Ndugu zangu kwenu biashara zinakwendaje?

Ndugu zangu kwenu biashara zinakwendaje?

Bora nusu shari kuliko shari kamili, ngoja niendelee kula mshahara na posho awamu hii ya sita.

Niwakumbushe tu vijana wekezeni kwenye kilimo na ufugaji, mtakuja nishukuru siku moja.

Hutoona TRA akitaka kodi kwenye mauzo ya maziwa hata siku moja.
Aisee ni kweli maana mimi biashara ya vinywaji tu TRA kutaka kunikagua milolongo kibao
 
Ndugu zangu Wajasiriamali, wafanyabiashara vipi hali za biashara huko kwenu zikoje? Kadri siku zinavokwenda naona maluweluwe biashara inazidi kuwa ngumu afu ukicheki unatakiwa ulipe kodi ya pango, huku TRA wanataka kodi zao, mara manispaa wanakagua leseni hujakaa vizuri watu wa taka na fire wanataka pesa ukicheki biashara ngumu hakuna wateja yaani daah mpaka unaona kizunguzungu. Bank unadaiwa yaani tabu tupu.

Nagoli hapa kariakoo nauza mashuka/mapazia ila naona dalili za kufunga nicheki sehemu nyingine au niangalie upepo wa biashara nyingine vipi kwenu huko ndugu zangu biashara zikoje au mimi nimelogwa?? Ila ndugu zangu karibu wote wanalia biashara ngumu.

Kiukweli toka Mama aingie madarakani biashara zimekua ngumu sana sio hii nilikua na biashara ya kuuza lubricants za magari pale kamata ilibd nifunge nilikua sipati faida kabisa.

Ndugu zangu upepo kwenu unavumaje?
Naomba tumia na online pia tumia mitandao kutangaza biashara yako huku ukiendelea na kazi ya biashara yako.
 
Maisha NI magumu Sana nowdays natamani niwashauri acheni biashara tafuteni kazi za kuajiriwa muwe wafanyakazi
 
Maisha NI magumu Sana nowdays natamani niwashauri acheni biashara tafuteni kazi za kuajiriwa muwe wafanyakazi
Umepotea njia wewe. Ugumu wa kitu sio mwisho wa kitu, mapambano lazima yaendelee.
 
Pole, nilidhani ni Mimi Pekee Ila kwakweli Hali ni mabaya Sana ,Mungu aturehemu
 
Back
Top Bottom