabu nin!?”

Askari mmoja alihoji kwa Dharau, lakini muda huo huo Mamake Rich aliingia siku hiyo alikuwa amevalia gwanda yupo kikazi zaidi ile walivyomtizama wote waliogopa wakasogea nyuma.

Gorii” alichukuliwa kupelekwa Hospitalini, alifika akaongezewa Dreep ya maji, Kisha alisafishwa kidonda. Mama Baada ya kuona anaendelea vizuri alimuachia Jolvin amuangalie Kisha alirudi kituoni kuendelea na kesi!

Gorii ndio anaamka huku akihisi maumivu mwili mzima alitazama Kama Kuna mtu pembeni yake ndio anamuona Jolvin alimuita…

“” Kaka White!! Upo hapa kunitizama muda wote!?”

Jolvin aliona aibu hata kumtizama, aliona yeye ndie chanzo Cha yote hayo! Alisimama ili atoke nje lakini Gorii alimuita akaomba chakula.

Ilibidi arudi Kuna hotpot ilikuwa imeshaandaliwa tayari kwa chakula alipakua kwenye sahani Kisha alimpatia.

Gorii” alibaki akimtizama tu make hawezi kula kwa kutumia mkono kutokana na maumivu ya kidonda.

“” Nahitaji msaada wako nipate kula!!”

Jolvin hakuwa na budi kufanya vile, alianza kumlisha taratibu Kisha alimuuliza.

“” Mimi ni mwema kwako!?”
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA

“” Hata mimi Sina majibu! Make sikuelewi tu!?”

“” Vipi walikufanyia michezo michafu!!?”

“” Sa’ Mbona unaongea huku waona aibu, ila yule Askari nilivoongea kuwa nitamuua, Basi nitalipiza kwa hawa Askari Wenzake, hasa huyu alobaki kunisimamia jana! Yaani kanifanyia vitu vya ajabu! Sipendi hata nisiseme.”

Jolvin alishituka Kwanza huku akishusha sahani ya chakula chini.

“” Kwahiyoo wamekubaka!?”

“” Sio hivyo bhana na wewe!!’ , Mimi sipo hivyo! Unaona huu mguu kwenye kisigino na goti alivyokuwa akinipiga Rungu! Lakini nitapona tu! Vipi mama kaja hata kuniulizia?”

Jolvin alifanya kumsitikia tu, sio rahisi Mamake kujireta kituoni wakati ni mualifu.

“” Kaka White! Itakuwa hajaja ee!? Vipi Bibi nae yupo wapi!?”

Kabla hajajibu, simu yake iliita alikuwa ni Anelisa! Alimuelekeza Hadi sehemu alipo akawa amefika pale.

Alifika akamtizama Gorii ambae alikuwa akimtizama tu huku alikumbuka maneno aliyoambiwa mara ya mwisho na Anelisa anatakiwa kwenye chumba Cha mahojiano, aseme vizuri kuhusu familia yake ilipo, ilibidi Gorii ajiwahi make hakutaka kuhojiwa.

“” Da Anelisa!! Vipi Kama mtanihoji siku nyingine sahii bado naumwa!”

“” Uhojiwe Nini tenaa!?”

Jolvin aliuliza.

“” Ni kuhusu Familia yangu! Naona Kama nitaongopa kwa hili, Mimi namjua Mama tu, labda Kama ningempata ningemuulizia vizuri.”

“” Aaa basii… Kama hujui hatuwezi kukuhoji ukadanganya mahakama matokeo yako kesi ikazidi kukua!!”

Jolvin alibaki kumtizama Anelisa huku akimfikilia vitu vingi, mbona Kama analeta hoja nyingi nyingi!.

Anelisa nae alijishitukia lakini alifanya Kama kuvunga alimtizama Jolvin Kisha alimsogelea huku akimtengenezea nywele.

“” Itabidi leo ukapumnzike Nyumbani! Halafu hewa ya hapa naona ni nzito! Mwili wako utafadhaika sana!”

Gorii” alibaki akimtizama Anelisa kwa namna moja au nyingine alihisi sio mtu mzuri kwa Jolvin.

“”‘ aaa!! lakini Mama kaniachia kumtizama Gorii, siwezi nikaondoka nikamuacha pekee.”

“” Kaka White.. wewe unaweza ukaenda tu! Mi sahii ninazo nguvu, kuhusu Mama atanikuta! Hata hivyo Rich yupo njiani, tuliahidiana jioni atakuja kukaa na Mimi.”

Jolvin ilibidi aitizame Kama kweli yupo sawa.

“” Nipo hapa nje! Usifikili nimekuacha mwenyewe make huchelewagi kuniwazia vibaya!”

“” Haina Shida ila unakumbuka maneno ya Bibi lakini!? Mimi nakustua karibu anafika hapa, kwahiyo tembea vizuri.”

“” Ilibidi asimame Kwanza Kisha alimgeukia Gorii” “” Ulisikia alichozungumza!?”

Gorii” aliishia kutabasamu Kisha alijifunika Shuka.

“”” Samahani Anelisa!! Naomba uniache kwanza, kichwa hakipo vizuri! Bibi katuma Ujumbe nimsubili Chumbani kwa Gorii”

“” Okay! Hata hivyo naona upo mzito Sana leo kuongozana na Mimi! Nilitaka kukuaga tu, Byeee!”

Jolvin ilibidi arudi Chumbani kwa Gorii, alitaka kumhoji kuhusu maneno aliyoongea.

“” Gorii, wewe ulimsikia Bibi kasema Nini kuhusu Mimi!?”

“” Kwamba, Bibi hamtaki Anelisa! Kumbe mnataka kuoana siku zijazo!?” “Ila wewe Ndio utaamua lakini Kaka White….!! “” Ombi niliokuomba siku yenyewe unipeleke kijijini kwetu nikamuone Mama Muddy, na Muddy pia” itakuwa wamenimisi Sana! Kama ulivyosema Mimi kukaa Nyumbani kwenu nawanyima amani basii niruhusu niende.”

“” Ndio umezamilia kuolewa na Hammad!? ” Hivi Unajua nilienda kuongea nae vipi ili akuache!? Au ni kwakua hujui tu, ” Nilimwambia wewe ni mchumba wangu na siku za usoni nitakuoa! Ndio akakubaliana na Mimi! Kama utaenda……..,, Kijiji chenu chote kinajua umechumbiwa na familia ya Mishoki! Siona haja ya kwenda kujiaibisha huko!”

“” A aaa! Kwanini useme mi mchumba wako tena!? ” Si ungejitetea vinginevyo na sio useme vile! Basi Mimi naenda kwao Hammad kuvunja huo uchumba! Na nitasema ni uongo!! Nipo tayari kuolewa na Hammad na sio wewe!!?”

Mabishano yaliendelea baina ya wawili, muda huo alifika Bibi pamoja na Rich wakiwa wamebebelea vyakula mbalimbali kwaajili ya Gorii, khari walioikuta ndani ni kila mtu kakaa pembeni kajitenga huku akiwa kwenye wimbi la Mawazo.

“” Jolvin..!! Khari ya Gorii imebadilika! Mbona hauna raha!?” Bibi Alihoji.

Jolvin hata hakumjibu aliamua kutoka nje, yeye kilichokuwa kinampa Mawazo endapo Gorii” ataenda Nyumbani kwao halafu akatae yeye si mchumba wa Jolvin na alifanya vile ili kumuwekea ulinzi familia yake itafedheheshwa kwa uongo wa Jolvin.

Huku ndani Bibi ilibidi akae kitandani huku akimshika mkono Gorii” amtizame.

“” Mjukuu wangu kipi tena kinakusumbua! Unaumwa Sana ee!?”

Gorii alimtizama Bibi jinsi anavyomjali, alihisi upendo uliokisiri ndani ya Bibi, aliamua kumkumbatia huku akicheka mpaka Bibi akasituka huku akimtizama Rich.

“” Anapenda utani huyu! Ulitaka Mimi Bibi yako nikose furaha! Ndio umefurahi!?”

“” Hapana Bibi! Mimi nilichukia kwasababu umechelewa kufika! Rich nae sijui ndio mlikuwa mwakokotana njiani,, Ani mmechelewa!!?”

“” Basi Basi… Rich mpatie chakula Dada’ko! Naona kamepungua Kweli…

“” Bibi Nenda nje Jolvin kakusubili kwanza, Ila Kaka anadekaga huyo kwako daaah!”

Bibi ilibidi awapishe, Rich alipakua chakula kiasi Kisha alianza kumlisha Gorii” huku stori zikiendelea.

“” Vipi Kaka white kakujali kama Mimi navyokujali!? Make yeye muda wote hufurahikaga na Anelisa tu!”



“” Kafanya Kama wewe! Ila wewe ni zaidi, yeye ni kuulizaga maswali tu eti ” Mimi ni mwema kwako!?” Hivi ningemjibu vipi Rich!?”

“” Kaka nae mtata kwahiyo akawa anagongelea nyundo tenaa!!?”

“” Ushaanza viudadisi vyako vya kijinga! Nipe majibu kwanza.”

“” Ungemwambia huenda ni Mwema ila sijui Kama ni Mwema! Fanya kitu nipate majibu ya swali lako!?”

Ilibidi wote wacheke, lakini huku kwa Bibi Baada ya kukutana na Jolvin, ilibidi wakae sehemu kwanza wazungumze! Jolvin aliamua amweleze kilichotokea siku yenyewe mpaka Hammad akakubali kuwa mbali na Gorii, na mpaka maamuzi ya Gorii aliyoyachukua kwasasa.

“” Kumbe ni hicho tu Mjukuu wangu! Wewe mpeleke kwao akasalimie Ndugu zake! Najua kama utafika pale watakuchukulia Kama mme wa Gorii” make taarifa Kijiji kizima wanajua umemuoa Gorii! Kwahiyo Gorii hatokubali aaibike kuwa kakukataa mbele ya watu! Watamchukulia mtu wa ajabu lazima akubali tu!”

“” Lakini Bibi hii michezo michezo itakuja kunifunga baadae! Mimi nataka Gorii akaseme tu kuwa nilifanya vile ili kumlinda yeye! Na akishasema Mimi nitatafuta njia nyingine ya kukabiliana na Hammad!”

“” Najua unataka ujitoe kwenye dili lako ni sababu ya Anelisa!? Kwanza Binti huyu muongo, Mamako kafatilia kila kitu kuhusu hizo pesa!! na inasadikika ni milioni moja iliyochukuliwa na sio million tano! Nahisi Kuna kitu wanakitaka kwako au kwa huyu Binti wa watu.

Ghafra walisikia mtu akiwapigia makofi, alikuwa ni Gorii” kapatiwa muda wa kufanya mazoezi ili viungo vyake vikae vizuri, katika pita pita ndio akabahatika kusikilia maneno ya mwisho mwisho, aliamua kumjibu Bibi.

“” Bibi hata usihangaike kujua kipi wanachokihitaji, Wewe kubali Mimi nikakae mbali na hii familia ya Mishoki, uone Kama Anelisa ataendelea kuleta michezo ya kijinga! Sema yeye hawaambii tu.. ila ni kwamba, Anelisa hataki ukaribu wa Mimi na Jolvin! Kwasababu ndie Mwanaume wake wa ndoto zake kwa baadae! Halafu Jolvin wewe Ndio wataka kunifanya nichukiwe zaidi na Anelisa…

Kabla hajajua kuwa ulinitetea kwa Hammad ukidai Mimi ndie mchumba wako! Basi mwambie mapema nisije vunjwa miguu Mimi na Yule Askari wake aliyemlipa pesa!! Mamangu bado ananihitaji ujue!?”
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI



“” Askari yupi tenaa!? Bibi alihoji kwa mshangao.

“” Jana mlipoondoka tu, Anelisa alifika akamuita Askari mmoja! Yule aliyekabiziwa kunitazama nilimuona akimuachia nafasi yule Askari alieongea na Anelisa, alishikishwa kiasi Cha pesa alitoka akifurahi, Baada ya hapo yule Askari aliebakia alianza kunishurutisha vibaya mara simama, kaa, inua mikono juu, ruka kichura hata nilipomwambia nmechoka alinipiga na rungu huku akinitishia nikae mbali na hii familia! Kama nitaendelea kukaa karibu nayo Mama’ngu sitamuona Tena! kuliko nimpoteze Mamangu bora nirudi kijijini kwetu!

Gori alimaliza kuongea huku akirudi hospitali kubeba kila kitu chake aondoke. Huku kwa Jolvin alikuwa haamini Kama Anelisa anaweza kufanya vile!

“” Hivi Bibi unamwamini Gorii! Kwa Maneno aliyoyasema!? ” Naomba tulifanyie uchunguzi kwanza!”

Bibi muda wote alikuwa kimya akimfikilia Gorii Kama ataondoka itakuwaje!

“” Bibiii ..!!

Jolvin alimuita tenaa.

“” Niache kabisa! Kwa kumwamini Anelisa leo unaenda kunitenga na Mjukuu wangu anae nipa furaha muda wote!”

Gorii ndio anarudi raratibu huku kashikilia baadhi ya nguo zake kwenye mfuko! Alijitahidi kupiga hatua huku akimfuata Bibi.

“” Huu mguu nao unasumbua kweli! Huyu mla rushwa kajua kuninyosha!”

Jolvin na Bibi walibaki kumtizama Gorii jinsi anavyokuja akijivuta mdogo mdogo! Ilifikia hatua mguu ukagoma ilibidi asimame kwanza huku akiutizama mguu!

“” Atakuwa kaumia Sana Gorii!! lakini naona anajitahidi kujikaza!”

Huku kwa Gorii Baada ya kuutizama vizuri aliona ukivuja damu, Jolvin aliamua kumfuata baada ya kuona kasimama kwa muda mrefu! Alibaki kujiuliza kimya kimya.

“” Gorii itakuwa waumia Sana!!?”

Baada ya kumfikia Gorii” Ilibidi amtizame kwanza usoni kisha aliongea..

“” Muda mwingine ni Kama unakuwa mwema kwangu!?”

Jolvin aliamua kumbeba huku akimpeleka kwenye gari pasina kumjibu kwanza, Bibi nae alifatia pamoja na Rich ambae muda huo alienda kuongea na Doctor.

Baada ya kufika Nyumbani! Walimkuta mama kawaandalia chakula, ilikuwa ni surprise ya khari ya juu make mama alikuwa haingii jikoni na Kama akiingia huwa anaandaa chakula muhimu kwa mtu muhimu.

Walikaa mezani wakawa wakiendelea kula, siku hiyo meza ilichangamka kweli familia ilikuwa ikimpenda Gori na ilifurahi kumuona yupo mzima.

Gorii” aliona upendo wa hiyo familia akawa anawaza hata jinsi ya kuondoka pale familia ataiaga vipi, lakini alipiga moyo lazima ataondoka, baada ya kumaliza kula Gorii’ ilibidi akohoe kwanza Kisha aliongea.

“” Mama, Bibi, Kaka zangu! Kwanza nashukuru kwa kunihifadhi nikae hapa! Nimekaa muda mwingi lakini naona hata Mamangu nae kakaa mbali na mimi hataki hata kuniona! Mimi nilifanya makusudi kumpiga yule Askari ili nikamatwe nibakie pale nikiamini siku Mamangu akikamatwa ataletwa kituoni nami nitamuona! Kama alirudi kijijini kutaka msaada naimani atarudi tenaa kwa mara nyingine. Kitu ninachokiomba kwenu naomba Jolvin anipeleke Nyumbani tu.

“” Aa aa! Sa Gorii akiondoka humu ndani tutaishije! Kina Kaka nao likizo inaelekea kuisha! Mimi sitakaa mwenyewe labda niambatane na Gorii”

Rich aliongea huku akiwafanya Wenzake wamtizame.

“” Hata Mimi nimeomba uhamisho! Mafunzo yangu ya chuo nitamalizia huku kwa muda uliosalia, nahitaji kukaa na familia yangu karibu.”

Jolvin aliongea, ni kitu kilichowasitua sana, hata familia ilikuwa haina habari juu ya Hilo, Upande wa Bibi yeye alijawa na furaha aliamua kuongea.

“” Kama Jolvin atabakia Basi na Gorii abaki, hii nyumba itakuwa na furaha wawili hao Kama watakaa pomoja katika hii nyumba.”

“” Lakini Bibi… Jolvin atakuchukulia uangalifu! Kama atahamia hapa kimasomo Mimi naweza nikaondoka tu!”

“” Kama hutakubaliana na bibi, Basi hata Mimi sitakaa hapa nyumbani nitakufuata huko kwenu, si wewe umekaa hapa, Basi tupishane!?.”

Gorii” ilibidi acheke kwanza make akiangalia mazingira ya Nyumbani kwao kulivyo kijijini, bado chakula Cha kule ni mboga moja mezani siku imepita, alihisi kumhurumia kwanza.

“” Lakini Rich.. unayajua maisha ya Kijijini Kweli! Huko hawaishi Kama huku mara ule nyama, kuku huko ni mboga mboga pamoja na dagaa!”

Mama Ilibidi aingilie make mijadala ya Hawa watoto anaijua mwenyewe.

“” Gorii” mwanangu Mimi sikukatazi kwenda Nyumbani kwenu! Ila iangalie pia hii familia siku ukiondoka utaiachaje!? Familia kwa ujumla tunakupenda sana! Nilitaka ubakie hapa usome Kwanza, tayari nimekutafutia chuo na mwezi wa kwanza ulitakiwa uanze, Kuna baadhi ya mahitaji nimeyakamilisha! Naomba uamue mwenyewe ila nilitaka ukasalimie kwenu halafu urudi uendelee na masomo! Katafakari usiku wa leo utanipatia majibu kesho Asubuhi!.

Gorii alibaki amepigwa butwaa, Ndoto aliyokuwa akiipenda ni kusoma ili apate kazi, na Kama atashidwa lazima apambane kutafuta kazi, je ni kazi gani atapata endapo hajasoma!?” Hili lilikuwa swali Kwake lakini leo hii linatatuliwa.

Hata usiku alipoenda kulala alikuwa akiwaza Jambo Lile lile, kabla hata hakujapambazuka vizuri aliwahi kumgongea Mlango Mamake akimwambia ataenda kijijini Kisha atarudi kusoma.

Yapata wiki moja kuisha Gorii” alikuwa tayari kapona, afya yake ilirudi Kama awali, siku hiyo walikuwa mjini wakihemea baadhi ya zawadi ya kuondoka nazo, hata ilipofika siku ya kesho yake Gorii pamoja na Jolvin walikuwa njiani wakielekea kijijini.

Baada ya kufika walielekea Hadi kwa Mama Muddy, walipokelewa vizuri! Make walikuwa wameandaa chakula kingi Kama unavyojua mambo ya Kijijini ni wali nyama, soda! imeisha hiyoo.

Siku hiyo Jolvin alikalibishwa Kama mkwilima kwenye nyumba ile, Baadae Mama Muddy aliomba aongee na Gorii”

“” Tulisikia habari ya kuolewa na Kijana toka familia ya Mishoki, hongera Sana make mnaendana kwa kila kitu!”

“”Sawa’ Mama, lakini Muddy yukowapi mbona simuoni!? Vipi kuhusu Mamangu umenigusia kuwa ulipata taarifa kwamba kaiba pesa kwa watu! Sijui alienda kuzifanyia kazi gani!?”

“” Nimeshalipoti kwa mjumbe kwa pamoja wanamfafuta! Halafu Hammad kaoa! Kama siku tatu zimepita, kwasasa yupo kwenye mapumnziko mjini.”

Wakati wakizidi kuongea Muddy ndio anakuja, alikuwa na baskeli ndogo akiendesha kwa kasi kumuwahi Gorii, Alifika Nyumbani akapaki baskeli akimuita Gorii”

Gorii baada ya kusikia sauti alitoka mbio akikimbia alifika akamkumbatia Muddy huku wakiendelea kuruka ruka kwa furaha!

Muda huo Jolvin yeye alikuwa akitembea tembea na vijana wa pale Kama wenyeji wake, wakati anarudi ndio anakuta position ya Gorii akiruka ruka na Muddy. Jolvin alimtizama Muddy aliona Kama anamuumiza Gorii ilibidi amzuie.

“” Wewe kijana!! Anaumia huyoo!!?”

Gorii” ndio anageuka kumtizama Jolvin, alibaki akicheka tu.

“” Kaka White! Haniumizi bhana ni utani tu huu, hata hivyoo hii ni michezo tuliyokuwa tukiicheza na Muddy!”

Muddy mwenyewe hata hakuwa akijali, alisogea Tena akamshika kichwani.

“” Nywele yako sahii ina matunzo, hivi unakumbuka niliwahi kukwambia wewe ni mzuri!”

Gorii” alitabasamu Kisha alimvuta masikio huku akimwambia.

“” Nikiwa narudi! Nitaenda kukuombea ruhusa kwa Mamake na Jolvin na wewe uende shule!? Au ushabadili maamuzi ya shule!?”

“” Kwahiyo wewe sahii unasoma!?”

Kabla hajajibu Mamake Muddy alifika akamuita Muddy! Ilibidi amweleze kwa kina baada ya kumuona Muddy anamzoea Sana Gorii, kuwa kwasasa Gorii ni mchumba wa mtu anae muona pale!

Huku kwa Gorii” aliamua atembee tembee na Jolvin kuelekea kwenye mashamba yao! Walifika kwenye shamba la mihogo ilibidi wakae pale huku wakiendelea kutafuna mihogo.

Muda huo Jolvin alikuwa hoi kwa kutembea, make Gorii alikuwa akimtembeza umbali mlefu, alivyochoka aliomba apumnzike kwenye kimvuli Cha mti wakawa wamepunzika wote!

Huku kwa Jolvin ilikuwa mbinde kila akilala alihisi Kama anachafuka, Gorii aliliona vile ilibidi asogee karibu huku akimruhusu aegame miguuni Kwake.

“” Kaka White! Naona unahangaika Sana nilikwambia kwetu kijijini! Ani umepauka hiyo midomo kwa kutafuna mihogo.””

“” Nifute basii… Si Mimi mmeo!?”

“” Alitabasamu tu huku akimfuta..”

Jolvin aliamua kukaa ili amtizame vizuri Gorii akizungumza.

“” Huwa una macho mazuri na nywele zako laini Kama wale waarabu weusi!”

“” Utani huo!! Itakuwa nimefata kwa mama! Make hata yeye ana nywele Kama zangu!”

“” Mamako anaonekana kuwa mrembo Sana! Halafu Gorii Unajua leo uliniuzi sana! Tabia gani ya kuchekeana na Muddy mpaka muanze kushikana, mkumbatiane! Bado unaniita Kaka white! Hujui Mimi na wewe tu wachumba!?”

Mara Simu yake iliita alikuwa ni Anelisa, alimtizama kwanza Gorii, nae kamtolea jicho alijua kabisa atakuwa ni Anelisa. Ilibidi asimame pale awapishe waongee kwa uhuru lakini Jolvin alimshika mkono huku akimruhusu abakie, Gorii ilibidi akae Kama afande make hakuna kitu ataongea mbele ya wapenzi wawili wakiongea na yeye ni mtu baki.

Jolvin alipokea Simu ili amsikilize Anelisa, alichoamua ni kumvuta Gorii” akamlaza miguuni Kwake huku akizidi kuchezea nywele zake!

“” Nipo kijijini! Kwao Gorii nimemleta kuona familia yake baada ya siku tatu tutarudi! Halafu nikirudi nina mazungumzo nawee!”

