Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Habari za uzima wenu ndg zangu hongereni sana kwa mapambano.Na wapenda sana.

Nimeona nianzishe huu uzi uwe wa General kwa kutuma changamoto zetu zote tunazopitia katika mifugo yote. Hii namanisha kila aina ya kiumbe kinachofugwa unaweza kuuliza swali lolote kuhusu mifugo yako, kutoa ushauri wako pia ni mhimu sana, ku share nasi kipi unafanya/umefanya hadi kufikia hapo ulipo,Tuambie kuhusu magonjwa ya mifugo yako na namna unavyo pambana nayo. Ningeomba wadau ukaambanisha na picha/clip fupi watu wajifunze kwako.

Hali kadharika kwenye kilimo iwe vivyo hivyo kama nilivyo sema hapo juu kwenye mifugo.

Ifahamike wazi kuwa mimi sio mtaalamu na wala sijasomea kilimo wala mifugo ijapokuwa nina uzoefu japo natambua Elimu haina mwisho napenda sana kujifunza leo, kesho na kesho sijawahi acha.

Nita share nanyi vyote nivijuavyo kwenye ufugaji na kilimo na nipo tiyari kukosolewa kwa 100% pale ukiona nipo tofauti na unavyojua wewe lengo ni kuelimishana. Usiogope kutoa maarifa uliyo nayo kwani ukitoa hapa kichwa chako kitafunguka kupokea maarifa mapya zaidi trust me hii ndo kanuni.

Pia nawiwa sana kufahamiana (siyo lazima) kwa wale watapenda wafahamiane hasa maeneo jirani na wanakoishi mfano watu GEITA,KAHAMA,MWANZA,SHINYNGA wakafahamiana na ikiwezekana kutembeleana ili kujifunza kwa vitendo ingefaa pia(mawazo yangu)

Imani yangu ni kubwa sana kuwa humu kuna watu waliosomea hizi taaruma zote mbili.

Hapa itakuwa sehemu sahihi kwangu kuwapa tiba asili na hata ikiwezekana nitakuwa natuma video ninavyo andaa hasa kwenye kuku na mbuzi maana ndo mifugo ninayo fuga. kwa sasa sina kuku kutokana na chanagamoto kadhaa.

Nategemea watu watakuwa Serious midhaha isichukue nafasi sana hadi kututoa kwenye lengo.

Kwa sasa natumia divice ya kazini sina picha lakini by saa1 nitaweka picha hapa.

Karibuni sana..........

MLONGE KAMA DAWA YA KUKU/KANGA NA BATA.
IMG_20230203_181846_516.jpg

Mlonge una vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde
na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12 chuja na wape kuku. Isiyotumika
mwaga na tengeneza nyingine.

Iwapo hutaweza kuloweka kwa masaa hayo 12 basi mimi huwa nafanya hivi

Nachukua magao kama4 au5 binafsi huwa nakadiria tu maana sijawahi ona madhara kwenye kuku kama nimezisha.

Baada ya kuyaponda ponda kwenye kinu nitaloweka kwa muda wa lisaa1 tu kisha nayachuja vizuri.Kisha yale makapi naya changanya na chakula chao. huwa nafanya hivi kwa siku3-4 tu na kushuhudia maendeleo mazuri sana. Siku 4 zikiisha kesho yake siku ya5 huwa nawapa mpapai nitakuja elezea kwa kina.

Mlonge hutibu:

Mafua.
Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga
Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
Kuongeza hamu ya kula
Homa ya matumbo
kuhara
Ini.

Huwa nashauri kila mfugaji awe na miti hii kwake
Alovera
Mpapai
Mwembe
Mwarobaini
Pilipili kichaa
Mkonge(katani)
Komfrey
kuna minyaa yenye majani mapana (Cactus)

Hii ni baadhi tu na Nitaileza kwa mti mmoja baada ya mwingine.

TUTAENDELEA*
 
Andiko zuri...litatujenga & tutajengana.
 
Pilipili kichaa.

Pondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa muda wowote

Hutibu na kukinga....

Hii ni Kinga ya kideri/mdondo.
Hutibu mafuta hasa ukichanya na bapa la mkonge likipondwa pondwa na kuchanganywa.
IMG_20240425_073715_056.jpg

Hizi ni Moja wapo ya aina ya pilipili kichaa lakini og ni vile vidogovidogo sana ukipata hivyo Kwa kwenye Lita Moja ya maji weka5 tu hizi weka Saba Hadi 10.
 
kipindi hiki ni vyema wafugaji wa kuku kuwapa dawa sinazotibu salmonella kwani kesi hii imekuwa kubwa kwa wafugaji wengi,visababishi ni uchafu kwenye chakula na maji,kutokuosha vyombo vya maji yani kufuga kwa mazoea.

dalili za haraka kuku kuhara uharo mweupe kama chokaa

dawa wape barosin kwa siku tano
 
Kuna njia za kuwaogesha ng'ombe bila kuwa na josho la kutumbukia?
Naona eneo kubwa la kujenga josho ni matumizi mabaya kwa ardhi niliyopata.
Nguruwe Huwa tunawaogesha ki kawaida tu.
 
Zile chanjo za matone hazina madhara Kwa kuku zikitumiwa sana
Mm natak kufuga wa kienyeji tu
chanjo hiyo inaitwa tatu moja

ni nzuri kwani kwa mkulima anayefuga kuku wachache hatoingia garama ya kununua chanjo ya kideri,gomboro na ndui zote zipo kwa pamoja kwa chanjo hii ya tatu moja

ushauri wangu kama unafuga au unatarajia kufuga kuku wengi nunua chanjo ya kideri kivyake wape kadhalika gomboro na ndui
 
unaweza kutumia bomba la kupuliza ikiwa unataka kuwapida dawa za kuua wadudu

muhimu zingatia unampulizia dawa maeneo yote ya mwili kwani josho linapenda kutumika kwa sasababu linahakikisha mnyama kaloa mwili mzima hivyo jitahidi kupika dawa pande zote usilipue
 
chanjo hiyo inaitwa tatu moja

ni nzuri kwani kwa mkulima anayefuga kuku wachache hatoingia garama ya kununua chanjo ya kideri,gomboro na ndui zote zipo kwa pamoja kwa chanjo hii ya tatu moja

ushauri wangu kama unafuga au unatarajia kufuga kuku wengi nunua chanjo ya kideri kivyake wape kadhalika gomboro na ndui
Ooh sawa Asante
 
Zile chanjo za matone hazina madhara Kwa kuku zikitumiwa sana
Mm natak kufuga wa kienyeji tu
Hakuna madhara. Lakini pia kama una kuku wengi tumia Ile ya unga(kidonge) ya kuweka kwenye maji kuku wanakunywa Kwa masaa2 Kisha unamwanga inaokoa muda kuliko kutumia masaa zaidi ya3.
MFANO tu ni ngumu kuchanja Kwa njia ya matone kuku500 ama zaidi itakuchukua muda mrefu sana.

Pia Chanjo ni baada ya miezi3 kama unaishi hasa kijijini sehemu isiyokuwa na mwingiliano wa kuku kutoka sehemu tofauti tofauti. Lakini kama ni mjini/ Senta chanja Kila baada ya miezi2 tu
 
Back
Top Bottom