NIMESIKILIZA tamko la jukwaa la wahariri Tanzania kupitia ndugu
Balile wakidai kuwa hawataripoti matusi ya wagombea, sisi wanachi tungependa kuwajulisha nyinyi wahariri ya kuwa msituchagulie nini cha kusikiliza na msiwachagulie wagombea nini cha kutueleza sisi.
Kama matusi ni sehemu ya sera basi acha sisi tuambiwe nyinyi kazi yenu ni kuripoti na si vinginevyo.
Mbona mnaripoti habari za mwanamke mmoja kubakwa na midume minne kwa kutumia kondom?
Sisi wananchi tunazo akili msituchagulie mtuache sisi tuchague mbichi na mbivu.
Mnapokimbilia tunapojua wagombea wakisema uongozi uliopita haukufaa nyie mtasema hayo ni matusi kisa utawala HUO ulilipa sanaa madeni ya jamhuri.