“” Jolvin umebadilika sana, unatoka hata kaniambia hamna, au yote ni sababu ya Gorii!?”

“” Ni mdogo wangu, Dadangu pia kwasasa ni familia yangu kwahiyo nafanya kama majukumu ya familia!”

Anelisa alichukia akakata Simu, Jolvin alibaki akimtizama Gorii, Kuna vitu alianza kuviona kwa Gorii vilianza kumvutia taratibu hata yeye akawa anashangaa!

“” Goryanah!! Usingizi tayari!!?”

“” Ooh! Umeniita Kama mama kabisa!! ” Bora hata nimepitiwa usingizi sijamsikia Anelisa, Lakini Kaka White… Huwa unampenda Anelisa tofauti na urafiki! Yeye anakupenda wewe!”

Jolvin ilibidi ang’ate midomo kwanza Kisha alimuinua Gorii, akimuweka sawa.

“” Aaa.. Goryanah! Anelisa ni rafiki yangu tu! Hata wewe unahisi kuwa mi nampenda!?”

“” Sijajua nyie! Mi nitajuaje Sasa! Make upendo huzaliwa ndani ya mtu! Ndio huanza kuhisi anampenda! Labda mshapendana tayari.”

“” Wewe unampenda Muddy!?”

“” Rafiki yangu bhana! Wewe hujui kutofautisha Mahusiano ya kirafiki!?”

Jolvin ilibidi atulie kwanza, akimtizama Gorii, kumbe huwa ana maneno ya utu uzima, ilibidi amuulize..

“” Goryanah! Sahii una miaka mingapi!?”

“” Ishirini kwa Sasa! Make nimeondoka huku siku ya birthday yangu ya kutimiza miaka kumi na nane! Hammad alipania kunioa eti mi mkubwa si Bora sahii nimekuepo.”

Jolvin alitabasamu tu, huku wakisimama waondoke! Wakiwa njiani ilibidi amuulize;-

“” Vipi Rich unamfikiliaje!? Naona mpo karibu Sana!?’

“” Aa kale.. ni kajinga kajinga tu.. Anyway, ni karafiki kangu huwa nafurahia kampani yake!”

“” Unavopenda kingeleza sasa…. Hivi Gorii Ushawahi kuwa kwenye kwenye Mahusiano! Kabla hujaja kwetu!?”

“” Kaka White! Mimi sipendagi mambo ya hivo! Nawazaga kutafuta pesa kwanza! Mamangu aishi vizuri ikiwezekana aishi Kama mamako anavyoishi.”

Jolvin alicheka huku akimbinya mkono.

“” Natamani Ndoto zako zitimie hata mimi! Nitakuwa karibu yako kuzitimiza!”

“” Wewe hapana! Halafu si bado wasoma lakini? Mimi nikianza kusoma wote tunakuwa wanafunzi! Hapo ni kila mtu atakuwa akitafuta maisha yake ya Baadae.”

“” Kaa kimya.. tumefika Nyumbani, make unaongea sana!”

Baada ya kufika Nyumbani, walikuta kumetulia japo umeme ulikuwepo muda huo Muddy alikuwa kwenye Mawazo Sana kila akikumbuka maneno ya Mama kuwa Gorii kaambatana na mchumba wake ilimuuma Sana, alitegemea siku moja angemuoa!

Gorii alimuacha Jolvin sebuleni wakiwa wamekaa na Muddy kila mtu kaupiga wa kimya! Ilibidi Jolvin amsemeshe.

“” Muddy!! Wewe ndie rafiki wa karibu na Gorii! Muda wote huwa haishi kukuzungumzia!”

Baadae Gori alirudi huku kashikilia sahani yenye papai zilizokatwa katwa alifika Hadi kwa Muddy akachukua kipande akamlisha. Kisha alielekea kwa Jolvin ambae alivunga kuangalia taarifa ya habari.

Gori alimsogelea karibu Kisha alikaa karibu yake, aliushika ule mkono uliokuwa umeshikilia remote akamshikisha kwenye sahani.

“” Ulivonuna,, ulizani hautakula? Kwa watu ninaowapenda huwa napenda wote wawe na furaha! Hata wewe nitakulisha!”

Jolvin alibaki kuenjoy, baada ya kusikia vile, alifanya kumlisha pia. Japo Gorii yeye alifanya Kama kamlisha Kakake ila yeye alichukulia tofauti kabisa, kale ka upendo kalizidi kuzalishwa.

Hatimae siku za kukaa kule ziliisha Gorii pamoja na Jolvin ilibidi warudi Nyumbani!

Huku maandalizi yalikuwa mazuri kila mtu alikuwa akiwasubilia kwa hamu Sana ili wawaone.

Upande wa Rich siku hiyo walikuwa wametoka na Sophia kutembea make zilikuwa ni siku za mwisho mwisho Rich aende chuo, siku hiyo waliamua kufurahi kwa pamoja huku wakitembea tembea baadhi ya sehemu zenye starehe!

Majira ya jioni Rich ndio anarudi, alimkuta Kakake Jolvin akimsubili getini, ile anagonga geti ndio anafunguliwa na Jolvin.

“” Wewe Rich, yaani nikishaondoka tu, unaanza kutembea tembea usiku ovyoo! Ndio ulienda kuonana na huyo Sophia?”

Rich alishidwa kujitetea ilibidi akubali huku akimuomba msamaha.

“” Na mkononi umebeba Nini!?”

“” Zawadi kwaajili ya Gorii!”

“” Zawadi…!!?”

“” Ee!!”

“” Si maua hayoo….!”

Rich ilibidi ampatie Jolvin, huenda kamchukulia tofauti alianza kujieleza.

“” Samahani Kaka.. hii ni zawadi huwa unampatia mtu aliyekuwa mbali na wewe! Ni kuonesha ulimkumbuka tu! Pia unamtakia kheri, ya kumshukuru katika Safari yake kafika salama.”

“” Oooh!! Sawa! Ila uwe unawahi! Humo ndani wote wanakuwaza wewe! Umewakosesha amani, hasa Bibi na Gorii!”

“” Nimekuelewa kaka! Sitarudia tenaa!”

Alifika Hadi sebuleni, familia kwa ujumla walisimama kumpokea.

“” Ulienda wapi Rich? Siku ile ulipotea ghafra aliyekuokoa ni Gorii, na leo tenaa unarudi muda huu! Huoni familia nzima haina amani! Muone Gorii kafika anakuulizia muda wote na wewe haupo! Kajisikia vibaya ujue.”

Rich alimtizama Gorii, ambae alikuwa akimtizama alijua kabisa ashajua kama alienda kuonana na Sophia, lakini Rich aliamua kumkonyeza asizunguze kitu!

“” Njoo bwana! Mi nilikumisi! Wewe hauwezagi hata kupiga simu unijulie khari! Sijapenda”

Rich ilibidi amsogelee Kisha alimkumbatia huku akikaa karibu nae! Walianza kula kwa pamoja huku michezo yao ikiendelea kimya kimya.

Jolvin alikuwa akiwatizama, mwisho kabisa alichukizwa na kitendo kile alitoka nje kupunga upepo make ndani kulikuwa na joto.

Esau aliona Kama Jolvin hayuko sawa aliamua kumfuata Hadi nje huku akiwa na kinywaji.

“” Vipi Jolvin! Safari yenu ilikuwaje!? Halafu mbona hauna furaha!?”

“” Hapana nipo sawa Esau! Rich amebadilika siku hizi! Yaani kawa na mazoea ya ajabu ajabu! Sijui kamuiga Gorii!”

“” Ni kawaida yake mbona.. au umemsahau!?”

“” Ndio wanakuwa wakikumbatiana na Gorii! Mbele ya Wazazi hata hawaogopi! Yaani tabia zingine humu ndani zinaboa!”

Alisimama huku akielekea chumbani Kwake! Muda huo alikuwa amefura hasira! Lakini Esau ni mtu mkubwa alielewa kipi kinamsumbua mdogo Wake, aliwaza namna ya kumsaidia japo itakuwa ngumu Gorii, akamuelewa kwa akili yake ya kitoto kitoto kazi ipo.
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU

Wakati kaondoka tu, Anelisa alitia timu nyumbani alikuja kumuona Jolvin.

“” Aa Shemeji! Mbona leo usiku sana! Itakuwa umemumisi rafiki yako!?”

“” Nimempigia simu.. nimeona mazungumzo yake Kama hayupo vizuri! Nikaona nije kumuona! Vipi Bibi yupo sebuleni!?”

“” Atakuwa kalala..! Wewe Nenda tu ukamuone!”

Esau ilibidi amuache huku akiendelea kupangilia mambo yake make karibia anarudi kazini, huku Joely na Jolvin wao walikuwa bado wanasoma! Essau yeye alikuwa akifanya kazi kwenye shilika la chakula.

Anelisa aliingia Chumbani moja kwa moja alimkuta Jolvin kalala kwenye sofa huku akiwa na Mawazo Sana.

“” Nilijua tu lazima utakuja ! Make huwezagi kuvumilia ukimuona rafiki yako hayupo vizuri! Vipi umeniletea mihogo!?”

“” Nimehangaika kweli kuipata! Yaani mpaka nimeenda mtaani kuitafuta!”

“” Nashukuru kwa kuwa unajali Sana! Vipi Mama, Baba wazima!?”

“” Of course Wazima! si hutaki kuwaona!”

“” Nitakuja, Chuo waenda lini!?”

“” Ilitakiwa nikareport leo lakini nilihofia utajisikia vibaya sijakuaga, nikaona nikusubili urudi.”

“” Muda mwingine usifanye hivyoo! Waweza ukapoteza kila kitu! Mimi nipo tu.””

Jolvin alimaliza kula Kisha alijilaza miguuni kwa Anelisa, ni kitu alikizoea make ni rafiki tu.

“” Anelisa wewe si rafiki yangu tu? Kuna kitu nataka nikwambie huenda wewe ni mzoefu wa vitu hivyo sijui utanishangaa! Make hata Mimi najishangaa!”

“” Aaah.. Jolvin kitu gani hicho tenaa!? ” Ila kabla hujasema Mimi nataka niseme kitu kwako nahisi sitapata muda wa kusema ukileta ajenda yako!?”

“” Basi semaa…!”

“” Nataka urafiki wetu upige hatua… Make imekuwa muda kweli urafiki wetu umebakia sehemu moja!”

“” Hatua ipi tenaa Anelisa? Mimi napenda hivi hivi tunavyoishi! kwani kunashida?”

“” Hamna shida, ila Mimi naona ndani ya urafiki wetu Mimi na wewe, moyoni kwangu kumezaliwa kitu kingine!! Nahisi kukupenda Sana Jolvin, mpaka Kuna vitu natamani nivifanye zaidi ya urafiki.”

Jolvin alishituka Kwanza, alikaa vizuri huku akikumbuka maneno ya Gorii kuwa Anelisa anamchukulia zaidi ya rafiki, halafu leo ndio anasikia live bila chenga, hata hivyo na yeye alilifahamu hilo Mwanzoni alitaka kumuwahi amwambie kunae mtu pia anampenda.

Alimjibu;-

“” Lakini Anelisa… Ni ghafra sana! Mimi napenda hiyo nafasi ya urafiki niliyokupatia hiyo nafasi nyingine hapana!!”

“” Jov..!! im sure!! nakupenda wewe! Ingekuwa kunae nafasi ya mtu mwingine moyoni kwangu nisingesema kwako!?”

Jolvin alishusha Pumnzi Kwanza huku akipepesa macho akiangalia pembeni, unaambiwa siku zote hakuna kitu kinachozoeleka machoni Kama kubadilisha hatima, Jolvin baada ya kuambiwa hivyo na Anelisa alianza kumuogopa Kwanza hata yale mazoea yakaanza kukata taratibu.

“” Lakini Anelisa.. Mimi sipo vizuri kwasasa, bado Nina uchovu wa Safari tutaongea siku nyingine! Nahitaji kupumnzika.. sijui umekuja na usafiri wako? Au nimpigie dreva aje kukuchukua!?”

“” Hauwezi ukanisindikiza? Halafu ulitaka kuniambia Nini labda, kabla sijaondoka?”

“” Aaa! Nilitaka nikushukuru kwa kuniletea chakula nikipendacho!”

“” Okay byee! Tayari nimeshaongea na dreva tax ananiijia! Nahisi atakuwa getini sahii! Kama nitaondoka kesho nitakujulisha.

“” Okay! usiku mwema! pia Ufike salama!?”

Wakati Anelisa anaondoka, alipishana na Esau bila kujua! Esau alimwangalia Kisha alirudi Chumbani kwake.

“” Huyu Jolvin sijui anashida gani? Nashidwa kuelewa yupo upande gani ni Anelisa au Gorii? Anyway atajua kuchagua yeye kipi moyo unataka!?”

Huku Chumbani kwa Jolvin akili yake ilizidi kuvurugika, Anelisa alizidi kumsumbua kichwa, bado Gorii nae kaanza kuchukua nafasi! Aliangalia picha ya Anelisa, ni rafiki yake wametoka mbali wamezoeana, kila mtu anayajua mapungufu ya mwenzake Kama ni kuoana hawatasumbuana, aliangalia picha ya Gorii anaonekana bado anae akili ya kitoto kitoto, mambo yake ndio usiseme! Hajui kuvaa vizuri yeye ni minguo ya kijijini ndio anapenda yaani hajui kuumode mwili wake ukakaa vizuri! Lakini ndio anavutiwa nae! Aliona isiwe shida wote aachane nao awaze masomo yake! Make karibuni atakuwa na mitihani.

Asubuhi yake hata kulipopambazuka Gorii Kama kawaida huwa anaamka kufanya kazi za ndani, siku hiyo nyumba ilikuwa kimya Joely, Esau walikuwa wamemsindikiza Rich kuriport chuo.

“” Humu ndani wote wameenda kumsindikiza Rich chuo, wanaupendo kweli! Mama nae kazini! Bibi sijui nae kaenda wapi!?”

Aliandaa chai, akisaidiana na wadada wa kazi waliweka mezani huku wakiendelea na pilika mbalimbali za usafi.

Muda kidogo ndio wanarudi wote, baada ya kumfikisha Rich Airport.

Gorii aliamua akatulie Chumbani kwake make kuleta shobo na matajiri ni Kama kujipendekeza.

Bibi baada ya kufika alimuulizia Gorii” huku akielekea Chumbani kwake.

“” Wewe Mjukuu! Njoo tunywe chai! Mbona meza ipo pekee!?”

Gorii” ndio anatoka Chumbani nusura apamiane na Bibi.

“‘ Sorry Bibi! Niliwasubili mfike ndio tunywe chai!!?”

Bibi alicheka tu.

“” Miguu yako hainayo break!?”

“” Aaah!! itakuwa ni njaa hii! “

Walifika pale mezani wakaendelea kunywa chai. Baada ya kumaliza kunywa Esau alimuita Gorii waongee nje.

“” Gorii Unajua kesho na sisi tunaondoka! Mimi narudi kazini Joely anarudi chuo! humu ndani mnabaki watoto wawili, wewe na Jolvin! Naomba mkae vizuri pamoja na Mama na Bibi! Muwapatie upendo hata kwa niaba yetu!”

“” Sasa.. Kaka mkubwa! Mimi nitakuwa shule na Kaka White! Bibi si atakuwa anabaki pekee mpaka turudi jioni ndio tunakuwa wote!?”

“” Huo muda mkirudi basi mkae nae kwa pamoja! Ila Kuna kitu nataka nikuombe!”

“” Uniombe tenaa!!?”

“” Kaa na Jolvin karibu! Make akikosa mtu wa kukaa nae karibu huwa ana vitabia vya kuzira zira ovyoo! Muda mwingine huwa anakataa kula! Wewe uwe unamsimamia endapo itajitokeza vile!?”

Gorii ilibidi acheke Kwanza huku akimtizama Esau.

“” Si mtu mzima Yule!!? ” Mbona anavitabia vya kitoto japo Yeye huwa ananiambia nina mambo ya kitoto kitoto!?”

“” Ndo hivyo Sasa! Wewe kaa nae vizuri!”

Muda huo Joely Alifika, Alisogea Hadi kwa Gorii akiwa na Simu kubwa alichukua picha Kama selfie, huku wakiungana kwa pamoja katika picha ya pamoja.

“” Leo Gorii umependeza kweli! Yaani umepigilia vitu vya mambele track na hilo prouva limekukaa Kweli!”

“” Wewe J wa pili! Piga picha bhana achana na hizo nguo! Unaniharibia pouze!”

Ilibidi wote wacheke, baada ya kumtizama staili aliyoweka kwaajili ya Picha.

” Halafu mbona uliikataa Simu, Sasa utakuwa unatupataje ukitaka kuongea na sisi!?”

“” Ipo ndani mbona.. nilimrudishia Kaka White akaikataa! Ila majuzi nilivoenda nyumbani! Nilimkuta rafiki yangu kanunua Simu nikawa nimechukua namba nikaisevu kwa Kaka White! Itabidi na nyie mniachie namba zenu nizisevu kwenye simu yangu make nilikosa mtu wakumpigia! kwa kuwa nyie mpo nitakuwa nawapigia?”

“” Kwahiyo na sasahivi! Unaenda kuzisevu kwa Jolvin tukikupatia!?”

“” Hapana bhanaa! Ngoja nifate simu mniandikie, zitakuwa kwenye Simu yangu!”

Muda kidogo alirudi na Simu Kisha Alimpatia Esau.

“” Ni Simu nzuri! Ila ukishajua kuitumia hii itabidi ubadilishe simu! Ununue kubwa!?”

“” Wewe Kaka mkubwa… Na hiyo pesa nitatoa wapi Mimi!?”

“” Zinatafutwa!

“” Aah! Sahii Joely nae ataninunulia si unaherufi ya mwanzo Kama Kaka White! Si J na yeye!?”

“” Halafu Gorii! Leo tunaenda kufungua duka la nguo! Atakuwa akilisimamia Bibi na wewe! Ile mchana ukitoka chuo utakuwa waenda kumsaidia Bibi! Mama kakufungulia wewe ili uwe unapata baadhi ya mahitaji mengine na Bibi atakuwa Kama mfanyakazi wako!!”

“” Khaaaa! Hapana Bibi tena! Nyie mnataniana!”

“” Ndio hivyo!!”

Bibi alimjibu muda huo alikuwa kaambatana na Jolvin, wakiwa wamejiandaa tayari kwenda kuzindua duka make kila kitu kilikuwa kimekamilika.

“” Twaweza kuondoka sahiii!” Jolvin aliongea.

Ikawa wote wamepanda kwenye Gari! Seat ya nyuma alikaa Bibi, Joely na Esau! Kukaa mbele Bibi huwa anaogopa.

“” Afadhari nimekaa karibu na Bibi! Make leo ndio! tunakuaga lazima tukufaidi!”

Joely aliongea huku akimuegamia Bibi.

Huku mbele ilikuwa ni kimya kimya, Gorii alikuwa akimchungulia Jolvin kwenye kioo, mwisho alianza kucheka kila akikumbuka kuwa huwa anatabia ya kuzira zira ovyo.

“” Muda wote huwa ni kucheka bila sababu! Utakuwa una matatizo wewe!?”

Jolvin alivunja ukimya, Gorii ni Kama anakela hivi!

“” Bora Mimi nacheka! Wewe umeushona mdomo na zipu, Hatimae umeufungua! Au ndio umezira tenaa!?”

“” Kwa kipi!?”

“” Huenda Anelisa hajakuaga ndio maana umenuna? Vipi ulipoenda kumsindikiza Rich, ulipita pia kwa Anelisa, na yeye anaondoka leo.”

“” Please Gorii! Naomba ukae kimya Kama huwezi…! Kakae Nyuma!”

Gorii” ilibidi akae kimya huku jicho likiwa nje.

Muda kidogo walifika Dukani! Walipaki gari pembeni. Duka lilifunguliwa Jolvin ndio alianza kutoa bei ya nguo! Huku Gorii akiwa anaandika, baada ya kumaliza kuelezea kila nguo na bei yake ilibidi akague kitu alichooandika Gorii”

Alichukua lile daftari mwishoe aliamua kucheka tu.

“” Kwamba umechora mtu pamoja na hio nguo kaivaa, ukaona haitoshi Hadi rangi ukaandika Kama ni suruali, shati, gauni, tisheti, vibode pamoja na aina za rangi yake?”

Esau, Joely na Bibi pia walisogea kutizama kila mtu alibaki kucheka tu!

Gorii yeye alibaki kuwashangaa!

“” Mbona kitu Cha kawaida tu nimefanya!”

Mwisho kabisa aliona Kama ni fedheha aliwanyanganya Daftari lake Kisha alienda kukaa nje aliwaachia wafanye wao Kama wao.

Wakati amekaa pale alianza kutizama maduka yaliyo karibu! Jinsi wanavyouza nguo! Juu ya Maduka yao kulikuwa na mabango yamewekwa na baadhi ya huduma zinazotolewa pale, aliangalia juu ya duka lao! Ndio anaona bango kubwa akiwa yeye, Jolvi pamoja na Bibi wakiwa wamevalishwa nguo nzuri kulingana na umri. Hakuamini macho yake make alikuwa kapendeza kuliko anavyovaaga, alimtizama Bibi nae kapendeza kweli Kisha alimalizia kwa Jolvin.

“” Kaka White huwa hapendi kucheka! Ila hapa kacheka vizuri, akifika Nyumbani kimya, halafu anazira, daah!”

Alipiga makofi Kama tabia yake ya kujipongeza, akifanya kitu kikafanikiwa! Alimuita Bibi huku akikimbia ndani kulikuwa Kuna mziki umeachiwa taratibu! Aliongeza sauti akaanza kucheza kwa furaha, Kuna furaha ilimuijia hata hakuelewa imetoka wapi!?

Wote walibaki kumshangaa jinsi anavyofurahia! Baadae alimshika Bibi acheze nae make ilikuwa ni nyimbo ya asili zilikuwa zikichezwa zamani, Bibi nae akaona wee! Kuliko kuvunga acha ajiachie.

Watu waliokuwa wakipita pale walibaki kushangaa na kusababisha watu wazidi kusogea pale! Walianza kujaa huku kila mtu akisoma bango lilokuwa pale walijua ni duka jipya limefunguliwa bado ni la familia ya mtu maarufu Mishoki, walianza kujazana dukani kila mtu akiulizia nguo na kununua atakavyovutiwa nayo, Wakawa wamepata wateja wengi kupitia furaha ya Gorii.

Kunae mapapalazi wao huwa hawapitwi kitu walichukua baadhi ya matukio yaliyoendelea pale huku wakipost crip ya video Bibi na Gorii wakicheza, hii iliwavutia sana! Kwa mtu alioiona Crip ile alitoa comments anatamani afike kwenye duka hilo siku moja anunue nguo pale.

Huku kwa mama akiwa yupo kazini hana hili wala Lile, alipokea Crip ya Gorii pamoja na Bibi wakicheza alibaki kucheka Kwanza, ndipo akaamua kufatilia kipi kimejili! Alifunga Safari ya kuja dukani ajue kipi kimeendelea ndio anashangaa kukuta watu wamejaa huku waandishi mbalimbali wakimhoji Gorii! Ilibidi abakie ndani ya Gari kuogopa jamu ya waandishi wangempotezea muda Kama atawasikiliza.

Alimua kuondoka akiwa na furaha huku akiongea pekee.

