SoC02 Ndoto yangu shuleni Sumbawanga

SoC02 Ndoto yangu shuleni Sumbawanga

Stories of Change - 2022 Competition

highmark

New Member
Joined
Aug 24, 2022
Posts
2
Reaction score
2
Nikiwa Form Six Sumbawanga Sec, Ilikuwa ni siku ya Ijumaa,Siku ambayo tulikuwa tunawahi kutoka Darasani kwani ilikuwa ni siku special kwa ajili ya Michezo.

Basi bwana me nkiwa na kibaiskeli changu nilichochukua kwa Dogo mmoja wa Olevel... chini nkiwa nmepiga Soksi na Sendo huku juu tisheti na track(shamba dress).

Nikiwa naelekea kwenye Shule flan ya wavulana Kantalamba kupeleka picha nilizowapiga kwenye sherehe ya mahafari ilyokuwa Sku kadhaa nyuma.

Haya bwana.. nkiwa nmebakiza kama mita 80 hivi nfike pale Kantalamba Boys nlisikia gari ikinipigia Horn..mara ya kwanza... nikavunga ,ya pili nikajisemea huyu vip haoni njia au dharau? Mara ya tatu nikajiuliza kwanini unanipigia horn wakati nipo na baiskeli yangu pemben kabisa mwa barabara.

Baada ya kuona inaendelea kunpgia horn ilnbidi nigeuke nyuma kuangalia kuna shida gani. NILITAHAMAKI nilipogundua kuwa kumbe ni gari ya Mkuu(headmaster) ndiyo ilikuwa nyuma yangu na Nilivogeuka tu iliniwashia taa ikinitaka nisimame. Sikuwa na jinsi ilinibidi nisimame nimsikilize.

Mara tu baada ya kusimama Mkuu akaniuliza dogo unaelekea wapi?..nikamjibu naelekea pale Kantalamba Boys..akaniuliza "Vipi una kibali cha kutoka nje ya shule"?..dah kibali chenyew sikuwa nacho basi kinyonge nikamjibu kuwa sina kibali Mkuu. Basi kiufupi kabisa akanijibu "ukirudi Shule tuonane"....

Niliganda pale kwa sekunde kadhaa Nikijisemea kimoyomoyo leo nmekamatika maana pale nilikuwa na kiswaswadu changu mfukoni na kwenye kikapu kwenye baiskeli kuna kibeg chenye Kamera ya Shule ambayo nilikuwa naitumia kipindi chote nikiwa shule, baada ya Mwl fulani aliyekuwa anakaa nayo kuniamin sana na kuniachia bila Mkuu kujua. Sasa nikajiuliza vipi angejua kuwa hapo nilipo nna kamera yake na bado natoka Nje ya shule bila Kibali na mavazi yasiyo rasmi na nna simu?

Basi nikaisindikiza ile gari kwa macho nkagundua kuwa inaelekea pia kwenye shule hyohyo nlpokuwa naelekea.

Basi bwana nkasema kuliko niende huko saiz naweza nkafka nka charazwa stick na Mkuu maana nae ameelekea Kantalamba Boys ngoja nimsklizie mahali nkimuoma ametoka na me ndyo naenda.

Bas nkafanya hvyo na Baadae nkarudi zangu School na ile naingia tu nkakutana na Academic.
Akanambia "Imma nimepata taarifa zako dawa yako ipo jikoni..nimepigiwa simu na Mkuu anasema nimekutana na kijana mweupe simjui jina..nikajua hakuna mwingine zaid ya Imma"

Nkasema dahh nimeisha!
Bas jion baada ya msosi nikaitwa ofisi ya Malezi na Ticha flani..
Ile kufika tu akanipa kibahasha kukifungua pale nakutana na Barua ya Sunspension ya week 2 na nkirudi nirudi na Mzazi...

Dah nkawaza pale inakuaje mbona kosa langu lmechukuliwa serious sana maana ni mara kbao tu tulkuwa tunatoka bila kibari ...muhimu isiwe muda wa darasani tu na sometimes wengine wanakutana mtaani na Mkuu wakiwa wamevaa mavazi ya nyumbani kabsa but Mkuu anatoa adhabu za kawaida tuu za kufyeka na life linasonga sasa inakuaje hapa ..naanzaje kumwambia Mzee anielewe maana Mzee wangu namjua ni mkorofi? ,,bora hata Bimkubwa angenielewa.. namtoaje Mzee mwanza mpaka Sumbawanga kwasababu ya Ujinga wangu.???!! nkamuomba ticha niombee msamaha akakaza hakunisikiliza.

