Ndugu Victoria Mwanziva: Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa afuatilia maelekezo ya Mhe. Rais kwenye Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Ndugu Victoria Mwanziva: Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa afuatilia maelekezo ya Mhe. Rais kwenye Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Cde. Victoria Mwanziva amefika Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki (Mb).

FcGuwbbXgAA30LR.jpg


Ndugu Victoria Mwanziva amefika Wizarani akiwa na lengo mahususi la kujadili nafasi ya vijana katika sekta hizo muhimu za uzalishaji na namna gani wanaweza kunufaika na fursa mbalimbali zitokanazo na Ufugaji pamoja na Uvuvi.

Aidha, Lengo kuu la Katibu wa Uhamasishaji limekuwa ni kupata mrejesho wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan; alilotoa katika maadhimisho ya NaneNane mwaka huu mkoani Mbeya Tarehe 08/08/2022 juu ya namna gani vijana wanaweza kunufaika na sekta ya ufugaji na uwepo wa mipango mizuri ya uratibu.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amemhakikishia kuwa tayari serikali imekwishafanya maandalizi ya mpango maalumu na Bajeti yake ipo ambapo vijana 240 watakabidhiwa Ng’ombe 10 kila mmoja na kuwa chini ya usimamizi wa wataalam wakitumia teknolojia mpya ya ufugaji na sayansi ya unenepeshaji na zoezi hili litawafanya kupata mitaji yao kujiendeleza, baada ya mpango huu wataongeza idadi ya kubwa ya vijana maradufu Bajeti ijayo.

Katika hatua nyingine, Waziri Ndaki amemweleza kuwa upande wa uvuvi serikali inaandaa vizimba zaidi ya 800 upande wa Ziwa Victoria ambapo hii inamlenga kijana kujihusisha na ufugaji wa Samaki kibiashara na serikali inagharamia hatua zote zilizokuwa zikimkwamisha kijana ikiwa ni pamoja malipo ya tathimini ya mazingira na gharama za NEMC na eneo husika.

Kwa ukanda wa Pwani Serikali inakwenda kuleta Boti za kisasa (Fiber Boats) ambapo jumla ya Boti 230 zitakopeshwa kwa vijana na makundi mbalimbali.

Uwezeshwaji na ukopeshaji; uratibu na usimamizi utafanyika chini ya Halmashauri husika ambazo zitakuwa na utekelezaji wa programu hizi.

Mwisho, Waziri Ndaki amesisitiza kupitia Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) serikali imewekeza fedha za kutosha kwa vijana kukopeshwa bila riba & kuwaomba wajitokeze na kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta hii kupitia halmashauri zao akihimiza Maafisa Uvuvi kufikisha taarifa kwa vijana.
 

Victoria Mwanziva uwezo mdogo..hajui kujenga hoja..sema nafasi hii kaipata kwa sababu baba Ake ni brigedia wa jeshi. Kwanza anajiona km mtumishi wa umma.​

 

Victoria Mwanziva uwezo mdogo..hajui kujenga hoja..sema nafasi hii kaipata kwa sababu baba Ake ni brigedia wa jeshi. Kwanza anajiona km mtumishi wa umma.​

Mkuu ccm ndio ilivyo ditopile mwanae leo kawa mpiga debe mkuu. Kikwete jr leo kawa naibu waziri,

Ni kurithishana kulamba asali.
 
Back
Top Bottom