“” Furaha ya Gorii! Leo naitimiza kwa niaba ya Binti yangu! Nilimpenda Sana lakini Mungu alimpenda zaidi! Naimani Gorii kaja kwa niaba ya Mwanangu Naina! Daima alikuwa ni mcheshi! Aliipenda familia yake! Kutimiza wajibu ilikuwa ni jukumu lake, naiona nafisi yake ipo ndani ya Gorii”

Huku Gorii Baada ya kumaliza kuhojiwa, waandishi walihitaji picha ya pamoja wakiwa na Bibi, Jolvin pamoja nayeye! Taarifa zake zikawa zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ule ucheshi wake hasa katika kazi yake!

Siku hiyo waliuza kalibia mzigo! Wote majira ya jioni walitoka pale wakiwa wapo hoi, lakini walikuwa na furaha kila wakikumbuka kilichotokea pale walibaki kucheka.

“” Bibi kumbe na Wewe huwa ni mtaalamu wa kucheza, Mimi nilifikili ni wale wa Bibi wa kihindi wanavyochezaga nachi! Kumbe ni Bibi wa kitanzania!?”

Joely alimtania, lakini muda huo Jolvin na Essau walikuwa busy wakisoma comments kwenye peji zao za Instagram, baada ya kupost Crip ya Gorii akicheza. Jolvin aliipost huku kaipa kipaumbele kaandika

“” Dadake na Kaka White! Akiwa kwenye harakati za kutimiza wajibu”

Comments zilizomiminika ni watu wengi walitaka namba ya Gorii! Wengine waliomba wafanye nae kazi kwa kuwatangazia biashara zao! Wengine walionesha kumtaka Gorii kimahusiano,Jolvin aliwaachia namba zake Kama watamhitaji Gorii kikazi.

Baada ya kufika Nyumbani Gorii alikuwa hoi! Mamake Alifika huku akiwa na furaha kuna zawadi alimletea huku akimshukuru sana, furaha aliyokuwa nayo ilimfanya mpaka atokwe na machozi, alimkumbatia Gorii Kisha alimshika usoni huku akiongea nae.

“” Wewe ni mrithi wa Binti yangu Naina!? Kila unachokifanya unanitia nguvu Mimi mamako niendelee kupambana kwaajili yako!”

Kila mtu alisikia vizuri maneno ya Mama, hutaamini baada ya kusikia jina Naina, kila mtu aliinamisha kichwa chini huku akijawa na simanzi Ghafra.

Gorii hakuelewa baada ya kuona watu hawana furaha, aliwaona hata watoto wakiume wakipikicha macho yao! Ishara kunae huzuni inayowatoa machozi na yeye alianza kulia, yeye kamkumbuka Mamake anatamani hata angekuwepo akamwelezea jinsi familia inavyopambana kwaajili yake! Angejisikia furaha Sana.
 
Baadae alinyamaza Baada ya kuona watu wote wakimtizama yeye! Aliinua kichwa akiwatizama Kisha aliongea.

“” Mama! Nashukuru Sana kwa kunifanya niwe binti yako! Mamangu alikuwa akinipenda Sana! Muda wote alitamani nitimize ndoto yangu, kutokana na mazingira aliniahidi siku moja nitaishi maisha ya kawaida Kama hatotimiza malengo yake ila maisha yawe ya kati! Kutokana na maisha ya kijijini! Mama alinipatia mtaji wa kuuza mboga mboga! Kwa yale maisha sizani Kama tungetoboa! Muda mwingine nawaza huenda zile pesa alizozichukua ni kwaajili yangu.

Gorii aliweka kituo Kisha aliendelea kulia, Mama ilibidi amshike mkono akimpeleka Chumbani Kwake.

“” Basi pumnzika! Leo umefanya kazi kubwa Sana! Usiendelee kuumiza kichwa! Kila kitu kitakaa sehemu yake! Nashidwa hata nikushukuru vipi kwa kazi uliyoifanya! Mungu akubariki mwanangu.

Siku iliyofuata Esau, Joely waliondoka wote wakirudi chuoni na kazini, Nyumba ikawa imebakiwa watoto wawili Jolvin na Gorii! Siku hiyo hiyo Gorii aliingia chuo Cha maendeleo! Alipelekwa na mama kuripoti, Jolvin pia alielekea chuoni.

Huku kimbembe kwa Gorii kilianza, Baada ya kukabithiwa kwa mkuu wa chuo alielekezwa darasa lilipo.

Kunae mwalimu wa darasa alikuwa akifundisha, Kama kawaida Mwalimu mara nyingi hukalili wanafunzi wake! Siku hiyo aliona sura ngeni ilibidi amsimamishe Gorii.

“” Wewe binti! Naona ni mgeni hapo! Majina yako unaitwa Nani? Na unatokea wapi?”

“” Gorii Goryanah! Natokea ndani ya huu mji.”

Wanafunzi wote waligeuka kumshangaa ni jina geni hawakuwahi kulisikia, ilibidi wacheke. Gorii hakupenda ilibidi awageukie kuongea nao.

“” Ndio Wazazi wenu wamewafundisheni hivyoo! Kwani jina Gorii ni jina lakushangaza sana mpaka mcheke! Hamna adabu kabisa!”

Wote walikaa kimya wasiamini Kama Gorii ni binti jasiri anaweza kuwajibu vile! Mwalimu mwenye alibaki kufurahi baadae alimuuliza tena Gorii.

“” Umesema waitwa Gorii Goryanah! Mbona usajili wako umesajiliwa Goryanah Mishoki.”

Gorii ndio anakumbuka kuwa kwasasa yeye ni familia ya Mishoki, ilibidi acheke kwanza Kisha aliomba msamaha kwa Mwalimu.

“”I’m sorry! Niliwatania tu ili wafurahi si wamecheka! Wengine wakaanza kunisema chini chinichini! Anyway wanizoee tu!?”

“” Unapenda kingeleza Sana!?

Mwalimu alimuuliza Gorii, lakini alibaki kutabasamu ukimuuliza zaidi hajui zaidi ya kuibia ibia tu.

Huku kwa nyuma Kuna wanafunzi walianza kusema chini chini.

“” Huyu si ndio Mjukuu wa Mishoki! Halafu majuzi kati wamefungua duka la fashion new clothes! Kame trend kweli mtandaoni.

Kuna baadhi ya wadada walisogea karibu huku wakiangalia ile video aliyokuwa akicheza! Wakaiachia kwa sauti! Kuna mkaka mmoja alisimama huku akimnyoshea mkono Gorii”

“” Wewe si ndie Gorii wa fashion clothes! Huku umeijia Nini Sasa wakati unakipato chako!?”

“” Heeeee! Nyie kimya! Mwalimu hebu endelea kufundisha!”

Gorii alirudi kwenye seat yake akakaa vizuri kusikiliza! Baada ya kipindi kuisha Gorii alibaki anamanga manga! Aliona kila mtu yupo busy na mambo yake! Wengine walikuwa wakifanya discussion! Jinsi ya kujiunga nao ikawa ni mitihani.

Alishika simu yake ndogo ili ajifurahishe ndio anatazama wenzake wanazo simu kubwa! Alibaki kujishangaa mwenyewe!

“” Daah! Mjini shule na shule inaanzia hapa! Yaani mabinti wadogo wadogo wapo busy na simu! Wengine wapo na mabwana hata hawahurumii Wazazi wao!”

Wakati amekaa pale Kuna vijana wawili walifika wakavuta kiti Kisha wakakaa mbele yake wakimtumbulia mimacho. Gorii nae Kama ni utundu utundu aliuzoea, ndio alikaa vizuri akawatolea jicho pasina kupepesa.

Kuna Kijana wa kwanza aligonga meza kwa nguvu, Gorii nae akafanya vile kisha alisimama akacheka huku akiwapatia mkono.

“” Tukubaliane!! Mimi napenda nyie muwe marafiki zangu make napendaga watu wenye akili Kama zangu!”

Walitazamana kwanza Kisha walimcheka.

“” Unatujua kwanza? Unaonekana ni binti jasiri halafu unajiamini Sana! Ila tuulizie kwanza “Shidy gang” ni kina Nani!?”

“” Oooh! Mbona inafurahisha Sana! Mimi nimetaja jina langu leo watu wote wakacheka! Mimi naitwa “” Gorii Goryanah” jeshi la mtu mmoja hili nyie mpo wangapi mniunge huko!?”

Ilibidi waondoke kwanza walijua wameingia Cha kike, binti mwenyewe hamnemo ila bomba niaje!”

Muda wa Lunch ulifika Kama unavyomjua kwa Gorii hawezagi kuvumilia njaa labda vingine ndio atavulimia.

“” Kaka White alisema analeta chakula! Muda umeenda hata haji kuniulizia kwa mkuu wa chuo! Sa nitakula wapi leo?”

Ghafra simu yake iliita ilibidi apokee.

“” Uko wapi!?”

“” Nani wewe! Sijakupata!?”

“” Kaka White!!”

“” Ooh! Sauti ni yenyewe kabisa! Halafu una namba yangu kumbe!?”

“” Acha maneno! Nipo nje ya geti hapa! njoo uchukue chakula!”

Gorii alitoka mbio, mpaka wanafunzi wenzake walibaki kumshangaa anavyowapita fulu.

Baada ya kumuona Kaka White! Ilibidi ashushe pumnzi kwanza huku akicheka.

“” Nusura nivunje mguu! Yaani nimepamiana na hao watu nahisi nikishiba nitaenda kujieleza kwao! Watu wa hapa hawanaga dogo!”

Jolvin alibaki akimtizama kupitia kioo, alimfikilia kwanza Kama hajafanya tukio leo sijui tu!

Muda huo huo alitokea mdada akamshika mkono.

“” Kanishonee begi langu! Hunaga break kwenye miguu yako? Sasa.. kashone begi langu!”

“” Wewe tulia kwanza nile nishibe ndio tuongee! Muda ule nakupita si ulikuwa una nguvu halafu umeshiba, ungenipisha tu!?”

“” Kajeuri kweli haka kamdada! Leo tu kametunyamazisha tukae kimya utazani ni kakubwa! Halafu ana majibu mabaya huyu.

Dada mmoja alikuwa akipita baada ya kumuona Gorii, ilibidi asogee make ni classmates mwenzake.

Jolvin ilibidi ashuke kwenye gari, Kisha alimshika mkono Gorii akiwageukia wale wadada.

“” Wewe mwenye begi Kushonesha huo mkanda, ni shingapi!? Halafu na wewe endelea na Safari yako! Namjua vizuri Gorii huwa anaongea point huenda kweli mlikuwa mkipiga kelele darasani, lazima awanyamazishe huwa hapendi makelele isipokuwa utulivu tu!”

Alitoa elfu tano akampatia mwenye begi lake akashone Kisha waliingia kwenye gari na Gorii akaanza kula.

“” Umefanya Nini huko darasani!?”

“” Kaka White…!! Nitakuelezea nishibe kwanza..!”

“” Mhuu…!!”

“” Nimeshiba sasa!! Ipo hivi nilijitambulisha darasani nikasema naitwa Gorii Goryanah Wakacheka na Mimi nikawanyamazisha wakae kimya kwani maajabu pale ni kusema naitwa Gorii Goryanah!? Mimi nimekosea wapi?”

“” Hujapigana? Make huwa unajiona unae nguvu nyingi zakuingia ulingoni.”

“” Nimekua sahii! Wewe si bado unawapiga watu makofi!?”

“” Hebu nitazame vizuri..!!?”

“” Nini tenaa…!?”

“” Hapo sawa! Nikahisi unae kidonda usoni! Halafu leo jioni tutaenda kupromote tangazo la biashara Mimi na wewe! Kuna mshiko mzuri ila Mimi nitafanya kukusaidia tu! Wao wanataka ma partiner wawili nafasi hiyo nitaichukua Mimi ili upate pesa!”

“” Na Bibi je!?”

“” Unataka uende nae?”

“”Je, Dukani!!?”

“” Ni baada ya kufunga! Make utaenda kufanyiwa Makeup ya live! Ile siku si walikuedit kwenye lile bango ukaona umetoka, leo ni live!”

“” Unafikili nitaweza kweli! Ungekataa tu, make nitaogopa! Na namba walitoa wapi!?”

“” Kwenye page yangu Instagram! Niliwaambia Kama watakuhitaji kikazi wanitafute Mimi!”

“” Hapo sawa! Halafu Simu yako inaita! Mbona hupokei!?”

Jolvin ilibidi aifunike na kitabu! Kisha aliendelea kuongea na Gorii.

“” Itakuwa ni Anelisa huyo! Pokea bhana huenda Kuna shida!?”

“” Nambie Anelisa!!! Nilikuwa busy kidogo darasani! Kuna shida lakini mbona unaongea kwa shida hivyoo!?”

Gorii ilibidi avunge hasikilizi mazungumzo yao, alianza kupekua kitabu Cha Jolvin akikagua kila page.

“” Umesema unaumwa kifua tena!? ” Vipi khari? Umetumia dawa lakini!?”

“” Nimetumia lakini bado! Nampigia mama nae kasafiri yupo kikazi! Baba nae yupo busy na kazi! Nakuomba basi kesho nenda nyumbani mpatie simu mdada wa kazi nimpatie maelekezo akupatie dawa Kisha uniletee chuoni!”

“” Sawa’ nitafanya hivyo hakikisha unaendelea kutumia dawa za maumivu! Kesho kwenye mida ya mchana nitakuwa hapo!?”

Baada ya kukata Simu, Gorii alibaki akicheka huku akijifanya busy anafunua kitabu! Jolvin aliamua kukifunika Kisha alimgeuza Gorii amtizame vizuri.

“” Si unanicheka Mimi! Anelisa huwa anaumwa kifua! Huwezi ukawa na huruma nae?

“” Muongo huyo! Eti anaumwa kifua! huyo analake jambo!!” “Kaka White… Naona umemisiwa na rafiki mpenzi!”

“” Nenda kwanza chuoni! Hunaga upeo wa kufikili katika matamshi yako “

Gorii aliondoka huku akiongea pekee.

“” Huyu Anelisa anafanya kila namna ampate Kaka White..! Namimi sitokubali nitafanya kitu ili asiende! Ingekuwa ana moyo safi ningemuachia aende!”

Majira ya jioni walikuwa wameshafunga Duka, Jolvin alienda kuongea na Bibi akawa amewaruhusu waondoke wote!

Walifika Hadi sehemu wanapofanyia tangazo, Gorii alianza kubadilisha mwendo huku akijificha ficha! Wadau baada ya kumuona walimuwahi make alikuwa tayari ameshajulikana kutokana na like tukio.

Aliingizwa chumbani kubadilisha nguo huku akifanyiwa makeup ya kutosha mwisho kabisa aliletwa sehemu ya kuchukuliwa picha, alitazama upande wa pili ndio anatokea Jolvin akiwa ameupara balaa, kila mtu alibaki kumtizama mwenzake asiamini alivyopendeza.

Modo wao alisimama huku akiwaongoza jinsi ya kupiga pozi kwa kujiachia.

”” Jolvin sogea ukae nyuma ya Gorii! Mshike kiunoni fanya Kama unataka kumkisi! Ewaa happy imekaa vizuri! Pozi la pili fanya Kama unataka kumdaka”

Tukio la pili lilichukuliwa! Baadae yakafatia mapozi mbalimbali wakiwa kwenye nguo tofauti!

Baada ya hapo walisaini wakapatiwa pesa yao! Safari ikaanza kurudi nyumbani! Huku Njiani kila mtu alianza kufikilia yale mapozi yalimfanya amuonee aibu mwenzake! Mpaka walipokalibia nyumbani Jolvin alitoa ile bahasha akamkabizi Gorii.

“” Pesa yako hiyo! Utaifanyia kitu unachokitaka!”

Gorii alichukua Bahasha akatizama pesa iliyopo, alichoamua alichukua nusu ya pesa akampatia Jolvin.

“” Wote tulishiriki! Kila mtu achukue nusu!””

Jolvin aliichukua ile pesa akatoa kiasi Kisha akairudisha tena kwa Gorii.

“” Sitaki unirudishie tenaa! Mchezo huu uishie hapa!”

Muda huo walifika nyumbani kila mtu aliingia chumbani Kwake!

Huku kwa Gorii” alibaki akiihesabu ile pesa huku akifikilia namna ya kuifanyia.

“” Pesa zote hizi! Hapa nitafanya kuzituma kijijini kwa Mama Muddy angalau wakarabati nyumba nipate pa kufikia!

Alilala kitandani huku akivuta picha ya muda mfupi akiwa na Jolvin, Yale mapozi ya hapa na pale yalimchanganya.

“” Haya mapozi si huwa ya faragha mtu na mpenzi wake ndio hufanya vile!? Mbona Jolvin kafanya Kama mimi ndie Anelisa wake!”

Vilevile huku kwa Jolvin moyo ulikuwa kwatuu, kila akifikilia jinsi picha zilivyopigwa alitamani iwe Kweli. Kila akijaribu kulala aliona hakulaliki alichukua Simu yake akampigia Esau huwa anamwelewa Sana japo ni Mtoto wa ba mkubwa walizoeana kuliko hata Ndugu yake Joely ambae ni wa damu.

“” Mmetutenga bhana huku! Hata hamumuulizii Bibi, Mama Gorii! Mpaka tunawamisi.”

“” Mama nishaongea nae! Bibi kila siku! Kwa Gorii simpati kwenye simu labda nikuulize wewe mtu wa karibu nae, anaendeleaje?”

“” Mzima tu! Kashaanza vituko vyake huko shuleni Kesi haziishi, mara kakata mkanda wa begi, mara kawajibu watu vibaya! Yaani ni shida tu!”

“” Leo nakuona umeongea kuhusu Gorii vizuri, na siyo kwa kumkalipia Kama siku zingine, inaonesha umeanza kumzoea tabia zake! Vipi Anelisa anasemaje!?”

“” Hapa nawaza keshoo…!! Alikatisha kwanza kuongea make alikuwa anaenda kuropoka kuhusu Anelisa! Kama akimwambia anaenda kwa Anelisa! Esau atalisanua kwa Bibi.

“” Nilitaka kukwambia.. kesho nataka nikahemee mzigo! Si Unajua dukani kumepungua! Kuhusu Anelisa yeye mzima tu..!”

“” Sawa!! Ila umeshamwambia Gorii! Unavyojisikia Kwake?”

Jolvin ilibidi ashushe pumnzi kwanza, alifikikilia kumbe Esau analitambua hilo, hapana lakini nitakuwa nimewaza tofauti, Ile anataka kumjibu Esau alikata Simu aliitiwa kazi.

Kesho yake Jolvin alikuwa kajiandaa Asubuhi aondoke, muda huo Alifika Bibi akimuita Jolvin kuwa Gorii anaumwa tumbo linamsumbua! Ilibidi aweke begi kukimbia chumbani Kwake!

Alimkuta akigalagala kitandani huku kashikilia tumbo akiliminya.

“” Gorii! Goryanah! Shida Nini Mama!? Ni tumbo linakusumbua!?”

“” Kaka White.. tumbo linanisokota Kweli!!?”

“” Sasa hukusema Kama huwa linakusumbua! Tukakutafutia tiba mapema! “Bibi amekula chochote huyu!?”

“” Hapana labda tumuulize!?”

“” Goryanah!! Usilale ngoja nikuletee dawa za maumivu.

Baada ya kutoka tu Gorii akawa mzima! Alimtizama Bibi yake Kisha aligonga tano misheni yao imeenda vizuri.

Wakati anarudi Bibi aliekiti kapigiwa simu na mteja anataka nguo yake aliilipia! baadae alikata Simu akawa amerudi kwa Gorii'”

“” Mjukuu wangu sijui nitakuacha na khari gani!? Wateja wanataka nguo zao! Duka limefugwa pia! Isitoshe huu ni msimu wa chrismass.”

“” Bibi wewe kafungue! Gorii akikaa sawa nitakwambia!”

Bibi alisogea karibu huku akidai anamuaga Gorii, alimtizama Jolvin ambae kachukua Simu akimpigia Doctor aje.

“” Bibi Doctor tenaa! Kuna sindano zinafata hapa!?”

Alifanya kuongea chini chini lakini Bibi alimpatia mbinu akawa ameondoka pale.

Baada ya kukata Simu, ilibidi akae akimtizama Gorii ambae alifunga macho akidai anausingizi, Kama angebaki macho angejikuta akicheka!

Jolvin aliamua kujiegesha kitandani huku akizidi kumtizama Gorii, akizania amelala! Aliamua muda huo kumtizama vizuri! Unaambiwa mtu akishalala ndio utaujua uzuri wake halisi kwa kumtizama.

Alibaki akimtengenezea nywele! Zilizokuwa zimesasambuka kuelekea usoni alifanya kuzirudishia vizuri huku akibaki akitizama Rip’s za midomo yake, baadae alijiegesha pembeni yake huku mkono wake akiunganisha na vitanga vya Gorii, aliongea maneno machache huku akitizama pembeni!

“” Nahisi kukupenda Goryanah!”

Gorii sauti ilipenya masikioni mwake, mpaka akahisi joto nimezidi nyuzi kadhaa!

Jolvin alisituka huku akifikilia huenda kasikiwa na Gorii! Lakini ndio Gorii anageuka upande wa pili huku akiongea pekee.

“” Leo ndio nitakoma! Naona nimechokoza nyuki kwenye mzinga wake!”

Jolvin alipokea Simu kutoka kwa Doctor kuwa kafika, Alishuka kitandani kumpokea Doctor!

Baada ya kutoka Gorii alishuka haraka akaurudishia mlango huku akishusha pumnzi ndefu huku akizunguka chumba akitafuta namna ya kumkwepa Doctor!

“” Mbona tukienda hospitali huwa tunaenda wazima lakini tukipimwa tunaambiwa tunae Malaria au UTI lazima na Mimi niambiwe vile!”

Alifungua mlango Kisha akarudi kitandani, alimsikia Jolvin akimwelezea Doctor.

“” Ni tumbo la ghafra tu! Limemkamata ameteseka kweli! Nimemkuta kitandani akiweweseka kwa maumivu! Fanya umsaidie haraka Doctor! Akipata nafuu Kuna sehemu naondoka itabidi niende nae Kama khari haitabadilika, na hii ni kwa usalama zaidi
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO



Doctor alimuasha Gorii! Baadae alimuuliza.

“” Kichwa kinasumbua pia? Halafu unaonekana Kuna Jambo linakusumbua, mapigo yako ya moyo yapo juu Sana!”

Alimaliza kupima akamgeukia Jolvin ili ampatie majibu!

“” Mgonjwa wako anaonekana mapigo ya moyo yapo juu! Na ndio imechangia kuumwa na kichwa! Kaa nae vizuri huenda ana stress ndio inachangia awe hivi! Kuhusu tumbo huwa ni kawaida ya wanawake wakikaribia kwenye siku zao wengi wao huwa wanaugua, ila utampatia dawa za maumivu atakuwa sawa!”

Doctor alimaliza kuongea huku akichukua vifaa vyake akisindikizwa na Jolvin!

“” Oooh!! Afadhari nimesalimika! Hapa Kaka White hataondoka kwa khari hii!”

Jolvin alirudi huku akiwa na sahani ya chakula aliweka mezani.

“” Unaweza ukatembea hadi mezani!?”

Gorii alifikikilia Kwanza Kama atasema ndio, Jolvin atajua anaendelea vizuri ilibidi asingizie mwili hauna nguvu. Jolvin ilibidi amletee huku akimshikilizia sahani ale, baada ya kula alibaki amekaa pale huku akiangalia simu yake masaa yanazidi kwenda.

