Kama amesoma kozi hiyo ya Utarii, hapa Nchini lazima atie kambi katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ikiwemo Zanzibar yenyewe. Hapo atakuwa anaishi katika mazingira rafiki na supportive kupata kazi kirahisi.
Sasa cha ajabu, utakuta mtu kasoma kozi hiyo na halafu unamkuta anakaa Dar es salaam, iringa, mbeya, mtwara, Shinyanga n.k.
Kuna jamaa yangu yeye ni mtaalamu wa lugha ya kifaransa, nakwambia toka amemaliza chuo amekuwa akiishi Arusha na Kilimanjaro na sasa ivi kapatia maisha Zanzibar. Kwa sasa yuko safi maisha bomba ndani ya sekta za kitalii.
Jamani, aina ya kozi ulosoma automatically inakudirect mahakama pankusihi na jamii ya kuishi nayo.