Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Sawa kumbe Kuna ya vidonge
 
Hujasema ni kuku gani wanaotakiwa kupewa pilipili kichaa. Je ni sawa kuwapa hawa kuku wageni i.e broiler?
 
Hujasema ni kuku gani wanaotakiwa kupewa pilipili kichaa. Je ni sawa kuwapa hawa kuku wageni i.e broiler?
Sijawahi Fuga broiler lakini na Imani Haina madhara.

Si shauri kuku kama broiler ujikite kwenye dawa Asili maana wao ni dhaifu sana kwenye kinga zao za mwili. Ni vyema ukienda direct kununua dukani.
 
Napenda kujua shamba la Ekari 50 kabla hujapanda unatumia mbolea ya samadi au hata ya madukani inatosha...?

Kama ni samadi na eneo hilo hakuna ya samadi shamba linaweza kufanya vizuri wakuu...?

Na pia, natakiwa kupitisha tractor na kuacha shamba litulie ndio nipande au naweza kupitisha tractor na kupanda kwa wakati mmoja ilhali mvua bado hazijaanza...?

Na kama napitisha tractor then nasubiria lipoe ndio nipande, natumia tractor kupandia au nguvukazi...? Najua kuna plante ila inaweza ikaongeza gharama za uzalishaji, hapo imekaaje wadau...?

Natanguliza shukran zangu za dhati kwenu. Ahsante sana.

Sehemu ya kulima ni Simanjiro mkoani Manyara.

Shukran.
 
Lily Tony
 
Nina maswali kadhaa nataka kufahamu chanjo zote nazotakiwa kumpa kuku kutokea kifaranga wa siku moja mpaka anapokuwa mtu mzima nataka kufahamu chanjo zinaaaply katika vipindi gani vya umri wa kuku anapoendelea kukua.Sijajua umebobea kufuga kuku wapi ila mimi nataka kudeal na sasso au kroiler
 
Mkuu Lily Tony tunaomba msaada wako kwenye hayo maswali kiongozi. Shukran.
Kwanza asante kwa mualiko huu mkuu.

Pili naomba nikiri kuwa siko vizuri sana kwenye kuelezea jambo au kumuelekeze mtu jambo kwa njia ya maandishi,hiyo ndio changamoto yangu.Hivyo endapo nitashindwa kueleweka nitakuwa tayari kurudia tena na tena.

Tatu KIOO umegusia mambo 3

Matumizi ya samadi Vs Mbolea za dukani.

Kulima na kupanda hapo hapo Vs kulima kwanza na kupumzisha shamba Kwa muda kisha ndio upande.

Kupanda kwa trekta Vs Nguvukazi.
 
KIOO
Uchaguzi wa aina gani ya mbolea ya kutumia shambani kwako, unategemea factors kama

Hali ya udongo
Aina ya udongo
Upatikanaji wa mbolea
Uchumi
Lengo la Kilimo
Kiwango cha rutuba n.k

Mbolea ya samadi ina faida na hasara zake.
Mbolea za madukani zina faida na hasara pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…