“” Unachelewa kwa Anelisa!!?” Gorii alimuuliza.

“” Aa aa! Unajua Anelisa anaumwa ilitakiwa nikachukue dawa kwao nimpelekee! muda nao unazidi kwenda sijui hata nafanyaje!?”

Gorii ndio anageukia upande wa pili huku akivuta shuka, akiambatanisha kikohozi Cha kutafuta baada ya kujua Jolvin bado anawaza Safari..

“‘ Goryanah!! Usilale basi! Kaa tuzungumze basi simama nikwambie!”

Simu ya Goryanah iliita alikuwa ni Bibi, Jolvin aliwahi kuipokea.

‘”‘ Bibi bado hajawa sawa naona anazidi kukohoa! Ila nimempatia dawa Wewe usijali endelea na kazi Mimi nitamhudumia.”

Baada ya kukata, simu yake ilipigiwa na Anelisa, alibaki akimtizama Gorii make mlio wa simu yake ulisikika, Gorii aliamua kumjibu.

‘” Kaka White!! Naona Kama nakusumbua Wewe nenda tu! Nitakuwa sawa! Hata hivyo Mamangu alipenda kuniambia nikiugua lazima niyazuie maumivu hata kwa kufanya kazi kuliko kulala! Hapa nataka nifue fue nguo zangu! Naamini nitakaa sawa”.

“” Hapana Gorii! Wewe unaumwa hauwezi ukalazimisha ukafanya kazi ngumu! Basi Mimi nitashinda na Wewe siku mzima, kwa Anelisa sitaenda tenaa, si unaweza kujiandaa twende wote sehemu! Jana wakati natoka pale Kuna nguo ulivaa ukapendeza Sana niliamua kuichukua basi utavaa hiyoo! Ila umepona Kwanza make ninakokupeleka kunae makelele!?”

Gorii baada ya kusikia kaailisha Safari ya kwenda, huta amini alijisau kabisa Kama ni mgonjwa aliamka na kukaa huku akimtizama Jolvin!

“Dakika tano tu nimemaliza kujiandaa”

Jolvin alitoka anacheka, aliingia Chumbani Kwake akamletea gauni Kisha alimsubili sebuleni. Baada ya Gorii kumaliza kuoga alivaa ile gauni ilimtoa vizuri! Ikamfanya hata Yeye asikatike kwenye kioo muda wote ni kujigeuza geuza mithili ya kambale awapo kwenye maji, Alianza kutembea kwa madaha taratibu Kama umemuona Afisa masoko toka Bank akishuka ngazi!

Alitoka taratibu huku akichungulia Kama kunae watu sebuleni, baada ya kujilizisha ndio alipita taratibu hakutaka hata wadada wa kazi wamuone! Alipiga hatua Kama mbili ndio anasikia sauti ya kidume ikimuita alibaki kasimama huku akimsikilizia afike.

“” Waoo ur so beautiful! Yaani umependeza sana., Kisha alimshika mkono kuelekea kwenye gari!”

Walipanda gari kuelekea kwenye hotel moja! Siku hiyo kulikuwa na Sherehe ya mwanafunzi mwenzake na Jolvin kutimiza miaka kadhaa. Kuna wanafunzi wengi walikuwa pale!

“” Kupendeza umependeza ila usiniaibishe! Naomba ukae sehemu moja halafu tulia na Mimi!”

Gorii alibaki kumtizama tu, Kisha alivuta kiti akakaa! Walichukua vinywaji huku wakiendelea kuangalia maigizo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea mbele.

“” Gorii.. !! Jolvin alimuita.

“” Aa Kaka White! Wanafanya maigizo mazuri! Mwangalie yule mkaka kachukua uhusika Kweli.”

Jolvin aliamua kumvuta mkono make hata kumsikiliza hamsikilizi yupo busy kuangalia mbele.

“” Ndo unakuwaga busy kiasi hiki!? Unapenda furaha Sana? ” Kuna kitu nataka nikuulize, Kwanini ulidanganya kuwa waumwa? hukutaka niende kwa Anelisa?”

“” Mhuu! Aa aa.. naumwa tumbo, kichwa! Halafu kumbe hukutaka nipone!?”

“” Swali…. Kwanini hutaki niwe karibu na Anelisa!? Kuna shida Mimi nikiwa nae?”

Gori alikuna kichwa Kwanza huku akiangalia upenyo wa kutoka pale, ikiwezekana aelekee bathroom!”

“” Unataka kunikimbia? Wewe nakujua vizuri! Najua ulipanga na Bibi! Sawa’ najua Bibi huwa hampendi Anelisa ndio, ndio hadi kwenye ugonjwa? Kwaajili yako nimezima simu ili Anelisa asinipate sijui hata ananifikilia Nini mtoto wa watu huko aliko!? ” Kama unafikili nikienda kwa Anelisa ni sababu nampenda Mimi sipo hivyoo!?”

“” Aaah! Kwani ni ugonvi Kaka White! Ishatokea bhana! Wewe tafuta njia nyingine na sio kunilalamikia hapa!”

“” Ee… Unasemaje make unang’ona chinichini!?”

Gorii alijua kubananishwa mpaka alihisi joto mwili mzima, aliwaza Kama ataendelea kumjibu ile tabia ya kuzira inaenda kutokea muda huo. Aliamua kufunga macho Kwanza baada ya kuona mawenge huenda Kofi linaenda kutua usoni, alishikilia shavu zake kwa mikono miwili Kisha alisema;-

“” I’m sorry.. Kaka White! Yote nimefanya ni kwasababu simwamini Anelisa huyu ni muongo kwako atakusababishia matatizo! Wewe niamini Mimi na usiende kumwambia mama kwa hiki kilichotokea! Mama ataanza kunichukia Mimi!”

Ile anakuja kufungua macho anakuta kiti kipo wazi lakini Simu ya Jolvin ilikuwa pale! Aliangaza huku na kule hamuoni mtu alichukua Simu ya Jolvin akawa anaikagua kila sehemu huku akiibonyeza! Kwa bahati mbaya aliiwasha, alianza kutetemeka huku akitizama sehemu ya kuizima kabla hajakutwa.

Message za Anelisa zilianza kumiminika, alianza kuzisomea kwa juu wakati zinaingia.

“” Jovii.. sikutegemea Kama ungenifanyia hivi leo? Mimi naumwa, kukwambia uniletee dawa ndio kosa langu?”

“” Jovii… Au unaniogopa baada ya kukwambia nakupenda! Unahisi ukija huku nitalazimisha unipatie majibu?”

“” Jovii… Au ni kwasababu ya huyo Binti wa kijijini! Ulivyompeleka nyumbani kwao Kuna kitu kiliendelea?”

“” Jovii… Siku yenyewe kabla sijakwambia nakupenda.. ndio ulitaka kuniambia unae mtu unae mpenda Kama si Gorii ni Nani huyo!?”

“” Kweli naumia Sana Jovii.. kwa ulichonifanyia huenda ni makosa yangu kukwambia ukweli wangu, au ulitaka niendelee kukuficha Hadi lini!? Ni kitu ambacho siwezi kukivumilia, naumia Jovii…

Gorii alimaliza kusoma Kisha alishusha pumzi ndefu, baadae alicheka Kwanza.

“” Huuu! Joviii… Naumia sana, au kwakuwa nimekwambia nakupenda ndio waniogopa? Jovii.. Daah! Anelisa huyu ana mambo yaani anajua kulalamika huyu! Kidogo tu Jovii…. Mhuu! Kupatwa kwa Kaka White, sa’ sijui ni ya kweli? Anyway watajuana wao.

Muda huo Jolvin ndio anafika pale alimkuta Gorii kaiweka Simu Kisha yupo busy na kitochi chake akicheza Game huku akicheka mwenyewe kana kwamba anafurahia sana.

Jolvin alimtizama Kisha akaangalia Simu yake imegeuzia kwa nyuma, alimtizama tena Gorii Kisha alishika simu yake ile anaigeuza anabonyeza aishike vizuri anakutana na mwanga.

“” Sheat!! Ndio Wewe umefanya hivi!? Gorii niseme kipi unielewe!? Nimezima kwaajili ya Anelisa, ona Sasa anapiga Simu hapa, shika umpokee!”

“” Kaka White! Mtoto wa Mishoki family” “unatizamwa hapo!?”

Jolvin ndio anageuka upande wa pili ndio anaona watu wote wamemtolea macho, ilibidi awe mpole alikaa huku akiendelea kusoma message za Anelisa.

“” Sherehe imemalizika, Twende nyumbani!”

“” Mbona badoo!!?”

“” Weee!! Unaenda huendi!!?”

“” Basi twende!!”

Baada ya kufika kwenye Gari, Gorii aliogopa kukaa mbele alikaa nyuma, Jolvin aliishia kumtizama baada ya kuona kafunga mlango aliondosha gari kwa speed Kali hadi walipofika nyumbani, alishuka kwenye gari Kisha alimshika mkono Gorii hadi chumbani Kwake akafunga Mlango.

“” Unajifanya kuogopa!? Wakati kwenye hiki chumba Ushawahi kuingia kabla! Ilikuwa ni masaa tu Mimi kufika ukaingia humu, halafu leo hii waogopa kukaa humu! Leo utalala humu.

“” Hapana! Hapana… Kaka White! I’m sorry! Naomba uniache niende sio tabia nzuri kukaa chumba Cha mkaka! Nitamwambia Bibi pia akuombe msamaha tulidaganya!”

“” Mhuu! Leo unaogopa kukaa kwenye chumba Cha wanaume! Siku ile chumbani kwa Rich ulifata nini! Au mnae Mahusiano hadi uingie!”

Gorii alishidwa kujibu ilibidi aanze kulia, alikumbuka siku yenyewe Jolvin amkalie kifua wazi, mara amwangukie hapo akajua ameisha.

Jolvin alibaki kumtizama Kisha alivuta kiti akakaa mbele yake.

“” Nijibu maswali yangu Kwanza ndio uondoke! Nataka uniambie ukweli!! Je, ulisoma message za Anelisa!?”

Gorii alifanya kukataa! Jolvin alifanya kurock mlango Kisha funguo akaweka mfukoni, Alimrudia Tena Gorii.

“” Namjua Gorii huwa ni mkweli! Yeye hadanganyi! Narudia tenaa… Ulisoma message!? Kwanini uliiwasha Simu!?”

“” Aaa… aa.. Niliwasha kwa bahati mbaya baada ya kuona umeondoka pasina kuaga ndio nikachukua Simu yako, kwa bahati nzuri Message zikaanza kuingia kwa juu nikawa nasoma ila sio zote!?”

“” Unajua kuongea ukweli ee! Baada ya kusoma ukachukua maamuzi ganii!?”

“” Nikaigeuza Simu! Nikaiweka mezani! naomba unisamehe tu.. ila Anelisa anajua kulalamika yule..'”

Jolvin aliamua kurudisha Kwanza kiti sehemu yake! Kisha alichukua funguo akafungua mlango.

“” Ayaa simama kwanza!”

“” Ahsante Kaka White… kwa kutonipiga! Niliogopa sana.””

“” Rudi hapa… Umeona ulivyosimama umepaachaje? Basi tandika kwanza.

“” Nimemaliza Mjukuu wa Bibi… Siku ile ulisema nisikuite Kaka White! Leo nimetengua kauli.

Jolvin alibaki kumtizama asiseme chochote, alifungua mlango akaushikilia huku akimwachia atoke.

Ile kutoka Gorii alikimbilia Chumbani Kwake akajitupia kitandani akifanya kugalagala kwanza, Ghafra mlango uligongwa alikuwa ni Jolvin.

“” Kaka aa. W.. sorry! Mjukuu wa Bibi’ si yameisha tenaa! bado unanifuata tu?”

Jolvin alifanya kumpatia simu yake muda ule aliisahau kitandani.

“” Thank you!”

Usiku Bibi alifika kutoka kazini alikuwa amechoka Sana! Jolvin baada ya kumuona Bibi kafika alimletea kinywaji kwanza atumie huku akimpa pole na majukumu.

Gorii muda huo alikuwa akichungulia akiangalia Jolvin atamwambia Nini Bibi! Kila akichungulia aliona wanaongelea maada za biashara! Baada ya kuona hamna dhari alitembea kwa kunyata akaingia jikoni kusaidiana na wapishi!

Mama nae muda huo alifika, alimuita Goryanah amletee Maji ya kunywa.

Huku kwenye hifadhi ya vyakula Gorii alikuwa tayari kabebelea maji kutoka kwenye frigi alianza kuzunguka muda wote akiwaza jinsi atavyo peleka maji sebuleni, aliweka jagi kwanza Kisha alikimbia kuchungulia ajue Jolvin kakalia upande upi ili amfikie Mama.

Wakati anachungulia Jolvin alikuwa katoka! Alirudi haraka akachukua jagi Kisha akamletea Mama sebuleni, alimimina kwenye Glass baada ya mama kumaliza kunywa alimuuliza..

“” Vipi khari? Jolvin kaniambia unaumwa kichwa kwasasa unajisikiaje!?”

Gorii alishituka kwanza kabla hajatoa jibu. “” Aaah huyu si kaniambia najiuguza imekuwaje tena amwambie naumwa?”

Wakati anataka kujibu Jolvin alifika huku kabebelea Dawa.

“” Mama nimemletea dawa zake! Atakuwa anatumia kutwa mara tatu!?”

Gorii pamoja na Bibi walitoa macho kutizama dawa huku kila mtu akijiuliza. “” Mbona ni dawa nyingi?”

“” Aa lakini Mjukuu wa Bibi’ Mimi naendelea vizuri! Nitachukua baadhi tu, hizo zingine kaa nazo nikiugua nitakuwa naja kuchukua!”

“” Wewe si unaumwa!! Au ulidanganya ndio maana hutaki dawa! Mtu nimejitoa kumuita Doctor! Akashauri nikuchukulie dawa halafu unakataa!?”

“” Basi Jolvin.. atakunywa tu hebu leta hizo dawa! Ni zipi anakunywa sahii!?”

Mama aliongea huku akimshika mkono Gorii, akae karibu yake! Jolvin alichukua Kama aina nne za dawa akampatia, Mama ilibidi amuulize…

“” Mbona ni dawa nyingi Jolvin!?”

“” Doctor ndio kasema!!”

Jolvin alijibu.

Gorii alichukua maamuzi magumu, alikunywa dawa zote huku akibaki kumtizama Jolvin ambae haoneshi kujali kabisa! Kwa Bibi muda huo aliamua kufunga macho asione kinachoendelea. Baada ya kumaliza kunywa aliomba akapumzike chumbani, mama akawa amemruhusu.

Baada ya kumaliza kula kila mtu aliingia chumbani akabakia Jolvin akisoma sebuleni, Bibi kila muda alikuwa akichungulia Kama Jolvin kalala akimbie chumbani kwa Gorii’ kumtizama. Jolvin alilijua hilo akawa amebakia pale makusudi.

“” Bibi haulali leo!? Naona muda wote unanichungulia? Wewe kalale Gorii” anaendelea vizuri nipo namlinda hapa!”

Bibi alirudi huku akiwa na aibu kafumwa.

“” Mjukuu nae anamlinda wakati yupo sebuleni, Gorii huko chumbani sijui anaendeleaje?”

Jolvin baada ya kumaliza kusoma alichukua chupa ya maziwa aliyokuwa nayo pale Kisha alielekea chumbani kwa Gorii, Aligonga mlango… Gorii ndio anasimama kuja kufungua.

“” Bibi sijafa bhana! Ila Mjukuu wako Kuna siku ataniua hivi hivi naona!!”

Ile anafungua mlango anashangaa kumuona Jolvin. Jolvin nae aliishia kucheka Kisha alimjibu.

“” Kwa tabia yako hiyo na utakufa kweli!”

Alimpatia maziwa anywe! huku akikaa kumtizama jinsi anavyoyanywa.

“” Kumbe unagopa kufa? Mimi nikajua muda ule waekit kuumwa ulitaka ufe Kweli! ” Naona Hujakataa maziwa?”

“” Na Wewe hupendi nife pia! Usingeleta maziwa..’ Mimi nisingekunywa” kuleta kwako unaonesha hutaki nife!”

“” Na siku nyingine urudie hayo maigizo! Muite Bibi aingie ndani naona kakaa mlangoni Kama mlinzi!”

Gorii ndio anafungua mlango alimuona Bibi akikimbia kuishilia chumbani Kwake ilibidi acheke tu huku akirudishia mlango.

“” Kaka White! Nashukuru!! Pia nisamehe!

Jolvin alimwangalia, mtu anaeshukuru na anaeomba msamaha kampea mgongo!

“” Gorii mtoto mwenye heshima, anae nidhamu, anaheshimu watu wadogo kwa wakubwa! Hii kuongea amekupea mgongo tuiweke upande ganii!?”

Gorii alimgeukia alikumbuka Yale maneno aliwahi kuyaongea Jolvin, siku wakutane kwenye chumba Cha Rich na leo kayarudia japo kayabadilisha kidogo, ilibidi amuulize;?

“” Kaka White…. Huwa ninakukosea Sana mpaka uanze kunielezea tabia kupitia mafumbo pale ninapokuuzi!?”
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA

” Kwasababu ndivyo ulivyo!”

Kisha aliinuka akitoka chumbani kwa Gorii.

Gorii aliinuka kufunga mlango! Akakaa kwanza kitandani huku akitizama picha ya Mamake ukutani.

“” Ee Mungu! Mlinde mamangu awe mzima huko aliko haijalishi nitachelewa kumpata ila hakikisha anaishi!”

Asubuhi kulipokucha Gorii alijiandaa kwenda chuoni! Siku hiyo hakutaka kumsubilia Kaka White. Alichukua usafiri wa bus hadi chuoni.

Wakati akiwa njiani Mawazo yake yalikuwa mbali alihisi Kama mamake anamuita! Alisimama kuchungulia dirishani! Kuna abiria alikuwa akishuka ilibidi aunge nae akachukua.

Alianza kuangaza huku nakule Kama ndie mama kweli kamwita kumbe ni akili yake tu! Ile anatuliza akili bus tayari lishaondoka aliangalia mfukoni Kama anae pesa hakuwa nayo.

“” Ooh! Kaka White sijui atapita hii njia!! Halafu mbona kule Kuna watu wengi wanakimbilia.

Ilibidi aliunge, lilikuwa ni gari la matangazo limepaki pembeni kidogo na barabara, walikuwa ni watu wa Tecno wakitangaza biashara zao huku wakiuza simu! Gori Alisimama akawa amejisahau kabisa! Alianza kuangalia vijana wanavyocheza pale! Akawa amevutiwa nao! Mtangazaji alitangaza anahitaji watu watatu watakaoweza kushindanishwa kucheza na akishinda atapewa zawadi ya Simu.

Gorii alitabasamu Kwanza! Aliangalia jinsi alivyovaa akaona Kama akienda pale atajulikana ni mwanachuo! Aliangalia kwenye begi lake huwa anatembea na prova! Pamoja na viatu vya wazi akitoka chuo hupitiliza navyo dukani.

Akaona wee! Hawezi kupitwa hivihivi na hiyo Simu, alibadilisha Ghafra akabaki kwenye suruali ya chuoni kwa juu akajazia prouva kuficha ile sale, akawa hatambuliki tena Kama mwanachuo!

Alizamia mbele, ile anakuja kuangalia kawa mtu wa tano! Dj alimwambia arudi lakini muda huo ndio alizidi kusogea kunako mziki! Watu ikawa ni oya! oya! Abaki… Abaki..!

Dj alimwachia acheze! Mziki ukawa umewekwa! Round ya kwanza mtu mmoja akaishia, Hadi ilipofika Round ya mwisho Gorii alikuwa bado akiongoza! Walibaki mabinti wawili washindaniehwe na atakae shinda ndio atapatiwa simu!

Gorii alimtiza mwenzake akaona kamnunia kweli! Yeye Tena! Aliamua kucheka kwanza huku akinyosha kiuno, kushoto kulia, hayo yalikuwa ni maandalizi tu!”

Mziki ulivyoachiwa Gorii alicheza Kama hatocheza tena, baadae Dj alisimamisha mziki kwanza angalau awahoji majina yao, binti wa kwanza alijitambulisha Amina! Alipofikia upande wa Gorii alifikikilia Kama atataja jina lake itakuwa kesi Tena, aliwaza baadae akasema

” Kaka White” watu wote walibaki wakicheka DJ ilibidi aachie mziki huku kila mtu akimshangilia na ndio akaibuka mshindi wa kwanza na Amina akiwa ni mshindi wa pili ilibidi na yeye pia apatiwe T-shirt na kotia.

Gorii alikabiziwa tshert ya Tecno, kofia na Simu! Aliziweka kwenye begi lake Kisha alipewa maiki neno moja aongee, alichofanya ni kusema “” Thank you” akarudisha maiki kwa bahati mbaya ile anarudishia maiki ule waya wa maiki ukafunua prouva, T-shirt ya ndani ikaonekana watu wakaanza kumjadili huyo si mwanachuo kabisa!

Gorii akashangaa watu wote wanamnyoshea kidole ilibidi ajikague kwanza ndio akaona T-shirt imeonekana.

“” Daaah!! Nini tena hiki? nisije nikawa sinema Tena hapa!”

Alichukua begi lake huku akitizama upenyo wa kutokea! Dj pia aliiona ile T-shirt ile anataka kumuita Gorii tayari kasharuka jukwaani akajichanganya katikati ya watu huku akiishia.

Baada ya kutoka sehemu ile ilibidi asimame kwanza kutafuta pumnzi! Aliingia hotelini akaomba maji ya kunywa! Kisha alianza kutafuta ramani ya kwenda chuoni aliangalia muda kwenye Simu yake tayari ilikuwa ni saa sita mchana ndio anakumbuka ni muda wa lunch karibia Jolvin atafika pale chuoni.

Alisimama barabarani huku akiwaza anafika vipi chuoni, aliingiza mkono mfukoni wakati yupo anacheza Kuna watu walikuwa wakimletea zawadi alikuta Kama kunae buku buku nyingi alizihesabu ni Kama elfu tisa! Kama kawaida yake alijipigia makofi kujipongeza kwa kazi aliyoifanya huku akipanda hiace za kuunga unga hadi chuoni.

Alifika Getini alikuta kumtulia ilibidi aingie kwa kujificha.

“” Wewe Gorii!!”

“” Daaah! Nani tena huyu!?”

“” Geuka huku! Unavunga husikii!”

Ilibidi ageuke ndipo anakutana na Mwalimu wake alimpokea siku ile darasani.

“” Sir Jacob! Aaa.. haupo darasani leo!?”

“” Mhuu! Sahii ndio waingia chuo! Halafu umevaaje hivyoo!?”

Gorii ndio anakumbuka muda ule atoke kule hakubadilisha ilibidi ajitetee.

“” Sir.. viatu vyangu nilifua Jana havikukauka ndio maana nimevaa hivi! Kuhusu prouva ni baridi tu!”

“” Na sweta la shule nalo bichi!!?”

“” Nililisahau Ofsini kwa Bibi'”

“” Unajua kujitetea Wewe.. haya nenda darasani!?”

Gorii alimtizama kwanza baada ya kuona yupo busy alikimbilia nyuma ya hostel akabadilisha mavazi Kisha aliingia darasani.

Ile anafika darasani alikuta Meza yake imekaliwa na kikosi Cha Ali gang” Aliwatizama kwanza! Alichofanya ni kukaa mezani akawapea mgongo!