Bas bwana skuwa na jinsi zaid ya kwenda Dormitory kufunga vilivyo vyangu maana nilipewa dakika chache tu nisionekane mazingira ya shule.

Uzuri ni kwamba nilifurahi kutoka shule bila Mkuu kujua kilichokuwa kinanipeleka Kantalamba na hakujua kama natumia kamera ya shule maana angejua huenda angeninyang'anya kabisa ..basi nilifanikiwa kutoka na kamera ..yule Mwl bado aliniamini ingawa Mkuu alinifukuza...Na kitu chema kabisa pale Sumbawanga kuna Familia ambayo iliniamin sana na ilinichukulia kama mtoto wa pale maana hata likizo fupi zote nilikaa pale. Kwahiyo ikawa rahisi kwangu kupata sehemu ya kuish nkajsemea hata Wazazi home siwaambii tena..wiki mbili zikiisha ntamchukua sister mmoja wa hapa home nkaseme huyu mamdogo wangu nirud zangu skull..

Baada ya kuendelea kupiga pesa mtaani siunajua tena vijana wanapenda mapicha ya location..

Sasa zikiwa zimebaki siku Tatu tu nirudi shule Si nikapata dili la kwenda kusaidia kushoot HARUSI..
picha likaanza sasa.

Wakati najiandaa nkashangaa naona simu kutoka home..Lol! Mzee anapiga simu?

Kuna nin tena..nilijiulza maswali mengi kabla ya kupokea ile simu.

Nlijifariji nkasema labda amepiga kunisalimia maana mzee alikuwa anafahanu kuwa nipo na simu shule japo hairuhusiwi.

Basi ikabidi nipokee na swali lake la kwanza lilikuwa upo wapi?

Nilitumia sekunde kadhaa kabla ya kumjbu ,nilijiuliza mpaka kuniuliza nipo wapi it means tayar kuna kitu itakuwa amekisikia..basi ikabidi nifunguke.

Ikabidi nimmwambie mzee ukweli bhana japo alnfokea sana..na pia aliambiwa na Mkuu kuwa mtoto wako hajatulia ni muhuni sanaa..Olevel ana wadada kibao wanamuita shombe shombe..na aspoangalia tutanfukuza kabisa huyu asfanye necta maana hawa ndyo mwisho wa siku wanatuletea 0 hapa shuleni.

Dah bas ilibidi nimsklize tu mzee mpaka amalize kuongea maana alkuwa ameshanyweshwa sumu..
Na alichukulia kama mwanae nishakuwa muhuni sanaa..na skuweza kumlaumu Mkuu maana ni kweli pale shuleni nlkuwa famous sana na sababu kubwa nilikuwa kiongozi wa Social(Starehe na Maafa)..kama mnavowajua wanafunzi na maswala ya Muziki..Ilikuwa Imma Social nikipita madarasani wanafunzi ni shangwe tu sasa hapo hata ujkeep busy vp wadada wa olevel wataacha kukupenda..? hata uspowajari wenyewe hata ukiongea nao tu tayari umedate nao sasa hyo ndyo ilinichafulia juu na kuonekana kama kijana Muhuni,japo nlkuwa natimiza Majukumu yangu tu coz bila kuwa Social na ni Kiongozi wa Social ilkuwa sio rahisi.

Haya sasa nikayamaliza na Mzee japo hayakuisha mzee aliendelea kukasirika sana na habari alzofikishiwa alizifikisha kwa ndugu zangu wengne hivyo kila mmoja aliniona mbaya na for sure hakuna nlompgia simu na akaonesha kuwa upande wangu kila mtu alkuwa ananchukulia kama kijana niliyeharbika tayari japo nilipita shule nying za boarding zkiwemo seminary na shule za kanisa na skuwah kusemekana kuwa mtovu wa nidhamu.

Basi maneno ya Mzee hayakunivunja Moyo kwani me nilijua natetea kile nnachokipenda ..Me nikajiandaa zangu niende nikashoot harusi.,ilikuwa ni nje kidogo ya mkoa basi nikachukua usafiri nikafika kule tukaweka vifaa sawa..na sherehe ya usiku ikaanza.

