Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Yaani Jana na juzi kuku wangu wengi wamekufa,walikuwa wanatoa kinyesi cheusi,kijani na cheupe.
Walikuwa wanakohoa au kutoa sauti kubwa ,wanatoa maji maji yanayovutika km kamasi.
Nikafikiri Ni mafua nikanunua dawa ya mafua,jamani jamani,wamekufa wa kutosha.
Sasa inabidi nitafute elimu sahihi ya ufugaji,Asante boss,naamini nitajifunza mengi humu
ulitumia dawa gani
 
IMG_20250109_141704_898.jpg
 
HIVI WAJUA POMBE AINA YA GONGO ILE NO1 NI TIBA KWA KUKU? VIPI KUHUSU MAGADI YA ASILI?SOMA HAPA UJIFUNZE KITU.
GONGO NO1


Hii ni pombe ya kienyeji inafahamika na imepigwa marufuku na serikali ya JMR. Pamoja na hayo yote mimi imekuwa ikinisaidia kwa muda mrefu sasa kama tiba kwa kuku wanao ugua kideri na kipindupindu.

Chakufanya Tafuta pombe aina ya gongo shart iwe no1 hakikisha hilo kuwa iwe no1.Mara nyingi hii no1 hata ukiiwasha huwa inawaka moto ina mfumo kama sprit hivi mimi huwa naitambua kwa jinsi hiyo pia huwa naitest kwa kuionja (kunywa) kidogo sana. Istoshe nachukua kwa mtu ambae namwamini.

Baada ya kuipata na ukajiridhisha ni og no1 chukua mils 5 ama kisoda mnyweshe kuku wako anayeumwa mara2 kwa siku hadi atakapokuwa sawa mara nyingi matokea huwa yanaonekana muda mfupi tangu umnyweshe.Kuku baada ya kunywa ile dawa huchangaka kama alikuwa hali ataanza kula muda mfupi.

Zingatia kila umalizapo kumpa hii dawa hakikisha baada ya dk10-15 umpe maji ya kunywa au umunyweshe kiasi chochote utakachoweza kisha muache.Sina utaalamu kuwa nini kilichomo kwenye pombe hiyo hadi kusaidia kupona
hii tiba nimeirithi tangu utoto hadi sasa.Kama imani yako haikurusu kutumia siyo lazima utumie.

MAGADI
Magadi hutumika kama kinga wazoeshe kuku wako kuwapa kwenye maji au chakula una saga hadi kuwa unga kabisa kisha unaweka kwenye maji kwa kukadiria tu hapa sijawahi kuwa na kipimo maalumu hivyo nawe utakadiria ama kwa kukusaidia chukua magadi yaliyo sagwa tyr vijiko5 vya chai kisha weka kwenye maji lita Tano.
Baada ya siku2 utaona kuku wako wanakunya kinyesi chenye minyoo lakini kama wanayo hiyo minyoo kama hawana hutaona kitu chochote.Magadi hukinga magonjwa mengi sana.
MAGADI KWENYE WANYAMA.

Huku kwetu tangu zamani magadi yametumika sana kutibia wanyama wafugwao kama ng'ombe,kondoo na mbuzi pale wanapovimbewa kuna mihogo fulani huwa inasumu kali kwa wanyama kwa sasa imeadimika sana kanda ya ziwa ilijulikana kama lumala(lyongo) mihogo michungu na majani yake ni sumu kwa wanyama hasa yale mapya ya mwanzoni mwa msimu wa mvua yalikuwa sana kwa mifugo.

Mnyama yeyote mwenye shida hiyo alikuwa ananyweshwa na muda mfupi tu ataanza kuharisha na hii ndo pona yake.Siyo hivyo magadi hadi leo hii wanao nenepesha ng'ombe kwa ajiri ya biashara huwa wanayatumia sana pamoja na kwamba kunadawa za kisasa kibao lakini magadi bado yana aminika sana kwa wafugaji.


Huku kipande ama kitofari (nitaweka picha )cha magadi huuzwa 2000-3000 tu hivyo unaweza nunua hata kumi ukatunza na kuwa unatumia taratibu taratibu maana kuna muda huadimika sana hasa masika kama una kuku hawazidi mia basi vitofali viwili vinatosha.

MATUMIZI. Saga magadi yako yawe kama unga kisha weka kwenye maji wanayotmia wanyama wako hakikisha maji ni mengi kwani huwa wanakunywa hasa maana yanakuwa na mvuto flani kama chumvi hivi. fanya mara moja tu kwa siku kisha wape maji ya kawaida iwapo utawazoesha hasa hawa mbuzi hawatakuwa wanakunywa maji ya kawaida kama inavyotakiwa.

Ukiona njia hiyo ni ngumu basi wape vipande kadhaa na weka mahali ambapo watakuwa wanalamba lamba kwa muda wao iwe usika ama mchana.

Mabadiriko ni ndani ya mwezi1 tu utaona wanyama wako wamenawili kuliko mwanzo maana hawatakuwa na minyoo na magonjwa nyemelezi.

IMG_20250108_185846_388.jpg



KISAMVU NI DAWA YA UTITIRI.
Chukua kiasi cha kutosha kisha twanga hadi vilainike kisha loweka kwenye maji kwa muda wa lisaa1 ama zaidi.Kisha chukua pump/solo yako pulizia bandani vizuri hii ni komesha.

Ahsanteni.........

Manyanza
 
Okay, ina maana Dengu inastawi popote ambapo inapandwa au itategemea na ardhi/udongo...?
Degu inakubali kwenye mbuga(udogo mweusi) haipendi kabisa mvua iwapo maji yatwatuama kwa siku nzima ama mbili tegemea hasara ya shamba lote. Hupandwa mwishoni mwa msimu kama huku kanda ya ziwa huanza kupanda mwezi wa4 nk
 
Back
Top Bottom