Ndugai: Lishe duni ya wachezaji wetu imechangia Taifa Stars kufungwa

Amegundua Hili baada ya kufungwa?
Salam zimefika. Nadhani Ndgu mwakyembe ajiangalie. Ule ushauri wa kutaka kupunguza wachezaji wa kigeni kwenye vilabu kwa kutegemea hawa waketu! Hata zile nafasi 4 za uwakilishi caf tutapoteza hivi karibunitu.
 
Alifanya Press hapo airport au!?
 
Mbona walikuwa wanashindwa kuwanyanganya mpira wachezaji wa Senegal kitaalam wanasema one to one battle Wachezaji wetu wialionekana dhahiri kushindwa

..I did not see it that way.

..Nitaangalia mchezo tena ili kujiridhisha.

..Ila nimeona Tz tuli-commit fouls nyingi kuliko wapinzani wetu. Hiyo inaonyesha kuwa sisi ndiyo tulikuwa na mabavu/ maguvu kuliko Senegal.

..Nadhani tunahitaji KIUNGO MCHEZESHAJI mzuri zaidi. Wasenegali walituzidi kwenye upande wa ball possesion and shots attempted. Hiyo ina maana kuwa hatuna kiungo/viuongo wa kumiliki na kusambaza mpira kwa washambuliaji.
Cc ChoiceVariable , severinembena
 
Lishe tu hakuna u giants hapo
Mfano mNigeria chakula anachokula kwa mlo mmoja ni mlo wa siku nzima kwa mtz
 
Mwakyembe na Shonza hakuna mahali wamewahi cheza mpira au mchezo wowote leo hii ndio wamepewa wizara unategemea nini
Kama hao mawaziri ni wabovu ni wabovu tu haihusiani na kucheza mpira hata wangecheza ndiyo vilevile tu
 
Ahaaaa Ndugai kweli walifungwa kwa ajili ya lishe tu? Kocha Amunike hakuliona hilo la lishe?Watanzania kwa sababu utawajua tu.
 
Lishe tu hakuna u giants hapo
Mfano mNigeria chakula anachokula kwa mlo mmoja ni mlo wa siku nzima kwa mtz

Hivi mtu ukiwa tu CCM ndo akili zinakuwa boga kabisa...!?

Na mnakubaliana na kauli hiyo ya Speaker!??
 
Hivi mtu ukiwa tu CCM ndo akili zinakuwa boga kabisa...!?

Na mnakubaliana na kauli hiyo ya Speaker!??
Nilichikiandika hapa hakiusiani na ccm na wala sijawahi kuielewa ccm katika maisha yangu
 

Mkuu kama kimo ni kigezo basi Messi au Maradona wasingekuwa wachezaji nyota.
 
Nilichikiandika hapa hakiusiani na ccm na wala sijawahi kuielewa ccm katika maisha yangu
Basi usisapoti hiyo kauli ya kijinga ya radio mbao...
 
udumavu kwa watoto wa tz kwa sasa ni 40%...tatizo lipo kwenye mlo kamili tangu utotono,huko nyuma kula haikua shida,mtazame pondamali,tenga,ken mkapa na wa vizazi hivyo...ngasa hata umlishe vp hawezi kua,spika kaonesha namna gani lishe imempiga chenga
 
zilikua faulo za kukwatua visigino
 
Basi usisapoti hiyo kauli ya kijinga ya radio mbao...
Ndugai sio mtu anayefaa kuwa kiongozi lakini ukiwa mtu wa kupinga kila kitu wewe utakuwa mwendawazimu hauko sawa

Mbali na kuongea Ndugai Mimi mwenyewe nalifahamu hilo nime confirm tu kwamba yuko sahihi
 
Hivi Warundi wana miilli mikubwa? Mbona ni wadogo tu kama sisi lkn wanacheza mpira mzuri kuliko sisi?

Nachojua soka sio mieleka wala masumbwi, ndio maana hakuna kupimwa uzito, soka ni akili na ufundi, maguvu ni nyongeza tu.

Vv
 

Inaonekana kuna kujichanganya kati ya lishe na kimo. Wengi kwenye huu uzi huenda na spika wanaonyesha lishe ni urefu na unene. Kama hiyo ndio ndio mantiki ya wengi basi Messi asingecheza mpira kabisa. Ni vyema ikawekwa wazi, tatizo ni lishe au kimo cha mtu mmoja mmoja?
 
havitengani hivyo vitu,vimo vya watanzania vimepungua sana kizazi hiki kisa mlo kamili ni tabu,nafasi anayocheza messi kimo si hitaji muhimu,plus messi si mchezaji wa kawaida
 
Ha ha ha kuna ukweli hapo ndugu
Upi huo? Tulizidiwa maarifa na uzoefu au afya? Hata kama hawajapenda matokeo kujiokoteza sababu ilmradi waiponde team yetu haikubaliki!

Hivi kabisa serious mtu amewaza akapata hii ndio sababu? Na wewe unaunga mkono?

Tuna safari ndefu sana. Na labda wajukuu watafika kwa mtindo huu!
 
Midfielder bora Roberto Carlos,Gatuso,Paul Scholes na mpaka sasa Kante anakimbiza Premier league, bila ya kuwasahau wataalamu wa wataalamu Maradona na Messi, mpira ni kipaji si umbile. Huyu jamaa anakipaji cha kuwanyanyasa wapinzani bungeni aendelee na kipaji chake mambo ya soka aachane nayo.
 
Angekuwa anatoa posho yake ili wakale vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…