Mmojawapo kutoka kwenye kile kikosi alimsukuma Gorii, akawa ameanguka chini. Gorii alinyanyuka akafuta kwanza mikono yake Kisha akatunisha kifua! Aliangalia mkono wake kwenye kiwiko unatoa damu aliifuta ile damu Kisha alimshika mmojawapo ambae kakaa mezani kwake! Akamuinamisha kwenye meza kwa kumgongesha.

Kama unavyojua wanafunzi huwa wanapenda fujo za aina hii! Ikawa kapigwa, apigwe ni kelele mtupu!

Wale wenzake baada ya kuona mwenzao kagogezwa hasira zikahamia kwao! Japo Gorii alijitahidi kupambana wao walimzidi walikuwa watatu!

Kuna wanafunzi walienda kuripoti Mwalimu akawa amekuja! Bahati nzuri au mbaya ndie Yule Yule aliyekutana na Gorii! Alivyomuona Gorii kabadilisha na mavazi wakati hakuwa vile akajua huyu ndie mkorofi! Walichukuliwa kwa pamoja wakawa wamepewa adhabu toka mchana Hadi jioni wanahangaika nayo.

Waliambiwa kuchimba Dampo la uchafu maana walionesha wanae nguvu za kupambana bora wakapambane na jembe.

Baada ya muda mfupi kila mtu alikuwa kachoka, Ilibidi stori zianze kupunguza uchovu.

“” Lakini Ally! Nyie ndie wakorofi mlikaa kwenye kiti changu! Kama msingekaa…. tusingekuwa tunahenyeka hivi.””

Gorii aliongea.

“” Sasa Wewe Binti gani unapambana na wanaume! Haya yote ni kwasababu yako.

Kijana wa pili aliongea, huku kijana wa tatu yeye aliendelea kuchimba baadae alimuita Gorii.

“” Wewe si unajifanya mwanaume bhana! Njoo uchimbe si mnataka haki sawa kwa wote!?”

“” Nimechoka bhana Kaka wa tatu! Halafu Wewe si ulinisukuma Lakini!?”

“” Hukupaswa unirudishie Sasa!”

“” Aa.. wee! Nisirudishe wakati umeniumiza.

Gorii aliamua kulala kabisa make alikuwa hoi taabani, ile kalala pale alianza kuwaza ndio anakumbuka ile Simu ilibidi anyanyuke haraka huku akiwaaga.

“” Nyie “Ali gang” kesho bhana tuonane! Hata hivyo nyie wa kiume!

Ali aliwahi kumrudisha Kisha alimkalisha.

“” Wewe mjanja mjanja Sana! Umesahau tunakuja kukaguliwa! Huoni ukikutwa haupo ni Adhabu nyingine!”

“” Aaa powa bhana! Muwe na huruma muda mwingine Mimi ni wakike hata hivyoo! Malizieni Chapu tuondoke!

“” Bora nyie mkitoka hapa Adhabu yenu imeisha.. Mimi ninae Kaka mkorofi huko Nyumbani! Sijui hata nitaenda mweleza Nini leo!?”

“” Gorii njoo uongee na Simu yako hapa!?”

Mwalimu wake alifika pale! Ilibidi achukue Simu! Alisikia Hello! Akajua moja kwa moja ni Jolvin. Aliwaangalia kwanza wenzake Kama wanamtizama akaona wako busy ilibidi asogee mbali kidogo aongee.

“” Samahani leo mchana nilikuwa busy! Sikukuletea chakula! Nilikutumia ujumbe ukaonane na Mwalimu wa darasa nimemwachia maigizo! Ulimuona!?”

Gorii alifikilia jibu kwanza, akagundua kumbe mchana hakuja ilibidi ajibu!

“” Leo tulikuwa busy na masomo sijashika simu!?”

“” Kwahiyo umekula!?”

“” Alitabasamu Kwanza make kala mandazi na jamaa zake muda si mrefu.”

“” Nimekula.!”

“” Okay! Njoo getini nakusubili wanafunzi wenzako wameanza kutawanyika wewe bado tu!?”

“” Nakuja!!”. Kisha alikata Simu.

Mwalimu alimuita ilibidi arudishe simu!

” Adhabu yenu imeisha! Ole wenu mrudie tenaa! Tutawafukuza chuo!”

Gori aliwatizama wenzake, aliwaona wanaelekea bombani kunawa ilibidi awafuate!”

“” Alii… Nywele zangu zimekaa vizuri lakini!?”

“” Wewe sitaki mazoea!! Muulize Khamisi.

“” Mhuu! Sasa ndo umenuna wakati Adhabu imeisha nijibu basi! Unajua sahii tushakuwa marafiki.

“” Na wewe…!?”

“” Ee Mimi.. si tunashilikiana.

Ali ilibidi amtizame vizuri Kisha alimpangusa kulikuwa Kuna mchanga!

“” Upo vizuri.. kakako ndio alipiga? Muwahi bhana..”

“” Khamisi.. mbona wewe husemi nisaidie hata wazo la kuzungumza na Kaka.

“” Kaseme ukweli.”

Khamisi alimjibu mpaka wenzake walianza kucheka.

“” Muulize Hussein!? Ali alijibu kwa kumjaribu make aliona Hussein haziivi kabisa na Gorii tayari kamtoa ngeu.

Alimtizama Hussein ambae alikuwa akipikicha majani ya mgomba akiweka kwenye paji la uso, akaona isiwe noma alimfuata.

“” Sisi wote ndio tulitakiwa tupatiwe Adhabu! Make ndio tulileta vurugu! Hapa tumeumia wote! Kesho asubuhi nikumbushe nikupatie dawa ya hicho kidonda!”

Gorii alichukua begi lake huku akiwaaga wenzake akaondoka, alifika Hadi Jolvin alipo! alionekana yupo busy akisikiliza mziki.

“” Kaka White!!!

Jolvin ndio anasituka, alimtizama kwanza Gorii huku akimkagua hata yeye alikuwa amemmisi kwa vituko vyake.

“” Ndio umetoka hivo Nyumbani!?”

Gori alianza kujikagua kwanza akijiweka sawa, Kisha alimkubalia kwa ishara.

“” Hizo nywele hizo…!!?”

Gori akaona isiwe tabu alifungua mlango wa nyuma akakaa.

“” Kaka white sorry! Nipeleke Nyumbani kwanza leo sitapita dukani nimechoka kweli!”

“” Hapo ndio unakomaa akili! Na wiki kesho hakikisha unaweka ratiba ya kujisomea! Nikiwa nasoma Mimi na Wewe unajisomea!”

Jolvin aliongea pasina kujua Gori huyo! Leo kashinda na pilika pilika hata daftari hajashika.

Baada ya kufika Nyumbani Gorii alipitiliza chumbani kwake! Alifanya usafi wa mwili Kisha alitoka kuanika nguo nje, inaonesha hata kufua alifulia ndani!

Siku hiyo Gorii aliwahi kulala kutokana na uchovu! Jolvin Kama kawaida yake yeye huwa anasoma kwanza! Baada ya kumaliza kusoma aliingia mtandaoni achati na marafiki zake wa chuoni, alikokuwa akisomea walikuwa wamemumisi sana! Waliongea mengi huku wakimuomba kwenye graduation asikose make Huku alikuwa kajiegesha tu hata mitihani alikuwa akifanyia chuoni kwake kwa mara ya kwanza.

Wakati akiendelea kuchati Rich alimtumia video What’sup, alizifungua ndio anakutana na Gorii akicheza, aliangalia Hadi mwisho ndio anaona hata jina kasema ni la Kwake! Hapo ndio alichoka baada ya kuona na zile zawadi alizopewa, wakati anamalizia kuangalia video ile Kuna nyingine tenaa inaingia ni ile aliokuwa shuleni akipigana pamoja na ile akichimba dampoo.

Aliamua kumpigia Rich ambae alipokea simu huku akicheka.

“” Yaani Broo! Nyumbani tunae Mandoga, mtu kazi! Unaona alivyopambana ulingoni akapigwa na mtu tatu! Bado akaomba pambano na wale jamaa achimbe dampoo! Nakwambia Kaka, Gorii ni wa kiume, siku ile alipigana na Hammad na leo tena! Mara acheze mziki wa promotion na Tecno! Hivi kunae mwanaume atakaemuoa kweli, au tu akampenda labda nae awe na akili Kama zake ila Hammad waliendana!”

Muda huo Jolvin alikuwa hata bado hajazungumza, ilibidi amuulize;

“” Umetoa wapi hizi video!?”

“” Mimi si mzaliwa wa hapa” ninao jamaa wengi! Si huwa wananiona nipo karibu na Gorii wamenitupia picha nioshe macho! Halafu mwambie Gorii awashe simu! Alijua nitamtafuta Nini!!?”

Jolvin aliamua akate simu Kisha aliiweka pembeni, akimfikilia Gorii”.

“” Sijui tumuachishe shule.. aanze kunengua kwenye makasino! Make kawa too much kwa kila kitu!”

Aliamua kulala huku akimsubilia asubuhi! Video zote azituma kwenye group la familia What’sup kila mtu akaziona.

Asubuhi yake Bibi na mama pamoja na Jolvin walikuwa mezani wakimsubili Gorii afike.

“” Bibi muamshe Mjukuu wako! Naona bado anaota michezo ya jana!

Jolvin aliongea huku akimtazama Bibi.

Bibi ilibidi aende chumbani kwa Gorii alimgongea mlango ndio anakurupuka, alikuja kufungua huko akijinyosha mwili auweke sawa’

“” Ooh! Good morning Bibi’ nimechelewa chuo! Ngoja nijimwagie haraka!”

“” Usijali Jolvin kakuombea ruhusa upumnzike make Jana ulichoka sanaa!”

Gorii ndio anakumbuka tayari Jolvin kajua ni msala tenaa!

“” Yupo wapi yeye!?”

“” Katoka!!”

“” Hadi mama!?”

“” Eee! Hawapo..!”

“” Hapo sawa..!””

“” Njoo tunywe chai mezani.

Bibi alitoka huku akimsikitikia, sijui hata watamaliza vipi? Gorii alijiandaa haraka akawa amevaa peans jinsi, alipendelea kuivaa Nyumbani na t-shirt.

Ile anafika mezani anakuta watu wote wakimgoja. Alishituka kwanza Kisha aliwasalimia, aliangalia sehemu ya kukaa ilikuwa ni seat imebaki Karibu na Jolvin.

Alivuta kiti akawa amekaa kwa kuogopa ogopa! Muda huo Jolvin alichukua chupa ya chai akamumiminia ni kitu ambacho huwa hafanyi vile! Waliendelea kunywa chai huku stori zikiendelea tofauti na Gorii alivyofikilia sangapi asijisahau akaanza kudakia maada huku akikoleza kicheko.

Walibaki wakimuenjoy kabisa ili asijisikie vibaya! Baada ya kumaliza kunywa chai walitaka ashibe kwanza maada ikaanza.

Jolvin alishika simu yake akawasha Kisha aliplay video zote akamuonesha Gorii ambae hakuzishangaa ila aliwaza kazipataje Jolvin!

Hapo hapo alianza kulia Kisha alipiga magoti akiomba msamaha kwa Jolvin.

“” Gorii sitaki maigizo! Ni hivi nikirudia ule msemo wangu huwa unaniuliza kwanini napenda kusema vile! Tulikabiziwa kuwa wewe ni binti, msitaarabu, unae nidhamu, unaheshimu watu ila Wewe hujiheshimu! Leo unarudi kwenye familia yako ukakae kwanza huko utulie huenda utajifunza!? Ayaa!! Mama ingia…

Gori aligeuka kuangalia Mlangoni alikuwa ni Mama Doreen akiwa na Doreen wamemuijia.

Bibi ilibidi aingilie kati.

“” Lakini Jolvin! Mtu huwa anaonywa na sio kumuondoa hivi hivi! Anajisikia vibaya!”

Muda huo Mama Doreen alimuinua Gorii Kisha alimshika mkono huku akimuomba akusanye nguo zake waondoke.

“‘ Jamaniii naombeni mnisamehe kwa hiki kilichotokea! Nashukuru hata kwa muda mliokubali kukaa nae! Leo nitamchukua kwakuwa Mimi ndie nilimchukua kumlea nitaenda kukaa nae mmewangu kaenda kikazi atakaa muda wa nusu mwaka! Nitakua Nishajua jinsi ya kukaa nae nitamrudisha hosteli ikiwezekana!”

Jolvin Alisimama Kisha alimkumbatia mama Doreen!

“” Afadhari Mama! Wewe mchukue tu! Angalau nitasoma make sio kwa vituko humu ndani! Inatosha hata kwa huu muda tuliokaa nae! Watoto wasiojulikana huwa hawajulikani tu! Ukute kweli hata mamake aliiba zile pesa!”

Jolvin aliongea maneno mengi hata ambayo hakuyastahili ayazungumze! Muda huo Gorii alikuwa pale aliyasikia vizuri! Yalimfanya aanze kulia huku akiichukia familia kwa ujumla aliweka ahadi moyoni mwake hatakanyaga tena katika familia ile!

Alichukua begi lake akirivuta kutoka nje! Bibi alimuwahi amzuie lakini Jolvin aliwahi akamshika mkono akampeleka chumbani kwake”

Huku Mama Rich na Mama Doreen walitoka nje huku wakizungumza.

“” Ni hasira tu! Naomba mjisikie vizuri, Jolvin anae hasira! Zikimuisha yeye ndio atakuja kumuomba Gorii amrudushe ndio maana nimekaa kimya! Jolvin mwanangu kafata tabia za Babake kweli! Ila Kuna siku zitamuumiza vibaya! Huwa anafanya kitu bila kufikilia lakini baadae hujutia maamuzi yake!”

Gori baada ya kufika nje ya Geti alibaki akitizama ile nyumba! Alikumbuka mambo mengi jinsi alivyopokelewa, furaha waliyompatia lakini leo hii imetoweka ghafra! Alilia Sana huku akimlaumu mamake yote yanayotokea yeye ndio chanzo!.

Muda huo Mama Rich alifika pale alitaka kumkumbatia Gorii amuage, lakini Gorii alimgeuzia mgongo hii ikamuumiza Sana! Alijua tayari chuki aliyoisababisha mwanae Sasa imehamia familia nzima kwaaajili ya mtu mmoja leo furaha haipo tenaa!

Gorii siyo haipendi ile familia ila aliamua aisahau kabisa! Alihisi ni kwasababu ya umaskini wake ndio chanzo hata hawamuani Tena, Alimtizama jinsi mama Rich akiwa anarudi ndani kwa unyonge ilimpelekea hata yeye azidi kulia.
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA

Baadae walifika nyumbani! Gori alikalibishwa tena kwenye chumba chake akawa amepaki begi zake! Siku hiyo ilikuwa ni siku ya huzuni kwake hata kula hakula alikuwa akimkumbuka mamake! Mama Doreen alijitahidi kumbembeleza Lakini wapi! Mwisho kabisa alimuacha akae pekee huenda Kuna mambo anataka afanye mwenyewe!

Huku nyumbani kwenye familia ya Mishoki kulikuwa hakukaliki Bibi nae alikataa kula akimhitaji Gorii! Jolvin ilibidi amfuate aongee nae Lakini Bibi alimgomea! Aliamua kumtafuta mamake aongee nae ndipo anamkuta Chumbani akiwa ameshikilia picha ya mmewe pamoja na picha ya Naina.

Alibaki amesimama akimtazama mamake Kisha alisogea karibu na mamake akawa amekaa.

“” Mamaa kipi umekumbuka leo? Sio kawaida yako kuangalia picha ya Baba pamoja na Naina! Wametangulia mbele za haki mamaa!”

“” Namkumbuka binti yangu Naina! Sahii angekuwa umri wa Gorii! Ile haikuwa siku yao ila ni ajali ya kusababishwa tu ndio iliwatanguliza.”

Mama alishikilia picha ile kwa uchungu huku akiwa analia! Jolvin alimkumbatia mamake huku akivuta taswira ya kipindi kile ajari ilivyotokea.

Ilikuwa ni siku moja Babake alitoka kutembea akiwa na Naina muda huo Naina alikuwa na miaka kumi na mbili! Ilikuwa ni siku ya birthday yake Baba aliamua amtembeze sehemu mbalimbali yenye vivutio vitakavyomfanya siku yake iwe vizuri! Baada ya kumaliza kuzunguka majira ya jioni wakiwa njiani wanarudi ghafra lilitokea roli kubwa mbele yake, alijitahidi kulikwepa Lakini kwa bahati mbaya gari yao iliangukia kwenye daraja! Ile wanakuja kuokolewa tayari walikuwa wamepoteza maisha papo!

Kumbukumbu ya Jolvin iliishia hapo! Na kwa muda huo ilikua imepita kama miaka tisa tangu wapoteze maisha!

Bibi nae huko ndani kulikuwa hakukaliki alikuja Chumbani kwa mwanae ndipo anawakuta wapo kwenye simanzi nzito! Ilibidi na yeye aliunge pale wakaanza kulia wote!

Jolvin aliona ile khari inazidi kumuumiza ilibidi atoke! Aliingia Chumbani Kisha akampigia Esau simu waongee! Alimwelezea kilichotokea lakini ushauri wa Esau alimwambia hii yote ni kwasababu Gorii hayupo! Na hii imewapelekea kuwaza vitu vya nyuma ili kurudisha khari ya awali ni kumrudisha Goryanah!

Esau alikata simu huku akimkumbuka Kweli Gorii, aliamua kumpigia lakini namba yake haipatikani! Ilibidi awajulishe wenzake kile kinachoendelea nyumbani ikiwezekana Kama watampata Gorii wamsihi arudi nyumbani.

Ilipita miezi kadhaa Gori alikuwa amezoea mazingira mapya! Muda huo alikuwa akiishi Hostel! Ule utundu utundu wake ulipungua kidogo huenda ni vile anakua!

Siku hiyo ilikuwa ni weekend baada ya kutoka Chuoni, aliamua kuja kusalimia nyumbani. Baada ya kufika aliingia Chumbani kwake siku hiyo aliikumbuka simu yake aliiwasha angalau atizame watu waliomtafuta! Ile kawasha tu alikutana na message nyingi kutoka kwa watoto wa Mishoki! Aliamua kuzipuuzia lengo lake lilikuwa ni kutafuta ujumbe wa mamake kama kapatikana! baada ya kuona hamna ilibidi azime simu tenaa! Huku akiendelea kusoma.

Alifungua kitabu chake kwa bahati nzuri au mbaya alikutana na picha aliyopiga na Bibi pamoja na Jolvin siku ile wanazindua duka! Ilimsononesha kiasi fulani make Alianza kuikumbuka ile familia! Alikumbuka jinsi Bibi yake walivyokuwa wakitaniana, baadae kabisa alimtizama Jolvin alikumbuka mambo mengi wamewahi kufanya tangu wakutane nyumbani hata ile siku kampeleka kwao! Pia ile siku walienda kufanya tangazo alimwachia pesa ndefu ambayo imekarabati nyumba yao kijijini.

Mwisho kabisa furaha yake inakatishwa baada ya kukumbuka maneno aliyomtolea siku yenyewe aondoke kwenye familia yao hii ilimuuma Sana!

Wakati akiendelea! Kukumbuka Doreen alifika pale akiwa na ile simu kubwa alimletea Gorii.

“” Gorii! Leo nimeingia What’s up kupitia namba yako! Ile nimefungua tu Rich kapiga yaani kakukumbuka balaa!

“” Umenikosea bhana! Sikutaka niwe hewani!”

“” Tatizo Wewe huelewi! Si umeshakuwa maarufu! Nimekufungulia page Instagram nikaweka ile picha ulikowa ukifanya matangazo! Hutaamini watu wengi wamekufollow wanataka ukawafanyie matangazo Tena! Hapo utakuwa ukikusanya pesa pasina kutarajia! Kwani hutaki kumalizia Nyumba yenu kijijini!?”

Gorii baada ya kusikia Nyumba tena ilibidi wakae vizuri huku wakianza kuzijibu zile message zilizotumwa na wadau! Kuna mtu alimpigia Gorii kwenye namba ake akimuomba leo jioni aonane nae, muda mrefu Kweli amekuwa akimtafuta hata alipotumia ile namba ya Jolvin aliambiwa yupo busy na masomo ilibidi awe mpole.

Baada ya kukata simu walibaki wakitazamana na Doreen huku akimuomba aende! Watatafuta namna ya kumtoroka mama tenaa!”

Majira ya jioni walijiandaa haraka Kisha wakatoka kimya kimya kuelekea kwenye Hoteli ilipo! Baada ya kufika walimuulizia mhusika! Mhudumu aliomba mlegwa ndio aingie! Gorii alimkabizi begi Doreen huku akimuomba amsubili pale.

Baada ya kufika hutaamini watu wengi walianza kumshobokea Gorii! Huku wakimuuliza habari za alikokuwa make wengi waliamini yupo shuleni na huku karudi likizo!

Gorii Alibaki kuwakubalia huku akiingia kwenye chumba maarumu akawa ameandaliwa vizuri! Ndio akarudishwa kwenye stage afanye shoo kidogo ya kucheza Kisha ndio picha zichukuliwe!

Kwaujumla zoezi lake lilifanikiwa alipatiwa pesa yake nzuri Kisha alirudi kwa mwenzake.

“” Gorii umekosea wambie wakuwekee picha kwenye simu! Tuweke kwenye akaunti tuendelee kupata wateja!

“” Nitamuomba boss! Si akaunti yake tunayo! Atashea lile tangazo nami atanitag huku!”

“” Ooh! Sawa! Kumbe huwa unaakili Sana.

Walifika sehemu ya kuchukua usafiri! Lakini siku hiyo usafiri ulikuwa wa shida Kila daradara itakayopita imejaza! Mwisho kabisa waliona gari private inafika pale! Doreen alifanya kuisimamisha! Ile imesimama tu waliingia kwa haraka haraka.

“” Kaka Masaki.. tuache!”

“” Afadhari tumepata usafiri! Nilikuwa nawaza Kama tutachelewa tutamwambia vipi mama!”

Gorii aliongea huku akiangalia kile kitita Cha pesa Alibaki akizishika shika tu kwa furaha.

“” Nishukuru Mimi! Laah hivyo usingezipata!”

Walicheka kwa pamoja huku wakifurahi! Zile sauti zao zilimfanya Dreva aliyekuwa akiwaendesha alitoa earphones masikioni Kama vile sauti aliifahamu, lakini alijua ni wenge tu! Alionekana ana mawazo Sana kila akipiga hatua anakumbuka maneno ya ndugu zake.

“” Mrudishe Gorii! Familia haina furaha! Hata biashara ya Duka haiendi tena! Wateja wote wamemkimbia Bibi wanamtaka Gorii!””

“” Wewe Kaka tumefika! Tuache bhana! Mbona husikii.

Gori na Doreen walikuwa wakisaidiana kumuita make alikuwa hawasikii kaweka Earphones. Gorii akaona asimchezee alianza kutafuta upenyo hadi akamfikia dreva Kisha akamtoa ile prouva yenye kofia Kisha akashika usukani akisimamisha pembeni!

Baada ya kusimamisha ndio anageuka amfokee vizuri! Kabla hajafungua mdomo alibaki amestaajabu baada ya kukutana uso kwa uso na Jolvin!

Jolvin pia alipigwa na butwaa huku akipepesa macho yake huenda ni Kama vile haamini! Aliishia kumuita Gorii huku akimshika uso! Ahakikishe Kama ni yeye!

