Its true. Huyu dada hakuwa hivi, alikuwa sista duu ila alikuwa na adabu kiasi fulani.
Nakumbuka kwenye page yake ya Instagram kuna kajamaa aliwahi kukarusha hewani, inanonyesha ndio kalikuwa ni rasmi wake na alikuwa ana malengo ya kumkunjia goti, sasa mwisho wa siku naona mambo yakaenda mrama na hawapo pamoja.
Kikawaida wanawake wanaofanya vituko mitandaoni wakifanya mambo yanayodhalilisha majina ya familia zao na wao binafsi wakijidhalilisha huwa ni matokeo ya kukata tamaa kunakoambatana na hasira za kukwama mambo yao.
Pale jamii inapowashangaa na kuhoji mwenendo wanaokwenda nao wao ndipo huzidisha ikiwa ni ishara ya kutaka jamii iwape attention na kutaka kujua nini hakipo sawa.
Huyu binti, asimamishwe kazi, apatiwe muda wa kupumzika na kuonana na watalaamu wa afya ya akili ili aweze kupewa msaada kabla hatujasikia siku amemeza sumu na kujiua au akafanya vituko vizito zaidi.
Sent using
Jamii Forums mobile app