Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Ndugu wa wagonjwa wanaopatiwa huduma za matibabu katika Taasisi ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wameeleza kuridhishwa kwao na huduma wanazopatiwa wagonjwa wao.
Pongezi hizo wamezitoa leo Ijumaa Mei 23, 2025 katika eneo la kusubiria huduma, MOI Clients' Lounge lililopo katika Taasisi hiyo.
Bw. Emanuel Magembe mkazi wa Morogoro, ambaye ni ndugu wa mgonjwa aliyelazwa kwa ajili ya upasuaji wa mguu, amesema kuwa huduma zinazotolewa MOI zimeboreshwa ukilinganisha na miaka ya nyuma.
“Madaktari na wauguzi wanatoa huduma kwa heshima na kujali, na hata mazingira ya wodini ni safi. Maneno tunayoyasikia mtaani na tukija hapa ni tofauti. Tunashukuru kwa jitihada hizi,” amesema Bw. Magembe
Naye Bi. Neema John, ambaye ni dada wa mgonjwa , amesema amevutiwa na ushirikiano kati ya wahudumu na ndugu wa wagonjwa.
“Wanatusikiliza, wanatupa taarifa kwa wakati na tunajisikia sehemu ya matibabu ya wapendwa wetu,” amesema Bi. Neema
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mapato wa MOI, Bw. Chediel Mziray, amesema uongozi wa MOI unathamini mrejesho kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa na kuendelea kuboresha huduma kila siku.
Hata hivyo, ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha ndugu wa wagonjwa kuwa makini na matapeli (vishoka) wanaojipenyeza katika taasisi hiyo kwa lengo la kuwadanganya na kuwatoza fedha kwa njia zisizo halali.
“Tunaendelea kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya utapeli. Tunawasihi ndugu wa wagonjwa kushirikiana na uongozi kwa kutoa taarifa mapema endapo watabaini uwep
o wa watu wasiohusika na taasisi hii, malipo yote yafanyike kwa control namba,” amesema Bw. Chediel