Gorii ndio hakili inakaa vizuri alipepesa macho Kwanza kutoa wenge alilokuwa nalo Kisha akaushika mkono wa Jolvin akaushusha chini.

“” Leo ni siku mbaya kwangu! Na hii ni baada ya kukutana nawewe!”

Alitoa pesa Kama elfu kumi akamkabithi Kisha aligeuka afungue mlango ashuke! Doreen alikuwa bado haelewi kinachoendelea alifungua mlango akashuka ili asogee upande wa Dreva aangalie kinachotokea.

“” Khaaah!! Kaka Jov!!? Ni wewe tena!? Mbona hauji hata nyumbani kutusalimia! Au ni kwasababu ulimfukuza Gorii!”

Doreen alikuwa Kama anatonesha kidonda kwa Gorii na Jolvin! Ilibidi Jolvin amfungulie Kwanza mlango! Wakawa wameshuka wote!

Gorii hakutaka hata kumsikiliza Jolvin alimshika mkono Doreen waondoke lakini Jolvin alimshika mkono Doreen kumzuia wasiondoke!

“” Kaka White!! Unataka nikujazie watu! Naomba mwachie Doreen! Pia sitaki upite njia yangu tenaa!”

Jolvin aliamua kumuachia kwani kimbembe Cha Gorii anakijua vizuri! Alibaki kuwatizama mpaka wanaishilia Kisha alipanda kwenye gari huku akijiinamia kwenye usukani! Akijilaumu sana yote yaliyotokea ni makosa yake!”

Hata alipofika Nyumbani alikuwa na Mawazo Sana alipitiliza Chumbani kwake! Ile anafika alimkuta Anelisa kamsubili alifika akakaa kwanza Kisha alichukua grass ya maji akanywa.

“” Anelisa!! Leo tualishe ratiba yetu ya kujisomea naona kichwa hakipo vizuri! tufanye kesho!”

“” Kwanini Jolvin!? ” Mbona siku hizi umebadilika Sana! Kila tukipanga ratiba unaialisha Nini shida lakini!?”

“” Ane… Wewe si unawazazi wote! Mimi Sina Baba!”

Jolvin aliongea kwa ufupi lakini hakumanisha vile Kama angesema ni sababu ya Gorii angemkosea Anelisa. Anelisa alimsikitikia Sana Alisimama akamkumbatia kwa muda mrefu Kisha alimkisi kwenye paji la uso huku akichukua Mkoba wake aondoke.

“” I’m sorry Jov!! Sipendi nikuone unakosa furaha! Natumia muda mwingi kukufanya uwe na furaha sijui nakosea wapi tu! Kama ndo familia wanakulaumu umemuondoa Gorii basi mrududishe uziepuke hizi stress!”

Jolvin alijisikia vizuri! maneno ya Anelisa yalimfariji alitabasamu huku akiongea mwenyewe” ” ukifanya hivyo tutakuwa pamoja na wewe wala hakutaharibika kitu” alimuita kwanza.

“” Anelisa! Ni wait..!”

Anelisa alibaki amesimama huku akifikilia kweli Jolvin! Ameshamkazia kabisa japo siku za karibuni Jolvin alimwambia awe rafiki ziku moyo wake ukianza kufumguka kwake atamfanya mchumba na ndio makubaliano yao! Mpaka Anelisa kurudisha mazoea kati yake na Jolvin.

Jolvin baada ya kumfikia alifanya kumkumbatia! Kisha alimtengenezea nywele zake huku akiongea nae.

“” Kama Gorii ndie furaha ya hii familia! Basi nitamrudisha ili nibaki na amani tu!”

Anelisa alimkumbatia pia! Japo alikuwa na maumivu baada ya kugundua Jolvin ashaanza kumpenda Gorii na Kama atarudi Nyumbani ndio atamkosa kabisa! Hakuwa na jinsi zaidi ya kumsapoti tu.

Waliagana pale kwa furaha huku kila mtu akiendelea na kazi zake! Jolvin akiwa Chumbani kwake siku hiyo alitoa picha zote za Anelisa na Gorii walizopiga hivi karibuni, alichukua picha ya Gorii na Anelisa akaanza kuzipambanisha!

“” Tofauti ya Anelisa na Gorii, Gorii anae nywele ndefu za kisomari! Pua yake midomo yake! Ni mizuri! “” Anelisa ni mrefu anashep ana mtazamo mzuri na yeye ana macho mazuri! Ila midomo yake sio Kama ya Gorii, mguu wa kawaida… Gorii yeye wa bia! Kuhusu vidole ni vilaini vipo vizuri kwa massage! Gorii vimekomaa sijui kwasababu ya kazi!! Kwenye kupika Anelisa hajui.. Gorii anaweza! Kwenye tabia Anelisa ni mnyenyekevu! Anajua kuomba msamaha! Gorii ndio anawaza kupambana ikiwezekana hata kukudhalilisha anaweza.. lakini ni mtu jasiri anapambana halafu anapedwa na familia hii karibia wote, pia huko mtaani ndio usiseme!! Sijui ni Nini kinanikuta mpaka naanza kumfikilia yeye Anyway nitamrudisha Nyumbani! Kwa Anelisa anaonekana ananipenda kweli sijui nimkubalie hata hivyo familia yake ina uwezo mkubwa.

Huku Nyumbani kwa Gorii siku iliyofuata alirudi chuo akiwa na simu yake kubwa! Muda wote ilikuwa ni kusikilizia apate dili la kutoa matangazo apate pesa ndio yalianza maisha yake rasmi!

Wakati ametulia hosteli aliijiwa na Madam Kuna watu wanahitaji kumuona! Ile anaenda kuwatizama Alishangaa kumuona Bibi akiwa na Anelisa na ndio wageni wake.

Alifurahi Sana kukutana na Bibi! Siku hiyo walimletea zawadi mbalimbali pamoja na vyakula! walikaa wawili na Bibi waongee! Anelisa aliwapisha.

“” Gorii uje Nyumbani Mjukuu wangu! Kazi zimekuwa ngumu wateja wamenikimbia wote wanataka urudi! Natamani kulifunga duka lakini nashidwa kwasababu Lile duka lilifunguliwa kwaajili yako! Na pesa muda wote tunaziweka kwenye akaunti yako! Uwe unakuja mara moja moja kupaangalia angalau upachangamshe tu!”

Bibi alijitahidi kumuomba mpaka Gorii akahisi huruma! Alimwahidi Bibi kila weekend atakuwa akimtembelea dukani! Lakini sio kuuza.

Walifikia mwafaka lakini baadae Gorii alimuuliza.

“” Bibi hivi ni Wewe ndie umeambatana na Anelisa? Au tayari ameshakuwa mkamwana katika familia?”

Bibi alitabasamu tu Kisha akamshika masikio.

“” Muda ule nawaza kuja huku alikuwepo Nyumbani! Akaomba anilete, Jolvin yeye kaamua kulizindua upya duka hebu ona crip aliyotupia kwenye page yake!”

Gori alishika simu akaitazama kwa makini, mpaka ikamkosesha furaha!

“” Mishoki desginer group kwasasa tumewaletea nguo mpya zitakazowapendesha na Sikukuu pia yule Binti yetu mumiliki atakuwepo kuanzia tarehe ishirini na ndie atakuwa msimamizi hapa! Kwahiyo karibuni Sana Sana ukutane na Gorii Goryanah! Anawasalimia Sana huko aliko pia ana hamu ya kukutana na nyie!

Gorii baada ya kumaliza kutizama ile video alimrudishia Bibi simu Kisha alimuuliza.

“” Kwanini mnadanganya!?”

“” Hatudanganyi inatakiwa Wewe uwepo ili kufufua lile Duka! Jolvin hakuwa na njia nyingine ya kufanya hivyo! Kajitahidi kukutafuta muda mwingi ili aongee na Wewe lakini uliomba kwa mkuu wa chuo hutaki kuonana na mtu yeyote akutembelee na Kama utataka kitu ulisema utaenda Nyumbani, Jolvin amekuwa akija hapa mara kwa mara angalau akuone lakini imeshindikana! Siku ile ndio alibahatika kukuona kwenye Gari hata alipotaka kuongea na wewe hukumpa nafasi! Alikuja kunihadithia yote haya! Mwisho kabisa akaahidi kusimamia duka lako haijalishi utarudi lini! Anataka awekeze zaidi kwenye account yako kwa kulikuza duka lako!?”

Bibi aliweka kituo, Gorii hadi machozi yalianza kumlenga ndio akamuuliza.

“” Mama yeye yuko wapi!?’

“” Tangu uondoke Nyumbani Mama kwasasa khari yake sio nzuri! Muda wote anamkumbuka Naina pamoja na Babako aliyetangulia mbele za haki siku moja na Naina! Na leo ameenda kuomboleza makabulini huko Nyumbani kwao na Babako!”

“” Naina… Kwani Bibi ilitokea Nini make huwa namsikia Naina tu!?

Bibi alianza kumsimulia jinsi ilivyotokea Hadi wakapoteza maisha! Baadae alimalizia kumwambia.

“” Yote hayo yatokee! Mama Doreen huwa ni rafiki mkubwa na mamako! Alijua mama anapitia wakati mgumu hata alipokupata Wewe toka kituoni alimshilikisha Mamako akakuomba ukae Nyumbani akufanye kama binti yake! Maana hana watoto wa kike! Ujio wako hapa ndani ilikuwa ni furaha mno hasa zile tabia ulizonazo mmefanana kweli na Naina ndo maana familia nzima ilikupenda!”

Gorii Alibaki kulia tu! Mwisho kabisa Anelisa alifika make muda ulikuwa umeisha alimwomba Bibi waondoke huku akimuaga Gorii na kumtakia masomo mema, wao wakaondoka.

Siku hiyo ilikuwa ni siku mbaya kwake! Hata mood wa kujisomea hakuwa nao aliamua akakae nje pekee kutafakari maneno ya Bibi pamoja na ile familia walivyomuonesha upendo, alichukua simu yake akatizama namba ya Mama Rich akaona isiwe mbaya Kama ndie mama anamkubali acha amjulie khari.

Alipiga Kama mara tatu simu haipokelewi, mwisho kabisa alikata simu akaendelea kukaa pale muda mrefu!

Baadae simu iliita tena ilikuwa ni namba ngeni ilimwelekeza kesho Asubuhi afike kituoni Kuna mtu anahitaji kumuona!”

“” Atakuwa ni Mama kajisalimisha kituoni ee!?”

Aliongea vile baada ya simu kukatwa! Kisha aliingia ndani kulala.

Usiku huo huo kwenye simu ya Jolvin kuliingia message ikimuarifu afike kituoni Asubuhi.

Asubuhi kulipokucha kila mtu aliwahi kituoni! Gorii alikuwa wa kwanza kabisa kufika kituoni! Japo kulikuwa Kuna watu wengi wamejazana Kuna wafugwa walikuwa wakiletwa kituoni huku ndugu zao walifika kuwaona.

Wakati ule Jolvin alikuwa kashikilia simu yake huku akijiuliza ni kipi kaitiwa pale!? Na yeye aliwaza huenda ni mama Gorii kapatikana!

Gorii alikuwa akipenyeza mbele za watu ili atizame vizuri mbele, na Jolvin nae alikuwa akifanya vilevile atokeze mbele! Mwisho kabisa Gari la wafugwa lilipita likielekea kituoni! Watu walianza kusukumana huku kila mtu akitaka aone ndugu yake ikawa ni vurugu! Police ilibidi wasogee pale kuimalisha usalama waliripua bomu la machozi baridi ndio usalama ukaonekana.

Lakini Gorii” alikimbilia bombani kunawa Kisha alirudi huku akiita Maama kwa sauti ya juu!

Bahati nzuri katika wafugwa wale Mama Gorii alikuwepo! Alisikia ile sauti ikimuita! Siku zote unaambiwa Damu ni nzito kuliko maji, mama Alisimama na kuangaza kuangaza huku na kule! Baadae ndio anamuona Gorii akija mbio akikimbilia Lile Gari! Aliangalia nyuma kulikuwa Kuna gari linakuja full.. Gorii nae hakuangalia nyuma yeye alikuwa akimtizama Mama muda wote!

Watu wote walipiga kelele huku wakifunga macho! Wasiamini tukio linaloenda kutokea! Ilisikika sauti ya break lakini kwa pembeni kuliruka damu Hadi kwenye gari! Kisha ukimia ukafata Kama dakika kumi kila mtu akiwa ametulia huku kainamisha kichwa chini haaamini kilichotokea.
 
SEHEMU YA KUMI NA NANE

Gorii ndio wa kwanza kuzinduka, alivuta mkono wake akahisi mzito! Ndio anageuka vizuri! Anakuta pembeni yake kunae Jolvin kaugandamiza ule mkono japo unatoka damu, alivyomtizama vizuri Jolvin alikuwa akimtizama Kisha alimuuliza.

“” Upo sawa Goryanah! Nimemuona mamako! Kweli mmefanana Sana kwa kila kitu! Ulivyomsifia ana nywele ndefu Kama zako kumbe hukuongopa!? Mtizame mama kwanza!”

Jolvin alimaliza kuongea vile Kisha alianza kukohoa huku akitoa Damu mdomoni! Gorii ndio anageuka upande wa pili ndio anamuona mamake sura yake ilikuwa imebadilika Sana hata ile rangi ya usoni ilikuwa haipo tenaa! Mwili wake ulikuwa umedhoofika kwa vidonda vingi!

Gorii alivyomuona alianza kulia upya Kisha alimkumbatia Mamake, unaambiwa Mama ni Mama hata watu wote wangemkataa ila kwako hubaki kuwa mama tu!.

“” Mama ulikuwa wapi lakini? Nilikutafuta muda mrefu sikukuona! Nilitoa Hadi yale matangazo! Lakini hukupatikana!? Uliishije huko ulikokuwa lakini!? Tayari ile nyumba yetu nishakujengea sahii tukitoka hapa tunaenda kuishi maisha mazuri! Hatutakuwa duni tena Kama hapo awali tunaenda kuishi maisha ya kati! Na wewe ulinikumbuka lakini huko ulipokuwa!?”

Mama alimkumbatia Binti yake ni Kama miaka minne imepita pasina kumuona leo anamuona! Alimfuta machozi Kisha alimuuliza.

“” Huyo kijana Ndie mmeo nilieambiwa kakuoa!?”

Gori alishituka kwanza huku akimtizama Jolvin ambae bado yupo chini! Aligeuka haraka akamfuta damu iliyokuwa ikimtoka puani.

“” Pole Kaka White lazima upone tu! Gorii amemuahidi Bibi anarudi Nyumbani ile furaha inaenda kurudi tenaa! tena itakuwa mara mbili yake Mamangu umemuona lakini! Ila atakaa vizuri sahivi amechakaa na Dunia lazima nimfanye Mamangu awe binti tenaa!?”

Jolvin alibaki kutabasamu japo alikuwa na maumivu hakutaka kumvunja moyo Gorii! Alimtizama mamake kwanza, aliona ana khari mbaya hata hapo anajikaza tu!

Mamake Gorii” alisogea hadi alipo Jolvin Kisha alimshika mkono akimuunganisha na Gorii Kisha aliwatamkia.

“” Naamini nyie ni mke na mme! Kijana naomba umfanye Binti yangu awe na furaha siku zote! Kwaajili yako leo binti yangu umemfanya akutane na Mimi! Kama usingetokea binti yangu asingeniona Tena! Kwasababu yako nimewaona wote naomba mbaki na furaha siku zote! Nina ombi kwako.. najua umeumia Sana hata Gorii” kaumia ila ni vile ana furaha kukutana na Mimi hahisi maumivu! Ukipona naomba umtafute mtu anaeitwa Mishoki Kuna mfanyabiashara mmoja waliwahi kuunganisha Shea zao kwa pamoja lakini walikuja kutaharukiana akatoa Shea zake…

Kabla Mama hajamaliza kuongea alianza kukohoa mwisho kabisa alikohoa damu!

Muda huo watu wote walikuwa wakishangaa kinachoendelea baada ya kuona Mama anakohoa sana! Gorii nae alianza kulia ile anataka kusimama ndio anagundua mguu wake haujiwezi Tena! Hapo hapo Ambulance ilifika pale kuwachukua.

Walikimbizwa hospitali kwa emergence rooms! Matibabu ya haraka yalianza kutolewa!

Upande wa Mama ile wanataka kumtundikia Dreep ya maji! Wakati Madaktari wanamtafutia mshipa! Kila wakichoma sindano mshipa unafeli walikuja kumtizama vizuri tayari kapoteza maisha! Walifanya kuufunikia mwili Kisha wakampeleka Mochwari.

Huku kwa Jolvin muda ule alivokuja kumsaidia Gorii! Kwa bahati mbaya ile anamvuta aliteleza mguu wake ukawa umepigizwa na gari akaanguka, muda huo alikuwa tayari kumsaidia Gorii lakini na yeye alienda kuangukia chuma akawa amevunjika nyonga!

Matibabu yaliendelea kwa watu wawili Gorii yeye alikuwa akijitambua, alianza kuwasumbua anamtaka Mamaa mpaka wakaamua kumchoma sindano ya usungizi!”

Ile anakuja kuzinduka anashangaa chumba kizima kimejaa watu. Alitazama vizuri ndio anamuona, Rich, Esau, Joely ,Bibi, Mama Rich, Mama Doreen na Doreen. Alishusha pumzi kwanza kisha aliongea.

“” Hivi hatujafa tu!?”

Ilikuwa ni ile dawa ya usingizi inamletea mawenge!

Wote walisikitika ilikuwa ni Yale majibu ya Doctor! Kuwa Mamake katangulia! Jolvin anaendelea vizuri lakini atatembelea magongo kwa muda ila atakuwa sawa! Kwa Gorii pia atatembelea magongo lakini kaumia Sana nyonga kwenye kuzaa itakuwa ngumu, japo atazaa lakini ni kwa Operation.

Bibi alisogea karibu Kisha akamshika mkononi make alikuwa kaumia anae bandage!

“” Bibi! Umemuona lakini Mamangu! Mbona simuoni yeye anaendeleaje!?”

Bibi alishidwa kujibu akaekiti kikohozi kimembana alianza kukohoa huku akitoka nje! Ma Doreen akawa amechukua nafasi ile.

“” Yupo sawa! Jali afya yako kwanza!”

“” Kaka white yeye Yuko wapi!! Kama vile na yeye aliumia! Damu zilimtoka puani!”

Wakati ule Esau, Joely na Rich walifika! Ile kuwatizama tu Gorii alijawa furaha aliwamisi pia!

Mama pamoja na Bibi walitoka nje ili wazungumze jinsi msiba utakapokuwa walikubaliana wafanyie kijijini kwao na Gorii, kazi ikabaki ni kumjulisha Gorii kuhusu kumpoteza Mamake.

Waliingia chumbani kwa Jolvin alikokuwa amelazwa walimkuta bado ana usingizi! Mama alikaa huku akimtizama Jolvin baadae ndio anaamka taratibu akipepesa macho.

“” Maama! Gorii anaendeleaje!? Vipi kuhusu mamake?”

“” Anaendelea vizuri ila kaumia nyonga! Na Doctor anadai kaumia Sana hata kuzaa itakuwa ni kwa Operation!”

“” Hapana! Operation tenaa!? Itakuwa kakosea vipimo! Mwambie arudie! Na vipi kuhusu Mamake?”

Mama alitikisa kichwa Kisha aliinama chini, Jolvin akawa ameelewa alimshika mkono mamake Kisha aliongea:

“” Gorii atajisikia vibaya Sana! Mpaka khari yake ikamrudie Kama awali inatakiwa nguvu nyingi! Wakati ule nipo na mamake chini! Aliongea maneno mengi Sana! Yeye anajua Mimi na Gorii ni mke na Mme! Alitushikisha mikono huku akiniomba nimuahidi kuwa nitamfanya Gorii awe na furaha!? Wazani mama Mimi nitaweza kweli kwa khari hii!? Nilitamani muda huo nimueleweshe kuwa hatuna Mahusiano kwa khari aliyokuwa nayo sikuweza kumkatisha! Lakini ombi la mwisho kaniomba nikipona nimtafute mfanyabiashara aliewekeza na Mishoki Shea zake kwenye kampuni nikimpata hakumalizia hata kuongea khari yake ikabadilika! Mpaka nawaza nitakamilisha vipi wakati hakumalizia sentesi yake.

Mama Alibaki akishangaa Mishoki family Tena! Ni familia yao au tofauti na hiyoo?”

Muda huo Joely alifika! Mama alipomuona ilibidi awapishe make alijua huwa hawapatani! Aliwaachia nafasi!

Joely alikaa kitandani Kisha aliushika mkono wa Jolvin huku akiupapasa akitizama ile mishipa ilivyosimama alimuonea huruma Sana! Make yeye alikuwa mkubwa kwake na Jolvin alimfatia Kisha Rich! Esau yeye alikuwa ni mtoto wa Ba Mkubwa.

“” Nakuombea kwa Mungu upate afya tenaa! Najua unapitia wakati mgumu sio Wewe tu! Hata moyo wako unamaumivu ya Gorii! Naimani mtakaa sawa!”

Jolvin alibaki akimtizama Joely alionesha ana huzuni Sana siku hiyo ndio alimuita kwa mara ya kwanza “Kaka” Joely hakuamini aligeuza shingo amtizame Jolvin vizuri Kama ndie yeye kweli kaongea, Alirudia tena baada ya kuona haamini.

“” Kaka naomba umuombee Gorii asiwe mnyonge! Ikiwezekana kaa nae karibu mmufariji! Khari yangu Kama unavyoniona sizani hata msibani nitaenda!”

Joely alihisi furaha Sana! Siyo kwamba hapendi ukaribu wa yeye na Jolvin! Ni vile Jolvin huwa anamkaziaga! Aliamua kumkumbatia palepale Kisha alimnong’oneza sikioni.

“” Vipi kuhusu Msamaha…!!?”

“” Nishakusamehe! Unazani ningekupatia nafasi ya kukaa karibu na Gorii tena, Kama hapo nyuma ilivyotokea!?”

Jolvin alimaliza kuongea huku akicheka, kumbe ugomvi wao ni Joely alimchukulia msichana wake ndio wakapishana! Wakati wanacheka pale Esau, Rich nao waliingia walishangaa wawili hao leo wanashea furaha ya pamoja!

Joely baada ya kuwaona aliwakimbilia akawakumbatia kwa pamoja Kisha aliwanong’oneza.

“” Kwaajili ya Gorii! Jolvin kafungua moyo kanisamehe! Kwasasa tunarudi Kama hapo awali!!”

Muda si mrefu Gorii aliletwa akiwa kwenye wheelchair akisukumwa na Mama Doreen huku Doreen kabebelea baadhi ya nguo huku akiwa analia Mama Rich ndio kamshikilia! huku Bibi nae kashikilia pia Wheelchair wakisaidiana kumwangalia Gorii, walielekea chumbani kwa Jolvin!

Jolvin baada ya kumuona Gorii alianza kuhangaika akae, angalau amtizame vizuri. Joely ndio alikuwa wa kwanza kumuweka sawa mpaka Mama na Bibi walishangaa.

Gori alibaki akimtizama Jolvin kwa sekunde kadhaa, machozi yalianza kudondoka kikifatiwa na kilio! Alijitahidi kujikaza lakini aliishia kuongea.