Basi me nikaendelea kupiga zangu kazi..ILA NILISTAAJABU nilipoona gari ya Mkuu pale nje😤 sasa nkajiuliza huyu Mshikaji amefikaje tena huku sasa ikabidi niangaze mule ukumbini kuangalia kama kweli yumo..na SKUAMINI macho yangu pale nlpomuona Mkuu na suti yake amekaa kwenye viti vya ndugu upande wa Mwanaume..nkasema Dah kweli nmekamatika.

Kuna muda nikamuona kama ametoka kuongea na simu nkasema hapa sina ujanja mshikaji ashaniona..inabidi nikamgei tu hata hi..huku nkjsemea kimoyo moyo hata kama ningekuwa mimi swez kukubari Form six wangu ambae anatakiw atulie shule asome na amebakiza miez kadhaa afanye mtihani lakini yeye yupo serious anasshoot harusi.

Basi nikamgei hi pale akaitikia vzuri tu kama vile amekubari nnachokifanya.

me nkarudi zangu kuendelea na kazi.

Siku ya kurud shule ikafika nikiwa na experience kutokana na kesi za nyuma za wanafunzi wenzangu ya kuwa mtu yeyote ukienda naye kama mzazi hawez kataliwa ili mradi umempanga vzur tu Basi me nikamchukua yule sister angu nikampanga aseme yeye ni mamdogo wangu nikampanga na mzee kama akipigiwa simu aseme hivyo pia..basi kwenda Skull yule sstr aliulizwa swari dogo sana na anashndwa kujibu na kuonekana sio hata ndugu yangu.

Basi nikawa na kesi mbili nyingine tena kesi ya kuidanganya shule na kesi ya Mwanafunzi kuingia kwenye kumbi za starehe.

Nikaongezewa wiki moja nyumbani na nikirudi nirudi na mzazi kutoka nyumbani.

Hapo ndyo nilipochanganyikiwa zaidi
Nkajiuliza nafanya nini maana mzee hawez kabisa kuja.

Basi kama muujiza vile kuna sehemu Nilienda kutoa hela na laini niliyokuwa natumia ilikuwa na usajiri wa majina ya Mama angu..ambayo jina la mwisho ni Manyangu nilipotoa hela pale yule dada akaniuliza wewe ni Manyangu wawapi..?mbona kuna akina Manyangu wengine wapo huku..kwani hauna ndugu huku?

Nikamwambia hapana sina kabìsa ndugu huku..Nkajisemea kimoyomoyo mimi SUMBAWANGA kabisa Niwe na ndugu? yule dada hakukubari niondoke alinitafutia mtoto akanambia mpeleke huyu kijana kwa Mzee Manyangu.

nilivofika pale nilistaajabu nilivokutana na watu nafanana nao kabisa ..kumbe ni akina anko na mamdogo Ndugu upande wa Mama watoto wa Babu alyefariki kitambo kidogo..basi kumpigisha story za Sunspension Bibi angu pale akanambia hilo ni jambo dogo sana mjukuu wangu kwasababu hata yule Academic wenu anakuja sana hapa na amesoma na mwanangu wa pili.

Basi wiki ilivyoisha Bibi alinipeleka shule na kesi ikawa imeishia hapo..Japo niliporudi shule sio Walimu sio Wazazi sio Wanafunzi wenzangu hakuna alyekuwa na imani na mimi katika elimu tena,Lakini nilishukuru sana Mungu kwani ufaulu wangu uliwashangaza wengi kwani nilifanya vizuri zaidi hata ya baadhi ya Wanafunzi wenzangu waliokuwa wanategemewa kufanya vizuri zaidi.

KWASASA nayaishi maisha ya ndoto zangu kwani sasa ni Waziri wa Habari, Ubunifu na Mahusiano ya Kijamii Serikali ya Wanafunzi NIT na ni Photographer na tayari nimeshinda tuzo ya SONIT SOCIAL AWARDS 2022 as the BEST PHOTOGRAPHER Chuoni NIT.

Hivyo ningependa kuwaasa vijana wenzangu wazipambanie ndoto zao,iwe ni kwa kuchukiwa,Kudharauliwa,Kutothaminiwa au kutopendwa jua kwamba lazima tu kuna wachache ambao Mungu atawaweka upande wako na kupitia wao atakupigania. Na sikuzote Mungu anapokuletea Changamoto fulani kwenye maisha Yako lazima kuwepo na Njia ya kuitatua.
#MuaminiMunguUtashinda
#truestory
@highmarkpixels
Imeandikwa na Emmanuel Castory Kulwa 0764005785

IMG_20220907_182219_055.jpg
 
Upvote 3
Back
Top Bottom