SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,338
- 4,676
Wataaalamu wa Kufikiri,tujadiliane hivi:
Si lazima Mungu awatokeeni Spika Ndugai na Mbunge Msukuma katika maisha yao physically kama ilivyotokea kwa mama Bikra Maria au Zakaria (mzazi wa Yohana Mbatizaji), ili kuwapasha wote hao wawili ujumbe mahususi.
Nasema si lazima Mungu afanye hivyo kwa Ndugai, Msukuma na wote wanaoonekana kuchelewa kuanza kufikiri eti ndio waelewe kwamba Mungu yupo au ndio waelewe kwamba kuna mambo wanapaswa kuyarekebisha katika kufikiri kwao,katika kutenda kwao, katika kusema kwao au katika kuwajibika kwao.
Ni hivi,Mungu (Omnipresent) yupo mahali pote.Yupo ndani na nje ya kila maada unayoifahamu wewe Ulimwenguni.Yupo hata katika Sayari ya Mars.Yupo Mwezini. Mungu anapatikana katika Vimondo na yupo katika Satelites zote zilizoko huko Angani. Yumo katika vyombo vyote vinavyoenda hata huko Anga za Juu. Ninasema leo akina Ndugai kwa sababu inaonekana kana kwamba kuna wakati wanasahau au wanasahaulishwa, kuwa Mungu yupo Bungeni na yupo katika Vitanda vyao wanavyolalia.
Licha ya kwamba Mungu yupo mahali popote,Yeye anao upendo wote(All Loving).Mungu Ni chanzo cha upendo na kilele cha upendo.Yeye anawapenda na kuwathamini binadamu wote, hata wale wasiowapenda wenzao au wale wanaowatesa wenzao.
Imeonekana na inaelekea kudhihirika sas kwamba, Spika Ndugai kwa utendaji wake,kuna baadhi ya mawazo yake, kauli zake, matendo yake na jinsi anavyowajibika, kunatokea picha kana kwamba anatindikiwa uelewa kuwa hata yeye ameumbwa na wala hajajiumba. Kwa nafasi yake, ya Uspika wa Bunge(Chombo kinachopaswa Kutunga sheria kwa ajili ya wanadamu ili ziwasadie kufahamu kwamba Mungu yupo mahali pote na kwamba sisi wanadamu hatukuwahi kumuandikia barua Mungu kumuomba atuumbe bali kwamba tuliumbwa kutokana na Upendo wake tu), anatenda kwa kugeuza asili ya Uumbaji ili watu wawepo duniani kwa ajili ya sheria badala ya sheria kuwapo kwa ajili ya kuwasaidia mwanadamu kuishi.
Ni kana kwamba yeye na baadhi ya wabunge ni Kristo mpya na kwamba wamepewa na “Mungu” ufunuo mpya.Ufunuo wa sheria kuwa na thamani kuliko damu za wanadamu.
Spika Ndugai na Mbunge Msukuma ni hivi, bila bila wanadamu, watanzania kuwepo msingalikuwa wabunge, nyote wawili na wala bila Mbunge Tundu Lisu wewe Ndugai usingalikuwa Spika. Sasa, ungalikuwa Spika kivipi? Kama Unanibisha, subiria Bunge livunjwe mwakani, uone kama cheo chako hakitabadilika na kuwa “Spika wa Bunge lililopita” Ndio hivyo. Pius Msekwa, Marehemu Samweli Sita na Anna Makinda,wote hao sasa wanaitwa Maspika Wastaafu na wala hawajawahi kuja kuombwa na Nyenyere, Simba, Nguruwe na wala Konokono wakawe Maspika wa viumbe hao.
Hivi ni kweli kwamba Mungu aliye mahali pote, hajawahi kukufunulieni ukweli huo, ninyi na wabunge wenzenu wenye kufikiri kana kwamba Mungu alikosea kuwaumba wanadamu wengi na badala yake mngaliachiwa ninyi tu muitawale dunia?
Mbunge Msukuma na Spika Ndugai, mnapaswa kuelewa kwamba hamjawahi na haitatokea hata mchangie atom au element yoyote katika primary au natural components zinazoufanya ulimwengu uwepo. Mimi na ninyi “tunakunywa” na kushiba Oxygen ambayo hatuna mchango nayo na wala hata maelezo ya lini ilianza kuwepo hatunayo.
Sasa katika muktadha kama huo najiuliza ni kwa nini masuala ya uhai wa wanadamu wenzenu munayachukulia kana kwamba Hii Dunia mliimba ninyi au kwamba ninyi ndio mliachiwa kazi ya Unyapara wa Dunia na Ulimwengu wote kwa Ujumla? NI kwa nini katika kuwajibika kwenu kwa watanzania,Spika na baadhi ya Wabunge wa CCM, munawajibika kana kwamba ninyi mko mahali pote?