“” Yote haya ni kwasababu yangu! Nisingemkimbilia Mama kwenye Gari wala asingepoteza maisha! Na Kaka White asingekuja kunikimbilia Mimi matokeo yake na yeye kaumia kwaajili yangu!”

Gorii alizidi kulia, mpaka na wale wengine walianza kulia! Ilibidi Doctor aje kuwatoa pale! Kilichofuata ni kilio pale!

Jolvin Yale maneno yalimuumiza sana! Kila akikumbuka maneno ya Mamake aliahidi hata yeye lazima ahudhulie mazishi make wameshaunganishwa mwili mmoja na ni ahadi ya Marehemu.

Alimtizama Esau pamoja na Joely walikuwa wakimtizama, alimwagiza Joely amwambie Mamake hata yeye ataenda kumsitiri Mamake mkwe wa kiapo.

Joely alienda kumwambia Mamake! Ilibidi afanye utaratibu wa kuongea na Madoctor! Baadae alirudi nao wakaomba wamfanyizie zoezi Kama ataweza kukaa kwenye Wheelchair ataruhusiwa kwenda kustili mwili! Jolvin alikuwa akiumia lakini alijikaza nia na malengo nikukamilisha ahadi yake tu!

Siku ya kesho yake walifanikiwa kuanza Safari majira ya jioni walifika! Walikuta wanakijiji wamekaa kwa huzuni wakisubili mwili wa Marehemu!

Mama Muddy ndio alikuwa Kama ndie familia yake na Gorii! Bahati nzuri Gorii ile hela aliyoituma Nyumbani kukarabati nyumba ilisaidia Sana! Tayari nyumba ilikuwa imekamilika ilikuwa ni mjengo mzuri wa kisasa! Ilipigwa lip na rangi ya kutosha pamoja Na Tails chini! Ni Kama alimwandalia mamake sehemu ya kupumnzikia akisubili apelekwe malaloni.

Upande wa Jolvin nae alikuwa haamini! Kipindi kile walipokuja waliishia kwa Mama Muddy japo na penyewe kulikuwa kumejengwa nyumba nzuri hizi zote ni juhudi za Goryanah!”

Muda huo Gorii aliachiwa abaki na wanakijiji wenzake ili wazidi kumfariji! Mama Muddy ndie alikuwa ni Kama Mamake mzazi alichukua nafasi hiyo! Waliongea mambo mengi Sana! Alimwelezea jinsi alivyoonana na mamake kwa muda mfupi hatimae kampoteza kwa huo huo muda mfupi! Pasina kumwambia wapi alipokuwa!?”

Mama Muddy alisikitika Sana, alimwambia pia kuhusu Mzee Rajab nae wamemzika Kama mwezi mmoja umepita kwa ugonjwa ule ule wa upungufu wa Kinga Mwilini!

Sitori nyingi ziliendelea ili kumfanya Gorii awe na amani! Lakini akili yake ilikuwa mbali Sana japo alijitahidi kujikaza!

Huku kwa Jolvin khari yake haikuwa nzuri ukiangalia kajilazimisha tu kufika! Ilibidi avumilie hivyo hivyo huku akiendelea na matibabu! Make walikuja na Doctor wao.

Siku ya kesho ndio ilikuwa ni siku ya kusitiri mwili! Zoezi lilimalizika lakini Gorii Alibaki amekaa pale pale malaloni akibaki kukumbuka mambo mengi aliyoyafanya na mamake leo hii hayupo tena! Ilibidi wamuache kwanza pale akiwa amekaa kwenye Wheelchair!

Jolvin alikuwaa amekaa mbali akiangalia! Alimuomba Rich amsaidie kufika pale! Ukiangalia jua lilikuwa linachoma Sana ilibidi amfuate! Na yeye ndie alikuwa akijulikana Kama mme tangu kizaazaa Cha Hammad na Gorii wakamini vile.

Gorii alimtizama Jolvin baada ya kuhisi yupo pale! Kisha aliongea.

“” Kaka White! Tayari Mama ameshatangulia mbele za haki! Njia hii hii Kuna siku na sisi tutairudia! Ila kifo ni fumbo…!”

Gorii aliweka kituo huku akiomba msaada wa kutoka pale Doreen alifika kutoa msaada! Ikawa wanasukumwa taratibu kwenye wheelchair mpaka wakafika kwenye umati uliokuwa ukiwazunguka, kwa mbali Gorii ndio akamuona Hammad kabebelea mtoto alijua kabisa atakuwa ni mwanae alimuta kupitia kidole akawa kafika, alimshika Yule mtoto shavu Kisha alimwangalia Hammad akamwambia.

“” Kitu nilichokuwa nakikataa katika maisha yangu kuwa na Wewe hatimae nilifanikiwa lakini Nilitegemea siku moja uje uwe na familia nzuri utakayoishi nayo kwa upendo Kama hivi leo! Nafurahi imekuwa hivyo! Ungelazimisha kuwa na Mimi usingepata familia nzuri Kama hii! Nakushukuru kwakuwa umekuja kumstiri Mamangu angalau hata kwa kumwandalia nyumba yake ya kulala umeshilikiana na vijana wenzako! Hongera kwa hilo!”

Gorii alimaliza kuongea Kisha alimuaga Hammad wakisogea mbele! Umati wa watu uliwafuata pia kupata chakula make ilikuwa ni wakati wenyewe.

Baadae kabisa Muddy ndio alipata muda wa kuongea na Gorii” Alimshukuru Sana Gorii kwa mchango alioufanya Nyumbani kwao! Bado kamfungulia duka kubwa la bidhaa anauza kwahiyo maisha kwao kwasasa yapo vizuri!

“” Gorii! Nakuomba uendelee kuwa na moyo huo! Halafu nimegundua kweli Jolvin anakupenda Sana Kama alikimbia kuja kukusaidia wewe bila kujali ataenda kuumizwa lakini aliachilia mbali naomba ukae nae karibu”

Gorii alitabasamu tu! Huku akiamini ni kitu hakiwezekani Kafanya Kama wajibu isitoshe ni mwanafamilia, hii haikumuingia kichwani.

Siku ya kesho yake watu walianza kusambaa wakielekea makwao! Gorii yeye hakutaka kurudi mjini make alienda kule kumtafuta Mamake na Kama kampata haina haja ya kurudi tenaa! Taarifa zilifika kwa Jolvin zilimuumiza Sana ukiangalia ndie jukumu lake kakabidhiwa inatakiwa arudi nae kivyovyote vile.

Mamake Rich ilibidi akaongee na Mama Muddy! Mwisho kabisa aliamua kufunguka jukumu aliloachiwa Jolvin na Marehemu! Mama Muddy ilibidi amuite Gorii aongee nae lakini Gorii alirudisha.

“” Huwa ni kawaida tu kuongea vilee! Mama alipata hofu baada ya kushuhudia ile ajari, Mimi naweza kujilinda mbona!?”

“” Gorii Mwanangu! Semi ya mwisho ya Marehemu huwa inasikilizwa kuliko kitu chochote! Unavyokataa Roho ya Mamako inahangaisha huko haitulii! Pia itakuwa inamsumbua Jolvin muda wote hajakamilisha ahadi yake!”

Gorii alikuwa bado haelewi ilibidi aitiwe wale wabibi wenye umri umeenda kidogo mwisho akawaelewa kidogo ila kuunganishwa kuolewa alikataa! Alikubali Kama ni kukaa karibu yake ili Mamake asiteseke hapo sawa! Na swala la pili ni kwaajili ya matibabu tu.

Walikubaliana na Safari ikaendelea! Jioni yake walifika, Jolvin alikuwa na khari mbaya ilibidi arudishwe hospitali! Na siku iliyofuata Gorii alikuwa akijaribu mazoezi ya kusimama pekee! Akili yake ilimtuma Kama atapona haraka atarudi Nyumbani kwao mapema! Siku hiyo ikawa mbaya kwake alianguka vibaya bahati nzuri walinzi walimuona wakawa wamemsaidia akapelekwa hospitali matibabu yakaanza upya.

Zilipita Kama wiki mbili Gorii alikuwa ni wa kitandani! Alikuwa ni wa kuamshwa kujisaidia make alikuwa kawekewa vyuma kwenye nyonga ili akae vizuri. Jolvin yeye alikuwa akiendelea vizuri alikuwa akitembelea magongo na mara nyingi alifika kumuona Gorii.

Siku hiyo alikuja kumuona Gorii alikuwa ametulia kitandani, Jolvin alifika pale akakaa make walizoea kupiga visitori vya hapa na pale, Gori alianza…..

“” Kaka White.. Afadhari umeugua Anelisa hayupo, make hapa hospitali ingekuwa Jovi… Unaendeleaje, Jovii.. nikuletee Nini?, Jovii… Umekula, Jovii… Sipendi kukuona unakuwa hivi, Jovii… Nikuletee mihogo… Yaani humu ndani tusingepumua..

Jolvin alicheka tu, Kisha akamuuliza.

“” Kumbe hupendi ukaribu wangu na Anelisa.. !?””

“” Sio Sipendi… Yaani napenda mpaka basii!! Huoni namisi.. hizo Joviii…

“Huwa zinakufurahisha Sana ee!?”

“” Achana nae tu! Na bora napumua make hapa ningekuwa nimebanwa balaa.. “

“” Huyo anakufaa bhana! Hivi kwanini nimecheka nilipokuona.. Ani ulivyoingia na hizo gongo unavohangaika kuingia.. umeviligisha kiuno Kama unacheza sidimba ndio ukakaa… Halafu eti Mama kasema Gorii, Jolvin” waje kuwa mme na mke… Viwete wote?.. Si nilikwambia alikuwa na Mawazo haukunielewa tu”

Jolvin alikuna kichwa kwanza huku akimsogelea Gorii akawa amekaa kitandani, Kisha alimtizama.

“” Kwahiyo Wewe hapo hauwezi kukili uzima!? Utakuwa wa kindani maisha yako yote!?”

“” Aaa Kaka White! Nishakukataza kunisogelea Sana! Mpaka huwa naogopa kukujibu! ” Sawa Wewe unazani mi nikiamka hapa si nitakaa kwenye Wheelchair muda wote Kama ile siku nilivyokaa!?”

Jolvin aling’ata midomo kwanza ni tabia yake alikuwa nayo Kisha alinyanyua mkono wake wa kushoto akamshika kichwani.

“” Mimi nakuombea upone! Ukaendelee na Duka lako! Kumbuka niliwaahidi msimu wa Sikukuu duka litakuwa wazi na Wewe utakuwepo! natamani iwe hivyo! Siku ya kesho utaelekea India kuchekiwa naimani ukirudi utakuwa haupo kwenye khari hii Tena!”

Jolvin alimtia moyo Kisha alisimama kuondoka! Lakini Gorii alimshika mkono, ilibidi ageuke kumtizama.

“” Ile siku nilipokaa kitandani kwako uliniambia nitandike! Na wewe umetandua shuka! Tandika!”

Jolvin ilibidi atandike kwa kutumia mkono mmoja! Kisha alimwaga aondoke.

“” Usiku mwema Goryanah! Kabla kesho hujaondoka nitakuja kukuona!”

Siku iliyofuata Gorii alichukuliwa akawa amepelekwa India kwa matibabu! Jolvin yeye alikuwa akiendelea vizuri baada ya wiki moja kuisha alikuwa akitembea bila magongo japo ni kwa hatua moja moja! Na hii ilidhihilisha anaendelea vizuri.

Yapata mwezi mmoja kuisha Gorii ndio alirejea Tena akiwa mzima! Siku hiyo Mishoki family walikuja kumpokea Airport! Kwa pamoja walimpokea kwa furaha huku kila mtu asiamini kumuona yupo sawa sema kilichobadilika ni ile speed ya kutembea haraka ilikuwa imepungua.

Mwanzoni walifikili labda ni kwa muda tu! Hata walipofika nyumbani! Mwendo ni ule ule! Wengine waliogopa kumuuliza lakini Rich akaliwasha!

“” Gorii hivi ni Mimi tu sikuelewi! Inaonekana ulivoenda kutibiwa Kuna ile nati moja ilikuwa imelegea sahii imeenda kukazwa, naona sahii hupamii viti, milango na sofa!?”

Ilibidi wote wacheke ndio wakachangia maada kweli, Kweli!

“” Yaani mlivyocheka hata Mimi nilicheka hivyo hivyo! Baada ya kumaliza kufanyanyiwa matibabu nilijaribu kutembea nikaona huu mwendo sio wangu! Ikabidi niangalie miguu huenda nimebadilishiwa! Aaa! kumbe ni yangu ila huku kwenye kiuno sijui wameweka Nini tu nashidwa kutembea vizuri!”

Wote waliangua kicheko tena! Gorii alizunguka kwanza, akatazama watu wote Baadae akaona kunae watu wawili wamepelea.

“” Macho yangu tu au!!? Kaka white Yuko wapi? Au na yeye tumepishana India kimatibabu! Na huyu J mkubwa yuko wapi!?”

Mama alisogea pale Kisha alimkumbatia kwa furaha.

“” Leo ni sherehe yenu! Tumewaandalia part kubwa ya kufurahia afya zenu! Ingia chumbani kwako ujiandae kila kitu utakachokikuta utakitumia! Halafu ndio utaenda kumuona huyo Kaka White! Na yeye katoka kwenye matibabu Pamoja na wengineo ambao hawapo hapa!”
 
SEHEMU YA KUMI NA TISA

Gori alifika chumbani alikuta Kuna nguo zimeandaliwa pale pamoja na viatu vyake alifanya kujiandaa, wakati huo Mama aliingia chumbani kumtengenezea nywele zake.

“” Waooo! Hapo umekaa vizuri sio Kama unavyochanaga wewe!”

Baadae walitoka ndani kuelekea nje make wenzao walikuwa wakiwasubili, kila mtu aliyemuona Gorii alimsifiwa kwa kupendeza!.

Safari ilianza walikuwa wakielekea kwenye Hoteli moja haikuwa ngeni machoni kwa Gorii! Ni siku moja kabla halijatokea tukio la kumpoteza Mamake walienda kufanya tangazo wakiwa na Doreen!

Gori baada ya kufika pale alianza kujishuku! Wakati wamefika pale taa zilizimwa Gorii akaambiwa aingie Kisha aelekee mbele! Ile anafika mbele anaanza kushangaa shangaa zile taa alibaki kukenua ovyo! Si unajua Kuna vitu vingine vinastaajabu machoni lazima vikuduwaishe kwanza!

Ile bado anashangaa kunae mziki wa taratibu uliachiwa! Aliona Kuna mtu anamnyooshea mkono acheze nae! Hutaamini alikuwa ni Kaka White! Siku hiyo alipendeza kuliko!

Gori alikuwa bado anamushangaa kwanza! Kama miguu imekaa vizuri lakini hata Kaka White nae alikuwa akistaajabu vile vilevile! Akaona wee! Atashangaa mpaka sangapi mziki ni wao! Na macho ya watu yote yanawatazama! Isitoshe sehemu waliyokuwa wakichezea ndie inayo mwanga pekee hivo walionekana vizuri!

Jolvin alimsogelea kwa ukaribu Kisha mkono mmoja alimshika kiunoni huku mkono mmoja wa Gorii aliuweka begani na kuanza kucheza nae taratibu pasina pupa yeyote wakizidi kutizamana.

Gori alikuwaa bado haelewi somo! Muda wote alikuwa akimtazama Kaka White akisitaajabu kwa muonekano wake mpya.

Jolvin alifanya kumkonyeza kwa ishara awe huru kucheza, alifunga macho kwa hisia huku akitafuta matamshi ya wimbo wenyewe unavyosikika ndani ya moyo Wake. Gori nae alikuwa bado akimshangaa Kaka White jinsi anavyovuta hisia na yeye akaamua kuzama mazima kwa ile song.

Mashairi mazuri yalisikika kutoka kwa mwimbaji maarufu aliyejibebea tuzo za uiambaji wa nyimbo zilizojaa hisia, sio mwingine alikuwa ni Westlife, wimbo wake uliachiwa masikioni kwa watu ulikuwa ukisikika taratibu huku ukivuta hisia zilizo ndani ya nyonyo za watu, anakwambia ” My love” Kisha ala za music zinafatisha zikiwa zimetulia kabisa! Baadae mashairi ya Mwandishi yanaanza, anakwambia….

“” An empty street

An embty house

An hole inside my heart.

I’m all alone the rooms are getting smaller.

I try to read,

I go to work

I’m laughing my friend.

But I can stop to keep myself from thinking o. no!

Nimejaribu kujisomea, nimeenda kazini ili nifurahi na rafiki zangu lakini nimeshindwa kujizuia kwa kila kitu.

I wonder how,

I wonder why,

I wonder where there are!

Hakuishia hapo alimalizia mashairi tena anakwambia

“the days we had the songs we sang together”

To hold you in my arms

To promise you my Love

To Tell you from the heart

Your all thinking of..

Mwisho kabisa maneno ya mwishoni mwishoni alimalizia kuyaongea.

“” natamani nikushike kwa mikono yangu, nikuahidi mpedwa wangu ni kiasi gani navyojisikia ndani ya moyo wangu! Wewe ni kila kitu kwangu”

Hatimae wimbo ulienda kumalizika Jolvin alishika kidole Cha Gorii kisha akamvalisha Pete ya uchumba huku akibaki kumtizama akishuhudia uzuri wa Gorii ulivyomchanganya, Upepo nao ulikaa karibu yao uliamua kutumia ile fursa ya kupeperusha nywele ya Gorii kuhakikisha Jolvin anachanganyikiwa zaidi.

Walibaki wakitazamana kwa sekunde kadhaa, baadae Jolvin alimalizia kumkiss kwenye paji la uso huku Gorii alikuwa bado anashangaa na asiamini kitu anachokiona.

Alijitoa mikononi kwa Jolvin, lakini Jolvin alifanya kumvuta taratibu Kisha akamkumbatia tena, Ile Gorii anataka kuongea alimuwahi akamwambia huku akimziba mdomo kwa kidole chake.

“” Because I love you”

Kisha alimshika mkono wakielekea kunako viti vyao maalumu viliandaliwa pale! Wakati wakiwa wanashuka taratibu Gorii alikuwa akikakamaza mkono hataki kushikwa, Jolvin aliishia kucheka lakini alianza kuchukua tahadhari mapema make hachelewagi kusanua jambo.

Wakati wamekaa Pale Gorii alikuwa akitafuta nafasi ya kuzungumza na Jolvin lakini Jolvin akawa anamkwepa, Gorii baada ya kuona anamkwepa ilibidi aanze kuunda stori.

“” Kaka White… Yaani Unajua kucheza ulivyokuwa umenikamatia mkono kiunoni! Nikahisi Kama nipo ulaya! Ila wao wanakuwaga romantic sio Kama wewe!?”

Jolvin alimtizama chinichini Kisha alimsogelea karibu kabisa ili amusikie vizuri.

“” Sio hivyo bhana…! Bibi anatuona” Halafu nilitaka urudie vile ulivyoniambia kwa kingeleza wakati tunatoka pale!”

“” Ooh! Kumbe ulitaka usikie vizuri.. “” Gorii Nakupenda Sana! Natamani nikufanye uwe mkewangu wa Ndoa! Muda mrefu nimeanza kuvutiwa nawe japo mara ya kwanza vituko vyako vilikuwa vinanifanya nishidwe kukuelewa vizuri! Umuhimu wako niliona tangu siku ile ulivyotoka nyumbani nilianza kujisikia vibaya kwanza nilianza kukumisi bila sababu! Ndipo nikajua nimejitenga mbali na mtu muhimu kwangu!

Jolvin alianza kusema ya moyoni lakini alikuja kukatiswa na Rich aliomba acheze na Gorii! Gorii akaona ndio nafasi ya kumuepuka make alimtoa jasho.

Wakati anataka kuondoka Jolvin alimshika mkono Rich! Kisha alimuonesha aangalie pembeni, alikuwa ni Sophia akimtizama.

“” Aaah Unabahati yako! Make nilitaka kumuonesha Broo kuwa Mimi ni zaidi yake kwenye kucheza.”

Rich alifanya kumuachia Gorii, akamshika mkono Sophia wacheze wote.

Gorii alikasirika kwanza huku akimtizama Sophia aliekuja kumharibia tgeti zake, Alijua kabisa Kama atakaa pale maada inaendelea tenaa! Alikaa kwa unyonge huku akisogea pembeni ajitenge na Jolvin! Make tayari ashaanza kumuogopa!

Muda kidogo familia ya Mama Doreen iliingia ikiwa imeaandaa zawadi ya kuwapongeza na kuwapa pole kwa nyakati walizozipitia! Hawajakaa sawa mama Muddy aliingia akiwa na Muddy na wao walikuja kuwaona.

Siku hiyo ilikaa vizuri Sana baina ya watu wawili! Na siku hiyo ndio walitumia nafasi ya kutambulisha Duka lao kwa mara nyingine! Kwani Gorii ndie atakuwa akilisimamia tena.

Muda ulizidi kwenda Sherehe ilimalizika walirudi nyumbani kupumnzika!

Chumbani kwa Gorii ilikuwa ni kelele muda wote hasa akikumbuka jinsi Jolvin alivyokuwa akicheza nae mbele ya watu, maneno ya Jolvin yalijirudia masikioni kwake. “” Because I love you” ndio lilizidi kumchanganya kabisa! Aliangalia ile Pete ikamfanya atabasamu kwanza.

Alianza kuzunguka mle ndani ndipo akamkumbuka Anelisa, alishusha pumnzi kwanza Kisha alicheka.

“” Because I love you!? Vipi huyu Mama wa kulalamika Jovii… Miss u… Jovii.. nikuletee Nini? Jovii.. Jovii…. ” Ngoja nimfuate nikamwambie!”

Huku kwa Jolvin alikuwa amekaa na Wenzake huku wakipiga stori, Esau alimpongeza kwanza.

“” Hongera kwa kuwa jasiri siku ya leo umeongea yamoyoni kwako! Niligundua zamani unampenda Gorii! Hata kumtizama kwako ulimtizama tofauti kuliko hata unavyomtizama Anelisa.”

Jolvin Alibaki kucheka cheka, ilionesha kabisa anae furaha kwa kitu kilichotokea.

Rich ilibidi alale miguuni kwake huku akimtizama.

“” Ila Gorii ilitakiwa Mimi niwe nae! Unajua ana akili Kama zangu! Isitoshe wewe bado hakupendi! Unajua wapenzi huitana majina mazuri ila Wewe Kaka White! Bora niwe Mimi!”

“” Na Sophia…!!?”

“” Wote bhana! Mimi nitaishi nao si wote wananipenda!”

Huku kwa Gorii alikuja kasi akiwa na furaha akiamini amepata majibu ya kumjibu Jolvin! Alifika akagonga mlango kutokana na ile spidi aliyokuwa nayo mlango uliegesha, akawa ameingia nao mpaka ndani.

Ile anatua macho anawakuta wapo wote alibaki ameduwaa, huku Esau, Joely na Rich walianza kumtania wakimuita ” Shemeji, Shemeji” Gorii akakosa ujasiri alitoka mbio huku akiwaacha watu hawana mbavu..

“” Hapa hamna mwanamke!!!”

Joely aliongea huku akizidi kucheka.

“” Nyie nyote ondokeni Mimi nilale.

Ilibidi wamuache make Kama ni chaguo kachagua yeye mwenyewe. Wakati akiwa amelala alikuwa anawaza ni namna gani atafanya kumbadilisha Gorii! Muda mwingine huwa anaboa.

