Uchaguzi 2020 Ndugu Balile na wenzako, Vyombo vyenu havipigi kura msiwachagulie wagombea na wachaguaji nini cha kuambiwa, hatutaki

Naona kuna jitihada za kuleta maana mpya ya neno matusi.
Tangu Mgombea Urais Tundu Lissu arejee nchini na kuzunguka kutafuta wadhamini, sijamsikia akiongea maneno ambayo siwezi kuyasikiliza nikiwa pamoja na watoto wangu.
Maana, kamwe siwezi kuvumilia matusi.
Lakini nimewahi kumsikia Mgombea Urais John Magufuli, hadharani, akimwambia Mhandisi wa Maji Masasi kuwa, "wewe ni mpumbavu sana''!!!
Sikumsikia Balile akitoa tamko la kukemea matusi.
Kwa bahati nzuri, watu walio na uhuru kamili, wametumia Sayansi na Teknolijia kuhakisha kuwa taarifa na habari zote zinapatikana kiganjani.
Magazeti hayana wasomaji siku hizi.
Nina hakika Balile anajua kwamba "magazeti ni habari za mwaka 47"!!
Pole sana Balile.
Matusi siyo ya nguoni tu bali ni pamoja na maneno ya uwongo dhidi ya mtu mwingine bila kuwa na ushahidi. Nikisema wewe ni mwizi au wewe ni mpumbavu wakati siwezi kuprove hivyo, hayo siyo ya maneno ya nguoni kwani yanaweza kusikilizwa na mtu yeyete hata watoto. Ila hayo ni matusi ya wazi kabisa dhidi yako, na hilo ni kosa. Kisheria wanasema hivi "Insult is the infringement of another human's honor by whatsoever means of expression, in particular an offensive statement or gesture communicated, and is a crime in some countries"

Ingawa anaweza kuyasema hayo mitaani na kwenye mikutano ya chama chake, hayaruhusiwi kwenye kampeini chini ya sheria ya Uchaguzi; ni matusi ndiyo yalimvua Ubunge wa Wassira baada ya uchaguzi wa mwaka 1996 na kuzuiwa kugombea uongozi wa umma kwa miaka 5 mfulilizo, ndiyo maana hakugombea tena mpaka 2005.
 
Matusi hayakubaliki mkuu
Waambie. Mleta mada hajielewi hata Jamiiforums tu ukitukana unapigwa ban sembuse kwenye media? Kama ilivyo Jamiiforums na huko nje hivyo hivyo ukileta matusi unapigwa ban
 
Matusi siyo ya nguoni tu bali ni pamoja na maneno ya uwongo dhidi ya mtu mwingine bila kuwa na ushahidi. Nikisema wewe ni mwizi au wewe ni mpumbavu wakati siwezi kuprove hivyo, hayo siyo ya maneno ya nguoni kwani yanaweza kusikilizwa na mtu yeyete hata watoto. Ila hayo ni matusi ya wazi kabisa dhidi yako, na hilo ni kosa. Kisheria wanasema hivi "Insult is the infringement of another human's honor by whatsoever means of expression, in particular an offensive statement or gesture communicated, and is a crime in some countries"

Ingawa anaweza kuyasema hayo mitaani na kwenye mikutano ya chama chake, hayaruhusiwi kwenye kampeini chini ya sheria ya Uchaguzi; ni matusi ndiyo yalimvua Ubunge wa Wassira baada ya uchaguzi wa mwaka 1996 na kuzuiwa kugombea uongozi wa umma kwa miaka 5 mfulilizo, ndiyo maana hakugombea tena mpaka 2005.
Nayakubali maelezo yako mazuri.
Nafahamu pia kuwa ukweli ni kinga ya mashitaka ya aina hiyo.
(Nitafurahi ukiielezea hapa kuwa "truth is defense against ....)
Watanzania tumeingiwa na hofu kuu ya kusema ukweli katika miaka hii mitano, kiasi kwamba kumsikiliza Tundu Lissu akisema ukweli hadharani, damu inatusisimka kwa woga.
Hiki ndicho kinachomtokea Balile na wenzake.
Tutofautishe matusi na ukweli.
Ukweli siyo matusi.
Hasa ukweli huo unapowahusu wakubwa ambao hawataki kusemwa.
 
