Ramthods
JF-Expert Member
- Jun 2, 2009
- 515
- 187
Maamuzi ya mtu, vitu anavyofanya, vitu anavyotoa, mchango wake kwa jamii, mazuri na mabaya yake yote tunayoyaona... yote ni matokeo ya uwezo wake wa kufikiri.
Na pia, uwezo wa kufikiri wa mtu, maamuzi yake na vitu vingine vyote unavyoweza kuviita "maamuzi yake" vinategemeana na nini "ANACHOKIJUA" kichwani mwake.
Kujua ni kuelemika, na ndio msingi wa maamuzi yetu na mchango katika jamii yetu. Elimu ni uwezo wa kuona - na ndio kujua kwenyewe huko! Je, kwani hakuna tofauti kati ya mwenye macho na kipofu katika giza totoro?
Hata kama tupo katika giza nene lisilopenyeka, bado mwenye macho ni zaidi ya kipofu, ingawa sote hatuoni mbele!
Na ndivyo ilivyo katika kujua. Hata kama kujua hakutubadilishi, bado kujua ni bora kuliko kutojua kabisa!
Mimi nafurahia kujua .... waache watu wajue!