Ndugu wa Mtanzania aliyefariki vitani Ukraine walala matanga siku 10 wakisubiri mwili

Ndugu wa Mtanzania aliyefariki vitani Ukraine walala matanga siku 10 wakisubiri mwili

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Ndugu wa Tarimo Nemes Raymond Raia wa Tanzania aliyefariki kwenye uwanja wa vita katika mji wa Bakhmut nchini Ukraine akipigana upande wa Urusi dhidi ya Ukraine wamedai hadi sasa wametumia siku 10 kuusubiri mwili wa ndugu yao kwa kulala matanga.

Taarifa zinaeleza kuwa kifo cha Nemes aliyekuwa anaipigania Urusi kupitia kikosi cha mamluki cha Wagner kinachomilikiwa na Yevgeny Prigozhin swahiba wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kimetokea tangu Oktoba 2022 lakini habari za kifo hicho zimefahamika jana baada ya kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Mjomba wa Nemes, Andrew Mwandenuka amesema familia hiyo ilipewa ahadi ya kuwa mwili huo utafika nchini hivi karibuni na kupata matumaini baada ya kuona picha mwili huo ukiagwa huku Urusi. "Tupo hapa tunasubiri mwili wa Nemes kila siku tunaambiwa utakuja lakini juzi tumeona anaagwa pengine wanamaliza taratibu utaletwa na hivi karibuni tumeambiwa huenda ijumaa ya wiki hii utaletwa sisi tunaendelea kusubiri".

Amesema msiba huo kwa upande wao una gharama kutokana watu kujianda kwa msiba kwa matumaini ya kuwa wataupata mwili wa ndugu yao bila mafanikio kwa siku 10 sasa.

Kwa upande wa Dada wa Nemes , Salome Kisale ameishukuru Serikali kwa kuwapa ushirikiano na kupata taarifa ya kifo cha ndugu yao.

“Tunamshukru Rais Samia pamoja na watendaji wake nchini Urusi kwa kweli wanatupa ushirikiano na tuna matumaini kuwa watatusaidia kuupata mwili wa ndugu yetu" Salome alipoulizwa kama anajua taarifa za ndugu yao kufariki vitani alikanusha akajibu kuwa Nemes hajafia vitani.



MWANAHALISI ONLINE
 
Hao ni wapumbavu. Hawajasikia kuwa ameshazikwa. Kabda wasubiri kupokea cheti na medali.

Wachaga Sifa zitawaua
 
Hao ni wapumbavu. Hawajasikia kuwa ameshazikwa. Kabda wasubiri kupokea cheti na medali.

Wachaga Sifa zitawaua

Mpumbavu wewe walahi!
Maiti imeagwa na hawajazika
Huyo sio mchaga!
Amechukua tu hilo jina lakini hana uchaga wowote
Angalia majina ya ndugu wengine, kuna mchaga hapo?
Idiot![emoji35]
 
Mpumbavu wewe walahi!
Maiti imeagwa na hawajazika
Huyo sio mchaga!
Amechukua tu hilo jina lakini hana uchaga wowote
Angalia majina ya ndugu wengine, kuna mchaga hapo?
Idiot![emoji35]
Kwenye mshono. Changemi mkamfuate serikali Haina pesa za kuchezea
 
Watu wengine bwana...mtu Ana hate hadi maitiii
 
Sasa mnatukaniana Nini? Maiti? Mpumbavu ,mjinga,sjui blablah.

Unatukanana na mtu hata humjui kwenye I'd fake kama hizi?wabongo tuna shida .
 
Hao ni wapumbavu. Hawajasikia kuwa ameshazikwa. Kabda wasubiri kupokea cheti na medali.

Wachaga Sifa zitawaua
Hawawezi kuzika yule Mwanafunzi Raia wa Zambia alisharudishwa pana vitu vina code number kama hauna utachukulia kirahisi sana ..hata kama itabaki miguu tuu atarudishwa Mazee
 
Back
Top Bottom