BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wanaume wanne wamekamatwa kwa madai ya kumuua dada yao waliompiga hadi kumsababishia umauti kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi waliokuwa nao kwa muda mrefu.
Tukio hilo limetokea siku ya Jumamosi usiku, wilayani Rukiga nchini Uganda, tovuti ya Monitor ya Uganda imeripoti.
Watuhumiwa hao ambao ni kaka wa marehemu wote ni wakazi wa Ibumba katika kata ndogo ya Rwamucucu, wanadaiwa kumshambulia kwa kipigo dada yao aitwaye Christine Kiconco mwenye miaka 41.
Msemaji wa polisi mkoani Kigezi, Elly Maate aliwataja washukiwa ni Innocent Tumwekwase, Samuel Atuhirwe, Christopher Bikorwomuhangi na Justus Mayumba.
"Inadaiwa kuwa familia ya marehemu imekuwa na mgogoro wa ardhi tangu baba yao aitwaye Selestino Byaruhanga alipoamua kuwagaia urithi watoto wake hao ndipo matatizo yalipoanza,” alisema Maate.
Inasemekana watoto wa kiume waliamua kuuza ardhi yao mara moja baada ya kurithishwa na kuanza kudai sehemu ambayo walipewa watoto wakike na tangu wakati huo, wamekuwa wakimtishia marehemu.
Kulingana na polisi, wamesema marehemu alirudi nyumbani akiwa amelewa majira ya saa nane usiku wa kuamkia Jumamosi ndipo umauti ukamkuta.
Polisi walifika eneo la tukio wakiwa na mbwa wa kunusa ambapo aliwaongoza maafisa wa uchunguzi hadi kwenye nyumba za washukiwa na hivyo kukamatwa.
Kesi hiyo ya mauaji ya kushambulia imefunguliwa katika Kituo cha Polisi cha Rukiga Kusini Magharibi mwa Uganda.
MWANANCHI