HongeraAisee Asante nilikuwa naplan kuanza ufugaji huu Uzi utanifaa sana
Ahsante mkuu,nasubiriaMkuu sijawahi lima hili zao halafu kuna tofauti kubwa kati ya pilipili kali na pilipili kichaa watu huwa wanaunganisha tu in fact hata iliyopo hapo pichani sio kichaa ambayo sisi tumekua tukaikuta na sasa ni nadra sana kuipata (kama upo kanda ya ziwa wasukuma huita bhukoloja)
Soko la pilipili kichaa/kali lipo sana nje ya nchi hata rwanda tu hapa wanalao.
kuhusu mbegu zake labda ukusanye kidogokidogo ila pwani niliwahi ona kama heka moja ya pilipili kali wao wanaita kichaa.
Sifa ya pilipili kichaa ukiimenya tu ile harufu yake lazima ukohoe pia ukizidsha matumizi lazima uugue kifue huwa ni vidogo sana nikienda kijijini nikabahatika kupata nitapiga pia niweke hapa.
Mkuu nashkuru sana mi nafkiri nitumie tu ya kiwandani kutokana na upatikanaji wa mbolea ya samadi kiongozi.Ninavyo jua hapa kwenye samadi na mboji unatakiwa uelewe kuna utofauti mkubwa mfano mboji unaweza izidisha na isilete madhara yoyote maadamu mvua ina nyesha ama kuna unyemvu wa kutosha.
Mfano usiokuwa wa kitaaramu ni kwamba ukichukua kg2 za mbolea ya mboji ukachanganya na mchanga kg1 ukipanda zao lako haitakuwa na shida bali litanawili mno.
Kwenye samadi nako imegawanyika katika sehemu kuu 2
1. Ni ile iliyoiva. ni mbolea iliyokaa muda mrefu ama pale kulikuwa na zizi mifugo ikahama kwa mwaka ama miaka2 mbolea iliyoachwa hapo itakuwa imeiva ama kuoza kabisa. Hii mara nyingi huwa nzito sana inakuwa kama mchanga kiasi kwamba ukichukua ndoo ya lita20 ukaijanza hiyo mbolea vilevile ukachukua ndoo ya lita20 ukaweka mbolea ya can ama urea uzito utakuwa tofauti mbali mno.
2.Nile ambayo haijaiva ama ni ile ya juu ipo kama vumbi ukienda mazizini hasa kiangazi utaona kuna mbolea juu juu na ni nyepesi mfano wa vumbi tu. hii ukichukua ndoo ya lita 20 ukaipima si ajabu ukapta kg4-5 tu wakati ile iliyooza unaweza pata kg23+ hadi hapo umepata picha.
Unapaswa kufahamu kuwa mbolea ya samadi/mboji humwagwa shamba lote bila kujali hapa utapanda ama hutapanda! hii lazima iende mbolea nyingi tofauti na mbolea za viwandani smbavyo mbolea hu wekwa moja kwa moja kwenye mmea/shina husika.
Chukulia mfano uchukue kg1 ya urea umwage chini pia chukua kg1 ya samadi mwaga pia bila shaka eneo halitatofautiana sana ndo picha halisi ilivyo.
Kwanini mbolea ya samadi inamwaga shamba lote? Kumbuka hapo mwanzo nilisema hukaa muda mrefu hadi zaidi ya miaka3 ikiwa inafanya kazi. hivyo hata usipoitumia kwa kipindi hiki ukija kulipa awamu ijayo utaikuta na itakuwa imeoza vizuri zaidi. Na ukweli uko hivyo awamu ya pili ndo huwa na matokeo mazuri zaidi,.
SahihiMkuu nashkuru sana mi nafkiri nitumie tu ya kiwandani kutokana na upatikanaji wa mbolea ya samadi kiongozi.
Kuna hii mbolea ya Minjingu sijui umeshawahi kuiskia mkuu...?Sahihi
Kuisikia Huwa najisikia sijawahi itumia.Kuna hii mbolea ya Minjingu sijui umeshawahi kuiskia mkuu...?
Pole sana asee.....Mkuu naweza pata picha ama ka video kafupi kabla sijakujibu?Yaani Jana na juzi kuku wangu wengi wamekufa,walikuwa wanatoa kinyesi cheusi,kijani na cheupe.
Walikuwa wanakohoa au kutoa sauti kubwa ,wanatoa maji maji yanayovutika km kamasi.