Hiyo post yangu uliyokwote ina maneno "....bila kuwa na ushahidi." Ukiwa na ushahidi independent hayo siyo matusi, ushahidi wa kutengenezwa kwa makusudi bila kuwa wa kweli huwa haukubaliki.
 
Katba ya nchi inatamka wazi kuwa kila mtu anastahili heshima na kuthaminiwa utu wake.Kumtukana mtu Ni kuvunja katiba .Matusi hayaruhusiwi na katiba.Hayo hakuagiza Balile Ni katiba ya nchi imeagiza

Yuko sahihi Balile .Vyombo vya habari haviwezi kuvunja katiba kwa kuandika matusi watafungiwa na TCRA

Weka orodha ya maneno ambayo ni MATUSI yasiyotakiwa kutumiwa na WAGOMBEA WA URAIS.
 
Kama anataka kuona matusi basi atizame na TBC mchana kweupe wanaonesha wanawake wamevaa vichupi wanacheza mziki. Sijawahi kuona BBC au CNN kuweka wanawake wamevaa chupi wanakata viuno!
 
Naona kuna jitihada za kuleta maana mpya ya neno matusi.
Tangu Mgombea Urais Tundu Lissu arejee nchini na kuzunguka kutafuta wadhamini, sijamsikia akiongea maneno ambayo siwezi kuyasikiliza nikiwa pamoja na watoto wangu.
Maana, kamwe siwezi kuvumilia matusi.
Lakini nimewahi kumsikia Mgombea Urais John Magufuli, hadharani, akimwambia Mhandisi wa Maji Masasi kuwa, "wewe ni mpumbavu sana''!!!
Sikumsikia Balile akitoa tamko la kukemea matusi.
Kwa bahati nzuri, watu walio na uhuru kamili, wametumia Sayansi na Teknolijia kuhakisha kuwa taarifa na habari zote zinapatikana kiganjani.
Magazeti hayana wasomaji siku hizi.
Nina hakika Balile anajua kwamba "magazeti ni habari za mwaka 47"!!
Pole sana Balile.

Balile ni mmoja wa makanjanja wasiojitambua waliovamia tasnia ya habari. Akili ndogo.
 
Huyo balile atutajie hayo matusi! Yaani wao eti ukisema ccm ni wezi eti ni matusi
 
Magufuli alisema tengenezeni barakoa imefanana kama titi la mwanamke si matusi hayo
 
huyu ni moja ya vuvuzela hata ukimuangalia tu kichwa chake unajua hayuko sawa na kaathirika kiakili kwa vitisho. Matusi huwa yanatoka upande ulee wa kijana wakishindwa kwa hoja na wanageuza ukweli kuwa matusi kwa upande mwingine. Mfano hao wasanii wanachoimba s matusi? Upuuzi huu wa kusahau ulichosomea na kutetea tumbo tu
 
Katiba ya nchi inatamka wazi kuwa kila mtu anastahili heshima na kuthaminiwa utu wake.Kumtukana mtu Ni kuvunja katiba. Matusi hayaruhusiwi na katiba.Hayo hakuagiza Balile Ni katiba ya nchi imeagiza

Yuko sahihi Balile. Vyombo vya habari haviwezi kuvunja katiba kwa kuandika matusi watafungiwa na TCRA
Wewe mbona uliandika humu kuwa mh. Lissu akirudi nchini tu unamzimisha.. pale hukuvunja Katiba??
 
Kampeini zitafanywa kama duniani kote wanavyofanya kampeini mambo ya kuwapangia wagombea cha kuongea sio sahihi, wapiga kura ndio watachambua pumba na mchele ni upi, oooh ! mara usimtaje mtu, kwanini asitajwe? kama alikuwa hataki kutajwa kwanin amegombea?
 
Back
Top Bottom