Ndugai: Mkitumia lugha hizo tutagawa mbao hapa, shauri yenu...

Bwana mkubwa hivyo unaweza ukaenda mbele ya watoto wako kama baba na kujisifia kubebwa na mwanamume mwenzio? Na kwanini unayembeba akisema nimechoka kubebwa usione afuweni? Pengine hali sio kama unavyofikiria kwani kwa akili ya kawaida kupe likibeep tu kupanga chumba chake unamsaidia haraka liondoke!
 
Nafikiri bado hamna ubavu wa kuwabeba Wazanzibari kwani msingetumia mbinu za kuwaviza katika harakati zao za kujinasua na huo unaouita kubebwa.
 
Hata kama kwa katiba hii muungano utanusurika, tujue tu kuwa hautadumu.

Nakubaliana nawe iwapo hatutokuwa na kuheshimiana kwa taratibu za kidola kwani muungano huu ni wa kidola.
 
Mara ya pili leo umenithibitishia kua unachoongeaga sicho unacho kiamini moyoni mwako, na hi ndio sifa ya Watanzania wengi!
Ngungai ameongea kitanganyika na kizalendo zaidi

Bora lawama kuliko fedheha.

Wagawane mbao kieleweke
 
Mara ya pili leo umenithibitishia kua unachoongeaga sicho unacho kiamini moyoni mwako, na hi ndio sifa ya Watanzania wengi!
Yaani ndugai akiwa 'peke yake' anatema point mpaka raha ...Ukweli mtupu. Wazenj wanalalamika sana wakati wao ndio 'beneficiries' wakubwa wa muungano.
 
hata Tembo huangushwa na Chura mtoni....!!! pumbavvzzz!!!

Siku zenu zinahesabika, jeuri, kibri na ujivuni sidhani kama vitawasaidia, hakika mtakuja lia na kusaga meno. Talaka yenu inaandaliwa.
 
Nakubaliana nawe iwapo hatutokuwa na kuheshimiana kwa taratibu za kidola kwani muungano huu ni wa kidola.
Heshima mpewe nyie tu, mna rais, bendera, bunge nk lakini mbona nyie hamna heshima kwa kaka yenu Tanganyika?
 
Heshima mpewe nyie tu, mna rais, bendera, bunge nk lakini mbona nyie hamna heshima kwa kaka yenu Tanganyika?

Unaitafsiri heshima kuwa ni kutoka kwa mkubwa kwenda kwa mdogo? La , heshima ni kuheshimiana mdogo kwa mkubwa na mkubwa kwa mdogo na msingi hasa wa heshima ni kukubali matakwa ya mwenzako kwa kitu anachokimiliki hata kikiwa robo ya punje mbele ya wingi ulionao.
 
Nimekuelewa mkuu, ngoja basi tuandae karatasi ya talaka ili tuachane kwa amani.
 
Hebu niambie mkuu Ngekewa, kwa mfumo wa muungano ni kipi hasa nyinyi kinachowabana??? mbona mambo mengi yamefanywa kwa kuwapendelea nyinyi kutokana na udogo wenu???
 
Last edited by a moderator:
Hebu niambie mkuu Ngekewa, kwa mfumo wa muungano ni kipi hasa nyinyi kinachowabana??? mbona mambo mengi yamefanywa kwa kuwapendelea nyinyi kutokana na udogo wenu???
 
Last edited by a moderator:
Wengine tumechoka,hapa ni maswala ya kila mtu kuchukua zake, ukienda kule passport ukija kwetu ivo ivo...hakuna cha udugu hapa, tumebembeleza yametufika kooni..
Ka kisiwa kenyewe na global warming katamezwa siku 0 tu, ebu tujali yetu kwanza...
 
Nimekuelewa mkuu, ngoja basi tuandae karatasi ya talaka ili tuachane kwa amani.

Ndowa za waume kwa waume huwa hzina cheti cha serikali, kila mmoja huvaa suruali yake akaenda zake. Iwapo huu muungano ulikuwa ndowa!
 
Hebu niambie mkuu Ngekewa, kwa mfumo wa muungano ni kipi hasa nyinyi kinachowabana??? mbona mambo mengi yamefanywa kwa kuwapendelea nyinyi kutokana na udogo wenu???

Tatizo ni kuwa mnadanganywa na wanasiasa kuwa kuna mengi yamefanywa kwa Zanzibar. Ningeomba unipe orodha ya hayo mambo lakini kwa upande wangu ningekwambia ovu moja kubwa linalofanywa kwa Zanzibar.
Zanzibar ni nchi yenye wananchi wanaohitaji huduma zote zinazotakiwa kwa mwanadamu wa kawaida, na unapoinyima Zanzibar uhuru wa kuamuwa ilitakalo na wananchi wake basi hilo ni ovu kubwa sana kwani linavunja msingi wa haki za binaadamu. Hivyo kwanini wanalotaka Wazanzibari kwa kipande chao cha ardhi (Zanzibar) iwe nongwa na lazima tuwapigie magoti? Na kila siku jawabu hapana kwa matakwa ya Wazanzibari. Yaani hii ndiyo ile ulioiita wewe ndowa kuwa nyie mabwana na muwe waamuzi wa nini cha kutufaa sisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…