mwanausangi
JF-Expert Member
- Nov 4, 2021
- 548
- 608
Dar es Salaam. Safari ya mwisho ya maisha ya daktari Mtanzania, Mohammed Ali Hafidh (37) aliyefariki dunia nchini Uganda kwa ugonjwa Ebola ilihitimishwa juzi, baada ya kufanyika maziko ambayo yalihudhuriwa na familia yake kwa njia ya mtandao.
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Dk Aziz Milima alithibitisha kufanyika kwa maziko hayo yaliyoshuhudiwa pia kwa njia ya mtandao na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula pamoja ndugu, jamaa na marafiki wa daktari huyo.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana, Balozi Milima alisema baada ya kutokea kifo hicho Serikali ya Uganda ilitoa taarifa kwenye ofisi za ubalozi na kuomba utaratibu kwa kuwa sheria hairuhusu kusafirishwa kwa mwili ambao kifo chake kimetokana na ugonjwa wa mlipuko.
Alisema baada ya mawasiliano kati ya ubalozi na familia ilitolewa ridhaa ya mwili huo kuzikwa kwa maelekezo ya kuwekwa alama katika eneo atakalozikiwa, ili janga hilo litakapokwisha familia iende kuzuru kaburi lake.
“Mazishi yameshafanyika nusu saa iliyopita na hili limefanyika wakishuhudia baadhi ya ndugu, jamaa na rafiki zake pamoja Waziri Mulamula. Serikali ya Uganda ilituwezesha kuwa na video link ya mazishi hayo.
“Hili lilifanyika baada ya familia kutoa ridhaa na kuelekeza baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anazikwa kwa misingi ya dini ya kiislamu na kweli taratibu zote zimezingatiwa, walikuwepo masheikh kwa uangalifu mkubwa, ili asiwepo mwingine anayekuwa kwenye hatari,” alisema Balozi Milima.
Balozi huyo alisema Serikali ya Uganda ilitoa ushirikiano kuhakikisha maombi ya familia yanazingatiwa, licha ya utaratibu wa nchi hiyo kuelekeza kila anayekufa kwa ugonjwa wa Ebola kuzikwa ndani ya saa tatu baada ya kufikwa na umauti.
“Kwa kweli tunaishukuru Serikali ya Uganda kwa kujali na kusikiliza maombi ya familia, kwa kawaida kifo cha aina hii mtu anazikwa ndani ya saa tatu baada ya kufa, lakini kwa huyu angalau muda umesogezwa na wametengeza video link, ili familia ishiriki.
Alipataje Ebola
Balozi Milima alisema kabla ya Dk Ali kugundulika kuwa na Ebola, aliwahudumia wagonjwa wanne wa familia moja ambao walikuwa na ugonjwa huo na watatu walifariki kabla ya kugundulika kama wameambukizwa.
“Akiwa katika mafunzo yake kwa vitendo hospitali ya Mubende, historia inaonyesha kwanza alimtibia mtoto wa miezi tisa akafariki, kisha akaja mama na mtoto pia wakafariki, lakini si yeye wala madaktari wengine waliobaini kuwa watu hao wana Ebola na walitoka familia moja.
“Baada ya hapo akamtibu kijana mwingine wa miaka 24 huyu ndiye alionyesha dalili za ugonjwa huo na alipochukuliwa sampuli kwa ajili ya vipimo ilithibitika kuwa ana Ebola. Baada ya siku chache daktari naye akaanza kuonyesha dalili na vipimo vikaonyesha kuwa ameambukizwa.
“Imekuja kugundulika kuwa yule kijana alitoka kwenye familia moja na wale wagonjwa wake wa awali na inaonekana familia hiyo watu wanane wamekufa, wengine hata hospitali hawakupelekwa walifia na kuzikwa nyumbani. Inasikitisha kuona mwanataaluma huyu amepoteza maisha akitekeleza majukumu yake,” alisema.
Katika hatua nyingine Kamishna wa wa polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad alisema licha ya daktari Ali alikuwa askari, alihudumu katika zahanati ya makao makuu ya polisi Ziwani.
“Ni kweli, ailikuwa askari wetu na alikuwa daktari katika zahanati yetu ya Ziwani, alikwenda Uganda kwa ajili ya kujiongeza ujuzi,” alisema Kamishna Hamad.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Mazru juzi ilieleza Dk Hafidh alikuwa akisomea udaktari bingwa wa upasuaji na alikufa wakati akiendelea na matibabu katika hopsitali ya Fort Portal Ishaka RRH.
credit: Mwananchi