Ndugai awaponda wana Mwanza kwa kuezeka nyumba zao na Mabati ya kizamani, Masufuria

Nyani siku zote haoni kundule
 
..Je, ni sahihi kufanya utani wa kikabila ktk shughuli ya KITAIFA?
 
Heri ya sikukuu ya wafanyakazi duniani(mei mosi) ndugu zangu watanzania. Nimeleta uzi huu kukosoa Kauli ya Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu Job Augustino Ngugai alipopewa nafasi ya kusalimia mbele ya mh Rais alisema anazungumza na watani wake na kusema;natamani mbadilishe hii milima kwa sababu mmejenga nyumba na kuezeka kwa Sufulia badala yake watumie mabati ya kijani.

Namuuliza ndugu yangu huyo,anao mchango wowote wa kujenga hizo nyumba? Bunge lake lina mikakati uliokwishaweka kuwasaidia wananchi kujenga nyumba za kisasa.

Je, alikwishajiuliza wananchi hao walijenga nyumba kwa muda gani.Watanzania wamezoea kudunduliza Kidogo kidogo Ili kukamilisha ujenzi huo.

Namuuliza Ndugai anawachangia kiasi gani Ili wananchi wa milimani waezeke kwa bati za kijani?
Amemalizia kwa kusema vijana wawe waaminifu sehemu zao za Kazi.
 
Mkuu

Hivi huwa unazingatia anachokisema huyo jamaa?

Mwambieni huyo spika kwamba ni bora kuezeka nyumba kwa kutumia sufuria ambalo limetengezwa kwa kutumia mali ghafi ya 'Aluminium' kuliko nyumba za kwao ambazo zinapaa la tope ambalo likinyeshewa mvua huotesha nyasi na kuvuta majoka kuingia ndani, hiyo ni sawa na kuishi kwenye kichuguu, je ni nani hapo yuko salama?

Dodoma haiwezi kulifikia jiji la Mwanza kimandhari, kimaendeleo, mabadiliko na bidii ya kazi bila kutegemea nguvu ya serikali kuweka miundo mbinu.

Dodoma inewezeshwa na inaendelea kuwezeshwa na serikali katika ujenzi wake lakini Mwanza wakakazi kwa nguvu zao binafisi wanajiendeleza hata Kampala Uganda watambua hilo.
 
Kwahio kwamba waweke mabati yaliopakwa rangi na sio sheet plain zile!
 
Mimi sio shabiki wa Ndugai..

LAKINI kwa Aliyoongea leo nadhani alimanisha usafi wa Mji na Kupanga Miji yetu na kwamba kule milimani watu wapande miti.

SIDHANI KAMA ALIKUA NA NIA YA kuwazodoa.
 
Mimi sio shabiki wa Ndugai..

LAKINI kwa Aliyoongea leo nadhani alimanisha usafi wa Mji na Kupanga Miji yetu na kwamba kule milimani watu wapande miti.

SIDHANI KAMA ALIKUA NA NIA YA kuwazodoa.
Huwezi kupanga mji juu ya milima ambayo wasisi wa taifa walishindwa tangu 1961 halafu uje uanze kokosoa kana kwamba mliwawezesha miundo mbinu ya viwanja na barabara.

Zamani mji wa serikali ulikuwa Isamilo karibu na hospital teule ya mkoa Sekou Toure walipoona umezunkwa na wenyeji pande zote kwenye vilima wakahamishia Capri-point barabara ya Nasser ambapo pia walishitukia wahamiaji wamevamia ujenzi wa nyumba za makazi upande wa pili wa mlima (idara ya maji) ambako hawakutarajia, ndipo matajiri na wafanyabiashara walipoanza kumiminika kushusha makasiri matata ambako hadi sasa wanaoishi huko ni sawa na Masaki/Msasani/Oysterbay ya DAR. Ni kama ilivyo Mtwara, maeneo ya Shangani waliowekeza na wale wenye vipato vya juu.

Au Mbeya eneo la Uzunguni na Forest Mpya weney nguvu za kiuchumi ndio wamehodhi.
 
OP umesahau kua Ndugai no Mgogo na Wagogo no watani wa sisi Wasukuma.

Au umesahau JPM alivyokua akimtakia Ndugai na Wagogo kua ni wale akina Matonya, ni mila na tamaduni za ki Tanzania, rudi darasani...
 
Wasukuma na wagogo ni wapumbavu sana.
Yaani mtu anapewa nafasi kuongea na Taifa anakunyakunya tu hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…