Burn the bridge _Tz
JF-Expert Member
- Apr 15, 2021
- 2,319
- 6,878
Nimezaliwa mtoto wa kwanza kwa mke wa tatu wa marehemu baba,
Tangu nakuwa shule ya msingi mpaka namaliza sikuwahi kumjua ndugu yoyote upande wa baba, ila nilikuwa nafahamu kubwa baba Ameshafariki mwaka 2001
Hata mama hakuwahi kuniambia chochote kuhusu ndugu zangu upande wa baba.
Sasa nimekuwa nimepata ufadhilii kwenda kusoma China, ila changamoto inakuja kwenye kupata hati ya kusafiria.
Nimelipa 130000/= pia nikalipa pesa ya maombi kwa njia ya mtandao 20000/=
Nikapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole. Baada ya wiki tatu afisa uhamiaji ananipigia simu kutaka kuthibitisha taarifa za marehemu baba yangu.
Anataka kujua makaburi ya wazazi wa baba yangu anataka kujua kaka na dada wa baba yangu (shangazi na mjomba)
Juhudi zikaanza kuwatafuta ndugu hao ili wathibitishe uraia wa marehemu baba mana ni ndugu wa kigoma
Changamoto hakuna ndugu ananipa usharikiano hata wa kunipa namba ya shangazi au mjomba ili waweze kuthibitisha
Kifupi sikuweza kujua lolote kutoka kwa ndugu upande wa baba na hata wao hawakuwahi kunitafuta maisha yangu yote.
Je nifanye nini ili niweze kupata passport na afisa uhamiaji anataka uthibitisho kutoka kwa ndugu upande wa baba?
Ahsante