Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Nasisitiza tumia vipimo vya mzani mkuu.

MIMI HUWA NAFANYA HIVI NA MATOKEO HUWA SI MABAYA

Mahindi kg50
Pumba mahindi kg15
Soya kg18 unaweza punguza kama huwafungii ndani
Mashudu alizeti pamba ama alizeti kg7
Dagaa/Uduvi/mabaki ya samaki kg4(dagaa zikaangwe huwa na wadudu nk)
Mifupa kg3
Chokaa kg2 au 1kama mifupa umeweka kg3 uhakika
Chumvi 0.5(gram 500)nusu kg
Vitamini kg2

Mkuu jaribu hii uone na usiache kuwapa majani

Ahsante sana
Asante mkuu. Ila huu mchanganyiko mbona kama kuku wa kisasa
 
Shubiri Mwitu (Aloe vera):
Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya
maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 - 7.
Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12.

Mchanganyiko huu unaweza kutibu:

Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka)
- inyweshwe kabla kwa kinga.
Homa ya matumbo (Typhoid).
Mafua (Coryza).
Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).

Mwembe:

Majani magao mawili, ponda na chemsha ndani ya lita 6 za maji hadi ibaki lita 1. Wape kwa siku
moja.

Mwembe hutibu:
Homa ya matumbo.
Mafua.
Kinga ya Kideri/Mdondo
 
Nimbolea gani nzuri yakupiga kwenye tangawizi
MBOLEA
Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 10 - 12 Kwa ekari na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK. N 40 – 48 kg, P2O5 31.2 – 32 kg, na K2O 40 – 48 kg. Mwanzoni tumia nusu ya Nitrogen na kiasi chote cha P na K, kiasi kilichobaki cha Nitrogeni kitumike siku ya 45 na 90 baada ya kupanda. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana. Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua magugu, Kama simazine hutumika.

Nimeitoa sehemu sijawahi lima tangawizi mkuu sina uziefu huo. Tusuburi wengine waje ama ingia hapo

Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau
 
Mimi kuna kuku amechomwa na mwiba ama msumari (sina uhakika) hapa pa kukanyagia..leo ndo nimemuona jioni wakati wanaingia ndani ya banda Amevimba na nimejaribu kupashika analalamika. Nampatia nini ? Antibiotics? Nilichokifanya nimemsafisha hapo palipoumia kwa maji then nikampaka alovera.
 
Pole saana! Tafuta dawa ya vidonda ile ya kupuliza
 
Habari za uzima wenu ndg zangu hongereni sana kwa mapambano.Na wapenda sana.

Nimeona nianzishe huu uzi uwe wa General kwa kutuma changamoto zetu zote tunazopitia katika mifugo yote. Hii namanisha kila aina ya kiumbe kinachofugwa unaweza kuuliza swali lolote kuhusu mifugo yako, kutoa ushauri wako pia ni mhimu sana, ku share nasi kipi unafanya/umefanya hadi kufikia hapo ulipo,Tuambie kuhusu magonjwa ya mifugo yako na namna unavyo pambana nayo. Ningeomba wadau ukaambanisha na picha/clip fupi watu wajifunze kwako.

Hali kadharika kwenye kilimo iwe vivyo hivyo kama nilivyo sema hapo juu kwenye mifugo.

Ifahamike wazi kuwa mimi sio mtaalamu na wala sijasomea kilimo wala mifugo ijapokuwa nina uzoefu japo natambua Elimu haina mwisho napenda sana kujifunza leo, kesho na kesho sijawahi acha.

Nita share nanyi vyote nivijuavyo kwenye ufugaji na kilimo na nipo tiyari kukosolewa kwa 100% pale ukiona nipo tofauti na unavyojua wewe lengo ni kuelimishana. Usiogope kutoa maarifa uliyo nayo kwani ukitoa hapa kichwa chako kitafunguka kupokea maarifa mapya zaidi trust me hii ndo kanuni.

Pia nawiwa sana kufahamiana (siyo lazima) kwa wale watapenda wafahamiane hasa maeneo jirani na wanakoishi mfano watu GEITA,KAHAMA,MWANZA,SHINYNGA wakafahamiana na ikiwezekana kutembeleana ili kujifunza kwa vitendo ingefaa pia(mawazo yangu)

Imani yangu ni kubwa sana kuwa humu kuna watu waliosomea hizi taaruma zote mbili.