Hivi,Mbunge Msukuma, miongoni kwa Kanuni za Bunge, kanuni ya kuomba miongozo ipo kanuni za Bunge la Jamhuri, kabla hata wewe hujafikiria kuomba kuchaguliwa Ubunge? Haujui kwamba Kanuni hiyo ipo hata wakati Mbunge mwenzio Tundu Lisu alipotaka kunyofolewa uhai wake na watu ambao hawajui kwa ukamilifu kanuni ya kukokotoa thamani ya uhai wa Lisu na wala wakati anaumbwa hawakuwahi kutumiwa meseji, hata kupitia WhatsApp au Insta kuulizwa au kuombwa kutoa ushauri ama Tundu Lisu aumbwe au asiumbwe kwa sababu kuumbwa kwake kungalikuwa kero na angegeuka kuwa Kinyamkera kwa uchumi na ustawi wa Tanzania?
Musukuma, Nakuuliza Msukuma: ulikuwa umesahau kwamba ulipaswa kuomba muongozo ili kufahamu ni kwa nini, kwa takribani mwaka mmoja toka Mbunge mwenzio atake kuondolewa uhai wake (na watu ambao hawana mamlaka nao), Mamlaka za Kiupepelezi au Kiuchunguzi hazijatoa taarifa yoyote hadi wakati huu (unapolilia pesa anazolipwa),kama iwapo zinaendelea na upelelezi wa shauri lake au zimeshafunga jalada la suala hilo? Nakuuliza hivi ulikuwa hujui utumie kanuni gani kuomba mwongozo wa kufahamu hali ya Lisu inaendeleaje au kwamba ni lini upelelezi wa waliotaka kumdhuru umefikia wapi?
Spika Ndugai,naomba kukuuliza kwa nafasi yako ya Uspika, ulishawahi kuomba Ikulu ruhusa ya kuomba kwenda kumtembelea Mbunge mwenzio na Mbunge wako Tundu LIsu na badala yake ukanyimwa ruhusa hiyo ila akapewa Makamu wa Raisi,Mama Samia Suluhu Hassani,aliyeenda kumsalimia Nairobi?
Hivi, Ndugai pesa za mshahara wa Tundu Lisu alizolipwa kipindi chote hiki akiwa mgonjwa, ndizo ndio Bunge lilipanga kuzitumia kama nauli ya tiketi ya Ndege,Chakula na Malazi ili kuweza kwenda kumjulia hali binadamu mwenzio (ambaye unalingana naye mbele ya Mungu) kiasi kwamba mpaka leo hujaweza kutoka kwenda kumjulia hali, binadamu mwenzio ambaye ana damu kama ambayo aliwahi kuwa nayo Yesu Kristu?
Spika Ndugai, ulizaliwa ili uishi chini ya miongozo na kanuni za Bunge au kwamba Mungu alikupatieni akili ili uzitumie kutunga kanuni na kuzitumia kwa ajili ya ustawi wa mwanadamu? Hivi,mbona kuna wakati unatenda kana kwamba kanuni na miongozo ndio zilimuumba mwanadamu? Hivi,mbona unaishi wakati mwingine kana kwamba wewe unajua zaidi kuliko Yesu Kristu aliyefika kuondoa Falsafa ya kuigeuza Sheria, Kanuni, tamaduni na desturi ziwe na thamani kubwa kuliko thamani ya Mwanadamu? Hivi, umepewa hayo mamlaka ya kuigeuza “Sabato” kuwa juu ya Mwanadamu? Wewe na Yesu nani Mkuu?
Mheshimiwa Ndugai, nakuuliza hivi: unapoombwa mwongozo juu ya jambo lolote ni lazima utoe majibu(Ruling) juu ya jambo au suala husika hapo hapo au siku hiyo hiyo au Bunge hilo hilo, na huhitaji kusuburia? Mheshimiwa, Ndugai, Ni kweli Kanuni zinatawala au zina uwezo wa kulazimisha akili yako kiasi kwamba huwezi kutoa nafasi ili kutafiti majibu muafaka na yanayochora busara katika mind yako, pindi utoapo maamuzi katika masula tata kama hili la ugonjwa wa Tundu Lisu? Au nikuulize hivi: ulipoombwa mwongozo na Msukuma, ulishindwa kumjibu Msuma kwamba unahitaji kama Spika na Ofisi yako, kumuandikia Mbunge Tundu Lisu Oficially, kumuuliza anapoonekana katika Ziara zake, anazoonekana, ieleweke kwa watanzania kwamba anazurura au kwamba ni sehemu ya Matibabu yake?
