Ndugu wawili Yanga na Simba wote wamepigwa Algeria, nchi imetulia tuli

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mungu fundi kwelikweli. Yanga (Damas) kapigwa 2-0 na Simba (Ndumbalo) ni kama tu wamepigwa pia 2-0 ukiondoa bao la kubahatisha la Shabalala. Nchi imetulia hakuna vuvuzela hata moja lilisikika mtaani, ni utulivu kwa kwenda mbele.

Yanga wanasema walifungwa kwasababu waliwakosa wachezaji wake hatari kama Mzize, Job, Aucho na Boka, Je, Simba walitoa kisingizio gani?

Tuache ushabiki lopolopo, tuzipe timu zetu ushauri wa kimpira utakaowasaidia kuvuka vizingiti.
 
We chura na mazembe wanaenda kuwakanda tena huko na mpaka mrudi dar itakuwa imetanuka vya kutosha.
Ateba na Mukwala hawafungi, anafunga Shabalala, wewe huogopi? Hakuna kitu hapo bro. Beki kufunga goli ni fluke tuu.
 
Mungu fundi kwelikweli. Yanga (Damas) kapigwa 2-0 na simba (Ndumbalo) ni kama tu wamepigwa pia 2-0 ukiondoa bao la kubahatisha la Shabalala. Nchi imetulia hakuna vuvuzela hata moja lilisikika mtaani, ni utulivu kwa kwenda mbele.

Yanga wanasema walifungwa kwasababu waliwakosa wachezaji wake hatari kama Mzize, Job, Aucho na Boka, Je, Simba walitoa kisingizio gani?

Tuache ushabiki lopolopo, tuzipe timu zetu ushauri wa kimpira utakaowasaidia kuvuka vizingiti.
Tatizo lako(siyo changamoto)hauhudhurii kliniki ya wagonjwa unyooshe viungo.Lile goli la Mohamed Hussein ni la kubahatisha?Kijijini kwetu walipoliona lile goli nimezawadiwa punda nibebee maji mtoni.
 
Sikatai kuwa lile lilikuwa goli kali sana na linaweza kuwa miongoni mwa magoli bora ya mashindano, LAKINI LAKINI LAKINI ile ilikuwa cross iliyokatika na kuelekea golini moja kwa moja. Hata mfungaji alishangangaa kuambiwa limeingia golini; fluke
 
Alikuwa anaangalia wapi?Alitaka kutoa pasi au kufunga goli?Acha wivu aisee!
 
Sikatai kuwa lile lilikuwa goli kali sana na linaweza kuwa miongoni mwa magoli bora ya mashindano, LAKINI LAKINI LAKINI ile ilikuwa cross iliyokatika na kuelekea golini moja kwa moja. Hata mfungaji alishangangaa kuambiwa limeingia golini; fluke
Uliwahi kuona magoli aliyofunga Yahya Tostao akiwa timu ya taifa au lile goli la free kick alilofunga Robert Carlos dhidi ya Ufaransa.
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Mipang'ang'a SC.
4. Malalamiko (Lialia) SC.
5. Makelele SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyaunyau (mapaka) SC.
8. Mwakarobo SC.
9. Mikia SC.
10. Miso Misonda SC.
11. Manyang'au SC.
12. Mazumbukuku SC.
13. Mazombi SC.
14. Kinyume nyume SC.
15. Ngada SC.
16. Kolowizard SC.
17. Zuwena SC.
18. Bebwabebwa (Mbeleko) SC.
19. Panya roads SC.
20. Kikanuni SC.
21. Kufa Kiume SC.
22. Ubaya ubwege SC.
23. 5imba SC.
24. Visingizio (Visababu) SC.
25. Manguruwe SC.
JamiiForums-31645776.jpeg
 
Wewe mkuu wewe!Tunyamaze.Hakuna aliyekuwa kwenye akili zake.
Akina aliyekuwa kwenye akili zake lakini tabia ya mchezaji uwanjani wote tunaijua, huwa hafanyi vile alivyofanya. Kwenye takwimu ile tunaiita "outlier"
 
Uliwahi kuona magoli aliyofunga Yahya Tostao akiwa timu ya taifa au lile goli la free kick alilofunga Robert Carlos dhidi ya Ufaransa.
Ile haikuwa free kick bro. Tena naomba Mungu lile goli liingie kwenye magoli bora na lishinde tuzo ili jamaa apate kifuta jasho baada ya kuutumikia mpira kwa miaka mingi bila kupata bao kama lile. Lile goli sio tabia ya shabalala.
 
Unaweza kuniambia sababu ya msingi iliyomuondoa NDUMBARO kwenye WIZARA YA UTAMADUNI NA MICHEZO?
 
Tuzungumzie mambo mengine. Tusikumbushane machungu, kila mmoja ameumia
 
Sikatai kuwa lile lilikuwa goli kali sana na linaweza kuwa miongoni mwa magoli bora ya mashindano, LAKINI LAKINI LAKINI ile ilikuwa cross iliyokatika na kuelekea golini moja kwa moja. Hata mfungaji alishangangaa kuambiwa limeingia golini; fluke
Mtaalamu wa kuona magoli ya bahati kutoka Tanzania
 
Back
Top Bottom