Ndugu Wana JF Nimekuwa napata changamoto ya Kufungua Gmail Account Kwa Wiki sasa. Kila namba Ya Simu ninayojaribu kuweka kwa ajili Ya Verification inagoma. Ukizingatia kipindi hiki Wanafunzi wanatuma maombi Mbalimbali na wanaitajika kuwa na Email. Imekuwa changamoto sana kwangu na kwa hao ninaohitaji kuwafanyia maombi mbalimbali.
Ninaomba Msaada kwa yeyote anaweza nisaidia kutatua changamoto hii au kuniunganisha na wahusika watusaidie, kwani Nimepokea simu za watu tofauti kutoka mikoa mbalimbali na wao wanapata kadhia kama yangu.
Nawasilisha