Ndugu, jamaa na marafiki njooni tumtetee Makonda dhidi ya mapapa wauza unga wanaomzushia

Pascal Mayalla ni mchochezi sana. Kwa umri na uelewa wangu,nimeipata hoja yako. Badala ya kumtetea,unaalika watu wamuumbue zaidi au ajitokeze na kujitetea

Mzee Tupatupa

Na mimi nilijiuliza nikampotezea mdogo mdogo niandike vyangu, ila anauwezo wa kwenda kote alikopita Makonda maishani akitaka kusaka habari. Oops anajitegemea pia, so maybe hakuna bahasha za khaki kama kabla. Ananifurahishaga as kiki nayo inatafutwa, hapa kazi tu inavutia wengi
 
Tabia zetu WaTanzania wengi NI kuona kila kitu NI kejeli.Ukisifiwa umevaa vizuri utasema ooh unanisanifu.Ukiambiwa unapendwa oooh Toka lini.
Pascal ameandika watu waje mkutetea Makonda uzi mzima wana mshambulia eti mchochezi.
Sasa huo uchochezi uko wapi?
Wengi humu JF wanajiona wajanja lakini sio Na wale wachache ambao hawajioni ndio wanaona ukweli Na sio kejeli.
 
Sio watanzania ni tabia za upande wa watu wako tu!
 
Paskali.
Kipofu aliyeponywa upofu wake na Yesu alifuatwa na wanafiki na wengine waandishi kama wewe wakimuuliza kuwa ameponywa na Mungu au Mapepo?
Jibu lake lilikuwa "Sijui. Ninachojua mimi ni kuwa nilikuwa sioni lakini sasa ninaona"
Hayo majina yake yawe halali au la ni upuuzi wa wauza madawa ya kulevya na watetezi wao kumvunja moyo. Hivi kama sio halali ndo itahalalisha Madawa ya KULEVYA? Nonsense! Tunaacha kujadili issues tunajadili MAJINA. Haya. wenye majina sahihi mnafanya nini cha maana kupambana na MADAWA ya kulevya? Hivi cha maana kwenu ni uhalali wa majina yake au DHAMIRA yake?
 
Mayalla nachelea kusema kwamba hiki Kitendo ulichokifanya kwa Mhe. Makonda si kizuri hata kidogo.Una lengo la kumdhalilisha.Linapokuja suala la uongozi,kuna wakati vyeti vinasaidia kuna wakati havisaidii.Uongozi ni kipaji bro.Mfano,kuna mtu mmoja anafanya vizuri kwenye safu ya awamu hii ya tano ambaye nimeambiwa hana digrii.Tunahitaji deliverance kwa sasa.
 

Mkuu, nikuulize swale moja. Huyo ambaye hana hata digirii moja na anafanya vizuri takwimu zake kuhusu elimu na majina yake
Katika makarabrasha ya ajira anatumia majina yake ya halali aliyopewa na wazazi wake?
Na takwimu za elimu yake ni zilezile kama kaishia darasa la nne, la saba, la nane, la kumi na mbili,au la kumi na sita? Isije kuwa ni wale Wale?
 
Usisahau kuna watanzania wenzetu wametumbuliwa kwa kufoji vyeti... na walikuwa wakifanya kazi kwa tija...Kusiwe na double standard... kama naye kafoji atumbuliwe tu..
 
Mkuu Paskali, hapo nilopobold the opposite is the onus us upon the person himself and not otherwise. Maswali yote 6 anayeweza kufahamu ni yeye mwenyewe, Zaidi ya yeye itakuwa ni minong'ono na majungu ! I note the sarcasm in your submission! brilliant !
 
Wewe ungechagua yupi kati ya hawa.Huyu ana cheti cha darasa la saba lakini anakufanyia kazi yako,tuseme commercial unavyotaka na analeta tija kwenye Idara yako.Mwingine ana digrii kumi lakini lakini kila ukimpangia kazi anachemsha?Sipingi watu kwenda shule ila nadhani ni vizuri pia kuangalia uzoefu na experience ya watu.Mimi nina experience ya serikalini na private na nimebahatika kufanya kazi nje ya nchi kama expert.Nina digrii lakini nchi zote nilizofanya.kazi sijawahi kuulizwa niwaonyeshe vyeti vyangu!Ukifika pale HR wanachukua taarifa zako chache wanakupeleka kwa boss wako.Pale unapangiwa kazi uliyoomba,unapewa probabation say miezi.3.Ukichemsha ni out.Wanataka uwatatulie matatizo yao ukiweza kuyatatua wanakuongezea $$ kila mwaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…