“” Hapana hapana! Mbona nataka kuwa kichaa! Nimeenda kumwambia Kaka white kuhusu Anelisa, nawakuta hawa nao wamo halafu wananiita mi Shemeji yao! Usikute wao wanachukulia serious wakati Mimi natania!”

Ni mojawapo ya Pilika alizokuwa nazo Gorii chumbani katika kuwazua mpaka kunapambanzuka .

Asubuhi yake Familia kwa ujumla waliamka kusaidiana kazi mpaka mida ya mchana kila kazi ilikaa sehemu yake! Mama Muddy pamoja na familia aliyokuwa kaambatana nayo waliaga kutoka na familia ikabakia Kama hapo awali.

Gorii alikuwa Chumbani kwake akipanga panga baadhi ya vitu vyake make tangu apate ajari hakupata muda! Ile katika kukagua ndio anakutana na picha ya Mamake! Ilimfanya akumbuke maisha ya nyuma aliyokuwa akiishi na Mamake kwa furaha leo hii hayupo tena, aliamua kuzihifadhi vizuri kama kumbukumbu!

Baadae alitoka nje ili kutizama mazingira kwanza ya familia ya Mishoki! Siku hiyo alianza kukumbuka maneno ya Mamake kipindi kile wamepata ajari wakiwa wote Kuna maneno aliyoongea, ilibidi amtafute kwanza Jolvin aongee nae.

Alifika Chumbani kwa Jolvin lakini alikuta kumerudishiwa Aligonga mlango kupo kimya mwisho aliingia akichungulia lakini hakunae mtu.

Alitoka kumuulizia Kwa Bibi, majibu aliyoyapata ni Jolvin karudi chuoni kufanya mitihani kaondoka asubuhi, na kuhusu simu kaziacha mpaka atakaporudi.

“” Sasa Bibi… Mjukuu wako yupoje lakini, akipata shida huko itakuwaje!?”

Gorii alitoka akilalamika akiingia Chumbani kwake lakini alirudi tena kwa Bibi.

“” Sasa ndio kaacha chumba wazi!?”

Bibi alimrushia funguo.

“” Kasema ubaki nayo! Atakuwa akikutafuta kwa namba za wanafunzi wenzake!”

Ilipita wiki moja tangu Jolvin aende chuoni pasina kupiga simu yoyote Nyumbani! Esau, Joely, Rich na wao warudi kwenye Pilika zao! Nyumba ikawa ni kimya! Kwa Gorii ilimpatia Mawazo Sana, alianza kukumbuka ukaribu wa Jolvin, furaha aliyomuoneshea kwa muda mfupi ilitengeneza kumbukumbu kubwa, muda mwingine aliwaka hasira akikumbuka Yale maneno aliyoyasema anampenda hakuyaamini Tena alichukulia ni vile alimdanganya! Ilifikia hatua zile fikra zote za kumkumbuka Jolvin alizihamishia kwa Mamake siku akionana na Jolvin alitaka ajue ni kipi alimwambia siku ile anapata ajari.

Majira ya jioni akiwa Chumbani kwake, alikuwa akipitia picha walizopiga hivi karibuni akiwa na Jolvin alibaki kuzitizama! Siku hiyo Mamake Rich! Alifika kumtizama Gorii baada ya kumuona muda mrefu kajifungua.

Mama Alifika akamshika begani huku akitizama picha zilizokuwa pembeni Gorii alizificha na nguo yake, alitambua kabisa Gorii kaanza kumkumbuka Jolvin!

“” Utakaa ndani mpaka lini!? Leo hujaenda chuo umejifungia humu! Bibi yako anakuhitaji Chumbani kwake na wewe upo huku!”

“” Hapana Mama! Nilikuwa nasoma tu! Unajua mitihani ipo karibu kwahiyo muda mwingi nautumia kusoma!”

Mama ilibidi amuache Gorii make alikuwa akielekea kazini!

Baada ya Mama kuondoka Gorii aliingia kwenye chumba Cha Jolvin kwa mara nyingine, alianza kukagua kila kitu kilichokuwa pale, Kuna nguo baadhi alizoea kuzivaa…. Gorii alibaki amezikumbatia!

“” Kaka White.. Nimekumisi kweli!! Leo nimekumbuka maneno yako uliyoniambia siku ile ya party! Nakumbuka siku yenyewe ulivyokuwa ukicheza na Mimi! Nakumbuka siku ile tulivoenda kule kijijini tukaenda kutembea shambani! lakini ni lini utarudi?

Ni siku tatu zilisogea Gorii alikuwa ameanza mitihani ya kumaliza chuo ilichukua Kama siku tano akawa amemaliza mitihani yake! Akawa yupo Nyumbani akisubili matokeo.

Huku kwa Jolvin siku hiyo alikuwa akifungasha mizigo yake kurudi Nyumbani baada ya kumaliza mitihani yake alitizama muda kwanza, aliona bado unatosha alipita Mjini ili aangalie mazaga yoyote Yale ya kupeleka Nyumbani.

Majira ya jioni Jolvin ndio anaingia Nyumbani alikuta nyumba nzima imetulia kila mtu alikuwa amejizoelea ni kumaliza kula na kulala!

Alikaa sebuleni kwa muda wa dakika kadhaa Kisha alienda kumgongea Bibi yake!

“” Gorii haulali na leo tenaa!? Nishakwambia Jolvin atarudi tu!”

Bibi ile anafungua anashangaa kumuona Jolvin yupo pale, alifanya kumkumbatia huku wakikaa.

“” Mjukuu wangu hata simu hupigi Jamanii! Huku mwenzako umemuacha ana khari mbaya! Yaani muda wote anashinda hana furaha akikufikilia!”

‘” Usijali Bibi nitaongea nae tu! Funguo yangu iko wapi lakini!?”

“” Gorii kairudisha Jana kwa hasira kweli analamika kachoka kutunza chumba Cha mtu aliekimbia chumba chake!”

“” Kana matatizo haka! Hebu nisaidie funguo kwanza angalau nitue mizigo ndio nimtafute Goryanah! Wewe Bibi tutaongea kesho pumnzika kwanza.

Jolvin alielekea chumbani Kwake alikikuta chumba chake kimependeza kweli!

“” Waoo Gori mi nakujuaga Wewe ni msafi sana, sema ni akili yako inavokuwa na wenge ndio maana huwa wajisahaulisha!”

Aliingia bafuni kuoga baada ya kumaliza alichukua simu yake akawasha siku hiyo akague baadhi ya jumbe zilizoingia alikutana na ujumbe wa Anelisa akilalamika baadae alimtumia ujumbe wa kumtakia mtihani mwema, kwa Gorii alikuta jumbe zinazomuuliza kurudi kwake aliamua kumtumia ujumbe. “” Leo nimerudi”

Hutaamini Gorii kumbe alikuwa hajalala! Alikuwa akichezea simu yake huku akisubili kutafutwa na namba ngeni, baada ya kuona message imetoka kwa Jolvin ilibidi amjibu” Sitaki matani Bibi’

Akili ilimtuma atakuwa ni Bibi kachukua simu ya Jolvin akimchezea akili, lakini ujumbe uliingia tena “” By Jolvin ( Kaka white) njoo chumbani kwangu.

Aliinuka taratibu huku akiwa kashikilia simu yake! Akijua ni Bibi ndie atakuwa chumbani kwa Jolvin make hata funguo alimrudishia. Aligonga mlango lakini alianza kuhisi Yale marashi ya Jolvin nakubaki kusema huenda ni kweli Jolvin karudi.

Jolvin alikuja kufungua mlango, huku Shauku yake ilikuwa ni kumuona Gorii! Walikutana uso kwa uso huku kila mtu akibaki kumtizama mwenzake akionesha kumkumbuka.

Gorii alimtizama mpaka machozi yakimtoka alionesha ni kweli kamumisi mtaaramu! Jolvin pia alijisikia huruma Sana hata yeye alimumisi sivyo kawaida alimkumbatia kwa sekunde kadhaa! Akawa amemsogeza Hadi kwenye sofa alibaki akimtizama huku macho yake hayaishi hamu.

Alimtizama vidole vyake vya mkononi Kama anae Pete! Kisha alinyanyua mkono wake akashika ile Pete na kumtizama Gorii usoni, alihisi furaha ya ajabu! Alimsogelea karibu Gorii ambae alikuwa ameduwaa kila akizidi kumtizama Jolvin alimuona wa tofauti Sana machoni kwake tofauti na siku nyingine.

Jolvin aliona ile midomo aliyokuwa akiitolea tofauti na ya Anelisa kipindi kile leo ndio ataenda kugundua utofauti ulioshidwa kuamini kuwa ile yote ni midomo! Aliamua kujirizisha mazima isiwe kuona tu pasina kugusa akawa amepata deep kiss! Lililojibu majibu ya maswali yake!”

Hatimae kunapambanzuka! Jolvin aliwahi kuamka asubuhi kabla ya Gorii hajaamka alibaki akimtizama zaidi na zaidi huku akitabasamu tu! Aliamua kumfunika shuka huku akiamka kuelekea bafuni! Baada ya kumaliza kujiandaa aliwahi kukifunga chumba Cha Gorii ili wasimsitukie na Kama watamuuliza itabidi awadanganye kaitwa chuoni Kuna form ya kujaza.

Alirudi chumbani kwake ndio anamkuta Gorii kaamka akijaribu kushuka kitandani, Alibaki akimtizama kumuonea huruma Sana! Aliamua atoe msaada alifika akambeba kumpeleka bafuni Kisha alimutaka radhi.

“” Nisamehe kwa yote yaliyotokea! Lakini hakutaharibika kitu! Najua unagopa Bibi atakutafuta! Ila nimewaambia umeenda chuoni utarudi jioni! Na leo utashinda chumbani kwangu halafu jioni nitakutoa naimani utakuwa sawa
 
SEHEMU YA ISHIRINI

Majira ya jioni Jolvin alifanya Kama walivyokubaliana na Gorii, alitazama mazingira ya pale Kama kupo salama Kisha alimtoa Gorii Chumbani kwake akampeleka ndani kwake!

Alirudi Chumbani kwake kisha alijitupia kitandani na kuchukua simu yake akimpigia Esau.

“” Yaani Kaka mkubwa! Leo najisikia kuwa na furaha Sana! Kale katoto bhana kana akili za juu juu ila kapo Safi! Unajua nataka tuanze vikao vya harusi mapema nataka nikamiliki mazima!””

“” Si nilikwambia unagopa bure tu! Vipi mama mideko unampeleka wapi!? Mama wa Jovii… Anakupenda yule!!?”

“” Ni Kama rafiki tu kwangu! Na sijawahi kuwa na Mawazo nae tofauti !”

“” Okay! Mimi nishaongea na Joely pamoja na Rich! Ajabu Rich nae anataka aoe siku hiyo hiyo amchukue Sophia!”

“” Bado mdogo bhana! Yaani yeye mwanaume lakini akili yake Kama ya Gorii Sasa huyo mke atammeneg Kweli?”

“” Baadae bhana ngoja nifanye kazi za maboss hapa! Wewe sahii si unasubili ajira tu! Halafu mbona hujaenda dukani kwa Bibi!? nikija huko nitaangalia ila kumbuka kuulizia usia wa Mama Gorii tujue imekaaje pale!”

“” Wewe si nimekwaambia nilikuwa na msala na Shemeji yako! Jioni nitamfata Bibi! Anajua nimetoka nafatilia mambo ya kazi.

Jolvin alikata simu huku akifikilia jukumu alilokabiziwa na Mama Gorii, alimpigia simu Mamake apate majibu lakini alimjibu yupo busy kwanza!

Mida ya jioni jioni wakiwa wamekaa pale sebuleni, alikuwa ni Jolvin akimuelekeza Gorii jinsi ya kutuma maombi ya kazi.

Ghafra mlango ulifunguliwa kwa kasi sana, walishituka wote kwa mshangao alikuwa ni Anelisa katia timu huku kashikilia picha zikimuonesha Gorii na Jolvin siku yenyewe wakiwa wamekaa sitaili za wapendanao, Alifika akazirusha mezani zikawa zimesambaa meza nzima, Alianza kupandisha sauti huku Gorii akibaki kutetemeka kwa woga!

“” Jovii… Kumbe umefanya yote kwa sababu ya Gorii! Kila mara nimejaribu kukuoneshea hisia zangu hutaki kuzisikia kabisa! Muda wote nimekaa kukusubili wewe lakini leo ndio umenifanyia ukatili kiasi hiki.. Jovii… Mbona lakini unaiaibisha familia yangu siku zote! Nmekataa wanaume wangapi wenye hadhi kukuzidi hata wewe, sababu yako tu nimekuganda! Ona leo unavyoenda kuurarua moyo wangu!

Anelisa alizidi kulia huku akimsogelea Jolvin Kisha alimkumbatia akizidi kumwaga machozi mgongoni kwake.

Gorii Alibaki akishangaa huku moyo ukianza kumuuma, aliamua aondoke angalau akalilie Chumbani ile anageuka tu Jolvin alimshika mkono, huku akimpatia ishara asiondoke lakini kwa Gorii akawa Kama kamchochea aongee japo pale alikuwa Kama anataka kujizuia asiseme kitu.

“” Kaka White… Siku zote huwa unachukulia simple simple tu! Nilikwambia Anelisa anakupenda wewe, wewe huwa husikii anavyolalamikaga muda wote ni Joviii.. Joviii wewe hujui anakupenda!?

Jolvin alimkata jicho lilimpa majibu abaki kimya Kisha alimshika mkono Anelisa akampeleka Chumbani kwake akafunga Mlango.

“” Anelisa unajielewa kwelii.. lini Mimi niliwahi kukufungukia wewe kuwa nakupenda? Lini nimeijulisha familia yangu au yenu nikatangaza kuwa Mimi na wewe tuna mahusiano!? Please Anelisa hupaswi kuongea vile mbele ya Gorii kajisikia vibaya Sana! Isitoshe hata Gorii analitambua hilo kuwa wewe sio mtu mzuri kwangu pamoja na familia yako kwa ujumla! Siku ile ulipanga mipango gani pindi unaniomba nikuletee dawa chuoni! Si ulitaka nikifika uniwekee madawa ya kulevya nilewe ili nitembee nawe! Na asingekuwa Gorii kuleta maigizo yake kuwa anaumwa leo ningekuwa nimedumbukia kwenye shimo nisiloweza kutoka! Vipi kumtesa mtoto wa watu ukamlipa yule Askari amfanyie ukatiri? Huna hata huruma mtoto wa watu amebakiwa na alama kwasababu ya roho yako mbaya! Anee… Mbona unapenda maigizo Sana!?

Jolvin alimaliza kuongea mpaka mwili wake ukawa unatetemeka kwa hasira! Unaambiwa Omba Sana usikutane na mtu mpole akachukia siku hiyo itabaki mbaya kwako.

“” Lakini Joviii…..!!?”

“” No.. Anelisa nimechoka maigizo yako! Naomba ondoka kabla sijachukua maamuzi siyo!”

Jolvin alimshika mkono akamtoa nje Kisha alifunga mlango akaanza kujirusha rusha kitandani kwa hasira!

Huku Anelisa alifika sebuleni alimkuta Gorii kabebelea mabegi aondoke, baada ya kumuona Anelisa ilibidi asimame kwanza.

“” Anelisa.. tuondoke tu humu Ndani! Jolvin mwenyewe ndio haeleweki sijui anampenda Nani? Nisaidie kubeba begi zangu nitaenda kutafuta nyumba za kukaa nje!”

Anelisa Alibaki akimtizama Gorii akaona nae anamletea maigizo aliyapiga teke mabegi yote yakaanguka chini.

Jolvin alitoka kuangalia kinachoendelea pale ilibidi amshangae kwanza Anelisa Kisha alikaa kwenye kiti.

“” Nyie piganeni bhana! Mabegi yamekosea Nini hapo!?”

Gorii alimtizama Jolvin kwanza Kisha aling’ata midomo kwa hasira akamgeukia Jolvin amtwange ngumi ya pua, Jolvin akawahi kumdaka Kisha akaurudisha mkono.

“” Nipige huku naona sio kwa kuniibia ibia! Mimi sio muwindwaji!?”

Baada ya Anelisa kumaliza kusasambua pale Jolvin alimsogelea Kisha akamkamata mkono.

“” Nimekwaambia sitaki kukuona humu Ndani! Halafu sitaki ufike nyumbani uniletee Drama zako hukawii kuja na familia yako nyumbani.

Gorii Alibaki akimtizama Jolvin asiamini ni Kama anaweza kumtetea vile mbele yake! Anelisa aliondoka kwa hasira huku akipigiza miguu yake chini Kama kakosa nafasi ya kushindania umisi.

Jolvin Alibaki amemshikilia Gorii mkono! Alisimama akaanza kukusanya zile nguo huku wakiwa wanasaidiana kwa pamoja! Baadae walirudisha nguo ndani. Gorii alikuwa bado akimtizama Jolvin jinsi alivyobusy kukunja nguo, Jolvin nae anainua kichwa Kisha alitabasamu kwanza akaongea.

“” Mimi na wewe tuliandikiwa tuishi pamoja! Kama utakimbia mbali na mimi! Mimi sitaweza kuishi bila wewe!”

Gorii alitabasamu huku akiangalia pembeni, hutaamini katika kuongea kwake kote lakini wakiwa faragha na Jolvin huwa anashidwa kuongea kitu zaidi ya kutabasamu na kucheka.

Jolvin alimsogelea karibu Kisha alimuwekea mkono wake kwenye bega akimwegamia.

“” Najua unahamu ya kujua kuhusu maneno aliyoongea Mamako siku yenyewe ila leo majibu utayapata! Kazi hii nimemuachia mama, tayari kanitumia ujumbe kuwa anae majibu!

Gorii Alibaki ametoa jicho asiamini, aliamua kumkumbatia kwanza Jolvin, baada ya furaha kuisha ndio anakumbuka kumbe alizidisha mazoea na muda huo yupo mikononi kwa Jolvin! Aliijiengua haraka mpaka Jolvin akabaki kumcheka.

Usiku huo wakiwa mezani mama alianza kuelezea majibu aliyoyapata.

Mishoki alikuwa na rafiki yake Kama mnamfahamu Mr. Shejoh! Ni mfanyabiashara maarufu hapa Nchini! Miaka ya nyuma aliomba kuwekeza Shea katika kampuni yetu wakawa wameshindana na Mishoki akaamua kujiengua katika biashara!

Sitori yake ya maisha anae familia yake inakaa nje ya nchi huku alikuja kibiashara tu! Alifikia kwenye hotel moja kipindi hicho akiwa bado ni kijana katika kutembea tembea ndio alikutana na Mama Gorii yeye akiwa bado ni binti mdogo walianzisha urafiki baadae yakazaliwa mahusiano ndani yao, mwisho kabisa alimbebesha mimba ya Gorii. Muda huo Mama Gorii alikuwa kachukuliwa na familia moja iliyokuwa ni rafiki wa familia yake kumsomesha kutoka kijijini.

Wazazi wake baada ya kugundua hilo walimkemea vibaya asirudi nyumbani tena! Alimtafuta Mr. Shejoh akawa ameikataa ile mimba! Lakini aliondoka huku akisema “” Naamini hii mimba nimembeba mtoto wa kike hata akizaliwa nitamuita Goryanah atakuwa ni mpambanaji siku zote daima atauchukia umaskini, nitakaa mbali na familia yako hata yeye nitamtenga mbali na wewe hautakuja kumuona kamwe labda mtoto ndie akutafute na sio Mimi” aliweka Ni Kama kiapo.

Mama Goryanah aliamua kujitenga na ile familia ndipo alipohamia kijijini ambako alikokuwa akikaa mpaka Sasa, aliamua kubadilisha mfumo wa maisha akaanza maisha ya kawaida Sana kwa kujichanganya na kile Kijiji, alimlea mwanae mpaka akakua na hakuwahi kumwambia kitu chochote kuhusu maisha yake ya nyuma! Aliamua kufutilia mbali familia yake pamoja na mzazi mwenzake na ndio maisha aliyomlelea binti yake!

Mama alimaliza kuongea huku kila mtu alikuwa kimya akimuonea huruma Mama Gorii kwa maisha aliyoyapitia ila kila mtu alibaki kushangaa maamuzi yake aliyoyachukua.

Gori yeye Alibaki akilia kumbe Mamake alipitia maisha magumu kiasi kile, Jolvin alimuuliza mama kuhusu Mr. Shejoh watampata vipi?”

Gorii alikohoa kwanza Kisha alifuta machozi akaongea..

“” Mamangu hakutaka Mimi nijue familia yangu! Kuhusu Baba hakutaka kabisa amsikie! Kama angekuwa ni Baba anataka amuone binti yake angenitafuta? Hapa inaonesha hata huyo Mr. Shejoh hakutaka kusikia kuhusu Mamangu pamoja na mwanae! Mimi naona iwe hivyo daima! Sitaitafuta ile familia iliyomkana Mamangu wala familia ya Mamangu.

Siku zote watu unaoishi nao vizuri hao ndio familia yako ya Baadae! Naamini katika hili familia yangu itakuwa ni Mishoki Family nami nitasimama kwa niaba ya Naina katika nyumba hii kamwe sitaikimbia, nitabaki na Kaka white nitampambania pia kufikisha malengo yake! Namimi nitapambania Duka la Bibi, Daima nitatoa Ushirikiano kama mwanafamilia tena nitasimama Kama mkamwana wa hii familia!

Gorii alimaliza kuongea Kisha aliwahi kumkumbatia Mamake huku akilia kutoa maumivu ya nyuma na, kuanzisha familia mpya ndani ya moyo wake! Alienda kumkumbatia Bibi tena kwa furaha huku akimuahidi hatomuacha tenaa.

Alimaliza akamgeukia Jolvin ambae alikuwa ametulia akizani amesahaulika, aliishia kutabasamu tu asifanye chochote! Jolvin akawa amejiongeza alifanya kumkumbatia huku akimuachia asikie neno kutoka kwake make kila mtu aliongea nae!”

Gorii alimtizama huku akiwa anamuonea aibu alimuita kwanza.

“” Kaka White.. Mjukuu wa Bibi. Siku ile ulivoingia ndani nilianza kukuita haya majina kabla hata sijakuona! Ila umeendana nayo kweli make wewe ni msafi wa moyo Hadi nguo zako ni nyeupe nahisi hata unae moyo wenye rangi nyeupe!”

“” Kwahiyo..

Jolvin alimhoji.

“” Kwahiyo Nini tenaa..? Maswali uliyokuwa ukiniuliza siku ile twacheza yalinitoa jasho Kweli!! Ila leo nayajibu kumbe nilitakiwa kusema ” ndio” namaanisha nipo tayari kuolewa na wewe!”

Jolvin alimpigia makofi, Mama na Bibi nao wakafatia wakifanya vilevile. Gorii Alibaki kuwashangaa nae akaliunga kufanya vilevile, mwisho kabisa Jolvin aliongea.

“” Daima Gorii huwa anajipongeza kila mara akifanya vizuri katika Jambo lake, Nasi leo twaungana kufanya vilevile Gorii huwa anafanya baada ya kushinda! Na mwezi kesho tayari kwa Ndoa make kila kitu tumeshakiweka sawa! Ndoto ya Mama Jolvin kumuoa Gorii Sasa inaenda timia na hakutakuwa na mbambamba tena. Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako

¶¶¶¶¶ MWISHO¶¶¶¶¶
 
Back
Top Bottom