Ndugu wang'ang'ania mwili wa marehemu waliyemtenga akiwa hai, wananchi wasema wataamua wao azikwe wapi

Ndugu wang'ang'ania mwili wa marehemu waliyemtenga akiwa hai, wananchi wasema wataamua wao azikwe wapi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hali ya taharuki na vurugu vimeibuka katika Mtaa wa Elkiroa Kata ya lemara Mkoani Arusha baada ya Wananchi kuweka kambi katika Familia ya Kijana Elibarik Tarimo kwa siku tatu baada ya kudaiwa kuwa Ndugu wamegoma Kijana huyo asizikwe katika eneo alilokuwa akiishi baada ya kutelekezwa na kulala kwenye eneo panapoisshi mbuzi na ng’ombe akiwa Mgonjwa.

Wananchi waliofurika katika eneo hilo wamesema Kijana huyo alikuwa akiumwa lakini Familia ilikataaa kumhudumia ambapo Majirani walianza kuchanga fedha.

Hata hivyo Mzee wa ukoo ameiingia kwenye matatizo na kuokolewa na Polisi ambapo Wananchi wamekubaliana waende katika eneo la Morovian ili waje na majibu ya kwamba atazikwa sehem gani.

===

Siku zote Maishani Watu wema sana na wenye Uchungu hasa na mwenye Shida / Uhitaji huwa ni Watu baki pekee.
 
Wakazi wa Mtaa wa Ilikirowa Kata ya Lemara Jijini Arusha, wamezua taharuki baada ya mkazi aliyefahamika kwa jina la Bariki Tarimo mwenye umri wa miaka 41 kupoteza maisha katika halingumu baada ya kusumbuliwa uvimbe kwenye koromeo uliosababisha Saratani, Ndugu zake walimtenga na kukataa kumsaidia matibabu wakidai ananuka na kulazimika kuwa analala kwenye zizi la ng'ombe.

Taharuki hiyo imezuka baada ya ndugu kujitokeza baada ya Bariki kufariki na kutaka kumzika sehemu nyingine ambayo si eneo la marehemu mama yake, Wananchi wamegoma na kusema wao ndiyo watamzika mahali wanapopataka kwani wakati wa uhai wake wao ndiyo walimchangia matibabu.

Chanzo: manaratv

Siku zote Maishani Watu wema sana na wenye Uchungu hasa na mwenye Shida / Uhitaji huwa ni Watu baki pekee.
Wachagga tena?🙁☹😣
 
Bariki mama yake mmarangu na baba yake mrombo, ametunzwa na bibi wa kufikia wakati ndugu zake matajiri wanaishi Nairobi na sehemu nyingine. Hao ndugu zake si masikini ni matajiri ambao wakati wa Krisimasi walikuja nchini wakiwa na mabmw! Hata hivyo hawakuweza kumuogesha na kumpeleka kwenye tiba ya kansa licha ya kujulishwa na hao wananchi! Hakuna hata ndugu aliyethubutu kumsogelea Bariki kwenye makazi yake ya zizi la ng'ombe, kumbuka Yesu naye alizaliwa kwenye zizi la ng'ombe, Bariki Mungu atambariki na hao nduguze matajiri watalaaniwa.
 
Bariki mama yake mmarangu na baba yake mrombo, ametunzwa na bibi wa kufikia wakati ndugu zake matajiri wanaishi Nairobi na sehemu nyingine. Hao ndugu zake si masikini ni matajiri ambao wakati wa Krisimasi walikuja nchini wakiwa na mabmw! Hata hivyo hawakuweza sana kumuogesha na kumpeleka kwenye tiba ya kansa licha ya kujulishwa na hao wananchi! Hakuna hata ndugu aliyethubutu kumsogelea Bariki kwenye makazi yake ya zizi la ng'ombe, kumbuka Yesu naye alizaliwa kwenye zizi la ng'ombe, Bariki Mungu atambariki na hao nduguze matajiri watalaaniwa.
Poleni sana ndugu.
 
Back
Top Bottom