Uchaguzi 2020 Ndugu Balile na wenzako, Vyombo vyenu havipigi kura msiwachagulie wagombea na wachaguaji nini cha kuambiwa, hatutaki

Ameshalishwa mlungula sasa anaanza kujaribu kuwahadaa watu kisaikolojia! Nijuavyo mimi Vyombo vya habari mkishakuwa mmelipwa chenu kazi yenu ni kuripoti tukio au habari husika, lakini haya mengine wanayoanza kuteleza hapa ni mauzauza yasiyo na maana! Wanaotakiwa kujibu hoja na wajibu hoja sio kukimbilia kwenye vyombo vya habari kuminya sauti za hoja!
 
Chadema mpaka sasa akuna ambae hawajatoa lawama kwake.mpaka wanawalaumu wapinzani wenzao kama Act,Nccr n,k.
washashindwa mapema sana kablamtanange wenyewe haujaanza.
 
Yani kwa kifupi habari ni habari tu, ukiona mhariri anaanza kupiga mikwara hivi ujue kuna jambo nyuma ya pazia, Na huyu Balile sijui amekuaje siku hizi.!! Na hayo matusi ni yapi sijui ..!? Usipohabarisha hayo matusi, na badae mgombea akachaguliwa kwenye nafasi anayogombea, nin itakuwa faida ya chombo cha habari..?! Na vip akiendelea kutukana huko atakapokuwa anawatumikia wananchi baada ya kuchaguliwa, utaripoti au bado utaacha ..?! Balile amekuwa wa hovyo siku hizi 🤔🤔🙉🙉
 
Lakini mbona mnajihami sana, ni wapi balile amesema hawataripoti habari za lissu? yeye kasema hawataripoti matusi? sasa kwanni mnamhusisha Lissu na hayo matusi?
 
Nilikuwa namuona Balile kama mtu huru kumbe ni mtumwa kabisa.
Hajawahi kuwa huru , ni mamluki wa kitambo , namfahamu , aliwahi kutumika kusawazisha mambo kipindi ambacho Mwandishi Meena ilisemekana amelishwa sumu na kukimbizwa South Africa , nilimpa za uso bila aibu
 
Matusi hayakubaliki mkuu
Matusi, matusi, WAPINZANI NI MABWEGE NA MALOFA! MGOMBEA WENU ANAJINYEA! NIGONJWA, hsya yote yalisemwa na yakaonekana sawa tu, ila wapinzani wanaambiwa wanatukana hapo matusi hayo hatuyasikii wala aliyetukana hajulikani na hii imekuwa ni wimbo wa CCM wanaimbishwa viongozi wa dini. Jana nilimsikia Padri huko Dodoma akituchagulia mtu wa kumpigia kura, tume haikemei kampeni za ndani ya makanisa, akina Ponda nao wakianza Tume italalamika!
Balile alionekana dhahili akiisimamia CCM kwa kututaka tumchague mgombea wake! Nilitegemea atakemea vyombo vya habari kutoripoti habari za upinzani lakini wapi!
 
Aliyejaribu kuweka mambo hadharani aliuawa kikatili. Phd sio makaratasi si tu bali hata tabia na uongezaji lazima viendane nayo
 
Kwani kuna mtu kamtaja? si amesema tu hawataripoti matusi? Sasa kwanini tunarusha lawama au mmeshajua kuna mgombea wenu, kazi yake ni matusi.
 
Nani alishawahi kutukana adharani?
 
Nani ulimsikia katukana na tusi lipi?
 
watu wanaonunua magazeti ni wale tu wanaotafuta tenda, magazeti kifo chao kilifika siku nyingi
 
Kwanini unakasirika Mkuu mbona wameeleza vyema, matusi si mazuri
 
"hebu we mama nieleze unataka kupanuliwa nyumba/ mbele?" ~JPM
 
Jukwaa lenyewe limeshanunuliwa na jiwe, wapuuzi tu. Social media zipo na habari zitamfikia kila mtanzania.
Acha hao waandishi uchwara waendekeze matumbo yao
 
CCM wakitukana wanaripoti na kushangilia. Upinzani wakikosoa hawaripoti. Lakini TLP ikisema inamuunga mkono CCM vyombo vyote meno nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…