Ndugu wananiita mchawi wakati walilelewa na baba yangu mzazi

Huyu dogo Mchawi kweli,ugomvi na babaake alitaka urithi mzee yuko hai,tena baada ya kushindwa loge huko.hana maana
 
Hiki chama watu wakew wako vipi sijui ati kwa umri huo bado unalelewa mpaka unafukuzwa !
 
Kweli wewe hauko sawa. Lazima ukapimwe. Hivi hapo umeandika wewe mwenyewe? Ndio una degree kweli? Daah...! I see wewe ni kilaza. Sidhani kama kuna mtu wa kukupa connection,kama tu babaako unataka kumnyang'anya mke wake wewe ni kilaza wa kuogopwa
 
Msomi mzima unamdanganya mama yako akavunje ndoa?????.

Unajua anayetaka kuvunja ndoa Kwa mujibu wa sheria hana chake (Mali)???

Mzee wako angepata washauri wa masuala ya sheria wangemwambia yeye akatae kuvunja ndoa ili ionekane maza yako ndio anavunja ( mkataba) so angeambulia patupu.

Kijana tafuta kazi acha kugombanisha familia ili upate urithi. Elimu uliyonayo ni urithi tosha
 
We jamaa unatakiwa kuchapwa fimbo nyingi tu. Kumbe ulikuwa shule ya mameneja, umemaliza mwaka gani?
 
Kati ya baba yako na ccm, nani anayekufaa?
 
Miaka 38 una mu advise mama yako aachane na baba ako eti kisa apate mali?

Kwani hukuona njia nyingne ya kutafuta solution?
 
Acha kupigana vita ndogo ndogo zisizo na tija. Sasa ukiitwa mchawi umekua mchawi kweli?
Pigana vita ya kuboresha Maisha ya familia yako.
Usisikilize umbea, umbea waachie wavaa Madera na wanawake wasio na waume aka single mothers
 
...Na miaka yako 37 unaunga Mkono Wazazi waachane kwa Sababu ya Vyama vya Siasa tu, halafu unakuja JF kulia lia?
Nenda Chamani ukaombe Msaada...!
 
Bro..!! Mbna kama ukwama hiv.... Yan ww umezaliwa umekuta baba yako na mama yako wanaishi pamoja leo hii umekuwa kiasi gan mpaka umeanza kumshauri mama yako aachane na baba yako..??? Aisee unahitaji kupimwa akili... Kijana 37yrs msomi unataka mama yako aachane na baba yako.... Kaa chini jitafakari upya kijana.... Kama kweli ww sio mchawi kama ndg zako walivyokwambia basi ww una matatizo ya akili.
 
Naona kila baada ya miezi 3 unamlalamikia huyo baba yako.

Kushindwa kwako kupata ajira ni kwa sababu huyo kiongozi wako wa ccm uongozi wake kutoweka mikakati ya kuboresha ustawi wa jamii, hivyo ni makosa kumlaumu baba yako maana tayari alishakupatia elimu.

Ushauri, kama hutobadili mwenendo wa kifikra utapatwa na msongo wa mawazo ambao unaweza sababisha kujiua au kuu ili upate mali
 
Huyu jamaa ana depression au anataka attention tu. Nimefuatilia nyuzi zake kila uzi lazima uwe na repetition ya elimu, umri na sehemu anayoishi sababu anatambua fika kua ndio sehemu atakayopata reacation na sio mada aliyowasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…