Naongeza hivi: Spika Ndugai, ofisi yako ikianzisha mawasiliano na Tundu Lisu kumuuliza hali ya matibabu ikoje, itakuwa ofisi yako hadhi yake imeporomoka au kwamba itaonekana ofisi yako inamtumikia Tundu Lisu badala ya Tundu Kuitumikia ofisi yako na kukutumikia wewe?
Mheshimiwa, Spika Ndugai,ningaliweza kukuuliza maswali mengi sana na utendaji wa Bunge lako,mintarafu jinsi ambavyo unaonekana kulichukulia suala la maisha ya binadamu mwenzako,Tundu Lisu, lakini nisiendelee sana maana sina hakika kama unao utamaduni wa kusoma mambo marefu namnan hii.
TUndu Lisu, anasemekana anazurura na kutanua kwa kodi za watanzania. Ndivyo munavyomuona ninyi. Sawa. Mbona mnajiuliza na hapo hapo mnajibu?
Spika Ndugai nisaidie: Msukuma amekuuliza iwapo Tundu Lisu anazurura au hicho anachokifanya ni aina ya tiba pia:
1. Je, majibu ya kwamba Tundu Lisu anazurura umeyapata saa ngapi na kwa utaratibu gani?
2. Je, majibu ya kuzurura kwa Tundu Lisu, ulikuwa nayo muda mrefu?
3. Na kama ulikuwa nayo muda mrefu, ni kwa nini ulikuwa hujachukua hatua za kufyekelea mbali malipo yake?
4. Je,kwa kuwa ulikuwa unafahamu kwamba Tundu Lisu “anapiga Misele” huko Ughaibuni na hukuwa umechukua hatua yoyote, ni nani hasa anachezea pesa za watanzania?
5. Je, wewe na Tundu Lisu mnatofautiana vipi katika upigaji wa pesa za watanzania?
Chimbuko la Fedha za watanzania ni damu za watanzania wenyewe.Hakuna fedha yoyote inayozalishwa na ndugu zetu marehemu.Watanzania wakiisha kutumia damu zao kuzalisha fedha,fedha hizo haziwezi kugeuka hapo hapo na kuwa na thamani kuliko damu zilizo sababisha pesa hizo kuwepo.
Niwaulizeni: hivi, munaweza kutusaidia kutenganisha fedha ambazo Tundu Lisu hajawahi kuzigharimia kwa damu yake na zile ambazo sisi tumezigharimia kwa damu zetu, ambazo ndio zinatuuma sana kuliko damu ya Tundu Lisu, iliyotaka kumwagika? Mwishowe, Naulizeni hivi: ninyi mko mahali pote(Omnipresent) kiasi kwamba ninyi mnafahamu uelekeo wa Afya zenu ujao kwa usahihi kabisa?
Nawaulizeni tena: hivi, kwa sababu Mungu yupo hapo Bungeni na hata katika Vitanda vyenu na Meza za kulia chakula katika sebule zenu, kwa hiyo mumeshaongea naye au mlishachati naye kupitia WhatsApp na yeye akawajibu na kuwahakikishia kwamba ninyi kwa maisha yenu yaliyosalia haitatokea kuja kupata “ajali” kama iliyomkuta Tundu Lisu, kiasi hata ninyi nanyi kuonekana pasipo shaka kwamba ikiwa utaratibu na ulazima wa kuomba vibali kwanza Ikulu ndio mkatibiwe utafuatwa, basi vibali vitapatikana wakati ninyi wakati huo mtakuwa Mochwari?
SASA, ikiwa hamna majibu ya maswali yangu hapo juu,nawaombeni hivi: Kwa kuweni wabunge na Maspika, msisahau kwamba kuna Mungu na ni yeye tu mwenye mamlaka juu ya maisha yetu.Ninyi hamukuulizwa juu ya kuumbwa kwa mwanadamu yoyote yule kiasi kwamba hata mkose utu,heshima na kujali maisha ya wenzenu na badala yake mguswe na tu na pesa zinazotafutwa na damu za watu.
Uongozi wa watu ni kwa ajili ya kulinda, kuboresha na kudumisha maisha ya wenzetu.Bila damu za wenzetu kuwa hai, hakuna cheo chochote unachokifamu hapa duniani kitasalia. Anayetaka kuwa kiongozi wa watu lazima akubali na ajitwike msalaba wa kuwatumikia wenzake na sio kuhitaji kutumikiwa. Anayehitaji kutumikiwa aende akafanye hivyo kwa Kobe,Mende na Punda. Yesu Kristu, Mungu alifika duniani kututumikia.Je,ninyi ni wakubwa sana kuliko Yesu Kristu aliyetuachia mfano Wa ki kutumikia na sio kutumikiwa?