Ndugu Rhimo Simeon Nyansaho Mkurugenzi mpya PSSSF mtazame vizuri huyo mhasibu hapo ofisini

Rigidity

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2024
Posts
763
Reaction score
1,077
Kwanza kabisa nikupongeze kwa kuamininiwa na mh. Rais kuisimamia taasisi hiyo nyeti inayohusika na maslahi ya watu wanaotaabika kwa miaka kibao.

Kumekiepo na malalamiko dhidi ya mtangulizi wako kwani alishindwa aidha nguvu na hao watumishi wa ofisi au ilikua ni maelekezo yake. Mambo yalikua hayaendi. Wanufaika wamefuarilia mafao yao siku tele lakini hakukua na mrejesho chanya.

Marakadhaa kipindi cha nyuma ukipiga simu ukiulizia unaambiwa taratibu zimekamilika lakini mhasibu ameenda likizo. Je hiyo ni taasisi ya umma kweli au nikikoba?

Majibu yaliyokuja kutolewa baadae hata baada ya huyo mhasibu kurudi yamekua mengine. Eti ukiwauliza UKOMO wa kupatiwa huduma wanasema hakuna ukomo. Yaani hiyo taasisi ilikua inaelekea kusiko.

Ndugu Nyansaho cheza na akili ya mhasibu na hao wapokea simu( huduma kwa wateja). Kuna dada mmoja hapo kisirani sana Kwa leo ngoja nimstiri jina lake lakini hakidhi vigezo vya kuhudumia wateja online

Nikushauri ujaribu kuingia kwenye mfumo utaona madai ya muda mrefu na wanufaika wameshakamilisha vigezo ila hela hawapewi

Nimalizie kwa kusema ukichelewa wakikuwahi wataendelea kufanya kazi kwa mazoea. Wadhibiti mapema hao maana wanawaona wanachama kama ombaomba
 
Mkuu kuna jambo pia linanisikitisha kama ulifukuzwa kazi pamoja na vigezo vyote vya kuchangia miezi180, Hustahili kulipwa Kila mwezi hii si hukumu hii!
 
Ulipokosea kutomtaja huyo dada, unamsitirije mtu asiyekusitiri wewe?
 
Bila kutaja jina la dada kisirani basi huu ni umbea na unafiki! Wabongo ni wanafiki nafiki sana, sasa kama unamjua mtu anaeharibu taswira ya taasisi na kuumiza watu wengi Kwa nini usimtaje?
Uko sahihi, mtu ananyanyasa wenye pesa zao we umamsitiri shetani km huyo? Kweli imekaa km umbea, wadada km hao sifa yao kuu ni ushirikina, hongo za ngono ndiyo maana wanakuwa na roho za kikatili na za kichawi. Nachukia sana watu km hao mm naweza kulazwa korokoroni nikikutana na mbwa km huyo
 
Amtaje nasi tuliopo Dodoma tumzodoe!
 
Mwanaume akiwa mmbea huwa hana ushawishi kwenye michongo ya hela
 
Watanzania hamjui adui yenu. Wewe unadhani hao wapokea simu ndiyo tatizo? Au huyo mhasibu?
 
Wafanyakazi iwe sekta binafsi au umma amri yao kuu ya kwanza na ya pili ni FITNA na MAJUNGU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…