field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 1,171
- 2,732
Huyo Speaker Ndugai ni shida sana kwenye hiki chama, hafai na hana quality ya kuwa mbunge licha ya kuwa speaker. Hivi anavyosema tusikope, anaelewa anachofanya? U.S, UK na nchi zingine zinakopa ili zipeleke uchumi mbele, huyo Ndugai anadai eti tusikope.
Kenya wamekopa na ku-invest kiasi kikubwa ingawa kuna corruption, leo wamekuwa na GDP kubwa ya USD Bil. 109 hivyo wamekuwa nafasi ya 6 kwa uchumi mkubwa Africa, sisi tulikuwa wa 10 kwa kiasi cha USD bil.69.2 na sasa tumekuwa wa 11 tumepitwa na Cote d'Ivore (hawa wamepanda nafasi moja juu).
Tukiwekeza train na ikamalizika, bwawa likaisha, LPG na bandari ya Bagamoyo ITAONGEZA GDP ya Taifa kwa zaidi ya Billioni USD 41 tutaipita Kenya au angalau tutakuwa kwenye 10 bora na watu wetu wataendelea kupata kazi na uchumi kupaa.
Hizi reli, barabara, umeme na ujenzi wa madaraja yatanyanyua uchumi wetu. Haya mambo ya madeni yapo tu na huyawezi kuyakwepa! Kipi bora bwana Ndugu, tukope leo kwa mikopo rahisi na tulipe kwa miaka 20? Au tuendelee kukusanya pesa ndogo ndogo za madafu ambayo itaipelekea reli kumalizika miaka 20 ijayo? Au tuache hizo reli kwa sababu hatuna pesa?
Wewe Ndugai, kama tuliweza kukulipia pesa zako za matibabu yako na hukulalamika, mbona walalamika sana weye?
Marekani wamekopa zaidi ya asilimia 159 (USD Trillion 19.2)ya GDP yao, Japan (254%) Kila mahali wanakopa ili mambo yaende mbele.
Hii kazi isikwame, kila kitu kiendelee. Ndugai aache kupepeta domo. Tuliza boli.