Ndugai: Lishe duni ya wachezaji wetu imechangia Taifa Stars kufungwa

Ndugai: Lishe duni ya wachezaji wetu imechangia Taifa Stars kufungwa

Spika wa bunge kwa hili umekosea sana. Huwezi kuwa kiongozi wa Serikali ukatumia kodi yetu vibaya kwamba unaenda kuwapa support wachezaji, matokeo yake wewe unaanza kuwaponda. Eti tumefungwa kwa sababu hatuli.

Hivi ni kweli hatuli au ni maumbo yetu? Hivi kessy hata akila usiku na mchana kama mchwa atarefuka ili apambane na Senegal.

Jambo la pili unasema tumefungwa kwa sababu ya viongozi wabaya wa mpira. Pale viongozi ulitaka wafanyeje? Au ulitaka wamwingile kocha majukumu yake kama unavyofanya mara zote.

Nimekusikia tena unasema kuna kiongozi mdogo hajitambui bila shaka huyu ni makonda kutokana na alichomwambia Rais.

Makonda yuko sahihi ndiyo maana umeona watanzania hawawalalamikii wachezaji bali kocha maaana yeye alipaswa kufanya zaidi ya hicho alichofanya kama fiziki hiyo ni kazi ya kocha.

Mheshimiwa tambua wewe ni kiongozi hupaswi kuwa na maoni binafsi kwa namna yoyote ile unapoongea na public.

Maoni tuachie sisi wadau wengine. Inabidi kama kiongozi ujitafakali. Naona utaanza kupambana na huyo kiongozi kijana kwa sababu amekuchallange na kukonyesha wazi ulichokosea.
Nani humleta kocha maswali fikirishi je kocha hujileta mwenyewe? muundo wa timu ya Taifa ukoje? kamati zinazoibuka za ufundi na nyinginezo kwanini huingilia mipinga ya timu ya Taifa?
 
Nani humleta kocha maswali fikirishi je kocha hujileta mwenyewe? muundo wa timu ya Taifa ukoje? kamati zinazoibuka za ufundi na nyinginezo kwanini huingilia mipinga ya timu ya Taifa?
Sijaelewa kocha kaingiliwa vipi maana kocha kaita wachezaji wake anaowataka
 
Kwani Ndugai kakosea nini japo Zito alimchokonoa makusudi
 
Ukweli usisemwe?Hatuna lishe bora ndomana stamina mbovu,viongozi hawausimamii mpira kisasa wanachotizama ni hela ipatikane...haiwezekani nchi kuuubwa kama mara 6 ya senegal na watu Mara tatu yao alafu wanatufunga kijingajinga wakati nasi futiboli ndomchezo mkuu!!
Kamakonda nako kanaropoka kijingahivi tukifungwa tena na Kenya kataongea mini maana kimsingi sioni tukiwaweza kwa kutizama tuu uchezaji wetu ulivyo teketeke
 
Spika wa bunge kwa hili umekosea sana. Huwezi kuwa kiongozi wa Serikali ukatumia kodi yetu vibaya kwamba unaenda kuwapa support wachezaji, matokeo yake wewe unaanza kuwaponda. Eti tumefungwa kwa sababu hatuli.

Hivi ni kweli hatuli au ni maumbo yetu? Hivi kessy hata akila usiku na mchana kama mchwa atarefuka ili apambane na Senegal.

Jambo la pili unasema tumefungwa kwa sababu ya viongozi wabaya wa mpira. Pale viongozi ulitaka wafanyeje? Au ulitaka wamwingile kocha majukumu yake kama unavyofanya mara zote.

Nimekusikia tena unasema kuna kiongozi mdogo hajitambui bila shaka huyu ni makonda kutokana na alichomwambia Rais.

Makonda yuko sahihi ndiyo maana umeona watanzania hawawalalamikii wachezaji bali kocha maaana yeye alipaswa kufanya zaidi ya hicho alichofanya kama fiziki hiyo ni kazi ya kocha.

Mheshimiwa tambua wewe ni kiongozi hupaswi kuwa na maoni binafsi kwa namna yoyote ile unapoongea na public.

Maoni tuachie sisi wadau wengine. Inabidi kama kiongozi ujitafakali. Naona utaanza kupambana na huyo kiongozi kijana kwa sababu amekuchallange na kukonyesha wazi ulichokosea.
Kweli kocha alinishangaza pale alipopata mpira yupo na kipa alafu akabutua.
 
Kabisa mkuu. Elimu yetu ina kasoro nyingi sana. Haya ilitakiwa watu wajifunze shuleni.

Mti wenye matunda.
Tunaibebesha elimu yetu matatzo kibao kila kitu elimu

Hili swala la lishe mbna linafundshwa toka huku primary mpk secondary

Mambo mengne ni matatzo yetu binafs tusisingizie elimu
 
Ina maana shule vinaingilia na kutokea huku mkuu.
Tunaibebesha elimu yetu matatzo kibao kila kitu elimu

Hili swala la lishe mbna linafundshwa toka huku primary mpk secondary

Mambo mengne ni matatzo yetu binafs tusisingizie elimu
 
Back line ilikuwa inakatikakatika kama ngoma ya mdundiko, ndani ya dk moja mnapigwa mashambulizi kama matano ya hatari, kwa mpira ule sioni kama kuna timu wataifunga
 
Lishe ina nafasi kubwa, ndo maana kwenye ligi ya mpira wa kikapu marekani NBA kama hujafikisha uzito unaotakiwa hawakuruhusu kucheza, utavunjwa mbavu
 
kingine unakuta mfupi anaoa mfupi mwenzie. japo swala la mapenzi unaweza kumpenda yeyote. lakin pia mtu unaezaa nae basi kama wewe ni mfupi hakikisha ni mrefu.
Haya mambo ingekuwa tunapata matokeo mazuri kwa kutumia nguvu basi mbinu za CCM za kutumia mtutu zingefaa sana.
 
Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema miongoni mwa sababu iliyochangia Stars kupoteza mchezo wa kwanza jana dhidi ya Senegal ni lishe duni ya wachezaji wetu.

Spika Ndugai ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam akitokea Misri aliposhuhudia mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Tanzania uliomalizika kwa Taifa Stars kuchapwa 2-0.

Ndugai alisema ukiangalia kwa umakini utaona wale wachezaji wa timu pinzani walikuwa na miili mizuri ambayo inatokana na lishe nzuri.

"Kuna umuhimu wa kuwapa wachezaji wetu lishe nzuri ya kutosha ili kushindana na wapinzani wa aina ya Senegal," alisema Ndugai.

Katika hatua nyingine Ndugai alisema viongozi wengi wa soka na michezo mingine hapa nchini siyo watu sahihi wa kuongoza.

Source : Mwananchi

====

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema hakwenda Misri yeye kama yeye, bali alitumwa na Rais John Magufuli kwenda kuiwakilisha nchi.
Spika Ndugai ameyasema hayo leo Jumanne Juni 25, 2019 alipokuwa akifafanua kauli ya aliyemuita kiongozi mmoja mmoja wa Serikali kuwatuhumu baadhi ya wabunge kuwa wamewalaumu wachezaji na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Amesema: “Mimi nimetumwa Misri na Rais, halafu anakuja mkuu wa mkoa mmoja ananisumbua, siwezi kusumbuliwa na mkuu wa mkoa mmoja.”
Amesema kiongozi huyo wa Serikali amezungumza maneno yasiyofaa kuhusu Bunge la Tanzania na wabunge na kumdanganya hadharani Rais Magufuli, kuwa wawakilishi hao wa wananchi wamewadhihaki wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Spika huyo amesema hawezi kusumbuliwa na mkuu wa mkoa mmoja, kwa kuwa anatambua nini anakifanya.
Pia Soma
Amesema kati ya wabunge waliokwenda Misri ambako timu ya Taifa inashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon), hakuna aliyemlaumu mchezaji yeyote wala kuisema vibaya timu hiyo.
“Hayo ni mawazo ya mtu ambaye kidogo ndiyo hivyo. Ni bahati mbaya sana tuna viongozi wa Serikali wanadiriki kumdanganya Rais hadharani, kiongozi wa Serikali unapoongea mbele ya rais jipange uongea ukweli mtupu wa mwenyezi Mungu, usisingizie wala kumuonea mtu hatufanyi hivyo.”
Mapema leo asubuhi, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika ufunguzi wa Mradi wa Gesi, Kigamboni jijini humo, alisema ameshangaa wadau mbalimbali ambao wameizungumzia vibaya timu hiyo baada ya kupoteza mbele ya Senegal.
“Nimeumizwa na matokeo ya Taifa Stars, lakini nimeumizwa zaidi kwa watu kuwabeza wachezaji wetu ambao wametubeba Watanzania ambao ndani ya miaka 30, haikuwezekana lakini wao wamepambana mpaka tupo Afcon leo hii," alisema Makonda
Makonda alisema alizungumza na wachezaji hao pamoja na nahodha Mbwana Samatta na wamemuhakikishia kwamba watafanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya Kenya.
"Sisi Afrika Mashariki tunajuana vizuri kwahiyo Mhesimiwa Rais wala usiwe na wasiwasi tutafanya vizuri katika mchezo huu ambao tunahitaji ushindi na wachezaji wapo vizuri," alisema Makonda.
Aliongeza iwapo Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli aweze kutoa neno lolote la kuwapa moyo kuelekea katika mchezo ujao.
Tanzania itacheza na Kenya Alhamisi mchezo utakaopigwa saa kumi na moja jioni.
Akili nyingine hizi...hivi Lishe duni ni suala la kukurupuka kweli ! Upungufu wa lishe ni suala pana! Hata aliyetoa hoja hii yaelekea ana upungufu wa Lishe !Kwa kuwa Timu ya Taifa huandaliwa Kisayansi ikiwemo suala la lishe kuanzia miaka 0! Kama Kiongozi waJuu wa Serikali alitakiwa ajue hili...na kutojua maana yake na yeye ana akili ndogo iliyosababishwa na udumavu...aka Lishe duni!
 
Lishe duni husabaisha udumavu wa akili .Mojawapo ya vielelezo vya lishe duni ni akili zetu ukubwani1
Mfano ni mtu kama huyo akiwa kiongozi atakuwa na tabia hizi
-Ubabe wa kijinga,inaweza kutokea hata kumpiga mtu fimbo
-Udikteta na kushabikia udikteta
-Ubnafsi
-uzandiki
-Matumizi mabaya ya madaraka.
 
Back
Top Bottom