Nikafikiri Ni mafua nikanunua dawa ya mafua,jamani jamani,wamekufa wa kutosha.
Sasa inabidi nitafute elimu sahihi ya ufugaji,Asante boss,naamini nitajifunza mengi humu
Pole mkuu. Wana miezi mingapi Hadi Sasa?Mkuu asante sana umekuja wakati muafaka kwa sababu namimi nina changamoto yangu.
Kuku wangu (Malawi Breed) wameshafikisha umri wa kuanza kutaga toka mwaka jana mwezi 11 lakini mpaka leo hawajaanza kutaga. Yan ukiingia bandani unaokota mayai hafiki 8. Kuku wap 150 na wanapata chakula na mboga za majani enye mchanganyiko safi na salama. Tatizo ni nini?
Hahaaa yaani waafrika jamaniHuku Morogoro wakulima wa miwa wamezuia mvua mpaka watakapovuna miwa yao na kuuza kiwandani. Kama kuna mganga wa kupambana nao hebu tustue
Maisha kitendawili sanaView attachment 3195208
Picha kuku wakiushambulia mlonge.
Wapo Kwa ajiri hiyo mkuuMaisha kitendawili sana
Mnaishi kirafiki mwisho wa siku bila huruma wanapigwa kisu wanafukiwa tumboni
Sijui na sisi tupo kwaajili ya naniWapo Kwa ajiri hiyo mkuu
Funza. Binadamu ndo boss wa wote hao wapo chini yakeSijui na sisi tupo kwaajili ya nani
Chanjo uliwapa ya kideri?Yaani Jana na juzi kuku wangu wengi wamekufa,walikuwa wanatoa kinyesi cheusi,kijani na cheupe.
Walikuwa wanakohoa au kutoa sauti kubwa ,wanatoa maji maji yanayovutika km kamasi.
Nikafikiri Ni mafua nikanunua dawa ya mafua,jamani jamani,wamekufa wa kutosha.
Sasa inabidi nitafute elimu sahihi ya ufugaji,Asante boss,naamini nitajifunza mengi humu
Wana miezi saba mpaka sasa.Pole mkuu. Wana miezi mingapi Hadi Sasa?
Chakula unawapa Kwa uwiano Gani?
AsanteHongera
Hii Waganda wanatumia saana, shukrani mkuu.MTI WA PAPAI HUTIBU........
View attachment 3196098
Chemsha magao mawili ndani ya maji lita 6 hadi ubakie na lita 1. Poza kisha chuja.
Hutibu minyoo aina yote.
MBEGU ZAKE:Hutibu minyoo pia kusanya mbegu kiasi uwezavyo kisha kausha ziwe kavu kabisa weka sehemu salama hasa kwenye ndoo au mfuko usiopitisha maji/unyevu.
Chukua nusu kikombe cha chai changanya na kg5 za chakula chako kwa siku 4 tu hata kama hujaona dalili za minyoo zoea kuwapa tu kwani hutibu na kukinga magonjwa kadhaa.Pia wengine huweka kwenye maji lita3 kwa kijiko kimoja cha chakula.Kwenye minyoo pia ongeza na mbegu za mlonge punje tatu hadi5 zintosha kutibu maji lita 5 ya kunywa iwe binadamu au mifugo huwa nafanya hivyo mimi hasa kwenye mbuzi.
Mbegu za mlonge ukizisaga ni nzuri sana na maji huwa msafi kama umeweka shabu uchafu wote utaukuta chini.
MAJANI YA MPAPAI.
Hutibu kuharisha (Coccidiosis):
Mafua
Kipindupindu
Chukua majani ya mpapai matawi 3-5 ya ponde/twanga yawe kama kisamvu loweka kwenye maji lita6 kwa muda wa masaa2 chuja wape. makapi usitupe chnganya kwenye chakula chao.
UTOMVU WA PAPAI
Hutibu vidonda kama kuku kajeruhiwa na kupata jeraha tumia utomvu wake ni vyema ukatumia na maji ya tunda la ndulele kwa matokeo mazuri zaidi.
NB:Ili upate mbegu za mapapai za kutosha panda mipapai angalu 10 ni nzuri sana hii tiba ya mpapai kama nilivyo orodhesha hapa. hii itakusaidia wewe kulamatunda yake na kuuza hata usipouza kuku ni wadau wazuri mno wa kula mapapai hasa bata ndo mahala pake.
AHSANTE.