Nendubotho Sunguya
Senior Member
- Oct 9, 2019
- 126
- 109
Ndugu Mwita waitara ni aibu na fedheha hata kukupa jina la mheshimiwa naomba nikuite Ndugu tu.
Kwa urubuni na maneno uliyotumia ukiwa mpinzani 2015 na kwa dhati ya moyo wako ulijua fika ukabila ulibeba nafasi ya wewe kupendwa na kuona kwamba sisi tutaamini kwakuwa eneo hili lina wale wenye vinasaba vyako utaona huruma na kutekeleza japo kero kubwa ya ubovu wa barabara takribani aslimia 60 ndani ya jimbo lako barabara ni MBOVU.
Kama kuna siku nilitamani wanaukonga wangefungua akili ni kipindi ambacho waliendekeza dhana ya ukabila badala ya kuangalia kijana mwenye nia ya kufanya mambo. Hakuna mkamilifu ila bora angeingia bungeni Jerry Slaa kuliko wewe.
Hamna ulichofanya ukiwa mpinzani lakini wanaukonga walikuwa wana matumaini ipo siku utafanya jambo.
Katikati ya matumaini ghafla umeamia CCM ukiwa na uso ule ule usiokuwa na huruma na wana Ukonga. TUKASEMA TUSUBIRI...
Naaandika uzi huu kwa uchungu sana maana subira wanaukonga waliyonayo imefika kikomo. Baada ya kuteuliwa CCM ulitembelea baadhi ya kata zako ikiwemo Msongola na Chanika. Wananchi wakakuuliza barabara hii kutoka Mbande mpaka Msongola mvua zikinyesha hapapitiki kabisa tusaidie. Ukajibu kama mgeni wa hili eneo wakati ulikuwepo tangu 2015.
Ukaongeza, "Sasa hivi nina nafasi kubwa ya kuongea huko juu kwa hiyo nitaomba japo KIFUSI" KIFUSI? Siriazi watu wanahitaji lami barabara ni mbovu kuliko maelezo na ni miaka nenda rudi unasema kifusi? Na ni kweli baada ya wiki kadhaa kifusi kilimwagwa sikumbuki vilikua vingapi ila vichache na ni kilometa nyingi kweli vikasawazishwa na barabara kuchongwa kiaina.
Na huu utaratubu wa kuchonga chonga barabra ni wa muda na kuna maigizo yanafanyika na ni matumaini yangu unahisika. Unakuta barabara inachongwa (sio kuwekwa lami) kama kilometa moja hivi wanakaaa hata miezi. Inaleta usumbufu mzitoo ukizingatia barabara ni ya vumbi.
Uchaguzi serikali za mitaa umekaribia umesogeza sogeza magreda barabarani yamepaki pembeni hayafanyi kazi ya aina yoyote unafikiri hayo maigizo wanaukonga hawayaoni?
MVUA ZIMEANZA
Barabara hazipitiki ndani ya jimbo lako kwa asilimia kubwa hivi 2020 una mpango wa kuja Ukonga? Nakusihi USIJARIBU!
Nitaambatanisha picha za baadhi ya maeneo ya jimbo lako maana nahisi nyakati kama hizi za mvua hupiti kwa hiyo sidhani kama unaijua adha wananchi wanayoipata.
CCM ninaamini mna kuna watu wenye nia ya dhati na nchi hii. Huyu jamaa apishe, hana cha kujitetea kwenye uchaguzi ujao hana kabisa.