Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mtembea kwa miguu aliyegongwa na Basi la Abiria la "Mwendokasi" wiki iliyopita ambaye ndiye alikuwa Majeruhi pekee wa ajali hiyo aliyesalia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), ametambulika ambapo jina lake ni Osam Milanzi, Mkazi wa Manzese Midizini.
Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi amesema utambuzi huo umefanywa na Mke wa Majeruhi (Osam) aitwaye Isha Mohamed pamoja na Mdogo wa Osam anayeitwa Shaban Milanzi.
Mvungi amenukuliwa akisema “Afya ya Osam imeimarika kutokana na kazi kubwa ambayo imefanywa na Madaktari, Wauguzi pamoja na Watumishi wengine wa MOI.
“MOI tunatoa shukrani za dhati kwa vyombo vya habari pamoja na Watanzania wote wenye mapenzi mema ambao walishirikiana nasi kutangaza habari za kuwatafuta Ndugu wa Osam.”
Itakumbukwa jana Hospitali hiyo ilitoa taarifa kwamba Osam tayari ameondolewa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na kuhamishiwa wodi nyingine ya HDU baada ya afya yake kuzidi kuimarika ambapo pamoja na mambo mengine Majeruhi huyo ameanza kuongea na amejitaja kwa jina moja kwamba anaitwa Osam na Makazi yake ni Manzese, Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi akiwa katika picha ya pamoja na ndugu Osam Milanzi, katikati ni mke wa Bw Osam, Bi Isha Mohamed.