Hapa itakuwa sehemu sahihi kwangu kuwapa tiba asili na hata ikiwezekana nitakuwa natuma video ninavyo andaa hasa kwenye kuku na mbuzi maana ndo mifugo ninayo fuga. kwa sasa sina kuku kutokana na chanagamoto kadhaa.

Nategemea watu watakuwa Serious midhaha isichukue nafasi sana hadi kututoa kwenye lengo.

Kwa sasa natumia divice ya kazini sina picha lakini by saa1 nitaweka picha hapa.

Karibuni sana..........

MLONGE KAMA DAWA YA KUKU/KANGA NA BATA.
View attachment 3195205

Mlonge una vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde
na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12 chuja na wape kuku. Isiyotumika
mwaga na tengeneza nyingine.

Iwapo hutaweza kuloweka kwa masaa hayo 12 basi mimi huwa nafanya hivi

Nachukua magao kama4 au5 binafsi huwa nakadiria tu maana sijawahi ona madhara kwenye kuku kama nimezisha.

Baada ya kuyaponda ponda kwenye kinu nitaloweka kwa muda wa lisaa1 tu kisha nayachuja vizuri.Kisha yale makapi naya changanya na chakula chao. huwa nafanya hivi kwa siku3-4 tu na kushuhudia maendeleo mazuri sana. Siku 4 zikiisha kesho yake siku ya5 huwa nawapa mpapai nitakuja elezea kwa kina.

Mlonge hutibu:

Mafua.
Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga
Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
Kuongeza hamu ya kula
Homa ya matumbo
kuhara
Ini.

Huwa nashauri kila mfugaji awe na miti hii kwake
Alovera
Mpapai
Mwembe
Mwarobaini
Pilipili kichaa
Mkonge(katani)
Komfrey
kuna minyaa yenye majani mapana (Cactus)

Hii ni baadhi tu na Nitaileza kwa mti mmoja baada ya mwingine.

TUTAENDELEA*
Nitajie jina la viazi vya kulisha nguruwe tunavyo kaangiwa hapa dar es salaam kama chips...kisha niambie kwanini viazi vizuri vya chips vimepotea nchini ...kwanini serikali pumbavu ya samia inashindwa kuweka viwango na ubora na aina za mazao yaliyo chaguliwa kwa ubora kulimwa nchini na kupiga marufuku mbegu zote na kilimo cha mazao mabovu kama hivi viazi vya kulishia nguruwe ambavyo huyu msomali.mpuuzi kafanya vifulike nchini ...sifa ya hivyo viazi ni kama utapikia pilau basi vyenyewe vina anza kuchacha kabla ya pilau na kuozesha pilau lililo lala....kama unajua jina la hivyo viazi mviringo ni vyema ukatuambia jina lake?
 
Mimi kuna kuku amechomwa na mwiba ama msumari (sina uhakika) hapa pa kukanyagia..leo ndo nimemuona jioni wakati wanaingia ndani ya banda Amevimba na nimejaribu kupashika analalamika. Nampatia nini ? Antibiotics? Nilichokifanya nimemsafisha hapo palipoumia kwa maji then nikampaka alovera.
Samahani sana mkuu sikuona notification yako asee. Ulichofanya ni sahihi zaidi ya yote chukua maji ya mkonge (katani) unakuwa unaweka hapo kwenye jeraha kila umalizapo ku,safisha na maji ya vuguvugu yaliyotiwa chumvi kidogo.
 
Sawasawa. Ila nilitumia alovera tuu..asubuhi namnywesha na kumpaka, jioni nampaka tuu..siku tatu tuu akawa sawa.

Asante sana Mkuu. Hiyo ya katani sijui nitapata wapi niipande hapa kwangu...?
 
Sawasawa. Ila nilitumia alovera tuu..asubuhi namnywesha na kumpaka, jioni nampaka tuu..siku tatu tuu akawa sawa.

Asante sana Mkuu. Hiyo ya katani sijui nitapata wapi niipande hapa kwangu...?
EE UKIPANDA NI NZURI ZAIDI
 
Back
Top Bottom