Ndoto yangu: Watanzania niwauzie sato anayeishi

Lububi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,158
Reaction score
3,808
Nina mpango wa kufuga sato ziwani Victoria kwa mfumo wa cages. Lakini zaid natamani wateja wangu hasa Dodoma na Dar wamle huyo sato kwa kumnunua akiwa hai. Maadam anavuliwa akiwa hai.

Naomba kujua consultant wa wazo langu. Naona wachina uganda wamefanya vizuri sana eneo hili. Ndoto hii ikikwama sijui Mungu nitamwambia dunia niliitendea nini!
 
JKT Suma hua wanafanya consultation kwny shughuli hio,pia na wao huko ziwa victoria wana mradi kama huo boss.

All the best.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi SUMA JKT kwa suala kama hili hadi uende huko musoma walipofungua mrad au wana department dar? Neno JKT nalo linapunguza nguv ya kuwafata!
Nadhani JKT Suma wana branch kila mkoa unaweza kwenda kwny branch yao iliyoko kwnye mkoa uliopo wakakupa maelekezo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hongera kwa kuwa na wazo zuri, ninaamini ni jambo linalowezekana kabisa, niliwahi kuona documentary moja kutoka NHK JAPAN kuhusu jambo hili , jamaa alikuwa na lorry maalum lenye aquarium ndio alikuwa anatumia kusambaza samaki mtaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh...! Weweeeee...[emoji117][emoji117][emoji117][emoji117][emoji117]. Sitaki kabisa. Hata kudanganywa kwamba sijui ni wa nini wa nini sitaki. Nikija dar ni matunda tu na samaki fresh

Sent using Jamii Forums mobile app
70% ya matunda yanauzwa Dar pia ni zao la hybrid so kula vitu artificial kwa dunia ya leo haiepukiki mfano ukila papai la Dar basi ujue mche wake ulipandwa miezi sita hadi nane iliyopita vivyo hivyo mapera na kuna machungwa yanauzwa hasa kipindi hiki unabaki kushangaa tu jinsi yalivyo.

Sent using mazonge yamezidi
 
Ni kweli mkuu. Wazungu wametukamatia kweli. Siku hizi mbolea za kemikali hadi kwenye miche ya matunda na yanapuliziwa dawa pia ya kuua wadudu. Lakini huwezi kulinganisha na samaki wa kufugwa. Hawana test hata kidogo ya samaki,ni kama madudu. Ziwa nyasa limegawanyika,kuna upande wa malawi na Tz. Upande wa malawi wanafuga samaki ziwani. Yaani wanatenga eneo humo ziwani ambalo wavuvi hawatakiwi kulifikia kuvua. Hapo wanakuwa wanapeleka chakula mara kwa mara humo ziwani. Inafika kipindi serikali inawavua hao samaki mahala hapo,wanawauzia watu wa kuwatembeza mitaani. Wanawaleta mpaka upande wa Tz,lakini hawapati wateja kabisa,wananunua wapita njia wasio wenyeji. Lakini ukimuona huyo samaki kanona kichizi, lakini ndani kumla madudu kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…