Uchaguzi 2020 Ndugu Mwita Waitara hautoshi Ukonga. Umefeli ukiwa mpinzani, umeshindwa ukiwa CCM!

Uchaguzi 2020 Ndugu Mwita Waitara hautoshi Ukonga. Umefeli ukiwa mpinzani, umeshindwa ukiwa CCM!

Hivi Watanzania lini ujinga huu utatutoka? Mbunge hana fedha za maendeleo ya jimbo! Mwenye fedha ni serikali na kupitia halmashauri na taasisi za serikali miradi inajengwa. Sasa kumdai mbunge ni kumuonea au kumbebesha mzigo usio wake.
yeye kazi yake ni kuwasilisha matatizo yaliyoko kwenye majimbo yake na yafanyiwe kazi kama hafanyi hivyo unafikiri nani atafanya?
tumemtuma kuwakilisha.
au kazi ya mbunge ni NINI?
 
Wabunge wengi wa CCM waliopo mikoa ya Dar es salaam,Iringa na Arusha wanajisahau kutokana na mfumo wa uongozi ulivyo katika hiyo mikoa. Ni kazi sana kujua majukumu ya wakuu wa mikoa hiyo tajwa na viongozi wengine katika hizo sehemu. Wakuu wa mikoa wanataka kufanya kila kitu,usipokuwa makini watu wanaweza jua unazingua kumbe wakuu wa mikoa husika wamepora majukumu ya wengine.
Wabunge wengi hawafanyi majukumu yao.
 
Bila kusahau barabara ya kitunda shule kuelekea kibeberu magole ni mbaya kabisa,daraja linalounganisha mwanagati na magole limeshindikana kujengwa ni mwendo wa kuogelea mto mzinga.mheshimiwa mbunge kimyaaaaaa
TENA huko hali ndo mbaya sanaaaa
barabara ni mashimo matupu mvua ikinyesha unawaza unatoka vipi nyumbani
 
Ujinga hapa nimetumia kuonyesha uelewa wetu ni mdogo.

Sasa kama aliahidi kuwa atafanya hizo kazi ni kwa sababu alifahamu uelewa wa watu aliokuwa anawaahidi hawana uelewa, yaani ni wajinga.
kazi yake ni NINI HASA?
 
Wananchi wa jimbo la ukonga ni kama hawapo dar es salaam wala sio Tanzania hii, wao ni kama wametengwa hata na serikali kuu, barabara hata bodaboda wanachagua pa kukanyaga barabara zilivyombovu.

Mkuu wa mkoa muheshimiwa makonda afanye ziara ya kikazi maeneo ya majohe, msongolwa huko ajionee kama huko ni ndani ya jiji lake au ni mkoa mwingine.
 
yeye kazi yake ni kuwasilisha matatizo yaliyoko kwenye majimbo yake na yafanyiwe kazi kama hafanyi hivyo unafikiri nani atafanya?
tumemtuma kuwakilisha.
au kazi ya mbunge ni NINI?
Matatizo yenu anawasilisha lakini serikali iko hoi bin taabani kimapato.
 
Ukonga ipi mnayoisema?

Kutoka banana kitunda hadi frem kumi lami ipo tena nzuri tu, msongora hadi cha kenge ni lami, magreda yanazunguka kusafisha barabara za mitaani nk kazi inafanyika na tunaiona.
Ila ukikutana nae ukathubutu kumuuliza habari za barabara atakujibu hivi: kaa hapa unywe bia barabara itakusaidia nini
.MATAGA
 
Hv huyu mbunge nae ni member humu???
wapo wengi humu na id kama yako hiyo
kama hayupo atafikishiwa tu ujumbe
Wananchi wa jimbo la ukonga ni kama hawapo dar es salaam wala sio Tanzania hii, wao ni kama wametengwa hata na serikali kuu, barabara hata bodaboda wanachagua pa kukanyaga barabara zilivyombovu.

Mkuu wa mkoa muheshimiwa makonda afanye ziara ya kikazi maeneo ya majohe, msongolwa huko ajionee kama huko ni ndani ya jiji lake au ni mkoa mwingine.
yaani makonda aje afanye ziara hili jimbo limesahaulika kabisa
 
Kutoka mombasa kwenda moshi bar lami ipo mbovu tu, lakini kutoka Moshi bar kwenda bomba mbili hakupitiki kabisa , imesababisha madaladala kuwa machache sana , bajaj haziendi na hata bodaboda xinadengua pia!!!
 
tatizo ni kubwa katika eneo kubwa la jimbo la ukonga hakupitiki.Rais akipita hataamini kama ni eneo la mjini
 
Back
Top Bottom