Ndugu, jamaa na marafiki njooni tumtetee Makonda dhidi ya mapapa wauza unga wanaomzushia

Ndugu, jamaa na marafiki njooni tumtetee Makonda dhidi ya mapapa wauza unga wanaomzushia

Ngoja nimtetee kidogo
Daudi Albert Bashite hajaghushi vyeti bali majina haya{Paul Christian Makonda) ni yake halali aliyapata kihalali kabisa km ifuatavyo

[emoji117] Paul hili jina alipewa Primary kutokana na kipaji chake cha soka wakati akichezea timu ya shule akifananishwa na Paul Scholes
[emoji117] Christian hili jina alipewa na wanakwaya wenzake wakati yupo form two maana darasa zima peke yake ndo alikuwa Mkristo
[emoji117] Makonda hili jina alilipata akiwa form 4 alikuwa na rafiki yake ambaye walikuwa wanarudi pamoja Mwanza likizo na kufanya kazi kwenye daladala hivyo shuleni wakawa wanawaita Makonda

Hilo ndo chimbuko la majina yake wala hajaghushi jamani
We mtoto umekaa weee ukaanza haya mawazo au??????
 
Isijekua kama yule aliesema alipewa majina mara na dokta , akaeleza mara alipewa majina yale kwa ushauri ambao mama yake aliutoa kwa masista , mara kwa walimu.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la Mass Mobilization Kuunga Mkono Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Katika Vita Hii ya Madawa ya Kulevya Kwa Kuwaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki, Wanaomjua Makonda Kwa Karibu, Njooni Tujitokeze Kwa Wingi ,Kumtetea Makonda Tunayemfahamu Dhidi ya Uongo na Uzushi Anaozushiwa na Mapapa Wauza Unga Kupitia Kwa Vibaraka Wao Kumsingizia Ameghushi Majina, Amegushi Vyeti, Amesoma Chuo Kikuu Kwa Chati Cha Kughushi na Mpaka Sasa Anatumia Majina ya Kughushi!.

Tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaumbue wauza unga wakuu kwa kuwataja majina live, tena bila kupepesa macho wala kumungunya maneno, mafisadi hawa, wapambe wao, makuwadi wa ufisadi na wale wote wasilitakia mema taifa hili, wameanza kampeni ya kumvunja moyo na kumkatisha tamaa Makonda kwa kumzushia kila aina ya uongo.

Sisi tunaounga mkono vita hii, tunamsisitiza akaze uzi na asitetereke, wala asipoteze muda wake wa thamani kujibu uongo wowote wa kwenye mitandao, yeye achape tuu kazi, na majibu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake, hazina haja kabisa ya kujibiwa na Makonda mwenyewe bali ndugu zake na marafiki zake wenye nia njema, wanaweza kutusaidia.

Maswali ni haya.
1. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
2. Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale
3. Alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani? .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5.Alitumia majina gani matatu sekondari, tukiisha pata tuu majina, tutayaona matokeo yake ya Necta hivyo kuwakata vilimilimi wazushi wote.
6. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa majina gani? .

Majibu ya maswali hayo, yatawakata kabisa vilimilimi wote wanaotaka kumzushia kuwa hakusoma sekondari, alipata Div. 0 na kwamba aliiba cheti cha mtu!.

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda Kwenye Vita ya hii ya madawa ya kulevya dhidi ya mapapa wa madawa wanaotaka kumchafua Makonda wetu.

Paskali.
Peh ngo kwa vituko,
 
Kakukose nini huyu msukuma mwenzio, huu Uzi wa pili unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa, au nawe unaitaka nyamagana 2020?
 
Ngoja nimtetee kidogo
Daudi Albert Bashite hajaghushi vyeti bali majina haya{Paul Christian Makonda) ni yake halali aliyapata kihalali kabisa km ifuatavyo

[emoji117] Paul hili jina alipewa Primary kutokana na kipaji chake cha soka wakati akichezea timu ya shule akifananishwa na Paul Scholes
[emoji117] Christian hili jina alipewa na mwalimu wake wa darasa wakati yupo form two maana darasa zima yeye peke yake ndo alikuwa Mkristo
[emoji117] Makonda hili jina alilipata akiwa form 4 alikuwa na rafiki yake ambaye walikuwa wanarudi pamoja Mwanza likizo na kufanya kazi kwenye daladala hivyo shuleni wakawa wanawaita Makonda

Hilo ndo chimbuko la majina yake wala hajaghushi jamani
Ccm watauchukua utetezi huu na kuuamini
 
Makonda mm nimesoma nae chuo ushirika yeye alikuja kujiunga tukiwa mwaka wa pili BA of Arts in community economin development(CED) ambapo alipospond na sababu za kupospond ni kwamba ilikuwa adisco baada ya kufeli masomo mengi ndo pakachezwa mchezo akapospond matokeo yakawekwa sawa na kabla ya hapo alianza na BA CMA akadisco
 
Njooni tu
mouse-trap-bait.jpg
 
Hii vita ya Makonda inanikumbusha vita vya genge la muuza madawa maarufu Jamaika ambaye ambaye naitwa Dudu huyu alikuwa anatoa misaada mingi huko kwenye vitongoji vya akina yakhe kiasi kwamba serikali ilipomvalia njuga hao akina yakhe walienda barabarani kuandamana na kufanya fujo kisa Dudu wao asishikwe,na serikali kuonekana mbaya,ni vivyo hivyo hapa Tanzania kwani viongozi wa magenge ya kihalifu ndio wanaotetewa na kila mtu na hata baadhi ya wanasiasa,kwa kuwa tayari hao akina Dudu wamejipenyeza sehemu mbali mbali zinazowagusa akina yakhe ,mambo kama ya michezo,ufadhili wa kujenga mashule,mahospitali,kuanzisha vituo vya radio,au Tv kumiliki vyombo vya habari ,na yote hayo huyafanya kama kinga na pia kutakatisha pesa chafu.Tutasikia mengi kutoka kwa hao akina Dudu na wafuasi wao.Ningekuwa na uwezo ningemtunuku Makonda Nishani ya juu ya utumishi na Mungu azidi kumbariki kijana huyu jasiri.
 
Makonda nami nipo nyuma yako, wangekuwa na haya yote juu yako wangeyasema ulipoanza kuteuliwa vyeo ulivyopitia kabla. Mola yupo nawe na tunakuombea azidi kukulinda na kukuongezea maarifa ili tuzidi kujivunia kuwa Watanzania.

Effective leader.
 
Back
Top Bottom